Kichwa Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,726
- 312
Heshima yenu.
Nilikuwa nasumbuliwa na tatizo la kula chakula kidogo sana, kitu hiki kilikuwa kinafanya nijione sio wa kawaida, kwani ilikuwa hata chips siwezi kumaliza, ugali lile tonge moja la mama nitilie siwezi maliza wakati wenzangu wanaagiza mawili. Pia njaa ilikuwa inaniuma kwa nadra sana, naweza kunywa chai na maandazi miwili asubuhi nisijisikie njaa mpaka saa kumi na moja.
Licha ya kuwa na umri wa miaka 33, urefu wa cm 162 uzito wangu ulikuwa kati ya 52kg-55kg nilikuwa na hofu ya kuwa underweight.
Wiki tatu zilizopita wife alienda clinic siku hiyo hatukwenda wote baada ya vipimo wakamshauri atumie asali ili kuongeza damu,aliponipa majibu hayo nilimtafutia asali akawa anatumia.
Baada ya muda nikakumbuka comments za mzizi mkavu na wanajamii hapa kuhusu umuhimu wa asali. Basi nikaanza kutumia kwenye chai nimepata maajabu sikutegemea kabisa na wala halikuwa lengo langu.
Kilichotokea nikinywa chai saa mbili yenye asali ikifika saa sita njaa inaniuma sana tu lazima nile, nikifika saa kumi na moja lazima nile na usiku saa nne lazima nile na nikiamka asubuhi njaa inauma na ulaji wangu sio kama ule wa awali nakula sana sasa.
Sijui nimejiponya hata sijielewi. Kwa sasa sukari nimeiweka pembeni mimi na asali kwenda mbele.