USHUHUDA: JamiiForums imenipa mtoto wa kiume

Che Mkira

Senior Member
Jul 8, 2014
117
250
Habari wakuu.

Niliwahi kuomba ushauri hapa kuwa nimehangaika sana kutafuta mtoto wa kiume bila mafanikio.

Rejea Uzi Wangu >> Nimetafuta mtoto wa kiume bila mafanikio. Nifanyeje?

Nashukuru sana kwamba nimefanikiwa baada ya kufuata ushauri wenu hasa ule wa kalenda ya kichina > Chagua jinsia ya mtoto umtakaye

Nina furaha sana kwani nilikuwa na watoto 6 wa kike na wingi huo ulitokana na jitihada za kutafuta mtoto wa kiume.

Asanteni sana.
 
Sumu

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
6,825
2,000
Obama ana mali za kila aina ana watoto wawili wa kike.

Mwenzangu na mimi wa Mabibo Mpakani na kibanda chako cha vyumba vitatu unazaa watoto sita ili utafute wa kiume.

Ukiulizwa utajibu unataka kuendeleza ukoo. Sasa wewe na Obama wa kuendeleza ukoo ni nani? Aliyetuloga alishafariki.

Hongera hata hivyo kwa kupata haja ya moyo wako.
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,594
2,000
Habari wakuu. Niliwahi kuomba ushauri hapa kuwa nimehangaika sana kutafuta mtoto wa kiume bila mafanikio. Nashukuru sana kwamba nimefanikiwa baada ya kufuata ushauri wenu hasa ule wa kalenda ya kichina. Nafuraha sana kwani nilikuwa na watoto 6 wa kike na wingi huo ulitokana na jitihada za kutafuta mtoto wa kiume. Asanteni sana.
Sasa fanya maombi na toba kwa Mungu, usije ukawa unajisifia umepata kidume kumbe umewaletea wanaume chakula haramu...

Mtoto wa kiume huwa tunajivunia pale tunapothibitisha yu rijali.

Sali sana
 
Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,909
2,000
Obama ana mali za kila aina ana watoto wawili wa kike.

Mwenzangu na mimi wa Mabibo Mpakani na kibanda chako cha vyumba vitatu unazaa watoto sita ili utafute wa kiume.

Ukiulizwa utajibu unataka kuendeleza ukoo. Sasa wewe na Obama wa kuendeleza ukoo ni nani? Aliyetuloga alishafariki.

Hongera hata hivyo kwa kupata haja ya moyo wako.
Hatuwezi kumuigiliza Obama na maisha anayoishi. Ndo mana akaitwa Obama. So usi force mambo mkuu... Maisha ya watu na maamuzi yao.. Kwani wewe ndo unamsaidia kulisha familia yake?

Watu wengine sijui vipi
 
LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,147
2,000
Sasa fanya maombi na toba kwa Mungu, usije ukawa unajisifia umepata kidume kumbe umewaletea wanaume chakula haramu...

Mtoto wa kiume huwa tunajivunia pale tunapothibitisha yu rijali.

Salim sana
Allah atulindie watoto wetu
 
LadyAJ

JF-Expert Member
Oct 21, 2015
7,147
2,000
Obama ana mali za kila aina ana watoto wawili wa kike.

Mwenzangu na mimi wa Mabibo Mpakani na kibanda chako cha vyumba vitatu unazaa watoto sita ili utafute wa kiume.

Ukiulizwa utajibu unataka kuendeleza ukoo. Sasa wewe na Obama wa kuendeleza ukoo ni nani? Aliyetuloga alishafariki.

Hongera hata hivyo kwa kupata haja ya moyo wako.
Akili na Mawazo ya kiobama hayajawahi kuwa acha wamama wa kiafrika salama, ukizaa wa kike tupu lazima litakuangukia tu wakati msababishi ni baba
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom