Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Hiyo kazi ulipewa au ulijipa na hukuwa na kazi nyingine ya kufanya?.

uwezo wako wa kuchambua mambo ni wa kutiliwa mashaka nadhani ulikuwa unaota mkuu.

Nadhani umeenda dodoma ukaishia kushangaa maendeleo yaliyoletwa na ccm.

leo ni jumapili nenda kanisani upunguze hizo dhambi,na kaa ukijua dodoma ni ccm chadema wanaidharau kama kandambili tangu mbowe awatukane ndo basi tena.

Tunataka mabadiliko,yawe mazuri au mabaya tunayahitaji. Hata Ghadaffi aliwaambia Walibya kuwa hamuoni maendeleo? Lakini watu walimjibu "We need changes" David Malole hana lolote pale Dodoma ni sawa na Mbwa asiye na meno.
 
kuichukia ccm kwa maneno haitoshi, waonyesha chuki ya kweli 2014 kwenye chaguzi za serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, Dodoma haina hata jimbo moja la upinzani hata madiwani wa upinzani cjui kama wapo!

Kweli mkuu vitendo ndo jibu na siyo kulalamika tu tena wengi wao huwa hawapigi kura
 
kuichukia ccm kwa maneno haitoshi, waonyesha chuki ya kweli 2014 kwenye chaguzi za serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, Dodoma haina hata jimbo moja la upinzani hata madiwani wa upinzani cjui kama wapo!

Kweli mkuu vitendo ndo jibu na siyo kulalamika tu tena wengi wao huwa hawapigi kura alafu ndo wa kwanza kulalamika.... . .
 
Hiyo kazi ulipewa au ulijipa na hukuwa na kazi nyingine ya kufanya?.

uwezo wako wa kuchambua mambo ni wa kutiliwa mashaka nadhani ulikuwa unaota mkuu.

Nadhani umeenda dodoma ukaishia kushangaa maendeleo yaliyoletwa na ccm.

leo ni jumapili nenda kanisani upunguze hizo dhambi,na kaa ukijua dodoma ni ccm chadema wanaidharau kama kandambili tangu mbowe awatukane ndo basi tena.

Fikra mmfu ndizo zinazokupelekea kutoa kauli unazotoa ila mwisho wa siku utakubaliana na ukweli
 
1. Tujiandikishe kupiga kura. 2. Tupige kura. 3. Tulinde kura zetu. Haya yote mwisho wake ndo huo

Hofu yangu ni pale magamba watakaposhindwa kukubaliana na matoke ya sanduku la kura na mwisho wake yakaja kuwa kama yale Ivor cost japo nisingependa yawe hivyo.
 
Umechemka mzee. Wewe huwafahamu wana dodoma. Mimi naishi dodoma hapa na nina uhakika ulioongea nao wanasema tu kwa midomo lakini mioyoni mwao wanaipenda ccm. Subiri uchaguzi utaona hata kata moja tu ya dodoma haitaingia upinzani.
 
Chadema dodo iliwambia ni wajinga,wamelala na wanachelewesha ukombozi kauri hizi bado zinakumbukwa wala msipate shida kuja dodoma ni kujiptezea mda wenu.

Hata mkuu wa kaya aliwahi kukataa kura za wafanyakazi, na alishinda uchaguzi.
 
Ninavyoifahamu mimi, dodoma watakuwa wa mwisho kuichukia CCM, wakishapewa kofia na khanga, wanasahau yote
 
CCM bado iko dom tusilete visivyo na ukweli ndugu. Umekaa wiki tatu then unapost huu utumbo wa kujifariji na kuwadanganya wapinzani. Mimi nina miaka mitatu hapa dom najua zaid kuliko ulichokiandika hapa. Eti utafiti? Utafiti gan unafanya, sample yenyewe ndogo, watu gan umewahoji? Unahoji watu ambao hata kura hawapigi. Eg Issue ya ajira tusipende kudanganyana kama slaa anavodai atatoa ajira huo ni uongo mtupu.
 
Ccm wamebuni mkakati mwingine wakati wa uchaguzi wanahamishia vifaru na wanajeshi kwenye vituo ili kuwatisha wanamapinduzi wasipige kura, hivyo ndugu zangu 2015 mlioichukia ccm muwe jasiri wa kujitokezs kulinda kura zenu. Dawa ni kuondoa haya maradhi yaitwayo ccm
 
Umesha anza kupata akili kidogo, ukizidi kuitumia elimu ya gumbaru uliyoipata utazidi kuuona ukweli, naamini umefikiria vyema na kuandika haya kwa kuwa bado ni asubuhi tumbo halina njaa, kijua kikichomoza tu utaanza kufikiria kwa kutumia tumbo.

Wenzio wa buku 7 FC wakikusoma leo sijui kama utapewa mgao. CHAMVIGHA NE CHEFEFEWA.
Mkuu mohamed Mtoi, usidhani hawa jamaa hawana roho,wanazo ila wanaamua kujitia upofu kwa kuendekeza njaa. Kuna wakati hata wao wanauona ukweli na unawauma ndio maana wanajisahau nakuandika kama alivyoandika kinyume na matakwa ya Paymaster wao @Nape.
 
Last edited by a moderator:
Nikiwa katika mji wa Dodoma kwa takriban wiki tatu sasa nimebahatika kuzungumza na makundi tofauti ya watu katika maeneo ya Kikuyu, Mkonze, Ipagala, Swaswa, Chang'ombe, Majengo na Mailimbili.

Pamoja na ukweli Mitaa ya Dodoma mjini inapendeza sasa kwa kutandazwa lami bado raia wengi wanaonyesha kuichoka CCM.

Sababu nilizozigundua ni hizi kuu 4 ingawa zipo sababu nyingi zinazoashiria anguko la CCM kwa viunga vya Dodoma
1. CCM imechokwa. Kwa kuwepo kwake madarakani kwa muda mrefu kumewafanya wengi watamani mabadiliko. Vijana wengi wenye miaka 35 kushuka chini wamezaliwa wameikuta CCM. Wameenda shule kwa level zote wapo na CCM. Wameanza kazi wapo na CCM na sasa wana familia wapo na CCM. Wana Dodoma wanasema kuna ndugu zao wamezaliwa hadi wametangulia mbele za haki bado wapo na CCM. Ndipo nilipokumbuka usemi usemao KITU CHOCHOTE KITAKACHOISHI MIAKA MINGI KINACHOFUATA NI KIFO. Kwenye Product life cycle theory, baada ya stage ya Maturity kinachofuatia ni Decline(Death). CCM imeshaishi miaka mingi. Tumezaliwa tunamsikia Wassira, Kikwete, Mangula, Kinana na wengineo. CCM imeshapita Maturity stage na sasa inaanguka. Wakazi wa Dodoma wamethibitisha.
Ili kujihalalishia uhalali wa utawala CCM imeamua kumwaga damu.

2. Wakazi wengi wa Dodoma nilioongea nao Wanaiona CCM ya sasa kama genge la wahuni. Wapo watu zaidi ya Wanne waliosema CCM ni majambazi. Sababu kuu ni kuwa wapo tayari kuua mradi tu mambo yao waende. Wanashindwa kuona natural death inayowakabili. Mkazi wa Msalato alisema CCM imeacha majukumu tuliyowapa wao kazi yao ni Chadema tu. Bungeni Chadema, Mahakamani Chadema, Mawaziri kutwa kucha Chadema. Huduma za jamii ambazo kimsingi CCM ndio wenye ridhaa ya kutekeleza zimewashinda. Wako busy kuua raia wasio na hatia na kufungua kesi zisizomsaidia mtanzania na kusahau majukumu yao. Kifupi ni kuwa Dodoma wanawaona CCM kuwa ni Chama cha Wauaji. Nilipotaka kupata maoni yao kuhusu mauaji ya bomu la Arusha walinijibu wengine kwa hasira' NANI HAJUI KUWA NI CCM WALIOUA? Kijana mmoja wa Chuo cha Mipango akamtaja kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM anayetokea kanda hii ya kati kuwa ndiye anayepanga na kufadhili mauaji. Alikwenda mbali zaidi na kutabiri kuwa kiongozi huyo atakufa kifo kibaya sana.

3. Hali ngumu ya maisha ni jambo lililosemwa na wengi kuwa limesababishwa na CCM. Wanahoji kama tuna madini, gesi, mbuga za wanyama, bahari, Ardhi ya kutosha yenye rutuba iweje leo mtu aumwe akose huduma kwenye hospitali za umma? Iweje leo ukitoka tu kidogo mji wa dodoma hupati maji safi na salama? Iweje leo washuhudie anguko kuu la Elimu namna hii? Iweje leo Dodoma iwe na watu wanaokufa njaa?
Wapo walioamua kulima na kukamua alizeti. Hakuna masoko. Badala yake serikali imekazana na mfanyabiashara wa kiasia anayefanya biashara ya kuingiza mafuta ya alizeti akitokea nje ya nchi.

4. Vijana kukosa ajira. Wakazi wa Dodoma wameonyesha masikitiko yao hasa kwa namna vijana wanavyohangaika. Ni ukweli uliowazi kuwa vijana ndio wanao hold labour force kubwa Tanzania. Lakini VETA haijawasaidia, Elimu ya Chuo kikuu haijawasaidia, wapo wenye masters wanahangaika tu. Ukiwauliza viongozi wa kisiasa(wa CCM) wanawapa majibu mepesi eti waondoe dhana ya kuajiriwa wawaze kujiajiri. Hata mimi nilipowapa hiyo changamoto waliona kama ninawadhihaki. 'Brother mimi najiajiri naanzia wapi? Nitapata wapi uwezo wa kununua vifaa vya Capentry masikini mimi? Nani atanikopesha? Benki gani itaniamini bro? Alisema kijana mmoja wa Kikuyu aliyemaliza mafunzo ya Veta mwaka jana kwa level ya trade test two.
Madereva wa bodaboda wameponda sana sifa wasizostahili kupata CCM na serikali yake hasa kwa kuondoa ushuru wa bodaboda. Ingawa wameshukuru mkopo wa pikipiki wanaopewa na mbunge wao kwa masharti makali na magumu wamesema kabisa bila kupepesa kuwa ushuru ulioondolewa unawanufaisha wamiliki wa bodaboda na sio madereva wa bodaboda. Wao wangenufaika endapo tozo kwenye mafuta hasa petroli zingepungua na kushusha bei ya petroli hivyo kuwaongezea kipato kuliko bei ya sasa ambayo kwa madai yao kila wakipatacho kinaishia kwa mmiliki wa bodaboda.

Ni hayo tu kutoka Dodoma.
kama Mtwara wamebadilika hata Dodoma itawezekana, ccm kwa jinsi walivyojisahahu hilo hawalioni
 
Mimi najielewa vya kutosha wala siitaji kufanyiwa apreciation juu ya ufahamu wangu na nafahamu ninachokiandika na ninachokiamini. Situmikii buku 7 wala situmiki kuhongwa viloba na Dj ili niweze kusastain town kama mnavyofanya nyie mimi ninajituma wala si njaa za madaraka kwa ajili ya kushibisha tumbo kama nyie waganga njaa mnaolazimisha kuwatumikia mabwana zenu ili watoto wasilale na njaa. Elimu yangu ya Ngumbaru inanisaidia kujitambua si kama elimu yako iliyochanganyika na moshi wa sigara ulioupata kule msituni ulikosemea kiasi mpaka unashauriwa hauwelewi kwakuwa ubongo ulishaathiriwa.

Mkuu ungekuwa unajitambua usinge kuwa unatumia kujitambua kwako kucha kuaandika utumbo wa kishabiki humu ndani. Anaye jitambua huwa ana jicho la tatu kama moja ya macho yake mawili yasipo ona sawasawa.

Naamini huenda hata wewe ulitamani sana kusoma kule unako ita msituni lakini haikuwezekana! Si unajua marks nazo zilikuwa zina matter.
 
CCM bado iko dom tusilete visivyo na ukweli ndugu. Umekaa wiki tatu then unapost huu utumbo wa kujifariji na kuwadanganya wapinzani. Mimi nina miaka mitatu hapa dom najua zaid kuliko ulichokiandika hapa. Eti utafiti? Utafiti gan unafanya, sample yenyewe ndogo, watu gan umewahoji? Unahoji watu ambao hata kura hawapigi. Eg Issue ya ajira tusipende kudanganyana kama slaa anavodai atatoa ajira huo ni uongo mtupu.

namkumbuka Gadafi aliwafanyia mambo
mengi mazuri watu wa libya lakini alipoamua
kupambana na wanachi wake kwa kuwa
walikuwa wanataka mabadiliko sasa hivi sijui
kama kuna ukoo tena wa Gadifi Libya
 
Bye bye CCM na Mwingulu asiogope ikianguka CCM tuna shamba la mikorosho tutamfanya mlinzi
 
Back
Top Bottom