Mimi nilikuwa na Safari ya kushuka bondeni kwa madiba.
Hiyo ticket ilikatwa na mtu Mwingine wa kampuni Fulani tulikuwa tunakwenda kusaidiana kazi ya hiyo kampuni yao nikatumiwa tu soft copy ya ticket ,ndege ilikuwa iondoke saa sita na nusu ALFAJIRI nikakutana na huyo ninaesafiri naye siku moja kabla ya Safari akanisisitiza safari ni saa Sita na nusu KESHO, sikutilia maanani kwamba ni kesho ALFAJIRI Au MCHANA na sikuhangaika kuangalia muda kwenye Ticket
nikajua tu ni KESHO saa 6 na nusu Mchana
Nikalala kuja kuamka kesho asbh saa 12 ili nianze jiandaa kwa Safari ya saa sita na nusu mchana kumbe huo muda Ndege ishafika inakokwenda
nakutana na missed call Zaidi ya 70 za jamaa ninayesafiri naye na meseji kibao, nikapagawa muda huohuo nikakurupuka nikadaka bodaboda mpaka airport
Mambo yaliisha ila nilitoboa mfuko kweli kweli
Ilinifunza kuwa makini siku zingine