Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Ushawahi kuachwa na ndege ugenini?

Mimi sitasahau Nilivyoachwa na Kiazi Kitamu Express kuelekea kigoma mwisho wa Reli kwa mama Yangu ilikua nmekata tiketi ya kutoka Dar kwenda chuga nikachelewa nikalala daraja mbili wacha Kiazi Kitamu Express kiondoke kiniache nikaenda kukikamatia Dongobesh Karibu na Dareda kwa kina Katarina wa Karatu shabasshhhh!!

Punde Kidgo ntawahadithia story yangu moja Nliokula maindi ya kuchoma na Mtindi kwenye safar yangu ya kuzamia meli kwenda Kwa Malkia nkashushwa bahari ya Pacific kuchimba dawa
 
Daa usinikumbushe ndo ilikuwa first kusafiri na international. Nlikuwa naenda bangarole pia na ndege ya etihad as u know zile ndege lazima itua abudhabi. Nliondoka saa saba hivi mchana na saa mbili usiku ndo tulitua abudhabi nikiunganisha ndege ya saa sita usiku. Basi bwana nikatafuta gate hadi nikapata, nikajua bado nina muda wa kutosha tu acha nianze kuzurura mle ndani. Muda ukakaribia nikaanza kurudi kwenye geti langu. Ebanaeeeeh nikapotea nimekuja kupata gate mi ndo abiria wa mwisho. As u know ule uwanja ni kama kijiji
hamna watu wa kuuliza?
 
Mimi nilishawahi kuachwa na underground train Uingereza ikiwa ni mara yangu ya kwanza kwenda sehemu kutembea na wenyeji, ila nilichelewa kuingia na mlango ukafunga na train ikaondoka na nikabaki peke yangu na sikuwa na ramani mkononi na wala sikujua niko upande gani na nikitoka pale naelekea wapi. Kitu kilichonipa courage though ni kwamba mfukoni nilikuwa na £100. Hivyo, nilifikiria kwamba kama wale wenyeji hawatarudi kunitafuta (nami niliamua nibaki palepale kwa muda) nichukue taxi mpaka college nilipokuwa nimechaguliwa kusoma. Baada ya muda hao wakaja na kunikuta, then this time nilikuwa makini nisiachwe tena.
mzee na huko train mnagombania nini? wenyeji wako walikuwa wazungu nini? hukuwa na simu?
 
Mi nilichanganya muda badala ya saa kumi na moja na nusu alfajiri mimi nikajua kumi na moja jioni. Basi kwa mbwembwe zote na ma video call juu mchumba ananisubiri Nairobi huku akinidorishia kwa marafiki zake my man is coming. Basi nafika precision office kweupee duh nikasema nitakua nimewahi mara kumi na moja duh ngoja niulize. Kwa mbwembwe nikamdaka mdada ana jezi za precision nikamdaka kwa mbwembwe na kumuonesha ticket halahaulaa saa kumi na moja asubuhi. Akaniambia ni top up laki mbili na sabini nikate ya kesho yake. Nikatoka nimwenywea hatari.
safari ikafa
 
Nakumbuka sana usiku wa kuamkia X-mas mwaka 2009, nikiwa Schiphol Airport ama the Netherlands International Airport nikitokea DSM nikielekea Brussels, nilifika asubuhi kama saa mbili za kule. Siku hiyo kulikuwa na theluji kali sana hali ambayo ilisababisha safari kuharishwa mara kwa mara kupitia spika za matangazo kwa wasafiri hasa ambao tuliokuwa "in transit"

Nilikuwa abiria mmojawapo wa KLM, na pia nashukuru kwa huduma zao za kutukuka kwa wateja wao. Nikiwa ktk uchovu mwingi, kwa kuwa nakumbuka tuliondoka DSM yapata saa tano usiku, na siku hiyo nilikuwa na misele mingi kabla ya kuondoka nchini, na nikitegemea nitapiga mbonji la maana ndani ya ndege.

Hali haikuwa kama ambavyo nilitegemea, nilikaa Schiphol toka saa mbili asubuhi mpaka saa tatu usiku, ndipo ambapo nilipitiwa usingizi na kulala mazima. Ile nashtuka nakumbuka nilisikia tu neno Brussels, pale pana terminal nyingi sana, ile kufurukuta na kukakaruka kutafuta usaidizi wa kufanya "boarding" ikashindikana hivyo kupelekea kuachwa na ndege husika.

Nashukuru kwa huduma bora za KLM ambapo nilipata usafiri mwingine wa saa saba usiku, huku nikiwa nimebaki na siri nyingi za kuachwa na hatimaye kwenda kufanikiwa kukutana na wenyeji wangu, pale Brussels kwenye semina ya mwezi mmoja.
ulilala kwenye nini unavyosubiri ndege?
 
Nyengine Hearthrow to Dubai Qatar AIRWAYS,
Ilitokea hitilafu gani sikumbuki basi delay kama saa nzima tuko tu ndani mle tumepigwa stop traffic baada ya hiyo hitilafu zikawa zinaruhusiwa zilizokuwa zinaondoka mapemaa so air traffic ikatuhusu thanks to dreamliner 380a,
movie,documentary sijui nini na kilaji safi tu no limit.no bored
Mwisho ikawa pyee tunaondoka,usiku km sa saba hivi dude hilo likapaa

Njiani kama kawa tukapigwa biriani alafu mi nikawa naatwanga tu masanga kule juu sikupendi basi tu safari lazima uende. so huwa napiga mambo njia nzima.
Mara tukaland siku ya pili kama kawaida mi connection to bongo hapo nimejichokea.
Jina likatangazwa fulani bin fulani proceed to door your flight is about to leave,duh
poa nikasogea,simama pale no panic mpaka wafungue mlango.
Ile nashuka tu nikakuta kile kiberenge chao twende twende wahi,aah nilikua slow mpaka basi nimekipanda kikatushusha karibia na gate,naburuta kibegi changu kupanda juu kule namkuta afisa mwingine anakuja sijui muhindi yule au mwarabu siku hiyo alikoma na mimi
Yuko "KIMBIA KIMBIA NDEGE INAKUACHA" huku anabwabwaja na redio call aah wapi nani akimbie.
Nikamwambia nyie ondokeni tu.
Nilitaka waniache tu badae huo tuumizane kwenye fidia,walingoja nikapanda taratibu na kile kimbayuwayu kikaondoka spidi sana.
so wao ndo walichelewa kufungua geti au...
 
hamna watu wa kuuliza?
Wapo boss nliwauliza sana mpaka kupata get number so nikawanaogopa kuuliza tena ila nlichogundua nlikua umbali kama wa mita 100 hadi 70 kutoka getini kwenye ule mzunguko wanguzo kuu. So nlifaot hadi nikalipata
 
Kwa hiyo ambao hatujawahi kupanda ndege uzi huu mrefu hautuhusu? Na ukiwa huko juu kwenye ndege mawingu unayaona kabisa laivu au inakuwaje? Ndege huwa inatikisika au ni kimya tu kama umekaa kwenye kochi homu? Samahani kwa maswali mengi mkuu
Af! inavoonyesha wewe ni mzoefu sana wa safari za anga, kwa maswali haya!111
 
Mkuu hapo tulikua hatujafika kwenye uchumi wa kati. Lakini hata hivyo waungwana bado wanakwea mwewe tu
Pipa hawataki tena, Gogo linaelea angani, mara mwewe dauu wabongo kweli hawana imani
 
wengine huwa tunaachwa tu na ndege za wagombea wakija kuomba kura
 
Mi nilichanganya muda badala ya saa kumi na moja na nusu alfajiri mimi nikajua kumi na moja jioni. Basi kwa mbwembwe zote na ma video call juu mchumba ananisubiri Nairobi huku akinidorishia kwa marafiki zake my man is coming. Basi nafika precision office kweupee duh nikasema nitakua nimewahi mara kumi na moja duh ngoja niulize. Kwa mbwembwe nikamdaka mdada ana jezi za precision nikamdaka kwa mbwembwe na kumuonesha ticket halahaulaa saa kumi na moja asubuhi. Akaniambia ni top up laki mbili na sabini nikate ya kesho yake. Nikatoka nimwenywea hatari.
Ilinitokea hii nliachwa na fastjet nikiwa na familia
 
Mimi sikuachwa na ndege ugenini, bali hapahapa Bongo!

ilikua mwaka 2017 nimepata safari kwenda Germany! tiketi yangu ilikua inaonesha ndege inaondoka saa kumi jioni! (QATAR AIRWAYS). Kutokana na ushamba wangu enzi hizo sikujua kuwa natakiwa kuangalia mara kwa mara my flight schedule ili kama kuna changes za muda niweze kuona.

Kumbe bwana ndege ilibadilisha muda few days kabla ya safari, badala ya saa 10 jioni, ikabadilishwa saa saba mchana, me sikujua hilo.

Basi siku hio nmejipanga safi kwa safari, saa saba kamili niko airport, nafika reception ya qatar nakuta hamna mtu bas nkajitutumua nikadhani me ndio nimewahi wa kwanza kufika🤣🤣.

nikafika kwa ajili ya kufanya check -in! Wakaniuliza unaelekea wapi, nikasema angalieni ticket naelekea Munich - Germany! Shabaaaash wakasema mbona ndege yako ndio inaondoka saa hizi gate wamefunga dakika chache zilizopita! Damn it nliishiwa nguvu! ntaambia nini watu na nlishaaga🤣🤣

Basi wakasema huo uzembe wangu nilipe fine usd 50 wafanye booking ticket ya kesho. Nikasema huo ni izembe wenu kama mli change muda mlipaswa kutoa taarifa kwa wateja wenu, kama mnachukua email na namba zetu na hamtupatii taarifa za changes je nini maana ya customer service?. Tukabishana mpaka akaja boss wao bas wakakubali makosa ni yetu mimi nna kosa kutoangalia my flight na wao wana makosa kutotoa taarifa.

bas wakasema watanipa free accomodation wana schedule ndege ya kesho! basi tukaondoka wakanipeleka serena hotel.. sikuamini macho yangu kwa mara ya kwanza nililala serena hotel sehemu ambayo sikuwahi kuwaza hata katika ndoto.

basi kesho yake wakaja kunichukua saa saba mchana na nikaondoka saa 10 tukapaa mpaka Doha then nika change flight to Munich - Germany. Nikafika saa 12 alfajiri.
Safi
 
Mimi nilikuwa na Safari ya kushuka bondeni kwa madiba.

Hiyo ticket ilikatwa na mtu Mwingine wa kampuni Fulani tulikuwa tunakwenda kusaidiana kazi ya hiyo kampuni yao nikatumiwa tu soft copy ya ticket ,ndege ilikuwa iondoke saa sita na nusu ALFAJIRI nikakutana na huyo ninaesafiri naye siku moja kabla ya Safari akanisisitiza safari ni saa Sita na nusu KESHO, sikutilia maanani kwamba ni kesho ALFAJIRI Au MCHANA na sikuhangaika kuangalia muda kwenye Ticket
emoji3.png
nikajua tu ni KESHO saa 6 na nusu Mchana

Nikalala kuja kuamka kesho asbh saa 12 ili nianze jiandaa kwa Safari ya saa sita na nusu mchana kumbe huo muda Ndege ishafika inakokwenda
emoji3.png
nakutana na missed call Zaidi ya 70 za jamaa ninayesafiri naye na meseji kibao, nikapagawa muda huohuo nikakurupuka nikadaka bodaboda mpaka airport
Mambo yaliisha ila nilitoboa mfuko kweli kweli
Ilinifunza kuwa makini siku zingine
Dah noma
 
Mimi chupuchupu niachwe Copenhagen...ilinigharimu kukodisha taxi toka mji mmoja wa Sweden (vaxjo) hadi Copenhagen...hiyo ilikuwa ni baada ya kuachwa na tren kwa vile nilikuwa busy kuchat
Pole sana mkuu
 
Salute wakuu,

As per title hapo juu, Ulishawahi kuachwa na ndege ugenini? Ilikuaje na Ulifanyaje? Let’s share experience.

Back in 2014 nikiwa chuo mwaka wa pili nchini Oman kwa His Excellency late Sultan Qaboos bin Said (May his soul R.I.P) ndipo niliweka plan za kwenda kumtembelea rafiki yangu mmoja aliekua akisoma Bangalore nchini India.

MIPANGO YA SAFARI
Niliaanza kuplan my trip, kwanza Nikampigia simu swaiba kama ataweza kuni-accomodate for two weeks at his place, As u know accommodations ndio big issue kama hauna mpunga wa kutosha kufikia hotelini huko ng’ambo.

Baada ya kuweka mambo sawa na mshikaji nikaanza mchakato wa kutafuta visa.

Nikatembelea Agency ya India nchini Oman wanaohusika na utoaji wa visa. Nakumbuka ilinigharimu kiasi cha 20 OMR ambazo kwa kipindi hicho zilikua almost sawa na Tsh 97,000/= plus 5 OMR processing fee. Ndani ya siku 7 nikawa nimefanikiwa kupata 3 months visitation visa.

Baada ya kupata visa nikaanza kutafuta the cheapest flight to Bangolore India. Mind u that I was student so nilikua na save from my monthly allowance nilizokuwa nalipwa College kwa ajili ya kujikimu.

Katika kutafuta tafuta huko online nikakutana na Air India ambayo ndio ilikua nafuu kwa wakati huo na ilinigharimu 133 OMR for a round trip.

Baada ya kumaliza ku-book tiketi yangu na kuilipia nikaprint na kuihifadhi na kusubiri siku ya safari ambayo ilikua 01/02/2014.

SIKU YA SAFARI
Hatimaye siku ya safari ikawadia safari ilikua imepangwa kuwa ni saa tano kamili usiku. Mapema kabisa nika-show up Muscat IA two hrs earlier before departure for check in.

Baada ya kufanya taratibu zote za ukaguzi pale Airport tukaingia ndani kusubiri ndege yetu itakayotupeleka mpaka Chennai, India ambapo tungekuwa na two hours za kusubiri na kubadilisha ndege nyingine ambayo ingetufikisha hadi Bangalore.

Kwa bahati mbaya ile ndege ikachelewa kwa zaidi ya saa na nusu kufika pale Muscat IA. Hapa sasa ndipo shida ilipoanzia. Nakumbuka tulianza safari saa 6 na dk 43 usiku badala ya saa 5 kamili usiku.

Wakati tupo angani Air hostess wakawa wanagawa “Incoming Passanger card” au “Arrival card” kwa abiria ambao ni wageni kwa ajili ya kupunguza traffic tutakapofika.

Basi nikajaza ile card isipokua sehemu ya Anuani wapi exactly naenda huko Bangalore. Yani I took it easy as if kama tunapokua kwetu Bongo ukisema naenda TEMEKE bila kusem ni wapi TEMEKE. Mbaya zaidi hata hizo anuani za rafiki yangu sikuwa nazo kwa wakati huo. (Ieleweka hapa anuani namaanisha Mji, eneo ninaloenda ndani ya mji huo na namba ya nyumba anayoishi mwenyeji wangu)

CHENNAI AIRPORT
Tulipofika Chennai ilikua saa 9 na nusu Alfajiri na ilibaki nusu saa tuu ya kuingia kwenye ndege yangu ya pili ambayo ilikua inaelekea Bangalore.

Niliposhuka nikamkabidhi Afisa mmojawapo ile kadi yangu niliyoijaza. Alipo ikagua akakuta sehemu ya anuani sijajaza. Hapo balaa likaanza.

Akaanza kuniuliza naelekea wapi namwambia Bangalore; Anaanza kuniambia Bangalore ni kubwa wapi exactly unapoenda aisee sipajui, ikabidi aombe passport yangu kucheki kama nimetimia au nimekuja kimagumashi.
Akakagua akakuta nipo sawa, akaanza kunidai address halafu mimi siijui. Akanionesha sehemu ya kupigia simu akaniambia nimpigie rafiki yangu anitumie address alipo.

Kumbuka hapo ni usiku na jamaa anategemea kuja kunipokea saa tatu asubuhi Airport. Aisee nilipiga simu jamaa hapokei alikua amelala. Ikabidi yule Afisa aje kunichukuA akanipeleka kwenye ofisi ya Uhamiaji kwa Boss wao.

Wakati tunaelekea Ofisi za Uhamiaji Mara ghafla nasikia natangazwa kwenye vipaza sauti pale Airport nanukuu;

“Passenger Mr. XXX booked on a flight xxxx to Bangalore please proceed to the gate no 5 immediately for boarding”

Niliitwa pale mara tatu.
Thanks God my panic button huwa iko mbali nikawa nimetulia tu namfuata jamaa mdogo mdogo huku napanga na kupangua kichwani.

Basi tukafika kwa Afisa mkuu pale akaniambia wanachoweza kunisaidia ni kunipa simu ya bure kuwasiliana na huyo rafiki yangu ikishindikana ni kunirudisha nilipotoka.

Ikabidi nitulie kidogo kwanza then nikatumia simu yangu nikampigia jamaa finally after 5 attempts akapokea.

Jamaa akanitumia zile details nikarudi kule migration nikajaza details nikagongewa stamp ya kuingia.

Wakati narudi kule migration kumalizia kujaza zile taarifa Nikamkutana Afisa mwingine kaja kunitafuta kule migration baada ya kuachwa na flight.

Akaanza kunihoji na yeye Basi ikabidi nianze kudefense pale kwamba haikua kosa langu ila flight ilichelewa kufika na kutoka Muscat.

Thanks God nikaeleweka wakanipeleka kuchukua mabegi yangu (Hayakupakiwa kwenye ile flight iliyoniacha) Wakanipeleka kwenye upande wa domestic flight wakanikatia tiketi ya Jet to Bangalore.

Finally nikaingia Bangalore saa 6 mchana badala ya tatu asubuhi.

NB. Inaweza kuwa ni ndefu lakini unaweza kujifunza kitu.
Kuna rafiki yangu ni Mchungaji ilitokea sintofahamu akajikuta ndege aliyomo imetua sehemu maandishi yanaanzia kulia kuelekea kushoto.....salaaaleh!....hii story nitaileta hapa one day iwapo ataniruhusu.
 
Back
Top Bottom