Kuganda kwa asali

0605

Member
Nov 17, 2022
63
91
KUGANDA KWA ASALI.

Kitalaamu nyuki hutengeneza asali kwa kuchukua unga wa maua ujulikanao kama pollen (chavua) na majimaji matamu ya maua yaitwayo nectar (mbochi), kutoka katika vyanzo mbalimbali ambavyo ni mimea.

Nyuki anapochukua malighafi hizi kutengeneza asali, huzichanganya kwa pamoja (husindika) kwa ujuzi wake hivyo asali kupatikana na kuhifadhiwa ndani ya masega kama chakula cha akiba cha nyuki kwa ajili ya kuitumia katika kipindi cha njaa pale kunapokuwa na upungufu wa maua/chakula cha kutosha.

Kwa kawaida mchakato mzima wa nyuki unapokamilika na kuifanya asali kuiva ndani ya mzinga wake basi huzalisha asali yenye mchanganyiki wa sukari kuu za aina mbili ambazo ni;

Fructose
Glucose
Sukari hizi mbili ndiyo sababu ya kuganda kwa asali ya nyuki iwapo aina moja ya sukari itazidi zaidi. Lakini kuzidi kwa sukari hizo siyo jambo la makusudi linalofanywa na nyuki bali hutokea kutokana na upatikanaji wa maua mengi yenye aina moja ya sukari kwa wingi.

Ikiwa katika mchakato wa utengenezaji wa asali nyuki ametafuta malighafi zake kwa ajili ya kutengeneza chakula chake (asali) katika eneo alipo na kubahatika kupata au kuchukua chavua ya maua kwa ajili ya kutengenezea asali yenye kiwango kikubwa cha sukari nyingi aina ya Fructose zaidi ya glucose, basi asali hii haitokuwa na tabia ya kuganda.

Lakini ilitokea nyuki amechukua chavua yenye kiasi kikubwa cha sukari ya glucose kuliko ile ya fructose basi asali itakayozalishwa na nyuki hao mara nyingi itakuwa na tabia ya kuganda, hivyo baada ya kuvunwa ndani ya muda mfupi wa kutunzwa itaganda yote katika chombo ilimotunzwa.

Hivyo sasa ikiwa asali itaganda yote ndani ya chombo chako, siyo kwamba ina kasoro bali itakuwa imetokana na aina ya sukari iliyopatikana kwenye malighafi zake.

Asali hiyo pia ikiganda hutengeneza chengachenga nyingi ziitwazo Crystallize na humpasa mtumiaji anapotaka kuitumia, lazima aiweke kwenye jua au ndani ya maji ya moto ndiyo iyeyuke (siyo kuichemsha) kwa ajili ya kuitumia. Asali hii bado ni nzuri na bora kwa watumiaji.

Inapatikana kwetu 0769 776290…. Ya nyuki wadogo/wasiodunga 35,000/= @ ltr na ya nyuki wa kawaida 10,000 @ ltr…
 
Asante kwa somo.
Asante kwa Tangazo.

Mimi natafuta simu ya nyuki mkuuu inapatikana kwako?????

Au niifuate Dodoma
 
Huwa nasikiaga asali mbichi asali mbichi, juzi Kati nikakutana na banati (binti) mmoja anauza asali mbichi

Katika kutaka kujua jibu la Hilo akaniambia asali mbichi ukiimimina huwa haikatiki,Kwa maana kama IPO ktk dumu ukiimimina huwa haikatiki mpaka inaisha yote,ni kweli alinionyesha na nikaona Hilo na nzito Sana

Je Kwanza ni kweli ndio sifa ya asali mbichi?

Pili, je kuna sifa nyingine ambazo zipo kuhusiana na kuijua hii ni asali mbichi?
 
Huwa nasikiaga asali mbichi asali mbichi,juzi Kati nikakutana na banati (binti) mmoja anauza asali mbichi

Katika kutaka kujua jibu...
Inaweza kuwa sifa mojawapo lkn inategemea na muda ambao asali imekaa tangu ilipovunwa... Kama imekaa muda mrefu huwa ina tabia ya kukatika/kuganda na hata kubadili rangi na kuwa light-gold au kuelekea ktk weupe, lkn kama ni mpya haikatiki kwa wepesi kama alivyokuambia na aghalabu rangi yake huwa imekolea sana (kutegemea na aina ya maua)...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom