Ushuhuda: Kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri

Optimists

JF-Expert Member
Oct 17, 2021
278
686
Ndugu yenu wa damu naomba kupingwa na kuelekezwa kwa upole na kwa fact.
IMG_20220329_181509.jpg

After graduation mdogo wenu hapa nikapata sehemu ya kujishikiza Mimi ni mwalimu Physics na chemistry nikawa nalipwa 250k -300k huku nikipewa nyumba ya shule na huduma kama chakula cha mchana na asubuhi.
Maisha Yale sikuyapenda kabisa mshahara mdogo japo kazi sio kubwa saana ndoto zangu zilikua kua mfanyabiashara (ndio kitu ninachokipenda) na niliamini kufikia ndoto zangu ni kupitia kujiajiri.

Nimejitolea mwaka mzima kwa huo mshahara na kwa msoto Mkubwa nilikua nimesave Pesa kidogo na saving zingine zingine nikawa kama na laki 8 nikaona mbona naweza kujiajiri? Mbona watu wanaanza chini zaidi na wanapanda? Nikapata wazo la kujiajiri ili nikuze mtaji.

Kufupisha story, kuja kwenye ulimwengu wa biashara mambo ni tofauti kabisa. Tena uwe na mtaji wa kuunga kama Mimi ndio hakuna rangi hutoacha kuona 😃😃😃.

Nilikua na idea ya kufanya biashara kubwa kubwa biashara za matajiri mfano kusafirisha Mchele kuleta Vitunguu kutoka singida kuleta viazi na maharage natoa shamba naleta humu mjini vyote nilifanya nikajikuta naangukia pua yani nakula vitasa vya kutosha,(unafanya biashara unajikuta mtaji unaisha tu).

NIKASHTUKA nikagundua kwa Huu mtaji Mimi ni Machinga tu tena hoehae (aliechoka) ambae hawezi kulipia meza ya umachinga maana pale Kongo kupata meza ni laki mbili kwa mwezi na wanataka miezi 6. Pia sehemu kama manzese, tandika kote huko meza ya umachinga ni 100,000 -150,0000 na wanataka miezi 6.
FB_IMG_1641661569033.jpg

So baada ya kugundua sehemu yangu ilipo na hakuna mbinu mpya "nikadecide" niwe machinga tu labda nitapata namna ya kuongeza mtaji, huku ni zaidi ya mahangaiko tu maana jua na mvua vyote vyako. Leo naweka mzigo hapa kesho kule kukimbizana na migambo kila siku mda mwingine wanachukua mzigo wako.
Nikakumbuka kitu kimoja kuajiriwa ni bora zaidi ya kujiajiri, Kujiajiri ni bora sana endapo unao MTAJI wa kujitosheleza na una mazingira sahii ya kufanya biashara. wanaomaliza chuo kikuu wanapitia msoto Mkubwa sana maana hakuna mazingira wezeshi kufanya biashara, SERIKALI wajitahidi kutoa ajira pale inapobidi na kutengeneza mazingira rafiki kwa machinga wenye mitaji midogo maana vita ilioko huku kwenye kujikwamua kiuchumi si ndogo.

Mambo ni mengi sana kwenye mapambano ya umasikini KAMWE usione bora ujiajiri ukaacha kazi inayokupa mkate wa kila siku ukakimbilia huku utajikuta unatamani kurudi kule.
Huku utaachana na mambo unayoyapenda mfano kuangalia Mpira, kusali n.k

Sasahivi nimekua Dalali huku kariakoo nikivuta upepo nione mwelekeo unakuaje, nione dunia inataka nini. Pia chaka lolote naingia nafikiria sana kuhusu kilimo though sina mazingira wezeshi popote pale penye fursa mkoa wowote ule naingia.

Ukiwa mkoani unaweza niagiza chochote kile nikakutumia kwa gharama zangu utanilipa baada ya kuuona mzigo.
IMG_20220403_124227.jpg

Nawatakia mapambano mema na mfungo mwema.
IMG_20220310_115113.jpg
 
Ndugu yenu wa damu naomba kupingwa na kuelekezwa kwa upole na kwa fact.
View attachment 2176426

After graduation mdogo wenu hapa nikapata sehemu ya kujishikiza Mimi ni mwalimu Physics na chemistry nikawa nalipwa 250k -300k huku nikipewa nyumba ya shule na huduma kama chakula cha mchana na asubuhi.
Maisha Yale sikuyapenda kabisa mshahara mdogo japo kazi sio kubwa saana ndoto zangu zilikua kua mfanyabiashara (ndio kitu ninachokipenda) na niliamini kufikia ndoto zangu ni kupitia kujiajiri.

Nimejitolea mwaka mzima kwa huo mshahara na kwa msoto Mkubwa nilikua nimesave Pesa kidogo na saving zingine zingine nikawa kama na laki 8 nikaona mbona naweza kujiajiri? Mbona watu wanaanza chini zaidi na wanapanda? Nikapata wazo la kujiajiri ili nikuze mtaji.

Kufupisha story, kuja kwenye ulimwengu wa biashara mambo ni tofauti kabisa. Tena uwe na mtaji wa kuunga kama Mimi ndio hakuna rangi hutoacha kuona .

Nilikua na idea ya kufanya biashara kubwa kubwa biashara za matajiri mfano kusafirisha Mchele kuleta Vitunguu kutoka singida kuleta viazi na maharage natoa shamba naleta humu mjini vyote nilifanya nikajikuta naangukia pua yani nakula vitasa vya kutosha,(unafanya biashara unajikuta mtaji unaisha tu).

NIKASHTUKA nikagundua kwa Huu mtaji Mimi ni Machinga tu tena hoehae (aliechoka) ambae hawezi kulipia meza ya umachinga maana pale Kongo kupata meza ni laki mbili kwa mwezi na wanataka miezi 6. Pia sehemu kama manzese, tandika kote huko meza ya umachinga ni 100,000 -150,0000 na wanataka miezi 6.
View attachment 2176425

So baada ya kugundua sehemu yangu ilipo na hakuna mbinu mpya "nikadecide" niwe machinga tu labda nitapata namna ya kuongeza mtaji, huku ni zaidi ya mahangaiko tu maana jua na mvua vyote vyako. Leo naweka mzigo hapa kesho kule kukimbizana na migambo kila siku mda mwingine wanachukua mzigo wako.
Nikakumbuka kitu kimoja kuajiriwa ni bora zaidi ya kujiajiri, Kujiajiri ni bora sana endapo unao MTAJI wa kujitosheleza na una mazingira sahii ya kufanya biashara. wanaomaliza chuo kikuu wanapitia msoto Mkubwa sana maana hakuna mazingira wezeshi kufanya biashara, SERIKALI wajitahidi kutoa ajira pale inapobidi na kutengeneza mazingira rafiki kwa machinga wenye mitaji midogo maana vita ilioko huku kwenye kujikwamua kiuchumi si ndogo.

Mambo ni mengi sana kwenye mapambano ya umasikini KAMWE usione bora ujiajiri ukaacha kazi inayokupa mkate wa kila siku ukakimbilia huku utajikuta unatamani kurudi kule.
Huku utaachana na mambo unayoyapenda mfano kuangalia Mpira, kusali n.k

Sasahivi nimekua Dalali huku kariakoo nikivuta upepo nione mwelekeo unakuaje, nione dunia inataka nini. Pia chaka lolote naingia nafikiria sana kuhusu kilimo though sina mazingira wezeshi popote pale penye fursa mkoa wowote ule naingia.

Ukiwa mkoani unaweza niagiza chochote kile nikakutumia kwa gharama zangu utanilipa baada ya kuuona mzigo.
View attachment 2176492

Nawatakia mapambano mema na mfungo mwema.
View attachment 2176493
Mithali 3:5

Usiingie katika biashara na matarajio ingia ukiwa na matumaini
 
Ulifanya makosa kukimbilia kwenye ajira, huko ndipo Kulikokupa ujinga. Tambua kwamba ajira ni maisha ya muda mfupi
Sasa Mkuu mbona sasahivi nimejiajiri lakini napata msoto zaidi ya kipindi kile?
 
Back
Top Bottom