Ushuhuda wa dada yangu: Ukioa mdada wa chuoni ambae kwao anaweza kurudi kirahisi tegemea kusingiziwa unamfanyia ubaya akiona majukumu ya ndoa magumu

Sina maana ya kuwa mmbea ama kumkandia dada yangu ila hii ndio hali halisi ya matatizo haya ya sasa yanayofanya ndoa nyingi kubomoka, mimi nimeleta case study.

Mifano ipo mingi sana juu ya wanawake wasomi wa vyuoni kuwa wasumbufu kwenye ndoa ila wacha niweke kisa cha mtu naemjua kabisa wala si wa kihadithiwa.

Ni dada yangu huyu kabisa, aliitafuta sana ndoa na akaipata kimbebe kikawa kwenye maisha halisi ya ndoa.

Dada alikuwa kakariri sana maisha ya miss independent, haki sawa, ndoa za kitamthilia, n.k kwa bahati mbaya ama nzuri mme wake alikuwa hawezi vumilia haya mambo, kapata kazi hapa mjini na ni msomi ila kakulia sana maisha ya kijijini.

Dada alianza kuleta kiburi kumfulia mme wake nguo akashauri watafte house girl, mme wake akamwambia hata wakimleta house girl bado nguo zake haziwezi fuliwa na house girl, hilo ni jukumu la mwanamke wa ndoa.

Dada alianza kiburi kuamka asubuhi kumpashia mme wake maji, anamwambia mme wake apashe, walikuwa wanakorofishana sana.

Uvivu wa kupika, kuna muda anamwambia mme wake ale huko huko, yeye kachoka kupika.

Dada alikuwa bado hana kazi anashinda nyumbani, anaachiwa hela kila siku nje ya matumizi.

Vitimbwi vilikuwa ni vingi sana ila kwa ustaarabu wa kipekee wa yule bwana dada hakuwahi kupigwa hata kibao.

Baada ya miezi minne ya ndoa nikaanza kuona dada anapost status za kimafumbo za taasisi za kukemea uonevu kwenye ndoa, haki sawa kwenye ndoa, n.k.nikimpigia anadai anateswa na vitu vingine kibao, hio ilikuwa ni mbinu ya kupata tundu la kuchomoka / exit strategy, vitu vingi alikuwa anadanganya.

Alirudi nyumbani na mpaka sasa yupo nyumbani, mzazi hawakuwa na tatizo lolote kwa yeye kuridi na hata anavyoondoka chumba chake kilifungwa asilale mti mwengine.

vikao kama viwili hivi haonyeshi nia ya kurudi, nyumbani karudi na mtoto kuna house girl, anapikiwa, n.k.

Bwana yule anatoa laki 3 ya kumtunza mtoto kila mwezi lakini dada hakuwahi kusema hili, tulikuja gundua baadae, hapa nikaona kabisa sista alikuwa anataka atuvute upande wake tumuone mme wake hafai.

Pia napata stori pale nyumbani kwamba yule bwana akienda kumuona mtoto kuna mchezo mchafu unachezwa, dada anamwambia house girl ampeleke mtoto mtaa wa pili washinde huko hadi baba yake akiondoka, ni dada yangu lakini kwa kuwa nami pia ni baba, nikiona mwanaume mwenzangu anafanyiwa haya inaniuma.

Majukumu ya ndoa kwa mabinti wengi wa vyuoni ni tatizo, wanataka kuendelea na lifestyle za vyuoni ambazo haziwezi kuendana na maisha ya ndoa, wanataka haki sawa bila kutekeleza majukumu yao, wamekuwa brain washed na tamthilia, n.k.
Mume ni mstaarabu mpaka hapo....karudi kwao bado anatoa laki 3 kuhudumia mtoto.Lakini Dunia ndivyo ilivyo ...huenda huyo jamaa ameumiza mtu kumpata mtu aliyekosa utu
 
Wewe naye ni lijinga sana sasa mambo ya dada yako yanakuhusu nini ?

Tafuta demu uende uoe ili ujue ukweli wa mambo sio kuishi kwenye nadharia mshenzi .

Mkuu nisamehe tu ila ni vile sipendi watu wambea kama wewe .

Vipi lakini Yanga atashinda kweli ?
Umemshambulia bure.....aisee🤔
 
Mambo mengine yashapitwa na wakati....kwanini huyo shemeji yako asinunue washing machine na geyser.

Kama anafanya kazi kumfulisha mwanamke....kuchemshiwa maji kila asubuhi kutesana. Hawezi kujichemshia maji?
Washing machine haitakatishi nguo
 
Nyie mnaomponda mleta uzi ni feminised males kiufupi ni wanawake wenye penis. Hongera bro kwa kuwa mwanaume na kuona uovu licha ya kua ni ndugu yako
Wewe naye ni lijinga sana sasa mambo ya dada yako yanakuhusu nini ?

Tafuta demu uende uoe ili ujue ukweli wa mambo sio kuishi kwenye nadharia mshenzi .

Mkuu nisamehe tu ila ni vile sipendi watu wambea kama wewe .

Vipi lakini Yanga atashinda kweli ?
 
Imagine maisha ya leo wanawake wamefika point wanakataa kufua na kupika! yaani utafute hela afu upike na ujifulie, worker droid sio? Vijana wapo sahihi kukataa ndoa, mwanamke kazi za nyumbani zinampa feminine values, vinginevyo ni chombo cha starehe hupatikana hata bila kuoa.
 
Back
Top Bottom