Hii ni kwa wale wasioamini ushirikina, naombeni mnipe sababu za kisayansi kwenye mkasa huu

ukikaidi utapigwa2

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
13,827
27,259
Kijana Henry James (28) Mkazi wa Kijiji cha Kandaga Wilayani ya Uvinza Mkoani Kigoma ambaye aliyefariki na kuzikwa mwezi April 2022, amepatikana akiwa hai December 28, 2022 na kuungana tena na Familia yake huku akisema “mlipokuwa mnazika nilikuwa nimesimama pembeni kwenye mti”

Mama mzazi wa Kijana huyo ameiambia @AyoTV_ kuwa Mwanae alifariki kwa kugongwa na gari tarehe April 19 na kuzikwa tarehe 20.

"Huyu ni Mtoto wangu kabisa na aliyefariki alikuwa ni huyu ila nashangaa kurudi kwake wakati sisi tulimzika hii naona ni miujiza ya Mungu, kwasababu tulipokuwa tunamzika nililia sana nikimwambia Mungu naomba unisaidie sababu nilipata misiba ya kufatana ya Watoto wangu wawili hadi nikahisi vibaya"————Scholah Bukuru, Mama Mzazi.

Henry James alionekana Kijiji jirani cha Kaseke ambapo alionwa na Jirani aliyekuwa akiishi nae kipindi cha nyuma ndipo akaamua kuwapigia Ndugu zake simu na Mwenyekiti wa Kijiji ambapo nyumba anamoishi Kijana huyo imegeuka kama sehemu ya utalii kutokana na Watu kutoka Vijiji jirani kumiminika kwenda kumtazama.

Kamanda wa Polisi Kigoma Philemon Makungu amethibitisha kuwa na taarifa za tukio hili na kusema Polisi wataanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuruhusu uchunguzi wa kisayansi pamoja na kufukua kaburi. #MillardAyoMAAJABU
 
Kijana Henry James (28) Mkazi wa Kijiji cha Kandaga Wilayani ya Uvinza Mkoani Kigoma ambaye aliyefariki na kuzikwa mwezi April 2022, amepatikana akiwa hai December 28, 2022 na kuungana tena na Familia yake huku akisema “mlipokuwa

Kamanda wa Polisi Kigoma Philemon Makungu amethibitisha kuwa na taarifa za tukio hili na kusema Polisi wataanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuruhusu uchunguzi wa kisayansi pamoja na kufukua kaburi. #MillardAyoMAAJABU

Watanzania wengi wana tabia ya kukubali habari wanazoambiwa bila kuzi challenge.

Umehakikishaje aliyefariki na kuzikwa ni huyo aliyepatikana akiwa hai?

Watu wenyewe wako vijijini, hawana vipimo, mtu kagongwa na gari hatujui maiti ilikuwa katika hali gani ya kuweza kutambulika vizuri, huyo mama ana elimu gani kiasi cha kuweza kumtambua mtu akiyekufa kwa kugongwa na gari?

Watu wanapenda sana habari za uchawi na misukule. Unajuaje kwamba hakuna mpango mahsusi wa kutumia ajali kusingizia watu wamekufa halafu kuwateka kisaikolojia na kuwapeleka sehemu nyingine?
 
Mpumbavu wewe, unajitia ujuaji kuliko mama aliyemzaa??

Huu ujuaji wa mitandaoni ni shida sana.
 
Umeamua kuamini maneno matupu? Usichokijua hapo wanatafutwa watu wa kuingizwa king wapigwe hela.
Mombasa waliwahi kukutwa watu wanacheza uchi, pembeni ya gari.

Maelezo yalikuwa kwamba, hao ni wezi, wameiba gari. Sasa hawakujua kwamba ile gari iliwekewa ulinzi maalum wa kichawi, atakayeiiba achanganyikiwe akili, acheze uchi.

Ukiangalia kitendo cha kucheza ngoma uchi kilivyo serious, watu wakaamini kuwa kuna mchawi anaweza kukinga magari yasiibiwe hivyo.

Baadaye, ikaja kugundulika kuwa ule ulikuwa mpango tu kati ya huyo mchawi na hao watu, wamepanga pamoja hao wezi wacheze uchi, ili apate wateja zaidi.

Kama mtu una kichwa cha kuamini uchawi kirahisi, unachotwa na mipango ya watu wajanja tu.

Habari imeandikwa kirefu kwenye link hapo chini.
 
Unahakikushaje huu ni uchawi na si shere za ujanjaujanja wa watu tu kama karata tatu?

Mababu zetu walipooneshwa raedio wakasikia mtu anasema na muziki, walifikiri ni uchawi.

Kumbe ilikuwa sayansi tu ambayo hawakuijua.

Unajuaje unachoita uchawi leo si sayansi tu usiyoijua?
Ujanja ujanja upi? Na kwanini umehitimisha ni ujanja ujanja?

Kama hujui kitu kwanini usiseme hujui badala ya kuhitimisha kuwa ni ujanja ujanja?

Acha ujuaji wewe.
 
Nahisi ni uongo...kuna harufu ya upigaji.

Watu wengi wanaopenda watu waamini uchawi ni wapigaji.. hapo kuna mganga ama nabii anataka apige watu hela.. katumia mbinu ya kuanziaa mbaliii

Hii stori haina tofauti na ile ya mlandizi jamaa aliyejifanya kiroba cha wizi kimenasa kiuchawi. Hakishuki kichwani

Mombasa waliwahi kukutwa watu wanacheza uchi, pembeni ya gari.

Maelezo yalikuwa kwamba, hao ninwezi, wameiba gari. Sasa hawakujua kwamba ike gari iliwekewa ulinzi maalum wa kichawi, atakayeiiba achanganyikiwe akili, acheze uchi.

Ukiangalia kitendo cha kucheza ngoma uchi kilivyo serious, watu wakaamini kuwa kuna mchawi anaweza kukinga magari yasiibiwe hivyo.

Baadaye, ikaja kugundulika kuwa ule ulikuwa mpango tu kati ya huyo mchawi na hao watu, wamepanga oamoja hao wezi wacheze uchi, ili apate wateja zaidi.

Kama mtu una kichwa cha kuamini uchawi kirahisi, unachotwa na mipango ya watu wajanja tu.
Ukiwa hujui kitu kuna faida kubwa ya kukubali kusema kuwa hujui badala ya kujifanya mjuaji.

Sema sijui, utasaidika.

Ujuaji ujuaji tu, kila kitu unajua wewe, kila kitu mbishi wewe.

Upumbavu.
 
Ujanja ujanja upi? Na kwanini umehitimisha ni ujanja ujanja?

Kama hujui kitu kwanini usiseme hujui badala ya kuhitimisha kuwa ni ujanja ujanja?

Acha ujuaji wewe.
Ujanja ujanja kama huu.

Unahakikishaje hicho unachofikiri ni uchawi si mipango ya watu tu kukushikia akili wafanikishe mambo yao?
 
Hiyo ni sayansi katika ulimwengu wa roho, walifanikiwa kumrudisha kabla ya kumkata ulimi. Nafikiria waganga wanaofuata maadili ndio waliomrudisha. Ajali nyingi ni michongo katika ulimwengu wa roho.

Waliogundua maisha ni mchezo, wanacheza kweli kwa mastep. Ujue Kuna ambao wamezikwa ila kazi yao ni kulima mashamba usiku, kilichozikwa ni mgomba.
 
Ukiwa hujui kitu kuna faida kubwa ya kukubali kusema kuwa hujui badala ya kujifanya mjuaji.

Sema sijui, utasaidika.

Ujuaji ujuaji tu, kila kitu unajua wewe, kila kitu mbishi wewe.

Upumbavu.
Hata post yangu imejikita kwenye kuuliza maswali, kupata uhakiki, kuthibitisha.

Na wewenhujathibitisha wala kujibu maswali niliyouliza.

Pia, hujui hata kusima kwa ufahamu, hoja ikiletwa kupinga kukubali jambo, na kudai ushahidi nanuthibitisho zaidi, unaita "ujuaji".

Hujathibitisha uchawi upo.
 
Nahisi ni uongo...kuna harufu ya upigaji.

Watu wengi wanaopenda watu waamini uchawi ni wapigaji.. hapo kuna mganga ama nabii anataka apige watu hela.. katumia mbinu ya kuanziaa mbaliii
Uongo wa nini? kwa faida ya nani?

Na kwanini umehitimisha ni uongo?

Kama jambo hulijui kwanini usiseme kwamba sijui badala ya kujitia ujuaji na kuweka hitimisho?
 
Back
Top Bottom