shalet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 3,430
- 3,547
Wakuu pokeeni salamu zangu,
Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.
1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.
2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.
3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.
Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.
NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.