Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Mzito Kabwela

Platinum Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,908
Reaction score
7,751
Nikiwa katika mji wa Dodoma kwa takriban wiki tatu sasa nimebahatika kuzungumza na makundi tofauti ya watu katika maeneo ya Kikuyu, Mkonze, Ipagala, Swaswa, Chang'ombe, Majengo na Mailimbili.

Pamoja na ukweli Mitaa ya Dodoma mjini inapendeza sasa kwa kutandazwa lami bado raia wengi wanaonyesha kuichoka CCM.

Sababu nilizozigundua ni hizi kuu 4 ingawa zipo sababu nyingi zinazoashiria anguko la CCM kwa viunga vya Dodoma
1. CCM imechokwa. Kwa kuwepo kwake madarakani kwa muda mrefu kumewafanya wengi watamani mabadiliko. Vijana wengi wenye miaka 35 kushuka chini wamezaliwa wameikuta CCM. Wameenda shule kwa level zote wapo na CCM. Wameanza kazi wapo na CCM na sasa wana familia wapo na CCM. Wana Dodoma wanasema kuna ndugu zao wamezaliwa hadi wametangulia mbele za haki bado wapo na CCM. Ndipo nilipokumbuka usemi usemao KITU CHOCHOTE KITAKACHOISHI MIAKA MINGI KINACHOFUATA NI KIFO. Kwenye Product life cycle theory, baada ya stage ya Maturity kinachofuatia ni Decline(Death). CCM imeshaishi miaka mingi. Tumezaliwa tunamsikia Wassira, Kikwete, Mangula, Kinana na wengineo. CCM imeshapita Maturity stage na sasa inaanguka. Wakazi wa Dodoma wamethibitisha.
Ili kujihalalishia uhalali wa utawala CCM imeamua kumwaga damu.

2. Wakazi wengi wa Dodoma nilioongea nao Wanaiona CCM ya sasa kama genge la wahuni. Wapo watu zaidi ya Wanne waliosema CCM ni majambazi. Sababu kuu ni kuwa wapo tayari kuua mradi tu mambo yao waende. Wanashindwa kuona natural death inayowakabili. Mkazi wa Msalato alisema CCM imeacha majukumu tuliyowapa wao kazi yao ni Chadema tu. Bungeni Chadema, Mahakamani Chadema, Mawaziri kutwa kucha Chadema. Huduma za jamii ambazo kimsingi CCM ndio wenye ridhaa ya kutekeleza zimewashinda. Wako busy kuua raia wasio na hatia na kufungua kesi zisizomsaidia mtanzania na kusahau majukumu yao. Kifupi ni kuwa Dodoma wanawaona CCM kuwa ni Chama cha Wauaji. Nilipotaka kupata maoni yao kuhusu mauaji ya bomu la Arusha walinijibu wengine kwa hasira' NANI HAJUI KUWA NI CCM WALIOUA? Kijana mmoja wa Chuo cha Mipango akamtaja kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM anayetokea kanda hii ya kati kuwa ndiye anayepanga na kufadhili mauaji. Alikwenda mbali zaidi na kutabiri kuwa kiongozi huyo atakufa kifo kibaya sana.

3. Hali ngumu ya maisha ni jambo lililosemwa na wengi kuwa limesababishwa na CCM. Wanahoji kama tuna madini, gesi, mbuga za wanyama, bahari, Ardhi ya kutosha yenye rutuba iweje leo mtu aumwe akose huduma kwenye hospitali za umma? Iweje leo ukitoka tu kidogo mji wa dodoma hupati maji safi na salama? Iweje leo washuhudie anguko kuu la Elimu namna hii? Iweje leo Dodoma iwe na watu wanaokufa njaa?
Wapo walioamua kulima na kukamua alizeti. Hakuna masoko. Badala yake serikali imekazana na mfanyabiashara wa kiasia anayefanya biashara ya kuingiza mafuta ya alizeti akitokea nje ya nchi.

4. Vijana kukosa ajira. Wakazi wa Dodoma wameonyesha masikitiko yao hasa kwa namna vijana wanavyohangaika. Ni ukweli uliowazi kuwa vijana ndio wanao hold labour force kubwa Tanzania. Lakini VETA haijawasaidia, Elimu ya Chuo kikuu haijawasaidia, wapo wenye masters wanahangaika tu. Ukiwauliza viongozi wa kisiasa(wa CCM) wanawapa majibu mepesi eti waondoe dhana ya kuajiriwa wawaze kujiajiri. Hata mimi nilipowapa hiyo changamoto waliona kama ninawadhihaki. 'Brother mimi najiajiri naanzia wapi? Nitapata wapi uwezo wa kununua vifaa vya Capentry masikini mimi? Nani atanikopesha? Benki gani itaniamini bro? Alisema kijana mmoja wa Kikuyu aliyemaliza mafunzo ya Veta mwaka jana kwa level ya trade test two.
Madereva wa bodaboda wameponda sana sifa wasizostahili kupata CCM na serikali yake hasa kwa kuondoa ushuru wa bodaboda. Ingawa wameshukuru mkopo wa pikipiki wanaopewa na mbunge wao kwa masharti makali na magumu wamesema kabisa bila kupepesa kuwa ushuru ulioondolewa unawanufaisha wamiliki wa bodaboda na sio madereva wa bodaboda. Wao wangenufaika endapo tozo kwenye mafuta hasa petroli zingepungua na kushusha bei ya petroli hivyo kuwaongezea kipato kuliko bei ya sasa ambayo kwa madai yao kila wakipatacho kinaishia kwa mmiliki wa bodaboda.

Ni hayo tu kutoka Dodoma.
 
kuichukia ccm kwa maneno haitoshi, waonyesha chuki ya kweli 2014 kwenye chaguzi za serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, Dodoma haina hata jimbo moja la upinzani hata madiwani wa upinzani cjui kama wapo!
 
Mkuu kwa picha niliyoiona kwa macho yangu, CCM wanapumulia mashine hapa dodoma
 
Umenikumbusha kuwa hata mbunge wao ni mmoja wa wale wanaoingia na Shuka mjengoni kama Wassira,Ndugulile,Missanga,MTEMVU n.k
 
Hiyo kazi ulipewa au ulijipa na hukuwa na kazi nyingine ya kufanya?.

uwezo wako wa kuchambua mambo ni wa kutiliwa mashaka nadhani ulikuwa unaota mkuu.

Nadhani umeenda dodoma ukaishia kushangaa maendeleo yaliyoletwa na ccm.

leo ni jumapili nenda kanisani upunguze hizo dhambi,na kaa ukijua dodoma ni ccm chadema wanaidharau kama kandambili tangu mbowe awatukane ndo basi tena.
 
1. Tujiandikishe kupiga kura. 2. Tupige kura. 3. Tulinde kura zetu. Haya yote mwisho wake ndo huo
 
huo utafiti wako sample space zote ulizotumia ni za cdm kwa taarifa yk dom hawana ujinga km wa arusha na mbeya watu wanahangaika na kutafuta maisha ccm wangechokwa cdm wangepata hata jimbo moja juz uchaguzi mdogo bado jamaa wamepeta...danganya wajinga wenzako wa humuhumu jf ambao mpo kikazi zaidi kuitangaza cdm wazee wa sera nyepes sasa mnalia na mwigulu chama kizima
 
Huitaji kuandika maneno mengi kuonyesha kuchokwa kwa ccm na vijana wengi hapa Tanzania na baadhi ya makundi mengine ya watanzania, hauhitaji kufanya research ndio uje useme ccm imechokwa na kadharika hilo kila mwenye akili analijua na ukweli hakuna kijana ambaye ameenda shule akaendelea kuitetea Ccm bali akifanya hivyo anasababu zake tena za maana. Sababu kubwa hakuna chama mbadala chenye vision na mission za kumsaidia Mtanzania, kutumia rasilimali zilizojaa hapa nchini kwa maslahi ya wote. Hakuna chama kinachonekana kuwa kitawatendea watanzania haki bila ubaguzi wa kikanda, kikabila, kidini n.k
Hakuna chama chenye sera bali kuna vyama vyenye vioja Tanzania na hasa chadema haina dira hata kidogo tena naweza sema ni ccm B.
Kwamaana hiyo ndio utawakuta watanzania asilimia kubwa wanawapigia na wataendelea kuwapigia kura ccm mpaka hapo itakapotokea chama mbadala wa ccm.
Tia akilini haya na ujue kuiweka Cdm madarakani ni sawa na kuruka mkojo na kukanyaga mavi.
 
Chadema dodo iliwambia ni wajinga,wamelala na wanachelewesha ukombozi kauri hizi bado zinakumbukwa wala msipate shida kuja dodoma ni kujiptezea mda wenu.
 
Hiyo kazi ulipewa au ulijipa na hukuwa na kazi nyingine ya kufanya?.

uwezo wako wa kuchambua mambo ni wa kutiliwa mashaka nadhani ulikuwa unaota mkuu.

Nadhani umeenda dodoma ukaishia kushangaa maendeleo yaliyoletwa na ccm.

leo ni jumapili nenda kanisani upunguze hizo dhambi,na kaa ukijua dodoma ni ccm chadema wanaidharau kama kandambili tangu mbowe awatukane ndo basi tena.

Mmechokwa. Full stop! Mmebaki kuua tu
 
cdm wababaishaji tu chama hata kikikaa miaka mia swala ni nn kinafanya mmejengewa vyuo na ccm mmepewa uhuru wa kidemocrasia vyombo ya habari vipo huru bado mnadanganya watu mnataka ukombozi ju ya nn? alafu mlivyowatoto kisiasa na mbinu chafu mlizonazo mtu mmoja ndo anapa?bana na chama kizima cdm nzima mnamwogopa mwigulu kila kukicha mnamtaja nadhan hata mnamwota nyie ww mtoa mada kasali mungu akupanue akili usiwe unapost ujinga wk alafu unasema utafiti..fanya tafit ya kichwa chako..
 
huo utafiti wako sample space zote ulizotumia ni za cdm kwa taarifa yk dom hawana ujinga km wa arusha na mbeya watu wanahangaika na kutafuta maisha ccm wangechokwa cdm wangepata hata jimbo moja juz uchaguzi mdogo bado jamaa wamepeta...danganya wajinga wenzako wa humuhumu jf ambao mpo kikazi zaidi kuitangaza cdm wazee wa sera nyepes sasa mnalia na mwigulu chama kizima

Unakiri kuwa CDM imejikita mizizi Dodoma?
 
Mmechokwa!
 
hata ikatokwea ccm imechokwa stil sijaona chama mbadala cakututoa hapa tulipo na kwenda mbali bado sana wote hao wakina slaa si ndo wezi wa hela ndogo km sadaka tena za maskin ukimpa nchi ataiacha mixer na wakanda wenzie ma enterprener km mbowe.jambazi la magar lema vuta ndumu la fomu two sugu mwizi mwingine lissu aliejifanya anatetea wachimbaji wadogo kumbe anakula pia na wamigodi nani msafi cdm...
 
Huitaji kuandika maneno mengi kuonyesha kuchokwa kwa ccm na vijana wengi hapa Tanzania na baadhi ya makundi mengine ya watanzania, hauhitaji kufanya research ndio uje useme ccm imechokwa na kadharika hilo kila mwenye akili analijua na ukweli hakuna kijana ambaye ameenda shule akaendelea kuitetea Ccm bali akifanya hivyo anasababu zake tena za maana.

Umesha anza kupata akili kidogo, ukizidi kuitumia elimu ya gumbaru uliyoipata utazidi kuuona ukweli, naamini umefikiria vyema na kuandika haya kwa kuwa bado ni asubuhi tumbo halina njaa, kijua kikichomoza tu utaanza kufikiria kwa kutumia tumbo.

Wenzio wa buku 7 FC wakikusoma leo sijui kama utapewa mgao. CHAMVIGHA NE CHEFEFEWA.
 
huo utafiti wako sample space zote ulizotumia ni za cdm kwa taarifa yk dom hawana ujinga km wa arusha na mbeya watu wanahangaika na kutafuta maisha ccm wangechokwa cdm wangepata hata jimbo moja juz uchaguzi mdogo bado jamaa wamepeta...danganya wajinga wenzako wa humuhumu jf ambao mpo kikazi zaidi kuitangaza cdm wazee wa sera nyepes sasa mnalia na mwigulu chama kizima
Na ndio maana Wana maendeleo makubwa ya kuomba omba Kama alivyokuwa Yule tajiri Yao matonya
 
Na ndio maana Wana maendeleo makubwa ya kuomba omba Kama alivyokuwa Yule tajiri Yao matonya

Chakushangaza bado watu wa dodoma wanaishi maisha duni sana! Kilometa 20 kutoka kwenye mjengo wa bunge unakutana na nyumba za tembe (juu udongo chini udongo) nyingi kuliko unavyoweza kufikiri. Naamini siku wanadodoma wakiamua hawatarudi nyuma.
 
Back
Top Bottom