Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Kuachwa na ndege iwe ugenini au nyumbani huwa ni kielelezo Cha uzembe na poor planning ability ya mtu

Hujawahi kuachwa na ndege ndugu, na labda waliotangulia kuelezea hawajatoa mazingira tofauti tofauti. Sikia hii...
Nilikuwa natoka Ottawa via Montreal to Zurich then Bongo. Hali ya hewa ilikuwa ni winter kali Feb 2015, na kusababisha ndege kuchelewa kuondoka Macdonald-Cartier Intl airport. Tulikaa taxiing lane kama dk 40 hivi then kuruka na safari ya kama 1.30hrs au 2hrs. Ile Kufika Montreal-Dorval airport (au Trudeau kwa sasa) pipa la kuunganisha to Zurich ndio linakula mawingu, kimbembe kikaanzia hapo mzee.
Mfukoni nina $5 tu ya Canada, simu hazikamati mtandao, wenge likanijaa mwanaume. Sema penye matatizo akili nayo huwa inachaji fasta, ikabidi niwafate kwenye meza ya ndege husika. Nikapambana nao kama lisaa hivi mpaka kilipoeleweka na wakanipa na coupon ya $10 kwa ajili ya msosi manake route ikabadilika sasa kupitia Heathrow kisha Addis mpaka Bongoland.
Kwahiyo sio kila kuachwa kunatokana na uzembe na kutokujipanga mapema kisafari
 
Mimi sijawah kuachwa Ila Mara nyingi huwaga nanusuruki kuachwa

Safar ya mwisho ningeaachwa kwa uzembe wa kiwango Cha lami.. Nakumbuka nlikua natoka saudia(pombe hawanyi ni haramu) kuja bongo Ila hakukua na ndege ya moja kwa moja hivyo tukaingia Dubai,. Tukiwa pale airport tunatafuta gate letu lilipo tukaona kisehem wanauza pombe Yani ile kuona tu akili zetu Mimi na mshkaji wangu zilituruka,. Nakumbuka hatukuuliza hata Bei tukaanza kupga mtungi tu mwendo wa Heineken ile tunakuja kustuka lahaula tupo chakali na tumebakiwa na nusu saa tu tusepe halafu gate tulilopo ni kipande Cha kutosha tulihangaika ile siku mixer tunajikaza tusionekane Kam tumelewa Ila all in all 10min before tulikua tushaingolia chombon
 
Mimi nilikuwa nasafiri na bus toka Dar kwenda Kigoma, kufika ubungo saa moja nikaambiwa bus lishaondoka na hawarudishi nauli.

Nikamwambia bibi tayari msala na hatuna ela, bibi akasema hiyo kazi ndogo ila niamini.
Akaniambi funga macho shika sehemu ya siri, usifungue mpaka nikupige tako.

Kweli baada ya dk 7 nikasikia paaaa. Kufunguka macho nipo Kigoma pembeni ya ukuta wa uwanja wa mpira.
Chechezea digitali ya bibi
 
Hujawahi kuachwa na ndege ndugu, na labda waliotangulia kuelezea hawajatoa mazingira tofauti tofauti. Sikia hii...
Nilikuwa natoka Ottawa via Montreal to Zurich then Bongo. Hali ya hewa ilikuwa ni winter kali Feb 2015, na kusababisha ndege kuchelewa kuondoka Macdonald-Cartier Intl airport. Tulikaa taxiing lane kama dk 40 hivi then kuruka na safari ya kama 1.30hrs au 2hrs. Ile Kufika Montreal-Dorval airport (au Trudeau kwa sasa) pipa la kuunganisha to Zurich ndio linakula mawingu, kimbembe kikaanzia hapo mzee.
Mfukoni nina $5 tu ya Canada, simu hazikamati mtandao, wenge likanijaa mwanaume. Sema penye matatizo akili nayo huwa inachaji fasta, ikabidi niwafate kwenye meza ya ndege husika. Nikapambana nao kama lisaa hivi mpaka kilipoeleweka na wakanipa na coupon ya $10 kwa ajili ya msosi manake route ikabadilika sasa kupitia Heathrow kisha Addis mpaka Bongoland.
Kwahiyo sio kila kuachwa kunatokana na uzembe na kutokujipanga mapema kisafari
Hilo sioni Kama lilikuwa ni tatizo lako bali la airline,so ningekuwa Mimi ningedeal na airline/ agent na tatizo lingekuwa solved
 
Upo sahihi kabisa kwa mujibu wa halmashauri ya kichwa chako hapo ndipo ulipofikia
Kama huwezi ukaestimate muda utakaotumia kufika airport na ukafactor in some emergencies unawezaje ukaacha kujiita mzembe? I am a frequent traveler but for the past 10 years nimeachwa Mara moja kwa uzembe.Kuachwa na flight ya kuconnect somewhere kwa sababu za delays za ndege yenyewe huko kwangu Mimi si kuachwa maana ukiwa na akili zako airline will take care of it
 
Hahahaa, enzi tupo primary miaka ya 80, kulikuwa Kuna somo kuhusu uwanja wa ndege, Mwalimu akauliza Nani amewahi kupanda ndege?
Dogo mmoja akawahi kunyanyua mkono Basi darasa zima tukajawa na shauku kumsikiliza.
Mwalimu kwa furaha akampa nafasi atueleze, kwanza Mwalimu akamuuliza swali.., ehee ebu liambie darasa mlikuwa mnatoka wapi kwenda wapi?
Dogo kwa kujiamini akajibu ilikuwa imesimama uwanjani!
Kila mtu Hana mbavu. Duh!

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Dogo alitisha, itakuwa alimaanisha ndege mbayuwayu labda..
 
Nilishawah kuachwa na basi la kwenda songea,natoka zangu mbagala na usafiri wa daladala plus foleni kufika ubungo gari limeshatoka ubungo kama nusu saa imeshapita ikabidi nichukue bodaboda kulifukuzia nakumbuka nililikuta karibia na moro siwez kabisa kusahau
 
Mimi nilikuwa nakwenda Arusha kikazi.. nilikuw na ndege ya Precision Air saa 12 asub. Siku hiyo sijui nini kilifanya nichelewe kulala. Hamadi kuja kustuka asub ni saa moja asub
Kuwapigia Precision wanasema natakiwa kiasi fulani cha pesa kubadilisha ndege ili niondoke na ndege ya mchana.
Nikapiga mahesabu ya kubadilisha ticket na Tax elfu 40 mpaka airport.
Nikapiga mahesabu Tax mpaka Ubungo elfu 7. Bus mpaka Arusha elfu 20 kipindi hiko..
Nikaenda zangu Ubungo kukamata Osaka Coach
 
Sitasahau. Niliwahi kuachwa na ndege kwa jambo la kijinga na kutokuwa makini, nikalazimika kununua ticket nyingine. Ilikuwa hivi: Ndege inaondoka saa sita na dakika 5 usiku. Kitu ambacho nilisahau ni kuwa ikishafika saa sita na dakika 5, tayari ni siku mpya. Tiketi yangu iliandikwa depurture time ni saa sita na dakika tano, siku ya Jumanne. Kwa hiyo nilitakiwa niende Airport siku ya Jumatatu usiku. Nikafanya kosa la kusubiri ikafika Jumanne jioni saa 3, ndiyo nikaenda Airport, nikitegemea kuwa naondoka usiku huo. Kumbe ikishafika saa 6 usiku, tayari inakuwa imeingia Jumatano.
Watu wengi huwa wanaachwa sana.. zile ndege za Alfajiri
 
Kama huwezi ukaestimate muda utakaotumia kufika airport na ukafactoe in some emergencies unawezaje ukaacha kujiita mzembe? I am a frequent traveler but for the past 10 years nimeachwa Mara moja kwa uzembe.Kuachwa na flight ya kuconnect somewhere kwa sababu za delays za ndege yenyewe huko kwangu Mimi ni kuachwa maana ukiwa na akili zako airline will take care

Laiti kama ungesoma ukaelewa vema nilichoandika hizi habari za estimation unazoleta hapa ni irrelevant kabisa.

Anyways the key point hapa ni je ulishawahi kuachwa na ndege na ukafanyaje to resolve the situation. Weather you re a frequent traveller or Not is none of my business.

Ungejikita kueleza ulivyoachwa nadhani ungekua sehemu sahihi na wakati sahihi. Otherwise wewe ni mzembe kama wazembe wengine tu wanaoachwa na ndege.
 
Stockholm, Sweden <--> Dar es Salaam, Tanzania

Ilikuwa December 10, 2019 nikisafiri kutoka Stockholm (Arlanda Airport) kuja bongo kupitia Amsterdam kwa kutumia KLM Airlines. Ratiba ya safari ilikuwa nitoke Stockholm saa 12:30 asubuhi (yaani 6:30 am) na kufika Schiphol Airport (Amsterdam) saa 2:40 asubuhi (yaani 8:40 am) na kisha nipande ndege nyingine kutoka Amsterdam saa 4:15 asubuhi (yaani 10:15 am) kuja Dar na ambapo ningefika Julius Nyerere International Airport saa 4:30 usiku (yaani 10:30 pm).

Kilichotokea ni kuwa ndege ya kutoka Stockholm ilichelewa, badala ya kutoka Arlanda saa 12:30 asubuhi tulianza safari saa tano na nusu asubuhi (11:30 am), ambapo muda huo tayari ndege ya kutoka Schiphol airport (Amsterdam) kuja Dar ilikuwa imekwishaondoka na hivyo kuniacha. Bahati nzuri yangu ni kuwa shida ilikuwa kwao na hivyo nilivyofika Amsterdam, walinibukia ndege nyingine (Egypt Air) ambapo nilifanikiwa kufika Dar kesho yake saa 10 alfajili, yaani nilichelewa kufika kwa zaidi ya masaa matano kutoka kwenye ratiba ya awali.

Kutokana na usumbufu huo, nilivyofika Dar nilijaza form kupitia skycop.com (zamani ifdelayed.com), ambao wanahusika na kufuatilia "compesations" za wasafiri wanaopata shida ya usafiri wa ndege wa aina mbalimbali. Bahati yangu nyingine, majuzi kati nimepokea pesa ya Kiswidi 6300 (i.e. SEK 6300). Ticketi yangu ilikuwa ya thamani ya SEK 4200 (ambayo nilikata wakati wa promotion, miezi mitatu kabla ya safari) na hivyo nimepata faida ya SEK 2100.
 
Stockholm, Sweden Dar es Salaam, Tanzania

That is very interesting mkuu. Sikuwahi kujua hiki kitu ya kujaza form.

What if wakikupa accomodation hadi next day ndipo mkasafiri, still unaweza kujaza hiyo form ya usumbufu??
 
Mimi nilikuwa nakwenda Arusha kikazi.. nilikuw na ndege ya Precision Air saa 12 asub. Siku hiyo sijui nini kilifanya nichelewe kulala. Hamadi kuja kustuka asub ni saa moja asub
Kuwapigia Precision wanasema natakiwa kiasi fulani cha pesa kubadilisha ndege ili niondoke na ndege ya mchana.
Nikapiga mahesabu ya kubadilisha ticket na Tax elfu 40 mpaka airport.
Nikapiga mahesabu Tax mpaka Ubungo elfu 7. Bus mpaka Arusha elfu 20 kipindi hiko..
Nikaenda zangu Ubungo kukamata Osaka Coach

Hahaha mkuu ukaona ni heri nusu shari sio. Anyways ulipiga hesabu zako vema. Ila shukuru Mungu ilikua ni domestic flight laiti kama ingekua ni international flight ungenena kwa lugha tu.
 
Back
Top Bottom