Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,737
mstari wa mwisho tu hapo unakutosha. maana ya Mungu kuweka sheria mioyoni mwetu, au kuweka amri mioyoni mwetu unaelewa maana yake? ni pale Roho Mtakatifu anapoingia ndani mwetu na kutuongoza kututia kwenye kweli yote. sio kukariri vifungu vya biblia kimwili, kwa kufanya hivyo kimwili haikusaidii chochote zaidi ya kuwa mwanahistoria wa biblia. hiyo Biblia uliyonayo haitoshi kuandika mambo yote ambayo Mungu aliagiza, yapo mengine Yesu mwenyewe alisema wanafunzi wake wasubiri Yerusalem hadi atakapokuja huyo Roho, na huyo Roho atawatia kwenye kweli yote. Roho Mtakatifu anatuelekeza kutotenda dhambi hata zile ambazo hazijaandikwa kwenye hizo sheria zetu au Biblia kwa ujumla. huwezi kumwona Mungu ukienda kimwili kama ninyi wasababo, mnatakiwa kwanza muokoke kwa kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.Mtume paulo anaandika hivi: "maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; [War5:13].
Andiko hili limechanganya sana wanaojiita wakristo wengi kudhani kuwa uwepo wa dhambi hauhitaji sheria na kwamba hata sasa sheria haihitajiki kufafanua dhambi ni nini? lakini hili ni kweli?
Ni kweli kwamba Mungu kama mtawala wa dunia yote hana sheria za kuongoza utawala wake???
Paulo anaposema kwamba kabla ya Sheria dhambi ilikuwepo ulimwenguni, hapa alikuwa akimaanisja kuwa kabla Sheria za Mungu kuandikwa katika vibao vya mawe na katika magombo ya Musa pale mlimani sinai, dhambi ilikuwepo.
Kwa wanadamu sheria huanza kutambulika na kuwa na mamlaka baada ya kuandikwa. Na hili ni kweli. dhambi ilikuwepo hata kabla ya tukio la mlima sinai la Mungu kuandika Amri zake katika mbao mbili za Mawe.
Lakini paulo yupo wazi kuwa dhambi haiwezi kuhesabiwa pasipo sheria. Maana yake ni kwamba kila penye dhambi, maana yake kuna sheria fulani ya Mungu imevunjwa. Haiwezekani dhambi kuwepo bila sheria kuvunjwa. Kwa hiyo ni wazi kwamba Sheria za Mungu zilikuwepo hata kabla ya tukio la Mlima sinai. Paulo anaposema kuwa dhambi ilikuwepo kabla ya sheria, hana maana kuwa dhambi inaweza kuwepo bila sheria, ila anamaanisha kwamba dhambi ilikuwepo kabla ya Mungu kuziandika rasmi amri zake katika mbao za mawe pale mlimani sinai.
Hivyo ni dhahiri kuwa Amri za Mungu zilikuwepo hata kabla ya tukio la Mlima sinai.
Hapo Mwanzo Mungu alipomuumba Mwanadamu aliiandika sheria yake katika dhamiri zao na mioyo yao[War2:15]. Hata baada ya Uasi, Sheria za Mungu zilibakia ktk Mioyo ya wanadamu. Hata wanadamu waasi wanajua kabisa kanuni za haki na kanuni ziziso za haki. Haihitaji kufundishwa na mtu kuwa ukichukua mke wa mwenzako, ama ukimwibia mwenzako, ama ukimtukana mwenzako ni jambo baya. Sheria ya Mungu ya Upendo imo mioyoni mwa wanadamu wote.
Ni hali ya uasi ambayo Mwanadamu amerithi baada ya uasi ndo inamsukuma mwanadamu kuichukia sheria ya Mungu na kuivunja. Lakini Katika moyo wa kila Mmoja Mungu amejiachia ushuhuda wa sheria zake.
Amri ya Sabato ilianzishwa na Mungu Mwenyewe tangu Uumbaji, na hivyo kuwa Amri iliyozeeka na ya zamani sana kama Umri wa dunia. Sabato iliwekwa na Mungu kuwakumbushia wanadamu kuwa waliumbwa na Mungu na hivyo wanawajibika kwake katika kumwabudu na kumtii. Msingi wa Ibada uliwekwa mapema sana pale Mungu alipoianzisha sabato. Taz Mwa2:1-3.
Amri zote Kumi, ambazo ni mafafanuzi ya Sheria ya Mungu ya Upendo zilikuwepo tangu Uumbaji. Baadhi ya wakristo wanawaza kwamba kwa sababu Amri kumi ziliandikwa katika Mbao mbili za Mawe pale mlimani sinai, basi Amri hizo ni torati ambayo haiwahusu wakristo kabisa. wanawaza na kufikiri kuwa kwa sababu Agano la kale liliundwa kwa misingi ya utii wa Amri kumi, pamoja na Sheria zile zingine na maagizo yake na hukumu zake, basi kuondolewa kwa agano la kale kunafagilia mbali Amri kumi na Sabato. Huu ni udanganyifu Mkuu.
Na udanganyifu huu kwa sababu unalenga sabato tu, unakuja udanganyifu mwingine kuwa injili imezitaja sheria zingine zote tisa katika zile kumi kasoro sabato tu,na hivyo tuna uhalali wa kuzishika sheria zingine zote tisa kasoro sabato!!! Huu ni udanganyifu wa makusudi unaolenga chuki dhidi ya amri moja tu ya Mungu katika zile kumi.
Bwana wetu Yesu Kristo akiongelea juu ya Umilele wa Amri za Mungu, na kuwaonya watu dhidi ya kuzitangua, aliweka bayana hivi: "Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati. [Luka16:16].
Kama vile mbinguna nchi vitakavyoendelea kudumu, daima vitaendelea kushuhudia kuwa Sheria za Mungu ni za Milele. Amri za Mungu ambazo zilikuwepo kabla ya Agano la kale la mlima sinai; husimama kwa zenyewe hata bila Agano la kale.
Agano jipya halikuondoa Amri za Mungu bali linazirudisha Amri za Mungu katika sehemu yake ya hawali yaani mioyoni mwa wanadamu, na kuwawezesha wanadamu kuzitii Amri zake.
sijawahi kuona msabato hata mmoja amejara Roho Mtakatifu, na ninajua mafundisho yetu yanaelekeza kwamba sio wote wanatakiwa kujazwa. hii ndio sababu mnaishi kwa kukariri vifungu na kutumia nguvu kushinda dhambi, kwa nguvu za mwili huwezi kushinda dhambi ila kwa nguvu za Roho, na huwezi kupata Roho Mtakatifu hadi uokoke, na awaye yote asiyekuwa na huyo Roho wa Kristo huyo sio wake. ninyi wasababu sio wakristo kwasababu hamna Roho Mtakatifu na mnamkataa (hamtaki kujazwa). Roho Mtakatifu ni muhimu kwa ajili ya kututia kwenye kweli yote zaidi ya hizo amri kumi, na pia anatusaidia kuomba kwasababu sisi ni dhaifu tukienda kuomba kwa nguvu ya mwili tunaomba kwa tamaa zetu na hatujui kuomba ipasavyo, lakini yeye aomba ndani yetu akilia ABBA kwa kuugua kusikoweza kutamkwa....sasa ninyi kama hamna Roho, nani huwa anawasaidia kuomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa? no wonder hamna uwezo hata wa kukemea pepo na vibwengo. you are not different from the catholics and other unbelievers.