Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Hujawahi kuachwa na ndege ndugu, na labda waliotangulia kuelezea hawajatoa mazingira tofauti tofauti. Sikia hii...
Nilikuwa natoka Ottawa via Montreal to Zurich then Bongo. Hali ya hewa ilikuwa ni winter kali Feb 2015, na kusababisha ndege kuchelewa kuondoka Macdonald-Cartier Intl airport. Tulikaa taxiing lane kama dk 40 hivi then kuruka na safari ya kama 1.30hrs au 2hrs. Ile Kufika Montreal-Dorval airport (au Trudeau kwa sasa) pipa la kuunganisha to Zurich ndio linakula mawingu, kimbembe kikaanzia hapo mzee.
Mfukoni nina $5 tu ya Canada, simu hazikamati mtandao, wenge likanijaa mwanaume. Sema penye matatizo akili nayo huwa inachaji fasta, ikabidi niwafate kwenye meza ya ndege husika. Nikapambana nao kama lisaa hivi mpaka kilipoeleweka na wakanipa na coupon ya $10 kwa ajili ya msosi manake route ikabadilika sasa kupitia Heathrow kisha Addis mpaka Bongoland.
Kwahiyo sio kila kuachwa kunatokana na uzembe na kutokujipanga mapema kisafari
hela ulikuwa unataka ya hotel au?
 
Nilishawah kuachwa na basi la kwenda songea,natoka zangu mbagala na usafiri wa daladala plus foleni kufika ubungo gari limeshatoka ubungo kama nusu saa imeshapita ikabidi nichukue bodaboda kulifukuzia nakumbuka nililikuta karibia na moro siwez kabisa kusahau
 
Mimi nilikuwa nakwenda Arusha kikazi.. nilikuw na ndege ya Precision Air saa 12 asub. Siku hiyo sijui nini kilifanya nichelewe kulala. Hamadi kuja kustuka asub ni saa moja asub
Kuwapigia Precision wanasema natakiwa kiasi fulani cha pesa kubadilisha ndege ili niondoke na ndege ya mchana.
Nikapiga mahesabu ya kubadilisha ticket na Tax elfu 40 mpaka airport.
Nikapiga mahesabu Tax mpaka Ubungo elfu 7. Bus mpaka Arusha elfu 20 kipindi hiko..
Nikaenda zangu Ubungo kukamata Osaka Coach
we ndo hamna kabisaaa
 
Stockholm, Sweden Dar es Salaam, Tanzania

Ilikuwa December 10, 2019 nikisafiri kutoka Stockholm (Arlanda Airport) kuja bongo kupitia Amsterdam kwa kutumia KLM Airlines. Ratiba ya safari ilikuwa nitoke Stockholm saa 12:30 asubuhi (yaani 6:30 am) na kufika Schiphol Airport (Amsterdam) saa 2:40 asubuhi (yaani 8:40 am) na kisha nipande ndege nyingine kutoka Amsterdam saa 4:15 asubuhi (yaani 10:15 am) kuja Dar na ambapo ningefika Julius Nyerere International Airport saa 4:30 usiku (yaani 10:30 pm).

Kilichotokea ni kuwa ndege ya kutoka Stockholm ilichelewa, badala ya kutoka Arlanda saa 12:30 asubuhi tulianza safari saa tano na nusu asubuhi (11:30 am), ambapo muda huo tayari ndege ya kutoka Schiphol airport (Amsterdam) kuja Dar ilikuwa imekwishaondoka na hivyo kuniacha. Bahati nzuri yangu ni kuwa shida ilikuwa kwao na hivyo nilivyofika Amsterdam, walinibukia ndege nyingine (Egypt Air) ambapo nilifanikiwa kufika Dar kesho yake saa 10 alfajili, yaani nilichelewa kufika kwa zaidi ya masaa matano kutoka kwenye ratiba ya awali.

Kutokana na usumbufu huo, nilivyofika Dar nilijaza form kupitia skycop.com (zamani ifdelayed.com), ambao wanahusika na kufuatilia "compesations" za wasafiri wanaopata shida ya usafiri wa ndege wa aina mbalimbali. Bahati yangu nyingine, majuzi kati nimepokea pesa ya Kiswidi 6300 (i.e. SEK 6300). Ticketi yangu ilikuwa ya thamani ya SEK 4200 (ambayo nilikata wakati wa promotion, miezi mitatu kabla ya safari) na hivyo nimepata faida ya SEK 2100.
walikulipa sababu ya usumbugu? au hayo Ni matukio mawili tofauti?
 
Hii mistake ilimkuta demu mmoja wakishua ambaye mchizi wangu aliniunganisha naye ili nimtongoze nimmege. Japo wa kishua ila alikua mbovu sana....akawa rafiki tu. Sasa wakati anataka kurudi shule Uturuki (by the way ni Cyprus) akaniomba nimkatie ticket Turkish Airlines. Nikabook....akanipa mastercard yake details (demu sijui kwanini aliniamini yule akanipa hadi CVV namba) nikafanya malipo. Yeye akapata email kwake kuwa kila kitu kipo sawa na ticket akatumiwa soft copy.
Ndege inaondoka saa 9:45 usiku....tarehe 6. Hapo kimsingi ni usiku wa tarehe 5 maana ikishafika saa 6 tarehe inachange. Yeye si akalala weeee akaenda usiku wa tarehe 6 ambapo inakuwa tarehe 7. Akaambiwa kitu ikaribia kufika Instanbul.....ikabidi baba yake atop up dola 100 wampe ndege ya kesho yake.
mzee umechora tattoo?
 
Salute wakuu,

As per title hapo juu, Ulishawahi kuachwa na ndege ugenini? Ilikuaje na Ulifanyaje? Let’s share experience.

Back in 2014 nikiwa chuo mwaka wa pili nchini Oman kwa His Excellency late Sultan Qaboos bin Said (May his soul R.I.P) ndipo niliweka plan za kwenda kumtembelea rafiki yangu mmoja aliekua akisoma Bangalore nchini India.

MIPANGO YA SAFARI
Niliaanza kuplan my trip, kwanza Nikampigia simu swaiba kama ataweza kuni-accomodate for two weeks at his place, As u know accommodations ndio big issue kama hauna mpunga wa kutosha kufikia hotelini huko ng’ambo.

Baada ya kuweka mambo sawa na mshikaji nikaanza mchakato wa kutafuta visa.

Nikatembelea Agency ya India nchini Oman wanaohusika na utoaji wa visa. Nakumbuka ilinigharimu kiasi cha 20 OMR ambazo kwa kipindi hicho zilikua almost sawa na Tsh 97,000/= plus 5 OMR processing fee. Ndani ya siku 7 nikawa nimefanikiwa kupata 3 months visitation visa.

Baada ya kupata visa nikaanza kutafuta the cheapest flight to Bangolore India. Mind u that I was student so nilikua na save from my monthly allowance nilizokuwa nalipwa College kwa ajili ya kujikimu.

Katika kutafuta tafuta huko online nikakutana na Air India ambayo ndio ilikua nafuu kwa wakati huo na ilinigharimu 133 OMR for a round trip.

Baada ya kumaliza ku-book tiketi yangu na kuilipia nikaprint na kuihifadhi na kusubiri siku ya safari ambayo ilikua 01/02/2014.

SIKU YA SAFARI
Hatimaye siku ya safari ikawadia safari ilikua imepangwa kuwa ni saa tano kamili usiku. Mapema kabisa nika-show up Muscat IA two hrs earlier before departure for check in.

Baada ya kufanya taratibu zote za ukaguzi pale Airport tukaingia ndani kusubiri ndege yetu itakayotupeleka mpaka Chennai, India ambapo tungekuwa na two hours za kusubiri na kubadilisha ndege nyingine ambayo ingetufikisha hadi Bangalore.

Kwa bahati mbaya ile ndege ikachelewa kwa zaidi ya saa na nusu kufika pale Muscat IA. Hapa sasa ndipo shida ilipoanzia. Nakumbuka tulianza safari saa 6 na dk 43 usiku badala ya saa 5 kamili usiku.

Wakati tupo angani Air hostess wakawa wanagawa “Incoming Passanger card” au “Arrival card” kwa abiria ambao ni wageni kwa ajili ya kupunguza traffic tutakapofika.

Basi nikajaza ile card isipokua sehemu ya Anuani wapi exactly naenda huko Bangalore. Yani I took it easy as if kama tunapokua kwetu Bongo ukisema naenda TEMEKE bila kusem ni wapi TEMEKE. Mbaya zaidi hata hizo anuani za rafiki yangu sikuwa nazo kwa wakati huo. (Ieleweka hapa anuani namaanisha Mji, eneo ninaloenda ndani ya mji huo na namba ya nyumba anayoishi mwenyeji wangu)

CHENNAI AIRPORT
Tulipofika Chennai ilikua saa 9 na nusu Alfajiri na ilibaki nusu saa tuu ya kuingia kwenye ndege yangu ya pili ambayo ilikua inaelekea Bangalore.

Niliposhuka nikamkabidhi Afisa mmojawapo ile kadi yangu niliyoijaza. Alipo ikagua akakuta sehemu ya anuani sijajaza. Hapo balaa likaanza.

Akaanza kuniuliza naelekea wapi namwambia Bangalore; Anaanza kuniambia Bangalore ni kubwa wapi exactly unapoenda aisee sipajui, ikabidi aombe passport yangu kucheki kama nimetimia au nimekuja kimagumashi.
Akakagua akakuta nipo sawa, akaanza kunidai address halafu mimi siijui. Akanionesha sehemu ya kupigia simu akaniambia nimpigie rafiki yangu anitumie address alipo.

Kumbuka hapo ni usiku na jamaa anategemea kuja kunipokea saa tatu asubuhi Airport. Aisee nilipiga simu jamaa hapokei alikua amelala. Ikabidi yule Afisa aje kunichukuA akanipeleka kwenye ofisi ya Uhamiaji kwa Boss wao.

Wakati tunaelekea Ofisi za Uhamiaji Mara ghafla nasikia natangazwa kwenye vipaza sauti pale Airport nanukuu;

“Passenger Mr. XXX booked on a flight xxxx to Bangalore please proceed to the gate no 5 immediately for boarding”

Niliitwa pale mara tatu.
Thanks God my panic button huwa iko mbali nikawa nimetulia tu namfuata jamaa mdogo mdogo huku napanga na kupangua kichwani.

Basi tukafika kwa Afisa mkuu pale akaniambia wanachoweza kunisaidia ni kunipa simu ya bure kuwasiliana na huyo rafiki yangu ikishindikana ni kunirudisha nilipotoka.

Ikabidi nitulie kidogo kwanza then nikatumia simu yangu nikampigia jamaa finally after 5 attempts akapokea.

Jamaa akanitumia zile details nikarudi kule migration nikajaza details nikagongewa stamp ya kuingia.

Wakati narudi kule migration kumalizia kujaza zile taarifa Nikamkutana Afisa mwingine kaja kunitafuta kule migration baada ya kuachwa na flight.

Akaanza kunihoji na yeye Basi ikabidi nianze kudefense pale kwamba haikua kosa langu ila flight ilichelewa kufika na kutoka Muscat.

Thanks God nikaeleweka wakanipeleka kuchukua mabegi yangu (Hayakupakiwa kwenye ile flight iliyoniacha) Wakanipeleka kwenye upande wa domestic flight wakanikatia tiketi ya Jet to Bangalore.

Finally nikaingia Bangalore saa 6 mchana badala ya tatu asubuhi.

NB. Inaweza kuwa ni ndefu lakini unaweza kujifunza kitu.
kwa mtu anayesafiri kwa mara ya kwanza ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kubadilisha ndege ili asiachwe?
 
kwa mtu anayesafiri kwa mara ya kwanza ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kubadilisha ndege ili asiachwe?
Zingatia muda ,,,masaa mawili kabla ya boarding uwepo pale airport,
Usiogope kuuliza,,,ukiwapo pale,
Uwe karibu na airline check in point muda wote,,mambo ya kuingia madukani,,Mara shopping achana nayo.
 
hapo sawa.kuhusu mageti inakuaje maana kama uholanzi nasikia kuna uwanja mkubwa sana mara kumi ya wa airport
hapo bongo.wanatoa ramani au kuna mat
angazo
 
From Italy Fiumicino ilikua nipitie Zurich then connection to
Copenhagen.
Bana we njiani bado hatujafika kukawa na mvua ya hatari na wingu kibao
Mmh mi flight ya kuunga ilikua fasta tu pale Zurich. (time zote sijarecord nilikua monde arabe)
Zikaanza info mle kwamba ooh kuna wingu
Zito na mvua hivyo traffic ipo tunaweza chelewa au tukaland ontime.
Duh,
(hapo hata humo ndani ya ndege inabamizwa na mawingu inayumba km daladala la kwa mpalange)
Bwii lote likanitoka mswahili tena nikataka niwaambie nteremsheni nikimbilie ndege ingine.
Wananipoza Sir tulia Sir utawahi.
Ile tumekaribia hapo ndo kabisa delay ikatajwa tena na captain mwenyewe.
Kwamba hamna jinsi hatuendi kutua mpk waruhusu,so tutazugazuga huku juu kusubiri watachotwambia,mawee🙆‍♀️
Sasa itakuwaje?
Mara wakatangaza flani bini flani pita mbele,tulikua km watano hivi tukawekwa front.
Mda si mda Captain akasema sasa funga mkanda tukaland huku kuna tumoir sio ya kawaida.
Tumeshuka fasta kikaletwa kile kibajaj kutupeleka huko gate no ngapi sijui.
Shuka pale fasta panda juu kule mpk nafika check in gate langu.
Nikakuta foleni poa ndo hapa dah kumbe hao wamepiga foleni ni flight ingine aisee.
Nimepiga foleni pale nafika natoa boarding pass yule blonde ananambia this is not your flight sir "ayaa"
Ubishi wetu sasa wamakua,
"But this is gate no 47 to Copenhagen "
Mdada "yes its,but your flight is gone"khaa
Nikaona mi kosa langu nini
Na yule binti anasisitiza "pisha wengine waingie"
Kidogo nimwambie "siendi popote naingia na mimi"
Akaniambia nenda Office ya Swissair watajua la kufanya.
Dah,nikarudi ofisini nimefura nafika "what this,you delay us and now my flight is gone"
Nikajiongeza "im going to miss all my bussiness meeting"🤣🤣🤣
Walikonda
Cool down Sir,which flight you came with:
Nikabwaga document zote pale.
Wakacheck then relax nafkiri ilikua sa nane mchana,then wakaapologise its their mistake na ku recommend kwamba kuna flight yao sa 12
Jioni,nikawaambia poa.
Aah mzee,boarding pass ikatengenezwa chap nikapewa kaja binti pale kaburuta kabegi mpaka bussiness class lounge wakaambiwa wanihudumie chochote mpaka mda wa kuondoka.
Wacha nitie hasara mmakonde.😂
Gonga sana Hennessy mle na vyuku vya kutosha.
Ilibaki kidogo na hiyo ndege ingine iniache.
Wakatangaza abiria ndege no blaha blaha sogea getini.
Mi naona mbona wamewahi bana.
Mwisho nilifika🙂
 
From Italy Fiumicino ilikua nipitie Zurich then connection to
Copenhagen.
Bana we njiani bado hatujafika kukawa na mvua ya hatari na wingu kibao
Mmh mi flight ya kuunga ilikua fasta tu pale Zurich. (time zote sijarecord nilikua monde arabe)
Zikaanza info mle kwamba ooh kuna wingu
Zito na mvua hivyo traffic ipo tunaweza chelewa au tukaland ontime.
Duh,
(hapo hata humo ndani ya ndege inabamizwa na mawingu inayumba km daladala la kwa mpalange)
Bwii lote likanitoka mswahili tena nikataka niwaambie nteremsheni nikimbilie ndege ingine.
Wananipoza Sir tulia Sir utawahi.
Ile tumekaribia hapo ndo kabisa delay ikatajwa tena na captain mwenyewe.
Kwamba hamna jinsi hatuendi kutua mpk waruhusu,so tutazugazuga huku juu kusubiri watachotwambia,mawee
Sasa itakuwaje?
Mara wakatangaza flani bini flani pita mbele,tulikua km watano hivi tukawekwa front.
Mda si mda Captain akasema sasa funga mkanda tukaland huku kuna tumoir sio ya kawaida.
Tumeshuka fasta kikaletwa kile kibajaj kutupeleka huko gate no ngapi sijui.
Shuka pale fasta panda juu kule mpk nafika check in gate langu.
Nikakuta foleni poa ndo hapa dah kumbe hao wamepiga foleni ni flight ingine aisee.
Nimepiga foleni pale nafika natoa boarding pass yule blonde ananambia this is not your flight sir "ayaa"
Ubishi wetu sasa wamakua,
"But this is gate no 47 to Copenhagen "
Mdada "yes its,but your flight is gone"khaa
Nikaona mi kosa langu nini
Na yule binti anasisitiza "pisha wengine waingie"
Kidogo nimwambie "siendi popote naingia na mimi"
Akaniambia nenda Office ya Swissair watajua la kufanya.
Dah,nikarudi ofisini nimefura nafika "what this,you delay us and now my flight is gone"
Nikajiongeza "im going to miss all my bussiness meeting"
Walikonda
Cool down Sir,which flight you came with:
Nikabwaga document zote pale.
Wakacheck then relax nafkiri ilikua sa nane mchana,then wakaapologise its their mistake na ku recommend kwamba kuna flight yao sa 12
Jioni,nikawaambia poa.
Aah mzee,boarding pass ikatengenezwa chap nikapewa kaja binti pale kaburuta kabegi mpaka bussiness class lounge wakaambiwa wanihudumie chochote mpaka mda wa kuondoka.
Wacha nitie hasara mmakonde.
Gonga sana Hennessy mle na vyuku vya kutosha.
Ilibaki kidogo na hiyo ndege ingine iniache.
Wakatangaza abiria ndege no blaha blaha sogea getini.
Mi naona mbona wamewahi bana.
Mwisho nilifika
I am going to miss all my business meetings!! so kutokana na hali ya hewa ulichelewa hiyo ndege kama muda gani?
 
hapo sawa.kuhusu mageti inakuaje maana kama uholanzi nasikia kuna uwanja mkubwa sana mara kumi ya wa airport
hapo bongo.wanatoa ramani au kuna mat
angazo
Cha kuzingatia ni ile boarding pass yako imeandikwa geti namba,,hivyo unafata hadi kwenye geti namba yako ndy utakapo check in..hapo ndipo utakapokuta airline wa ndege yako,,so unapaswa uwe karibu,
Pia airport zipo kubwa nyingi tu,,mfano hiyo Munich airport ni balaa(German)
Zurich airport (uswis) ni hatari.
Alpacino airport ( Rome Italy) ukiwa haupo makini utapotea
 
I am going to miss all my business meetings!! so kutokana na hali ya hewa ulichelewa hiyo ndege kama muda gani?
Haikuwa muda sana but ,nakwambia nafika gate nakuta foleni nikadhani nimewahi kumbe ishatimka washaitisha ingine unajua bussy Airport ni bandika bandua
nafkiri hata runaway ilikua haijafika.
Ingekua Bus ungefukuzia na boda.
10-15 min hivi.
 
kwa mtu anayesafiri kwa mara ya kwanza ni vitu gani vya kuzingatia wakati wa kubadilisha ndege ili asiachwe?

Kwanza kabisa ni usahihi wa documents zako za kusafiria. Hakikisha vitu kama passport, visa na details za unapokwenda zipo sawa.

Pili verify muda wa kutoka kwa ndege yako ni upi maana wakati mwingine hizi PM na AM kama hujacheki vema unaweza kwenda jioni kumbe ndege imetoka alfajiri.

Tatu zingatia check in time, kama inavyoshauriwa masaa mawili au matatu kabla ya safari. Unaweza kufika nusu saa kabla ya safari ukakuta foleni ndefu ya kuchek in ukajikuta umechelewa. Au unaweza kupata katatizo kadogo tu cha kusolve ndani ya nusu saa ila kwa vile ulifika mda umeisha ukajikuta unaachwa.

Lakini nne zingatia sana geti lako unalopandia ndege. Kwa wenzetu viwanja vyao vya ndege ni vikubwa so ukicjanganya hizo geti mpk kulitafuta geti lako unaweza kujikuta umeachwa.

Hayo nadhani ya muhimu kuzingatia. Wadau wengine watajazia
 
Sitasahau. Niliwahi kuachwa na ndege kwa jambo la kijinga na kutokuwa makini, nikalazimika kununua ticket nyingine. Ilikuwa hivi: Ndege inaondoka saa sita na dakika 5 usiku. Kitu ambacho nilisahau ni kuwa ikishafika saa sita na dakika 5, tayari ni siku mpya. Tiketi yangu iliandikwa depurture time ni saa sita na dakika tano, siku ya Jumanne. Kwa hiyo nilitakiwa niende Airport siku ya Jumatatu usiku. Nikafanya kosa la kusubiri ikafika Jumanne jioni saa 3, ndiyo nikaenda Airport, nikitegemea kuwa naondoka usiku huo. Kumbe ikishafika saa 6 usiku, tayari inakuwa imeingia Jumatano.
Hii kidogo inicost Bangkok
 
Mimi nilikuwa nasafiri na bus toka Dar kwenda Kigoma, kufika ubungo saa moja nikaambiwa bus lishaondoka na hawarudishi nauli.

Nikamwambia bibi tayari msala na hatuna ela, bibi akasema hiyo kazi ndogo ila niamini.
Akaniambi funga macho shika sehemu ya siri, usifungue mpaka nikupige tako.

Kweli baada ya dk 7 nikasikia paaaa. Kufunguka macho nipo Kigoma pembeni ya ukuta wa uwanja wa mpira.
Chechezea digitali ya bibi
Hua hamkosekani wadau kama nyie kwenye nyuzi kama hizi watu tunaongelea Copenhagen unaleta story za kibirizi Waha buana
 
Stockholm, Sweden <--> Dar es Salaam, Tanzania

Ilikuwa December 10, 2019 nikisafiri kutoka Stockholm (Arlanda Airport) kuja bongo kupitia Amsterdam kwa kutumia KLM Airlines. Ratiba ya safari ilikuwa nitoke Stockholm saa 12:30 asubuhi (yaani 6:30 am) na kufika Schiphol Airport (Amsterdam) saa 2:40 asubuhi (yaani 8:40 am) na kisha nipande ndege nyingine kutoka Amsterdam saa 4:15 asubuhi (yaani 10:15 am) kuja Dar na ambapo ningefika Julius Nyerere International Airport saa 4:30 usiku (yaani 10:30 pm).

Kilichotokea ni kuwa ndege ya kutoka Stockholm ilichelewa, badala ya kutoka Arlanda saa 12:30 asubuhi tulianza safari saa tano na nusu asubuhi (11:30 am), ambapo muda huo tayari ndege ya kutoka Schiphol airport (Amsterdam) kuja Dar ilikuwa imekwishaondoka na hivyo kuniacha. Bahati nzuri yangu ni kuwa shida ilikuwa kwao na hivyo nilivyofika Amsterdam, walinibukia ndege nyingine (Egypt Air) ambapo nilifanikiwa kufika Dar kesho yake saa 10 alfajili, yaani nilichelewa kufika kwa zaidi ya masaa matano kutoka kwenye ratiba ya awali.

Kutokana na usumbufu huo, nilivyofika Dar nilijaza form kupitia skycop.com (zamani ifdelayed.com), ambao wanahusika na kufuatilia "compesations" za wasafiri wanaopata shida ya usafiri wa ndege wa aina mbalimbali. Bahati yangu nyingine, majuzi kati nimepokea pesa ya Kiswidi 6300 (i.e. SEK 6300). Ticketi yangu ilikuwa ya thamani ya SEK 4200 (ambayo nilikata wakati wa promotion, miezi mitatu kabla ya safari) na hivyo nimepata faida ya SEK 2100.
Lesson learnt.

Nasubiri siku wanicheleweshe
 
Desemba mwaka jana nikisafiri kutoka Durban kuliko Bongo Dsm ! Tiket ilionyesha ndege itaondoka saa moja na nusu asubuhi ! Babati mbaya usiku wa kesho yake safari kwenye Hotel niliyofikia hakukuwa na wifi kwa hyo ilipofika saa kumi usiku ili niondoke kwenda Airport nikakosa namna ya kuita uber bahati mbaya zaidi kila kitu ni self service unapewa funguo za kila kitu na nikipiga simu reception hazipokelwi.....mtu mzima misuli ilisimama ikabidi nikajikaza kiume nikatoka nje na mabegi yqngu nikaanza kuhesabu huku nikaogopa kuporwa (mana wasauzi ni kama wana laana ) ! Mungu saidia nilikuja kupata taxi saa kumi na mbili kasoro mpaka nafika Airport nakuta pipa linapepea ....daaaaah....Kenya Airways wakasema niongoze hela kidogo kama randi 2000 wakanipakia kwenye pipa lingine
 
Cha kuzingatia ni ile boarding pass yako imeandikwa geti namba,,hivyo unafata hadi kwenye geti namba yako ndy utakapo check in..hapo ndipo utakapokuta airline wa ndege yako,,so unapaswa uwe karibu,
Pia airport zipo kubwa nyingi tu,,mfano hiyo Munich airport ni balaa(German)
Zurich airport (uswis) ni hatari.
Alpacino airport ( Rome Italy) ukiwa haupo makini utapotea
so inabidi utembee kwa mguu au kuna usafiri?
 
Haikuwa muda sana but ,nakwambia nafika gate nakuta foleni nikadhani nimewahi kumbe ishatimka washaitisha ingine unajua bussy Airport ni bandika bandua
nafkiri hata runaway ilikua haijafika.
Ingekua Bus ungefukuzia na boda.
10-15 min hivi.
zile jeans zako ngumu za diesel ulinunua wapi?
 
Back
Top Bottom