Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Usichojua kuhusu makanisa ya kiroho

Soma neno takatifu Na ulielewe... Tatizo mnapenda sana miujiza bila kupata muda wa kusoma neno, Na kuomba katika roho Na Kweli, kufunga Kwa dhati. Acha dhambi uone jinsi MUNGU atakavyokutendea

Umenena hapo mm siwezi kusema makanisa haya maana wapo aina tofauti tofauti yapo makanisa maduka na yapo makanisa kweli wanaomba na watu wanapona.

Kuna mchungaji alinieleza hivyo ulivyosema hapo juu acha dhambi
Uwe unafunga na unamuomba mungu kweli mambo yatanyooka vizuri tu.
 
Ndugu mtoa mada pole sana kwa yaliyokukuta kama ni kisa cha kweli. Lakini kwa conclusion yako inanifanya niamini kuwa hicho kisa siyo kweli bali lengo lilikuwa kusema hicho ulichokisema.
Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ni Mungu aponyaye, aliponya zamani na leo anaponya kwa utendaji wa Roho Mtakatifu kupitia kwa jina la mwanaye mpendwa Yesu Kristo. Huyu Yesu kristo ndiye anayesamehe watu dhambi zao, anaokoa, anaponya na kutenda miujiza mingi.

Kikubwa zaidi habari za manabii na walimu wa uongo Yesu mwenyewe alishazisema tangu mapema kuwa zitakuja kutokea. Hivyo siyo kitu cha ajabu, alijua kuna watu wangeingia kwenye mtego wa shetani hivyo akatahadharisha mapema.

Cha zaidi sana hata wakati wa kufufuka kuna watu wa zamani hizo walijipanga kueneza uongo kwamba Yesu hakufufuka LAKINI haikusaidia na haiwezi kusaidia. Nawe usiungane nao kupinga kile Yesu anachofanya hata sasa maana haitakusaidia wala haitabadili ukweli wa Yesu mponyaji wa watu.
 
Usipoelewa alichosema dada lowassa hapa,basi itakuwa vigum sana kuelewa haya mambo.hongera dada uko vizur sana mungu aendelee uwezo wa kuelewa ili uendelee kuelimisha jamii
 
Mkuu mimi ni Mkristo kabisa
Kuamini ni tofauti sana na kuwa kwa maana ya ufuasi wa Kimadhehebu muamini Kristo leo.... mimi ninaushuhuda binafsi wa kumuamini Kristo. Mungu ni halisi mkuu na matendo yake ni zaidi ya wanadamu wanavyoweza kuyaeleza au kufafanua na ni dhahir kwelikwelii....Kristo alitoa mfano wa imani ndogo kama mbegu ya haladari kupokea.. sasa tatizo binadamu tunawaamni sana binadamu wenzetu badala ya kuelekeza Imani zetu kwake, Mungu hapakatwi wala hamilikiwi na mwanadamu yoyote... Tuache kuendelea kulaumu watu wengine kwa madhaifu yetu wenyewe..... Yeye achunguzaye mioyo kujua nia za wanadamu na kuzijaribu.... sasa mkuu sikuhukumu ila kwa ujumbe huu uliouleta kwenye social network inabidi ujichunguze mwenyewe kama Yeye Mungu Mkuu kupitia Mwana Yesu Kristo ulistahili kupokea uponyaji wakati ulipoumwa.
 
Pole sana mtoa mada kwa kukutana na kadhia hiyo,lakini ningependa usome sana neno la Mungu"BIBLIA"silikiza kwa bidii,tunza na fuata maagizo!(Kumb 28).ndicho kitu kikubwa ukitaka kumwona Mungu wa Isaka,Yakobo na Ibrahim kwa vitendo, haya mambo ya kuombewaombewa ni unataka kuota kipara kwa kushikwa shikwa kichwani biblia iko wazi sana kamautambwomba Roho wa Mungu akuongoze/akufunndishe na si kusoma kama kitabu cha alfu lela ulela!
REF_MANENO KUHUSU IMANI-:Warumi 10:17,-Mithali 3:5, 6,-Marko 9:23,-Luka 1:37,-Mathayo 9:29,-**Yakobo 1:5-8,-Yakobo 2:26,-*Warumi 14:23,-Waebrania 10:38,-1 Yohana 5:4,Waefeso 6:16,-Waebrania 12:2,-Warumi 5:1,-Mathayo 17:20,-
 
Kwan what makes one mhubiri wa kwel na the other mtumish wa uongo???
 
Wengi wanapenda kuombewa.
Inapaswa ujiombee kwanza....tena kwa kuamini wewe mwenyewe na si kutumia inani ya mchungaji....

Imeandikwa ..."imani yako imekuponya"

Pia biblia imesema "kuzichunguza roho hizo" tuache kukimbilia kwa wachungaji kila kukicha (ingawa shida ikikushika kuna mahangaiko ndio tunajikuta tunabadili makanisa kila kukicha)
 
mh makanisa makanisa..kizazi hiki kinataka maajabu tu hakina haja na imani .imani ya sasa ni nipe nikupe watu wanaenda kanisani ili wapate pesa magari kazi nzuri nyumba vyeo mke mzuri .na wachungaji wamegundua udhaifu wetu wanahubiri mali wanahubiri pesa nasi tumeingia ktk mtego huo mn tumekosa maarifa..yesu alisisitiza imani tu si miijuza
 
Tito 1
Maana imempasa askofu awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.
Kwa maana kuna wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, wadanganyaji, na hasa wale wa tohara, ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hao wanapindua watu wa nyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.
Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, Wakrete ni waongo siku zote, hayawani wabaya, walafi wavivu.
Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani; wasisikilize hadithi za Kiyahudi, wala maagizo ya watu wajiepushao na yaliyo kweli.
Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia. Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai.
Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima;
 
Kuna huyu bwana wa Mwanza anajiita sijui nabii Malisa,siku hiyo nyumbani sina kazi nikaona nipoteze muda kwenye tv..anawahubiria waamini kwamba watoe sadaka mpaka ziwaume na kila atakayetoa sadaka yake itarudi kwake maradufu kupitia tigopesa,m-pesa na airtel money sikuamini nilichokisikia nikajiuliza kwanini yeye asiziombee zaka zake zikarudi kwake,na watu wanaamini,muhubiri ibada nzima anasisitiza toeni sadaka toeni sadaka,zinakoenda hapajulikani wala matumizi yake hamsomewi watu hawashtuki tu.mie ni RC tukitoa sadaka zinaelezwa matumizi yake,tukiambiwa mchango kwa ajili ya kuongeza sehemu either darasa la watoto,may be kununua chochote kwa matumizi ya Parokia mahalia tukishachanga tunaelezwa zimetumikaje,salio lililobaki na litatumika wapi na kama mtu una wasiwasi unaruhusiwa kuhoji na mwisho wa mwaka tunasomewa mapato,matumizi,balance iliyobaki siyo watu wanatoa sadaka mchungaji ananunua Hummer anaishi kwenye kighorofa na hamuwezi kuhoji,ukihoji unaambiwa una pepo,nitake kuujua ukweli uniambie nina pepo?hapo juu kuna mtu kasema kwamba Catholics tunasali kwa mapokeo,nakuhakikishia mkuu wewe hujapata kuufahamu Ukatoliki umehadithiwa tu.
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
Kanisa Ni moja tu takatifu katoliki la mitume. Mengine madhehebu.Chunguza.
 
Tusipotoshwe, twendeni kanisani tumkabidhi mungu maisha yetu. Tena kanisani usiyumbishwe kuwa eti huku kuna moto na huku hakuna, Mkabidhi mungu maisha yako achana na binadamu.
wengi wa hawa wahubiri wa kileo ni matapeli. Siku moja niliona katika TV mzee wa ******** akipokonya elfu kumi alioshikilia muumini wake aliyekuwa anaenda kutoa sadaka na kuombewa, ile namna aliopokonya huyu mtumishi ilinifanya nihis hakuna maombezi wa uponyaji bali utapeli. Nikajiuliza kwanini anapokea sadaka kwa namna ile wakati hata hivyo muumini alikuwa anapeleka kwa hiari kabisa. tena akasema unapokea upako, mimio napokea PESA!
Jamani Mungu wetu ni Mungu wa mwenye busara, tumwendeapo tumwendee kwa hekima na sio mambo kama haya.
Ndio maana mimi na familia nitabaki kuwa Mlutheri mpaka dunia ifunikwe, kwenda huko kwingine ni kutanga tanga.
 
Mtoa mada unaweza ukawa na point lakini umeshindwa kufanya presentation vizuri. And I can only assume hii imetokana na ukweli kuwa umefanya conclusion based on kile kilichokutokea wewe na siyo kile ambacho Mungu anaongea juu ya manabii wa uongo. Manabii wa uongo hawapo kwasababu wewe ulienda kanisani ukatabiriwa mambo mawili tofauti na mtumishi mmoja. Manabii wa uongo wapo kwasababu Yesu alitabiri miaka 2000 iliyopita kuwa watatokea.

Mtu wa kwanza kutabiri kuwa kutatokea manabii wa uongo ni Yesu mwenyewe. Alisema katika Mathayo 24:5 kuwa wengi watakuja kwa jina lake wakisema wao ni Kristo. Lakini kwenye Mathayo 24:24 Yesu anarudia tena kuonya kuwa "watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza hata walio wateule". Kwenye Yohana 5:43 anaendelea kuonya tena kuwa "mimi nimekuja kwa jina langu wala hamnipokei mwingine akija kwa jina lake mtampokea".

Mifano hiyo michache kutoka kwa Kristo ni uthibitisho tosha kuwa suala la uwezekano wa kuwepo manabii wa uongo siyo habari mpya tena. Ni dhahiri kuwa lazima wawepo hata mtu asipotuambia kuwa wapo.

Kitu cha msingi ni kuelewa kuwa huwezi kuwa na NABII WA UONGO kama hayupo NABII WA UKWELI. Yaani neno uongo linatokana na neno ukweli. Huwezi kumwambia mtu anakudanganya kama hujui ukweli unafananaje. Kwa mfano, huwezi kusema simu hii ni FAKE ilihali hujui sifa za kuifanya simu kuwa ORIGINAL ni zipi. Hutaweza.

So Yesu aliposema tujihadhari na manabii wa uongo, alichokuwa anamaanisha wakati huohuo ni kuwa tujifunze ni sifa zipi zinamfanya mtu kuwa nabii wa ukweli. Alikuwa hana lengo la kutufanya kustick na kufocus kutafuta manabii wa uongo popote walipo halafu tuanze kudraw dangerous conclusions kuwa MANABII WOTE NI WAONGO TU, halafu hatufanyi jitihada zozote kuwatafuta wale walio wa ukweli. Huko kutakuwa ni kujidanganya na tutakuwa tunamsaidia Shetani kutupumbaza tu. Hatupaswi kutoa msaada wa aina yoyote kwa Shetani.

Sasa ili usitoe msaada wa aina hiyo kwa Shetani. Yaani ili uache kuhangaika kuishi kwa kutafuta makosa (faultfinding) ya watumishi na uanze kuconcentate on sifa nzuri zinazofanya mtumishi awe NABII WA KWELI, ni lazima uzame kwenye NENO LA MUNGU. Ukijifunza vizuri Neno la Mungu, utajua ni jinsi gani ufalme wa Mungu unafanya kazi na ni sifa zipi zinamqualify mtu kuwa mtumishi wa Mungu wa ukweli. In fact Biblia ina majibu ya matatizo yote binadamu anayokutana nayo kiasi kwamba ukiwa msomaji mzuri wa Neno, itafikia kipindi wala hautahitaji tena kwenda kuonana na nabii ili atatue tatizo lako. NENO la Mungu linatosha kabisa kumaliza matatizo yooooooooote unayokutana nayo makubwa au madogo. Kitu muhimu ni kuamini tu. PERIOD.

Kwahiyo anza leo kusoma Biblia yako kwa utulivu huku ukiomba uongozi wa Roho Mtakatifu ili uachane na habari za kwenda kutafuta msaada kwa manabii--wawe wa uongo au wa ukweli.
Mimi ni wa imani nyingine ila umenifundisha vitu vizuri sana. Always i appreciate what u represent madamme. God bless u, ila kakidhungu kamekosa ata kidogo leo.
 
Wakuu pokeeni salamu zangu,

Kutokana na kuhangaika na maradhi sugu nilijikuta naenda katika haya makanisa ya kiroho kuombewa hiki ndicho nilichokiona huko.

1. Pesa kwanza; hufanyiwi maombi mpaka ulipishwe pesa tena ukifika siku ya kwanza unaulizwa kazi unayofanya kabisa alafu watakuambia roho mtakatifu kakuambia utoe shilingi ngapi.

2. Unatolewa unabii feki kabisa; nilienda mara ya kwanza nikaambiwa tatizo langu nimerogwa kuna binti niliahidi kumuoa nikamkimbia, kwa kijana kuahidi kuoa mtu na kukimbia ni jambo la kawaida nikakubali ila naenda kuombewa tena mara ya pili akawa kanisahau kwenye unabii akasema tatizo langu linasababishwa na vifungo ambazo wazee wangu waliingia hivyo nahitaji kutoa sadaka ya ukombozi kumbuka huyo ni mtumishi mmoja anatoa unabii tofauti kwa mtu mmoja na tatizo moja.

3. Maombi hayasaidii kupona; kila ugonjwa kuna uwekano wa kupona na kutokupona wanachofanya hawa watumishi ni kucheza na probability wale wakupona wakija kutoa ushuhuda wanawavuta na wengine waje kuombewa, wale wasiopona hawana nafasi ya kuja kushuhudia tena hivyo tunawasikia waliopona tu wasiopona hatuwasikii, hivyo kuonekana watu wanapona kweli ila si kwa ajili ya maombi ni natural selection tu.

Baada ya kusema hayo naomba kuwasisitiza msidanganywe na matangazo ya redion kuhusu uponyaji ni feki uponyaji ni suala la asili hata bila kuombewa kuna watu wanapona wengine hawaponi, kazi hata bila kuombewa kuna watu watapata wengine hawawezi pata na mafanikio yoyote yale ni hivohivo.

NB: Unaweza ongeza matatizo uliokumbana nayo ulivoenda kuombewa.
Hivi niulize tu. Ni kanisa gani ukienda unaulizwa kama unazifata amri 10 za Mungu, lipo kweli? Make zile amri kwangu mie naamini ndo msingi na ndo uzima, ajabu ukienda kanisani hautakuja kuulizwa juu ya msingi huu wa kiroho. Kinachofanyika kule ni mbwembwe kibao, tusidanganyane, bila ya kuzifata hizo amri, make ndo dira yetu ..uponyaji haupo.
 
Back
Top Bottom