USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

USHUHUDA: Nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI

Habari wakuu,natumaini mko poa na Christmas na hata kama uchumi hauko sawa yapaswa kushukuru MUNGU maana kikubwa ni uzima na afya tu
Dhumuni la uzi huu ni kuwapa moyo wale wote wanaoishi na Virusi vya ukimwi wajione kama watu wa kawaida na kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha
Mimi ni kijana jinsia ya kiume,nilizaliwa na Virusi vya ukimwi miaka 24 iliyopita na mpaka leo niko mzima wa afya na ukiniangalia kwa macho hutofikiria kama naishi na Virusi,
Waathirika wote msikate tamaa na wala msihudhunike kila kitu kinatokea kwa sababu fulani
Natanguliza shukrani kwenu na muwe na Christmas njema,
Mwenye maswali au maoni nitamjibu hapa hapa
Kisukari
Blood pressure
Cancer
Pumu

Ndio magonjwa hatari kuliko upungufu wa kinga mwilini.

Mimi naamini ukimwi hausababishi vifo zaidi ya malaria,typhoid na amoebiasis

Wenye ngoma msiwe wapweke
 
Umefanya jambo la maaana la kufariji wengine. Mungu akubariki sana na akupe haja ya moyo wako
 
Mara ya kwanza kupima 2007, nikapima 2009, halafu nikapima 2015.

Nyakati zote nilikua uncomfortable kusubiri majibu. Ile moment haizoeleki.

Mleta uzi nakupa hongera kwa attitude yako, samahani sikupi pole unastahili pongezi
Ulienda kupima uliahidiwa dawa nini? Siji pima labda niwe mahututi,jamani watu wengine mna roho ngumu
 
Kisukari
Blood pressure
Cancer
Pumu

Ndio magonjwa hatari kuliko upungufu wa kinga mwilini.

Mimi naamini ukimwi hausababishi vifo zaidi ya malaria,typhoid na amoebiasis

Wenye ngoma msiwe wapweke
Pumu?
Ni ugonjwa wa kawaida sana na unatibika.
 
Kwanza hongera,na mungu akubariki Sana,je uliijua hali yako ukiwa na miaka mingapi ?
Hili ni swali langu mkuu ila umequote kwa mwingine? Kama ni swali langu jibu ni kwamba nilijua kama nimeathirika mwaka 2009 baada ya kumaliza darasa la saba mwaka 2008
 
Pambana na haliyako usikate tamaa bado kitambo kidogo ufalme wa mungu utachukua mamlaka ya mfumo huu wa mambo,hakuna mkazi hata mmoja atakaye Sema mgojwa China ya serikari hiyo ya mungu
 
Kijana,kuishi ni kismati kutoka Kwa Mwenyezi .Unapaswa usikalili kuwa unaishi na virusi na maisha yanakwenda miaka inaondoka na kufa haufi hii haitakufanya uishi bila kufa,bali unapaswa kuutambua uzima huo kuwa unapewa na Mungu kusudi lake umtukuze na umwabudu.Fanya jambo muhimu nenda kwa kiongozi wako wa Kiroho umweleze hali yako na ushike maagizo ya madaktari
 
Mkuu Arv natumia,dini pia nimeshika na kuifata,kufa najua nitakufa ila lengo la posti hii ni kuwafariji wote wenye Virusi vya ukimwi
 
Back
Top Bottom