Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Ushuhuda wa kweli: Dodoma waichukia CCM

Chadema dodo iliwambia ni wajinga,wamelala na wanachelewesha ukombozi kauri hizi bado zinakumbukwa wala msipate shida kuja dodoma ni kujiptezea mda wenu.
Haya majina yanayoishia na "YETU" ni ya watu wa TISS!!
 
Hiyo kazi ulipewa au ulijipa na hukuwa na kazi nyingine ya kufanya?.

uwezo wako wa kuchambua mambo ni wa kutiliwa mashaka nadhani ulikuwa unaota mkuu.

Nadhani umeenda dodoma ukaishia kushangaa maendeleo yaliyoletwa na ccm.

leo ni jumapili nenda kanisani upunguze hizo dhambi,na kaa ukijua dodoma ni ccm chadema wanaidharau kama kandambili tangu mbowe awatukane ndo basi tena.

mkuu Simiyu yetu , alichoandika huyu jamaa ndo hali halisi hapa Dodoma, kama unakumbuka niliwahi kuandika habari ya kuhusu daraja la mto Nyasungu na habari ya LIEKUWA MGOMBEA WA CHADEMA kuwashushua CCM. hali ni mbaya kuliko kwa CCM hasa vijijini, kwani sisi tunaamini kuwa Serikali ya ccm imeamua kwa makusudi kuwafanya wakazi wa Dodoma ombaomba kwa kuficha mafedha nje ya nchi huku sisi raia tunaendelea kufa njaa na kwa kukosa matibabu yanayofaa.
 
Unajua matonya kazaliwa lini au unajitekenya na kucheka mwenyewe,kwa tarifa yako matonya mkubwa hata yusuph makamba mdogo leo wewe umekula urojo unaropoka tu hata huna unachojua kazi kazi kutumika tu.
Iifikie wakati wana Dom tubadilike hivi ww unaweza unafaidika nn kua CCM huku ndugu zetu wakinyimwa huduma za ja jamii kwa muda mrefu? Ulifala sana agwe
 
ccm imechokwa nchi nzima,watu wanasubiri 2015 waizike kabisa
 
Iifikie wakati wana Dom tubadilike hivi ww unaweza unafaidika nn kua CCM huku ndugu zetu wakinyimwa huduma za ja jamii kwa muda mrefu? Ulifala sana agwe
Huduma gani dodoma unayoongelea usiongee hewa,taja huduma ambazo unazoona hazipo,wewe dodoma unakwama wapi.
 
mkuu Simiyu yetu , alichoandika huyu jamaa ndo hali halisi hapa Dodoma, kama unakumbuka niliwahi kuandika habari ya kuhusu daraja la mto Nyasungu na habari ya LIEKUWA MGOMBEA WA CHADEMA kuwashushua CCM. hali ni mbaya kuliko kwa CCM hasa vijijini, kwani sisi tunaamini kuwa Serikali ya ccm imeamua kwa makusudi kuwafanya wakazi wa Dodoma ombaomba kwa kuficha mafedha nje ya nchi huku sisi raia tunaendelea kufa njaa na kwa kukosa matibabu yanayofaa.
Unatumia majina ya wanasiasa fedha ngapi zimefichwa nje twende kwa data,

ziko mataifa yepi na kwenye acount zipi si busara kusikia neno na kubeba kama lilivyo bila hata kuchunguza.

Wanasiasa waongo wanapotosha watu kutafuta sifa za uongo wambie watwambie nani kaficha,sh ngapi na acount zao.
 
Mkuu kwa picha niliyoiona kwa macho yangu, CCM wanapumulia mashine hapa dodoma

Waambie wakaze hadi kieleweke!!hapa mwisho mwisho CCM wapo kama farasi anayekufa(Dying horse) huwa mateke yake ya mwisho ni mabaya sana (last kick)
 
Huna unachojua wewe umeona picha wanazopiga watu pale nyelele groung ndiyo unasema ccm kuchokwa.

pengine umeona picha za mzee yusufu zilizobandikwa ukutani ndiyo unasema ccm kuchokwa acha viroba wewe.

nyelele ni nini we kil@.za?
 
Nikweli kamanda mimi pia nimekuwa nafanya harakati huko kwa muda, ila Chadema Inapaswa kufanya Operation maalum kama iliyofanywa Morogoro, bado kuna shida elimu ya uraia na hofu ya utawala hasa majimbo ya vijijini!
 
naona simiyu yetu unajitahidi sana kupost hata unamshinda HAMY D, tatizo ni uwezo wako wa kureason! Huo ubunge wa viti maalum unaotaka unaweza kuupata tu! Wanawake mkiwezeshwa mnaweza! Jitahidi kufikiri vizuri na uendelee kupost ubunge wa viti maalamu +buku 7/day utapata!
 
Sio Dodoma tu ukweli uliopo ni ccm inakufa Tanzania nzima. Jana tu sms nzimeanza kutumwa na TTCL kuwa gharama za huduma zimepanda bado mitandao ya simu. Hivi kweli mkulima ambae kuweka 500 kwenye simu ni gharama leo hii unampandishia huduma ya mawasiliano unategemea nini, na kiujumla kutokana na mfumo wa ajira kutokuwa rasmi simu ndo zinatumika kama njia pekee ya mawasiliano kwa wajasiriamali.
 
Uchaguzi wa juzi wa madiwani chadema kiliongoza? Kama kweli ccm imechokwa.

Kwa mauwaji ya watu wasio na hatia mnayoyaendesha. Ukijumlisha na mpigiko wa maisha tulionao...hakika CCM inastahili kuchokwa
 
Ccm ni wapuuzi, wakipewa ukweli wao ni kukanusha tu,mtakufa bila kujijua jifarijini tu.
 
Nikiwa katika mji wa Dodoma kwa takriban wiki tatu sasa nimebahatika kuzungumza na makundi tofauti ya watu katika maeneo ya Kikuyu, Mkonze, Ipagala, Swaswa, Chang'ombe, Majengo na Mailimbili.

Pamoja na ukweli Mitaa ya Dodoma mjini inapendeza sasa kwa kutandazwa lami bado raia wengi wanaonyesha kuichoka CCM.

Sababu nilizozigundua ni hizi kuu 4 ingawa zipo sababu nyingi zinazoashiria anguko la CCM kwa viunga vya Dodoma
1. CCM imechokwa. Kwa kuwepo kwake madarakani kwa muda mrefu kumewafanya wengi watamani mabadiliko. Vijana wengi wenye miaka 35 kushuka chini wamezaliwa wameikuta CCM. Wameenda shule kwa level zote wapo na CCM. Wameanza kazi wapo na CCM na sasa wana familia wapo na CCM. Wana Dodoma wanasema kuna ndugu zao wamezaliwa hadi wametangulia mbele za haki bado wapo na CCM. Ndipo nilipokumbuka usemi usemao KITU CHOCHOTE KITAKACHOISHI MIAKA MINGI KINACHOFUATA NI KIFO. Kwenye Product life cycle theory, baada ya stage ya Maturity kinachofuatia ni Decline(Death). CCM imeshaishi miaka mingi. Tumezaliwa tunamsikia Wassira, Kikwete, Mangula, Kinana na wengineo. CCM imeshapita Maturity stage na sasa inaanguka. Wakazi wa Dodoma wamethibitisha.
Ili kujihalalishia uhalali wa utawala CCM imeamua kumwaga damu.

2. Wakazi wengi wa Dodoma nilioongea nao Wanaiona CCM ya sasa kama genge la wahuni. Wapo watu zaidi ya Wanne waliosema CCM ni majambazi. Sababu kuu ni kuwa wapo tayari kuua mradi tu mambo yao waende. Wanashindwa kuona natural death inayowakabili. Mkazi wa Msalato alisema CCM imeacha majukumu tuliyowapa wao kazi yao ni Chadema tu. Bungeni Chadema, Mahakamani Chadema, Mawaziri kutwa kucha Chadema. Huduma za jamii ambazo kimsingi CCM ndio wenye ridhaa ya kutekeleza zimewashinda. Wako busy kuua raia wasio na hatia na kufungua kesi zisizomsaidia mtanzania na kusahau majukumu yao. Kifupi ni kuwa Dodoma wanawaona CCM kuwa ni Chama cha Wauaji. Nilipotaka kupata maoni yao kuhusu mauaji ya bomu la Arusha walinijibu wengine kwa hasira' NANI HAJUI KUWA NI CCM WALIOUA? Kijana mmoja wa Chuo cha Mipango akamtaja kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM anayetokea kanda hii ya kati kuwa ndiye anayepanga na kufadhili mauaji. Alikwenda mbali zaidi na kutabiri kuwa kiongozi huyo atakufa kifo kibaya sana.

3. Hali ngumu ya maisha ni jambo lililosemwa na wengi kuwa limesababishwa na CCM. Wanahoji kama tuna madini, gesi, mbuga za wanyama, bahari, Ardhi ya kutosha yenye rutuba iweje leo mtu aumwe akose huduma kwenye hospitali za umma? Iweje leo ukitoka tu kidogo mji wa dodoma hupati maji safi na salama? Iweje leo washuhudie anguko kuu la Elimu namna hii? Iweje leo Dodoma iwe na watu wanaokufa njaa?
Wapo walioamua kulima na kukamua alizeti. Hakuna masoko. Badala yake serikali imekazana na mfanyabiashara wa kiasia anayefanya biashara ya kuingiza mafuta ya alizeti akitokea nje ya nchi.

4. Vijana kukosa ajira. Wakazi wa Dodoma wameonyesha masikitiko yao hasa kwa namna vijana wanavyohangaika. Ni ukweli uliowazi kuwa vijana ndio wanao hold labour force kubwa Tanzania. Lakini VETA haijawasaidia, Elimu ya Chuo kikuu haijawasaidia, wapo wenye masters wanahangaika tu. Ukiwauliza viongozi wa kisiasa(wa CCM) wanawapa majibu mepesi eti waondoe dhana ya kuajiriwa wawaze kujiajiri. Hata mimi nilipowapa hiyo changamoto waliona kama ninawadhihaki. 'Brother mimi najiajiri naanzia wapi? Nitapata wapi uwezo wa kununua vifaa vya Capentry masikini mimi? Nani atanikopesha? Benki gani itaniamini bro? Alisema kijana mmoja wa Kikuyu aliyemaliza mafunzo ya Veta mwaka jana kwa level ya trade test two.
Madereva wa bodaboda wameponda sana sifa wasizostahili kupata CCM na serikali yake hasa kwa kuondoa ushuru wa bodaboda. Ingawa wameshukuru mkopo wa pikipiki wanaopewa na mbunge wao kwa masharti makali na magumu wamesema kabisa bila kupepesa kuwa ushuru ulioondolewa unawanufaisha wamiliki wa bodaboda na sio madereva wa bodaboda. Wao wangenufaika endapo tozo kwenye mafuta hasa petroli zingepungua na kushusha bei ya petroli hivyo kuwaongezea kipato kuliko bei ya sasa ambayo kwa madai yao kila wakipatacho kinaishia kwa mmiliki wa bodaboda.

Ni hayo tu kutoka Dodoma.

Naunga mkono hoja 100%.
 
Back
Top Bottom