Ushirikina Kigoma: Mwanamke aliyefariki Oktoba 2018 na kuzikwa aonekana akiwa hai

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
7,057
13,711
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limetoa ufafanuzi juu ya taarifa za Mwanamke mmoja wa miaka 40 Mkazi wa Kazegunga ambaye anadaiwa kuonekana November mwaka huu baada ya kufariki October 17,2018 wakati akijifungua Mtoto katika Hospitali ya Baptist iliyopo Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na kuzikwa Kazegunga alipokua kaiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Filemon Makungu amesema kuna matukio mawili ya Watu ambao wameonekana wakiwa hai ingawa Familia wamesema walifariki “Matukio haya tumeyafatilia yote na inatakiwa kuthibitisha kisayansi tumeshapeleka vipimo kwa Mkemia Mkuu bado hatujaletewa majibu tukiletewa tutatoa maelezo yaliyokamilika lakini kwa matukio haya mawili bado upelelezi tunaendelea nao kujua kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hai”

Mwezi November mwaka huu Familia ilisema Mpendwa wao huyo alionekana katika eneo la Ilagala Wilayani Uvinza ambapo miezi 11 iliyopita tukio kama hili la Mtu kufariki kisha kuzikwa na kuonekana tena lilitokea Kijiji cha Kandaga Wilayani UVinza Mkoani Kigoma ambapo pia mazingira yake yanahusishwa na imani za kishirikina kutumika kupoteza Watu na kuonekana tena baada ya muda mrefu kupita.

AyoTV mpaka sasa imeshawahi kuripoti matukio matano kama haya ya kusemekana Mtu amefariki na kuzikwa na baadaye Ndugu kudai wamemuona tena Ndugu yako akiwa hai, matukio hayo yametokwa mwaka 2018 Kasulu, mwaka 2020 Kasulu, mwaka 2021 Kasulu, mwaka 2022 Uvinza na mwaka 2023 Kigoma DC.

#MillardAyoUPDATES

FB_IMG_1702320059347.jpg
 
#MillardAyoUPDATESView attachment 2839832
Muha ni mtu hatari sana kutoka fasi ya Congo...ulozi kwao ni kama chakula
 
Haiwezekani siri ya ufufuo na uzima chombo Cha Dola kisiifahamu,Kwa kuwa ndio wanasajili taasisi za Dini.
Huku ni kuleta mtafaruku kwenye jamii,lakini pia kwanini iwe Kigoma.
Lolote lawesekana baada ya hii story,mara ghafla mfufukaji kawa mganga au mtumishi wa Imani fulani ya Dini.
Kuelekea 2024-2025 kuna sarakasi nyingi sana,kikubwa ni uzima tu.
 
Kwa kigoma sishangai mbona hata huyu naniliu alirest in peace ila juzi kaibuka...ndio zao watu wa kigoma🏃
 
1702334095259.png

Na sio mara ya kwanza, haya matukio ni mara kwa mara Kigoma !!

Wananchi wapo kwenye sintofahamu kumshangaa mtu waliemzika yu hai, wanataka wajue amefufukaje, wengi wanachoamini mwisho wa dunia ni wote watafufuka sio mmojammoja kama ya huko kigoma

Mwanamke mmoja wa miaka 40 Mkazi wa Kazegunga alionekana November mwaka huu baada ya kufariki October 17, 2018 wakati akijifungua Mtoto katika Hospitali ya Baptist iliyopo Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na kuzikwa Kazegunga alipokua kaiishi.

MY TAKE:

Kwangu binafsi nauona huu ni ushirikina, mtu azikwe na afukiwe kaburini kisha arudi mtaani kivipi?

Hata kama alikuwa kazikwa akiwa kwenye Comma na kuzinduka baada ya kuzikwa atakufa kwasababu atakosa hewa na chakula, pia ule udongo wanaoujaza juu hawezi kutumia mikono kujichimbia kwenda juu.

Mama mjamzito anafariki akiwa ktk harakati za kujifungua baada ya jitihada za madaktari wenye degree / masters zao kugonga mwamba, kumbee kuna wachawi wanahusika.

Kwa hali hii wanakigoma hawataogopa kufa bali maisha baada ya msiba yanayoweza kuendelezwa kurudi duniani kama mtumwa / msukule

UCHAWI UPO !! Hata vitabu vya dini vinaukemea, Kwenye uislamu Mtume Muhammad aliwahi kurogwa, kwenye ukristo watu waliosumbuliwa na mauza uza waliponywa na Yesu, UCHAWI UPO !! Tusione aibu kuukemea, vitendo hivi havikubaliki.
 
Kwa hiyo unashangaa mtu mmoja mmoja kufufuka kabla ya siku ya mwisho wa dunia kuja, kama wangefufuka wengi usingeshangaa? Hapo kwa huyo mwanamke kuna kufufuka kweli au ni mauzauza ya kishirikina? Sasa hapo polisi watatoa maelezo gani ikiwa serikali haiamini ushirikina?
 
Back
Top Bottom