Hebu twende taratibu Mpwa
- Una miaka 34 na kidogo
- Ndoa yako ina miaka 8 sasa
- Unafanya kazi
- Wife anafanya kazi (?)
- Mmejaaliwa watoto wazuri wawili toka kwa MUNGU
- "Umepoteza hamu na Mpenzi wako"
Haya tuanze moja baada ya jingine taratibu kabisa
Umri unaonyesha kuwa ulioa ukiwa na miaka 26-27, kwa uzoefu wa kidunia ya sasa (msisitizo uko kwenye dunia ya sasa) vijana wengi katika umri huo bado huongozwa na tamaa, sio wote ila walio wengi. Ni umri ambao ungeutumia vyema kujijenga kiakili na kupata exposure ya baadhi ya mambo ya dunia na mambo ya mbingu pia. Je katika umri huo wakati unaoa mkeo alikua na umri gani? 22? Umri huenda isiwe tatizo sana, hivyo hebu tuuache maana umri huenda sio ishu but maturity na exposure.
Umri wa ndoa yako ni miaka nane (8) ambapo ndio muda huu una experience hayo mambo ya "kujifanya kumchoka" dada wa mwenzio. Kwa utafiti mkubwa uliopo na kwa kuthibitisha kangu mimi mwenyewe, hichi ndichi kipindi ambacho ndoa nyingi sana hukumbwa na matatizo ya namna hio, hili (pengine) huenda likachangiwa na mambo mawaili au matatu; Moja, Mama huhamishia mapenzi kwa watoto Zaidi ya Baba, au Baba hupata majukumu mengi Zaidi kuanzia kazini, nyumbani na maisha kwa ujumla na hivyo kupoteza concentration ya ndoa, na jingine pia ni kwamba sasa kila mtu anaanza kuonekana uhalisia wake halisi sasa, sio ule uhalisiia wa maigizo, yaani yule
Elli wa ndani sasa ndio anajitokeza, la mwisho katika hili pia huenda ikawa ni kule either kuijtoa ukaribu wako na MUNGU wako au kujisogeza kwa MUNGU Zaidi na ukayaacha ya familia. Hebu tufanye kama vile hili nalo si muhimu
Wakati mwingine (not always) baadhi ya kazi zetu hututenga sana na familia zetu kisaikolojia na kutufanya kuwa na "ulimwengu" tofauti na ulimwengu wa familia yako, yaani uko home lakini akili yako yote iko kwenye kazi, unawaza hili au unawaza lile hadi kuna kuccha, hili huweza kutokea kwa mkeo na kwako pia, lichunguze na badilisha mfumo wa utendaji kazi wenu
Je una kampani gani? Je marafiki hao wameoa wana familia je huchukuliaje suala la ndoa na mapenzi? Nini mitizamo yao juu ya ndoa, familia na mapenzi kwa ujumla? Jichunguze, hao nao wamechangia sana kwa baadhi ya ndoa na familia kuharibika.
Asikudanganye mtu eti umuache mkeo, imagine ni dada yako ndio anaacha na mtu, kisha ana watoto wako wa damu yako, imagine Mama yako angeachwa na Baba yako, asikudanganye mtu mapenzi ya mzazi mmoja yanawaumiza watoto sana kuliko tunavyoweza kudhani, kwanini ukubali kuharibu furaha ya watoto wako kwajili ya kutimiza matamanio yako ya mwili tu tena ya muda kwani uitese familia yako kwajili tu ya kutaka kujiona unaridhika? Hio selfishness itakuja kukugharimu.
Usikubali mtu aje kukulelea wanao ilihali wewe upo, usikubali wanao walelewe na Mama wa kambo ilihali mama wa watoto wako yupo, you will one day pay for that when it is too late. Ushauri wangu wa mwisho, ulishasikia watu wanasema tunaishi kama Kaka na Dada? unaelewa maana yake? Jifunze toka kwao, nakusihi sana sana usimuache mke wako uliepewa na MUNGU na zawadi nzuri ya watoto. hebu tizama video hii hapa chini, mimi ilinigusa sana nikabadilika, hope na wewe itakubalisha pia...