Ushuhuda: Kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri

Hatuwezi kufanana mkuu, wapo watakaoshindwa na wapo watakaofanikiwa.
Pia wapo walioshindwa na wapo waliofanikiwa. Ila cha muhimu ni kwamba business sio lelemama na ni kitu kinachohitaji Strong strategy, commitment, nguvu, muda na akili ya kutosha.

Hiyo kazi usingeiacha bali ungekuwa unafanya business na kazi pia means hata business ikifail basi una sehemu ya kushikia.
Then unatulia kidogo alafu unasimama tena mpaka kieleweke. Hii ndio maana ya Strategy. naweza sema ulikurupuka na hukujipanga kwa consequences za maamuzi yako, lakini cha muhimu ni kwamba umejiunza.

Alafu kama ulikuwa unapenda business kwanini usingesoma courses ambazo zinaegemea business moja kwa moja kama Economics na MBA?

Maamuzi ni yako na chochote kinaweza kutokea.
Wanasema if you're tired of starting over then stop giving up.
Nimekuelewa Mkuu kwa mazingira Yale nilikua babati vijijini na fursa iliyopo kule ni kilimo pia sikua na mtaji.
Ukiongeza pia kutoka chuo sikua na jicho Kali la kuchungulia fursa.
Changamoto ya vijana wengi haswa waliomaliza chuo ni kukosa mentor sahii wa "kumdirect" kumuonyesha njia ya kupitia so tunapambana kwa njia yetu wengine wanafanikiwa humo wengine pia wanashindwa humo lakini pia nilichoelewa ukiachana na mtaji business is not for weak.
 
Huu ni mkakati wa kibiashara..hili ni tangazo..unamuonea huruma unanua bidhaa zake.
Safi sana Mkuu
 
Optimists

Persistence is not always the answer, sometimes you need to change direction. Kama unaona mambo hayaendi rudi kwenye kuajiriwa.

Ujasiriamali unawaponza sana watu, mtu anaona bora awe fukara kuliko kuwa muajiriwa.

Hukupaswa kuacha kazi haraka hivyo. 2 sources of income is better than one.

800k is nothing kwenye biashara yeyote labda uwe mchuuzi tu kama ulivyosema. Lazima ujipange unapotaka kuanza on your own kimtaji na uwe na line of credit pale utapohitaji kuinject more capital into your business. Line of credit inaweza kuwa bank loans, your friends and family (Your network. Your networth).

Mwisho ukitaka kuwa maskini nchi hii ingia kwenye kilimo na mtaji wa mbuzi.
Ni kweli Mkuu umeongea fact tupu natarajia kulima alizet, ufuta au karanga mazao ambayo hayategemei mvua kwa wingi lakini pia sio Leo wala kesho mpaka nijipange kwanza
 
Huu ni mkakati wa kibiashara..hili ni tangazo..unamuonea huruma unanua bidhaa zake.
Safi sana Mkuu
Mkuu mbona hapa sihitaji huruma labda wewe ndio unaona huruma. Najaribu kutoa funzo na experience fupi kwa mtu anaetaka kuacha kazi ili ajiajiri.
 
Wewe ni tajiri tayari, namna unavyojibiidisha ndivyo pesa inaingia:-
  • Nenda huko fb n.k fungua ukurasa wako, usomeke:- Msambazazji wa vyombo vizuri kwa bei nafuu, huku ukilipa kidogo kidogo
  • Weka mawasiliano yako vizuri
  • Unga marafiki wa kutosha
  • Beba mzigo peleka mkoani, ukakopeshe walimu n.k
  • Mwisho wa mwezi zungukia makusanyo ya pesa
 
Upo k.koo mkuu? njoo PM kuna ishu nataka nikupe uifanye sio ya kununua wala nini

hutumii chochote zaidi ya akili na kuuliza,nahitaji taarifa flani Ukiwezesha kunipa details

za ninachokitaka na nikikipata ntakupa 50,000 (kama shukurani tu) sina muda nipo busy ila kuna mtu kanitonya kaniambia jambo

sasa nataka mtu nisiemjua asienijua aifanye hiyo kitu kisha aniletee mrejesho,Nahitaji MUDA wako..Sihitaji mtu yeyote eneo hilo ajue ni mimi naulizia hicho kitu,ndio mana nimeona kama unanifaa.

PM ipo wazi njoo tuyajenge...
 
Ndugu yenu wa damu naomba kupingwa na kuelekezwa kwa upole na kwa fact.
View attachment 2176426

After graduation mdogo wenu hapa nikapata sehemu ya kujishikiza Mimi ni mwalimu Physics na chemistry nikawa nalipwa 250k -300k huku nikipewa nyumba ya shule na huduma kama chakula cha mchana na asubuhi.
Maisha Yale sikuyapenda kabisa mshahara mdogo japo kazi sio kubwa saana ndoto zangu zilikua kua mfanyabiashara (ndio kitu ninachokipenda) na niliamini kufikia ndoto zangu ni kupitia kujiajiri.

Nimejitolea mwaka mzima kwa huo mshahara na kwa msoto Mkubwa nilikua nimesave Pesa kidogo na saving zingine zingine nikawa kama na laki 8 nikaona mbona naweza kujiajiri? Mbona watu wanaanza chini zaidi na wanapanda? Nikapata wazo la kujiajiri ili nikuze mtaji.

Kufupisha story, kuja kwenye ulimwengu wa biashara mambo ni tofauti kabisa. Tena uwe na mtaji wa kuunga kama Mimi ndio hakuna rangi hutoacha kuona 😃😃😃.

Nilikua na idea ya kufanya biashara kubwa kubwa biashara za matajiri mfano kusafirisha Mchele kuleta Vitunguu kutoka singida kuleta viazi na maharage natoa shamba naleta humu mjini vyote nilifanya nikajikuta naangukia pua yani nakula vitasa vya kutosha,(unafanya biashara unajikuta mtaji unaisha tu).

NIKASHTUKA nikagundua kwa Huu mtaji Mimi ni Machinga tu tena hoehae (aliechoka) ambae hawezi kulipia meza ya umachinga maana pale Kongo kupata meza ni laki mbili kwa mwezi na wanataka miezi 6. Pia sehemu kama manzese, tandika kote huko meza ya umachinga ni 100,000 -150,0000 na wanataka miezi 6.
View attachment 2176425

So baada ya kugundua sehemu yangu ilipo na hakuna mbinu mpya "nikadecide" niwe machinga tu labda nitapata namna ya kuongeza mtaji, huku ni zaidi ya mahangaiko tu maana jua na mvua vyote vyako. Leo naweka mzigo hapa kesho kule kukimbizana na migambo kila siku mda mwingine wanachukua mzigo wako.
Nikakumbuka kitu kimoja kuajiriwa ni bora zaidi ya kujiajiri, Kujiajiri ni bora sana endapo unao MTAJI wa kujitosheleza na una mazingira sahii ya kufanya biashara. wanaomaliza chuo kikuu wanapitia msoto Mkubwa sana maana hakuna mazingira wezeshi kufanya biashara, SERIKALI wajitahidi kutoa ajira pale inapobidi na kutengeneza mazingira rafiki kwa machinga wenye mitaji midogo maana vita ilioko huku kwenye kujikwamua kiuchumi si ndogo.

Mambo ni mengi sana kwenye mapambano ya umasikini KAMWE usione bora ujiajiri ukaacha kazi inayokupa mkate wa kila siku ukakimbilia huku utajikuta unatamani kurudi kule.
Huku utaachana na mambo unayoyapenda mfano kuangalia Mpira, kusali n.k

Sasahivi nimekua Dalali huku kariakoo nikivuta upepo nione mwelekeo unakuaje, nione dunia inataka nini. Pia chaka lolote naingia nafikiria sana kuhusu kilimo though sina mazingira wezeshi popote pale penye fursa mkoa wowote ule naingia.

Ukiwa mkoani unaweza niagiza chochote kile nikakutumia kwa gharama zangu utanilipa baada ya kuuona mzigo.
View attachment 2176492

Nawatakia mapambano mema na mfungo mwema.
View attachment 2176493
Haha waaambie hao si mchezo ndugu
 
Tatizo ni elimu duni uliyopata ndo maana unaona bora kuajiriwa!

Yaani mtu umesoma level hizo bado unafanya uchuuzi halafu unalaumu!

Elimu uliyopata haikuwezeshi kujitofautisha na gumbaru ( mtu ambaye hakusoma kabisa).
Elimu ikuwezeshe kujenga biashara yenye mifumo ( siyo uchuuzi)! najua kwa upeo wako mdogo utaaanza kuniuliza nitapata wapi mtaji!
 
Back
Top Bottom