Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
USHUHUDA BINAFSI: AWAMU YA TANO NILIISHI KWA HOFU.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel.
Nikiri wazi kuwa, licha ya kuwa mimi sio mwoga lakini siwezi ongopa kuwa sina hofu au wasiwasi. Hakuna binadamu asiye na mashaka, hofu na wasiwasi, labda kutofautiana kiwango cha hayo.
Moja ya mambo ninayoyapenda kwa kiwango cha juu kabisa basi ni "Kuandika na kusoma" mambo mbalimbali. Tangu nikiwa mtoto mdogo nilipenda sana mambo hayo. Kuandika kwangu ni kama mchezo, kusoma kwangu ni kama starehe. Haiwezi kupita siku pasipo kuandika chochote na kusoma. Ingawaje, nilipokuwa nasoma, nilikuwa sipendi kuanzika Notes za darasani, sio ajabu kunikuta katika adhabu za wanafunzi wasio andika notes kila mara. Hata hivyo nilikuwa na daftari moja kubwa ambalo nilikuwa naandikia somo la Hisabati, Fizikia, Kemia na Biology. Hata hivyo sio lengo langu kueleza haya.
Kama nitaulizwa, nini utakumbuka kwenye awamu ya tano, basi jibu langu ni "HOFU"
Kwangu awamu ya tano ilikuwa awamu iliyoninyima amani. Nilikuwa mtu wa hofu sana. Pengine ukajiuliza hofu hiyo ilisababishwa na nini?
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa, mimi hobby yangu ni "KUANDIKA" na "KUSOMA" basi kama mnavyojua kitu upendacho kukifanya huwezi kukizuia hata ufanyeje kwani kukizuia ni kuyafanya maisha kuwa magumu. Nilikuwa naandika makala za hapa na pal, zipo za kijamii, kiuchumi, kisiasa, riwaya, mashairi, na maandiko ya kitoto, yakizee, maandiko ya kusadikika basi ilimradi akilli yangu itakavyonituma.
Katika maandiko yangu mara nyingi nalenga kuijenga jamii, kuifundisha na kuielimisha. Kuikosoa, kuikemea na kuiburudisha. Mara zingine naandika bila dhamiri, naandika kwa vile roho yangu inataka niandike tuu yale yote yaliyomo akilini mwangu. Hivyo ndivyo nilivyo, na hiyo ndio furaha yangu.
Sasa kasheshe linakujaga pale ninapoandika makala za kisiasa hasa zenye maudhui ya kukemea, kukosoa na kuonya. Hapa ndipo kulinifanya niishi kwa hofu na kwa tahadhari kubwa sana.
Hofu yangu haikutoka ndani bali ilitoka nje kutoka katika sehemu zifuatazo;
1. Watu wanaonizunguka
Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wakiniambia niache kuandika mambo ya kisiasa, hasa yenye lengo la kukosoa, na kuwaonya wakubwa. Nakumba Mama yangu alinipigia simu akanikanya sana, na kunikemea, tuligombana sana, nikijaribu kumwambia asinifundishe kuwaogopa waovu, akaniambia kwa sauti ya kukata tamaa, akasema " Shauri yako hutatimiza ndoto yako" Mimi nikamjibu ndoto yangu ni kuona jamii yangu inaishi kwa haki na uhuru. Basi Mama yangu akasema amenawa mikono na kamwe hataongea na mimi tena kwa habari hizo.
Sisemi sikumuelewa mama yangu, nilimuelewa sana, alikuwa hataki nikutwe na madhila kama yaliyokuwa yanatokea, alionyesha upendo kama Mama. Mama yangu Mkubwa naye mara zote tuliingia kwenye migogoro ya namna hiyo hiyo, nilijaribu kumueleza lakini hakuweza kunielewa kama mimi nilivyoshindwa kumuelewa. Mjomba wangu mmoja naye kwa kujali alinipigia simu siku moja usiku wa manane, nilishangaa simu yake kwani hatukuwa na ukaribu wa kupigiana simu. Hivyo kuiona simu yake usiku ule ilinipa wasiwasi. Yeye naye alinisihi niachane na mambo hayo kwani ni hatari kwangu, aliongea kwa kilugha nafikiri ili nimuelewe vizuri kabisa.
Bibi yangu aliyenilea naye hakuwa nyuma, aliniambia niachane na hayo kwani maisha yangu yatakuwa mafupi, nakumbuka nilimjibu na kumuambia hivi " Bibi ni ipi faida uliyoipata kuishi miaka mingi na ipi hasara ya mtu aliyezaliwa akaishi siku moja?" Bibi hapo alipata kigugumizi. Nilijadiliana sana na Bibi yangu, hakutaka kunielewa.
Mchumba wangu naye hakuwa nyuma mara kwa mara alikuwa akinisihi nisiandike mambo hayo, kwani hataki kuniona katika hatari. Nilimuelewesha akanielewa kishingo upande. Marafiki zangu pia wanaonijua na wasionijua kwa sura(ana kwa ana) nao walinitisha na kunitia hofu..
2. MATUKIO YALIYOKUWA YAKIENDELEA
Baadhi ya matukio kama vile mauaji, utekaji na kutiwa korokoroni kwa baadhi ya wakosoaji nako kulikuwa sehemu ya kunitia hofu katika awamu ya tano. Hata hivyo kila tukio lililokuwa likitokea lazima awepo mtu wa kuniambia; unaona mwenzako, bado wewe. Yaani hiyo ilikuwa ni lazima.
Jambo moja ni kuwa mimi nilichokuwa najaribu kukieleza ndani ya jamii yangu ni kuamsha ari na ujasiri wa kukemea waovu, nilikuwa nahamasisha vijana wasioogope waovu hata kama wangekuwa na nguvu kiasi gani. Jambo moja nililowaambia watu wanitishiapo lilikuwa; sifundishwi kumheshimu na kumuogopa Muovu.
Hata hivyo nilikuwa mtu wa tahadhari, na kama nitakuwa mbali na nyumbani basi nilichunga mienendo yangu na wanaonizunguka, sikuweza kukaa chumbani pasipo kufunga mlango, sikuweza kufungua mlango unaobishwa pasipokusikia sauti ya mtu anayebisha. Sisemi tahadhari hizo zilinisaidia au zingeisaidia hashaa! nilifanya hayo kuepukana kukamatwa kizembe.
MAMBO NILIYOJIFUNZA KIPINDI HICHO;
1. Maovu yanazidi kwenye jamii kwa sababu ya watu wanaogopa kukemea waovu
2. Watu wa karibu wakiwemo wazazi , ndugu na marafiki ndio huwa waalimu wakuu wakufundisha watu uoga wa kumuogopa muovu. Hii ni kutokana na kukupenda na kuona usumbufu unaoweza kukupata na kuwapata
3. Uovu ukizoeleka unakuwa utamaduni ndani ya jamii kiasi kwamba waovu hutukuzwa na kupewa sifa au kujipa sifa
4. Hakuna mtu mwema anayenyamaza aonapo maovu, isipokuwa wanafiki
5. Waovu hutumia mbinu ya kuzima wasema ukweli ili kuhalalisha uovu wao uonekane ni wema
6. Uovu ukishatamalaki, akili ya jamii huwa yakiovu, waovu husifiwa na wenye haki hupondwa.
7. Kutokana na waovu kupenda kamera na kutenda wema mbele ya media, jamii ni hujikuta ikiwaona ni watu wema kumbe ni wabaya.
8. Uovu haufichiki kama vile ulivyo wema. Waovu hutumia nguvu kubwa kuficha ubaya wao, ila kadiri wanavyouficha ndivyo wanavyouibua uovu wao mwingine
9. Hata waovu hufa, tena hufa kabla ya wakati wao.
10. Muovu hana uhuru, kwani uhuru upo hivi; ukiuzuia nao unakuzuia, ukiuachia nao unakuachia. Waovu huzuia uhuru na kujikuta kumbe nao hawapo huru kupitia kuficha uhuru.
11. Muovu hawezi kuwa huru hata siku akifa, bado ataishi kama mtumwa huko aendako
Nilishawahi kusema na kila siku nasema; Taikon atakuheshimu na kukuogopa ukitenda haki na kufuata sheria za Mungu. Lakini kamwe dunia ingalipo, Taikon hataogopa mtu muovu hata angekuwa ni nani. Taikon haogopeshwi na elimu ya mtu, kazi ya mtu, cheo cha mtu, uzuri wa mtu au mamlaka. Ukitenda wema nitakupongeza, ukitenda mabaya nitakukemea na kukuonya, ukiwa na kiburi shauri yako.
Tuishi kwa upendo, upendo ndio utatufanya tuishi milele.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Iringa Mjini