Ushawai kusikia gari ya ubalozi au kampuni kubwa za kimataifa limepata ajali? Serikali ikajifunze kudhibiti mali zake

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
habari wadau..

nimeguswa sana na ajali iliyoua watu watano singida..

gari za serikali zinaua sana watumshi wake..

najua wengi tunasema siku zimefika.. au Mungu amependa..

ila hatujiulizi why Mungu hawapi ajali madereva wa balozi au kampuni za kimataifa? au mnafikiri hizo gari zao huwa hazisafiri ?

katika harakati za maisha nimewai fanya kazi ubalozi wa taifa moja kubwa...
nilijifunza mengi sana hasa jinsi ya kuweka controls na kuzisimamia... gari zote zimefungwa vingamuzi.. spidi yake popote.. transport manager.. na bosi wa department anaona .. na alarm inalia kwenye simu yake.. na anamfukuza kazi dereva fasta na hata mliokuwemo kwenye gari hilo.. mnaweza fukuzwa pia..

gari zote zina camera ndani.. haruhusiwi kupanda asiyehusika hata kama ni mke wako au mwanao.. ile camera inarekodi kila kitu ndani ya gari... ndio maana huwezi kuona ajali za kijinga magari yao..

pia nimewai kufanya kazi na kampuni kubwa tu vijana wanaita multinational.. napo kila gari lina kingamuzi... wao hawana camera tu.. ila spidi bosi wako anaona popote..

na pia hairuhusiwi kupanda kwenye gari asiyehusika...

na huu utaratibu wa wafanyakazi kibao kusafiri na gari moja ni wa wapi? au ndio kubana matumizi.. si wangekatiwa hata tiket za bus kila mtu asafiri kivyake
 
Tatizo watumishi wengi wa serikalini na binafsi ukiacha hayo makampuni makubwa ua kimataifa n.k tumezoea kusimamiwa/kufuatiliwa ili tuweze kutimiza wajibu wetu kwa ufanisi,tukiachiwa tujisimamie wenyewe shida ndipo zinapoanza. Tujirekebishe
 
hata makampuni makubwa na balozi niliyotoa mfano... huwa unasimamiwa kwa teknolojia.. sio kama unajisimamia mwenyewe..gari ina camera na kingamuzi.. kila unachofanya ma bosi wake wanapata taarifa
 
Yaani kuna saa unasafiri ila ukiangalia gari za serikali zinavyoendeshwa unabaki kuhuzunika tu. Unawaza hivi hili gari amepewa dereva wa serikali au ni mtu wa aina gani anayeliendesha. Wanaenda mwendo mkali na kuona kuwa wao ndio wenye haki barabarani kuliko magari mengine. Nafikiri ni wakati sasa gari zote kutii sheria bila kujali ni za serikali au mashirika ya serikali
 
Gari za Serikali zinajiachia sana barabarani 24/7 wapo 80+km/h na hawafatiliwi
Huyo dereva alipigwa tochi akakimbia
IMG-20181021-WA0022.jpg
 
habari wadau..

nimeguswa sana na ajali iliyoua watu watano singida..

gari za serikali zinaua sana watumshi wake..

najua wengi tunasema siku zimefika.. au Mungu amependa..

ila hatujiulizi why Mungu hawapi ajali madereva wa balozi au kampuni za kimataifa? au mnafikiri hizo gari zao huwa hazisafiri ?

katika harakati za maisha nimewai fanya kazi ubalozi wa taifa moja kubwa...
nilijifunza mengi sana hasa jinsi ya kuweka controls na kuzisimamia... gari zote zimefungwa vingamuzi.. spidi yake popote.. transport manager.. na bosi wa department anaona .. na alarm inalia kwenye simu yake.. na anamfukuza kazi dereva fasta na hata mliokuwemo kwenye gari hilo.. mnaweza fukuzwa pia..

gari zote zina camera ndani.. haruhusiwi kupanda asiyehusika hata kama ni mke wako au mwanao.. ile camera inarekodi kila kitu ndani ya gari... ndio maana huwezi kuona ajali za kijinga magari yao..

pia nimewai kufanya kazi na kampuni kubwa tu vijana wanaita multinational.. napo kila gari lina kingamuzi... wao hawana camera tu.. ila spidi bosi wako anaona popote..

na pia hairuhusiwi kupanda kwenye gari asiyehusika...

na huu utaratibu wa wafanyakazi kibao kusafiri na gari moja ni wa wapi? au ndio kubana matumizi.. si wangekatiwa hata tiket za bus kila mtu asafiri kivyake
Umeleta jambo la msingi sana mkuu
 
Back
Top Bottom