Ushawahi kufiwa na watu au mtu ambae ulimpenda sana kiasi ya kwamba haiwezi kupita siku, week au mwezi bila kumuwaza au kumuota?

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
3,653
Reaction score
8,000
Niaje waungwana

Ni nature kwa kila binadam kufa au kufiwa. Nikimaanisha kuwa kila mwana JF anaesoma, na asiesoma thread hii including myself tutakufa, tutafiwa au pengine tayari wengine tumeshafiwa.

Sasa kwa wale ambao tumeshawahi kufiwa na wapendwa wetu mfano mzazi, mke, mume, mtoto, ndugu au rafiki, kuna hali fulan ya maumivu humtokea mfiwa. Na hali hii hutokea kama yule aliekufa alikuwa ni mtu wako wa karibu uliempenda na yeye akakupenda, uliemthamini na yeye akakuthamini, uliemjali na yeye akakujali, na sometimes uliemtegemea na yeye akakutegemea.

Binafsi nimeshafiwa na ndugu zangu wa damu akiwemo mzazi. Vifo vyao viliniumiza sana lakini naweza kusema kwamba kifo cha marehemu mdogo wang ndio kimeniumiza zaidi na mpaka leo siwezi kupitisha mwezi au week 2 sijamuwaza au kumuota.

Huyu mdogo wang ni mtu ambae kiukweli tulipendana, tuliheshimiana, tulisaidiana na kujaliana sana. Alikuwa hawezi kufanya jambo lake la maana bila kuniomba ushauri. Na mimi pia ilikuwa ni hivyo hivyo.

Hata wazazi wetu sometimes walipotaka wamwambie dogo jambo lolote la serious, ili akubali ilibidi sometimes wapitie kwangu ili iwe rahisi jambo hilo kulikubali.

Dogo alikuwa fundi mekanika mzuri sana kiasi ya kwamba mpaka baadhi ya watumishi wa serikali, including viongozi wa jeshi walikuwa wanaleta magari kwake awatengenezee.

Siku mbili kabla ya kifo chake alinipigia simu kuniomba ushauri, kwamba kuna mteja wake mmoja (mjeshi) alimuomba waende nae bagamoyo wakachukue mkaa ili walete Dar kuja kuuza.

Kwanza nilisita kwa sababu huko wanapokwenda ni mbali na yeye ana mke tena mjamzito. Lakin pia niliogopa watu wa maliasili wanaweza kumkamata na kumfunga kutokana na kutokuwa na vibali vya biashara hiyo. Ila dogo akanambia kwamba mmiliki wa gari hilo ni mjeshi mwenye cheo cha kanali, hivyo haitokuwa rahisi yeye kukamatwa na maliasili yeyote, ukizingatia na mjeshi mwenyew atakuwa ndani ya gari.

Kusikia hivyo nikaafiki ila nikamwambia awe makini barabarani maana gari itakuwa imebeba mzigo mkubwa, akasema poa.

Safari ikafika dogo na mjeshi wakaingia Bagamoyo. Kweli walifanikiwa kupata mkaa wakajaza fuso na kuanza safar ya kurudi Dar. Ilikuwa usiku kama mida ya saa 4 hivi. Walivyofika karibu na mpaka wa Mkoa wa Pwani na Dar, gari ikapata pancha.

Dogo kwa vile ni fundi akaegesha gari pembeni ya barabara akatoa jeki na kuanza kupiga ili wabadilishe tairi. Walikuwa na spea tairi ndani ya gari hivyo dogo akatoa pancha akaweka zima. Ile ashamaliza kufunga anashusha jeki huku yule mjeshi akiwa amemshikia tochi ili aone vizur, ghafla bodaboda hata ilipotokea haijulikani akawapitia wote wawili, yani dogo na mjeda.

Ajali ile ikasababisha watu wajae kuangalia kuna nini. Wakati huo mjeda alikuwa hajitambui, bodaboda nae kazimia, ila mdogo wang yeye alikuwa fresh. Ni kama vile hakuguswa na kitu.

Baada ya pilika pilika za hapa na pale trafiki wakafika na kuchukua maelezo ambapo dogo ndio alikuwa anampa yule trafiki maelezo, na kueleza kuwa mmiliki aliekuwa pale chini ni afisa wa jeshi.

Hivyo ikabidi ifanyike juhudi za kuwawahisha hospital ya wilaya ya Bagamoyo yeye (mjeshi) na bodaboda huku dogo akiendesha lile gari akifuatana na trafiki hadi hospital kuandika maelezo.

Baada ya maelezo, yule mjeda ikaonekana hali yake sio nzuri hivyo inabidi awahishwe hospital ya jeshi Lugalo mara moja, na yule bodaboda nae apelekwe muhimbili. Mpaka hapo nyumbani tulikuwa hatujui kinachoendelea japo mimi nilikuwa naifahamu hiyo safari yake ya Bagamoyo.

Mida ya saa 7 usiku akanipigia sim kunijulisha kilichotokea, nikamuuliza kama yeye kwa upande wake yupo salama, akasema yeye yupo salama salmin, japo alichubuka kidogo mguuni lakini washamuweka dawa anataka apumzike pale Hospital, kisha asubuhi ndo ataanza safari ya kuja Dar. Kumbuka hapo ilikuwa ni saa 7 usiku, hivyo ilibaki masaa ma4 tu kupambazuke, ndomaana akaona bora alale tu pale kisha asubuhi aanze safari. Nikamshauri asimwambie kwanza mkewe kuhusu hiyo ajali mpaka atapofika nyumbani ili asije akampa wasiwasi na ukizingatia mkewe ana mimba.

Dogo akaniaga fresh nikakata simu na kulala.

Asubuhi mapema nilipoamka nikachukua sim kumpigia ili kujua ameamkaje, na safari ameshaanza au bado. Sasa kila nlipopiga sim ilikuwa inaita tu ila haipokelewi. Nikajua labda bado analala au anaendesha gari so anaogopa kupokea asifanye ajali nyingine.

Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi nikaona anapiga sim nikapokea haraka haraka, ila nilichokisikia sitokuja kukisahau. Yani nilisikia sauti ya mtu mungine ambayo iliniambia kuwa mdogo wangu alifariki asubuhi ya siku ile, yani alifariki saa 10 ya asubuhi baada ya hali yake kugeuka ghafla. Inasemekana aliumia ndani kwa ndani bila mwenyewe kujua.

Aisee nilihisi kama jamaa anatania nikamwambia naomba niongee na mwenye sim mwenyewe. Jamaa akanambia utaongea na mwenye sim gani wakati ameshafariki. Japo sikuamini ila ikabidi nipige sim kwa mzee kumuelezea kilichotoea. Hata mzee nae alishtuka sana kwa habari ile. Ila tukapanga tuanze safari ya kuelekea Bagamoyo ili kwenda ku confirm kama kile nilichoambiwa ni kweli au stori.

Baada ya kufika hospital kujitambulisha tukapelekwa monchwari kuhakikisha na kuthibitisha kama ni yeye kweli au wamejichanganya. Aisee tulipoingia na kuoneshwa maiti ya mdogo wang akiwa amekaushwa na balafu na wakati masaa kadhaa niliongea nae, nilitaka kuumwa kichaa, ilibidi nikamatwe na kupelekwa katika chumba fulan ambapo nilipewa vidonge vya usingizi. Nilipoamka kuna ndugu wengine walikuwa wameshafika ikabidi tufanye mpango wa kurudi na maiti nyumbani kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Ni miaka 8 sasa imepita ila picha yake haifutiki kichwani kwangu.

Je wewe ushawahi kufiwa na mtu wako wa karibu ambae mpaka leo haujasahau ulivyoumizwa na kifo chake?
 
Pols sana nimesoma nimejikuta nasikitika sana maana umeongea nae vizuri yupo mzima baada ya masaa kadha unaambiwa kafa inashutsha mno.May his soul rest in peace
Kifo cha gafla kinastua sana, nilikia kama mwendawazimu nilipofiwa na mtu wa karibu ambae jana usiku tumeongea fresh, kesho yake natoka shule naambiwa kafia usingizini.
 
Nilifiwa na rafiki...
Ilikuwa kama masikhara tulikuwa wadogo standard 7, rafiki nilijuana naye baada ya yeye kuhamia kwenye shule yetu standard 5 na mimi nikawa mwenyeki wake shuleni mpaka mtaani, tukawa karibu sana kiasi cha kupajua kwao na familia yao wote.

Rafiki umauti ulimfika tulipokuwa standard 7, tulitumwa fimbo shule na mwalimu wa somo la hisabati na mwalimu alikuwa mkali sanaaa, ilipofika juma3 siku ya kupeleka hizo fimbo asubuhi yake tulikuwa wote mimi,rafiki na wengine wawili tukiwa tunachuma fimboo za kumpelekea mwalimu, rafiki yangu alikuwa mtundu na tulikuwa na michezo ya kucheza kidali poo juu ya miti, basi kwa siku hiyo jamaa alidandia mti na kuanza kuchuma fimbo sisi tukiwa chini tunamuangalia, mimi nikamstua "oyaa cost.... fanya haraka tunachelewa au nije kukusaidia?" rafiki akanijibu "ndo nashuka hizo si zinatosha?" akiwa kwenye harakati za kushuka mtini si ndo akatereza, sijui ilikuwaje kuwaje wakuu mambo yalitokea kwa haraka rafiki alidondoka mtini na alingukia mgongoo,.. daah

Tulimfata alijaribu kuinuka kidogo lakini alishindwaa akalala chini macho yakabadilika rangi na kuwa meupe tu bila ya kiini cheusi huku akigalagala chini.... Alooh wakuu msimbee yawakute

Huyu ni rafiki tu lakini niumizwa sana na kifo chake,nililia sana msibani watu wakasema nilikuwa naleta utoto kwenye misiba ya watu, lakini haikuisha hapo yule rafiki nilimuota sana mpaka ukubwani, na mtaani walidai kifo chake hakikuwa cha asili, ndotoni nilikuwa namuota nikiongea naye namwambia wewe si umekufa? ananijibu mm sijafaa..!!!

Wakuu kifo kina kuja kwa taarifa lakini ni ngumu sana kung'amua mpaka kitokee... Ingawa tulikuwa wadogo lakini jamaa alinigusa sana kuna story alikuwa ananipa kipindi cha mwisho wa uhai wake nilikuwa sizielewe lakini zilileta maana baada ya kifo chake.
 
Niaje waungwana

Ni nature kwa kila binadam kufa au kufiwa. Nikimaanisha kuwa kila mwana JF anaesoma, na asiesoma thread hii including myself tutakufa, tutafiwa au pengine tayari wengine tumeshafiwa.

Sasa kwa wale ambao tumeshawahi kufiwa na wapendwa wetu mfano mzazi, mke, mume, mtoto, ndugu au rafiki, kuna hali fulan ya maumivu humtokea mfiwa. Na hali hii hutokea kama yule aliekufa alikuwa ni mtu wako wa karibu uliempenda na yeye akakupenda, uliemthamini na yeye akakuthamini, uliemjali na yeye akakujali, na sometimes uliemtegemea na yeye akakutegemea.

Binafsi nimeshafiwa na ndugu zangu wa damu akiwemo mzazi. Vifo vyao viliniumiza sana lakini naweza kusema kwamba kifo cha marehemu mdogo wang ndio kimeniumiza zaidi na mpaka leo siwezi kupitisha mwezi au week 2 sijamuwaza au kumuota.

Huyu mdogo wang ni mtu ambae kiukweli tulipenda, tuliheshimiana, tulisaidiana na kujaliana sana. Alikuwa hawezi kufanya jambo lake la maana bila kuniomba ushauri. Na mimi pia ilikuwa ni hivyo hivyo.

Hata wazazi wetu sometimes walipotaka wamwambie dogo jambo la serious ili akubali ilibidi sometimes wapitie kwangu ili iwe rahisi jambo hilo kulikubali.

Dogo alikuwa fundi mekanika mzuri sana kiasi ya kwamba mpaka baadhi ya watumishi wa serikali including viongozi wa jeshi walikuwa wanaleta magari kwake awatengenezee.

Siku mbili kabla ya kifo chake alinipigia simu kuniomba ushauri, kwamba kuna mteja wake mmoja (mjeshi) alimuomba waende nae bagamoyo wakachukue mkaa ili walete Dar kuja kuuza.

Kwanza nilisita huko wanapokwenda ni mbali na yeye ana mke tena mjamzito, lakin pia niliogopa watu wa maliasili wanaweza kumkamata na kumfunga kutokana na kutokuwa na vibali vya biashara hiyo. Ila dogo akanambia kwamba mmiliki wa gari na mjeshi mwenye cheo cha kanali, hivyo haitokuwa rahisi yeye kukamatwa na maliasili yeyote ukizingatia na mjeshi atakuwa ndani ya gari. Kusikia hivyo nikaafiki ila nikamwambia awe makini barabarani maana gari itakuwa imebeba mzigo mkubwa, akasema poa.

Safari ikafika dogo na mjeshi wakaingia Bagamoyo. Kweli walifanikiwa kupata mkaa wakajaza fuso na kuanza kurudi Dar. Ilikuwa usiku kama mida ya saa 4 hivi. Walivyofika karibu na mpaka wa Mkoa wa Pwani na Dar, gari ikapata pancha.

Dogo kwa vile ni fundi akaegesha gari pembeni ya barabara akatoa jeki na kuanza kupiga ili wabadilishe tairi. Walikuwa na spea tairi ndani ya gari hivyo dogo akatoa pancha akaweka nzima. Ile ashamaliza kufunga anashusha jeki huku yule mjeshi akiwa amemshikia tochi ili aone, ghafla bodaboda hata ilipotokea haijulikani akawapitia wote wawili, yani dogo na mjeda.

Ajali ile ikasababisha watu wajae kuangalia kuna nini. Wakati huo mjeda alikuwa hajitambui, bodaboda nae kazimia, ila mdogo wang yeye alikuwa fresh. Ni kama vile hakuguswa na kitu.

Baada ya pilika pilika za hapa na pale trafiki wakafika na kuchukua maelezo ambapo dogo ndio alikuwa anampa yule trafiki maelezo na kueleza kuwa mmiliki aliekuwa pale chini ni afisa wa jeshi. Hivyo ikabidi ifanyike juhudi za kuwawahisha hospital ya wilaya ya Bagamoyo yeye (mjeshi) na bodaboda huku dogo akiendesha lile gari akifuatana na trafiki hadi hospital kuandika maelezo.

Baada ya maelezo, yule mjeda ikaonekana hali yake sio nzuri hivyo inabidi awahishwe hospital ya jeshi Lugalo mara moja na yule bodaboda nae apelekwe muhimbili. Mpaka hapo nyumbani tulikuwa hatujui kinachoendelea japo mimi nilikuwa naifahamu hiyo safari yake ya Bagamoyo.

Mida ya saa 7 usiku akanipigia kunijulisha kilichotokea, nikamuuliza kama yeye kwa upande wake yupo salama, akasema yeye yupo salama salmin japo alichubuka kidogo mguuni lakini washamuweka dawa anataka apumzike pale Hospital, kisha asubuhi ndo ataanza safari ya kuja Dar. Kumbuka hapo ilikuwa ni saa 7 usiku hivyo ilibaki masaa 4 tu kupambazuke, ndomaana akaona bora alale tu pale kisha asubuhi aanze safari. Nikamshauri asimwambie kwanza mkewe kuhusu hiyo ajali mpaka atapofika nyumbani ili asije akampa wasiwasi na ukizingatia mkewe ana mimba.

Dogo akaniaga fresh nikakata simu na kulala.

Asubuhi mapema nilipoamka nikachukua sim kumpigia ili kujua ameamkaje na safari ameshaanza au bado. Kila nlipopita simu ilikuwa inaita tu ila haipokelewi. Nikajua labda bado analala au anaendesha gari anaogopa kupokea asifanye ajali nyingine. Ilipofika mida ya saa 2 asubuhi nikaona anapiga sim nikapokea haraka haraka, ila nilichokusikia sitokuja kukisahau. Yani nilisikia sauti ya mtu mungine ambayo iliniambia kuwa mdogo wangu alifariki asubuhi ya siku ile yani alifariki saa 10 ya asubuhi baada ya hali yake kugeuka ghafla. Inasemekana aliumia ndani kwa ndani bila mwenyewe kujua.

Aisee nilihisi kama jamaa anatania nikamwambia naomba niongee na mwenye sim mwenyewe. Jamaa akanambia utaongea na mwenye sim gani wakati ameshafariki. Japo sikuamini ila ikabidi nipige sim kwa mzee kumuelezea kilichotoea. Hata mzee nae alishtuka sana kwa habari ile. Ila tukapanga tuanze safari ya kuelekea Bagamoyo ili kwenda ku confirm kama kile nilichoambiwa ni kweli au stori.

Baada ya kufika hospital kujitambulisha tukapelekwa monchwari kuhakikisha na kuthibitisha kama ni yeye kweli au wamejichanganya. Aisee tulipoingia na kuoneshwa maiti ya mdogo wang akiwa amekaushwa na balafu na wakati masaa kadhaa niliongea nae, nilitaka kuumwa kichaa, ilibidi nikamatwe na kupelekwa katika chumba fulan ambapo nilipewa vidonge vya usingizi. Nilipoamka kuna ndugu wengine walikuwa wameshafika ikabidi tufanye mpango wa kurudi na maiti nyumbani kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Ni miaka 8 sasa imepita ila picha yake haifutiki kichwani kwangu.

Je wewe ushawahi kufiwa na mtu wako wa karibu ambae mpaka leo haujasahau ulivyoumizwa na kifo chake?
Waisome watu woteeeeeee, dada alinifundisha MATHS ku MAKE the SUBJECT...

Hesabu Kila kitu alinifundisha alikua ni dada boraaa Leo nikageuka nyuma dada hayupo...

Nili amini kwenye familia yetu hatufii/ hatufarikii aiseeee niliomba MUNGU dada asife...dada akafarikii...ilitokea UGOMVII USIO na mwisho wa Mimi na MUNGU...

Asante sanaaaaaa kwa maswahaba wa mtume Muhammad vijana Saba wa PANGONI nili ielewa vyema baada ya miaka kumi ya kufuru na kumtukana MUNGU
 
hii stori ulipotaja neno mdogo wangu nilipata majonzi ghafla kwa sababu inafanana na iliyonitokea mimi.

Itoshe kusema pole sana ni mapenzi yake Mungu na mimi pia toka 2006 mpaka leo simalizi wiki bila kumuota na kumkumbuka mdogo wangu,,, Mungu awalaze wote mahali pema .....Amina
 
Back
Top Bottom