Ushauri wenu juu ya siri hii inayonitesa kwa muda mrefu

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,486
2,000
Natumai hamjambo wakuu.

Miaka 7 iliyopita nili-date na binamu yangu, bahati mbaya alipata ujauzito nikamtaka autoe akakataa katakata. Nilimtaka autoe sababu mila zetu haziruhusu mahusiano ya kimapenzi na binamu, nyumbani aliwaambia aliyempa mimba ni mtu wa mbali ambaye walikutana shule na hawana mawasiliano tena.

Baada ya kukataa kuitoa ilibidi tufanye kiapo cha kutunza siri ili tusije leta ugomvi katika familia, alipojifungua mtoto alifanana na mimi kila kitu, wazazi wake wakaamua kumpa jina langu eti kafanana na mjomba ake.

Mila zetu zinasema ukilala na mtoto wa shangazi/mjomba ni sawa na kulala na shangazi/mjomba wako, na hapa ndo panaleta ugumu wa suluhu wa hii siri ya muda mrefu.

Wakuu nawaombeni kwa busara zenu mchangie mawazo ambayo huenda yakazaa suluhu ya jambo hili kwa hekima bila kuleta mtafaruku kifamilia.
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,486
2,000
Kwanza hongera kwa kulala na binamu yako,pili endeleeni kuitunza iyo Siri ,tatu leeni mtoto wenu vizuri,nne pole itakuja kubumburuka tu jiandae kisaikolojia tano
ni kweli inaweza bumburuka ndo maana nikahitaji ushauri utakaoleta suluhu bila kuivuruga familia
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,059
2,000
ushauri unaohitajika ni wa jinsi ya kuitoboa siri bila kuleta mtafaruku kifamilia
Angalia haya mazingira je,ukiitoa hiyo siri itakuwaje..??
Pima kwanza situation na hiyo ndo itaamua utoe au ukaenayo siri husika!..
Sasa we kalipue bomu ambalo hujui kuwa litaathiri umbali gani hapo ndo utajua ule usemi "Mwana kulitaka mwana kulipata!!" Inamaana gani
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,486
2,000
Angalia haya mazingira je,ukiitoa hiyo siri itakuwaje..??
Pima kwanza situation na hiyo ndo itaamua utoe au ukaenayo siri husika!..
Sasa we kalipue bomu ambalo hujui kuwa litaathiri umbali gani hapo ndo utajua ule usemi "Mwana kulitaka mwana kulipata!!" Inamaana gani
mkuu siri hii inamkosesha mambo mengi mtoto bt mazingira ya kuitoa nayo ni magum hata nikawa nataka niwatafute wazee wenye busara niwatume bt bado nipo mashakani nikiwaza je wasipoelewa wazee itakuwaje.
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
4,486
2,000
Kama mmeweza kutunza hiyo kwa muda wote huo na bahati nzuri naye kawa mwaminifu kama mlivyoapiana sasa wewe unataka kugeuka kiapo ili iweje kama sio kujitakia stress za kijinga.
mkuu mpaka leo mtoto anajua baba yake yupo mbali na hili ndo linaniumiza sana, nimejaribu kumwambia binadam tutafute suluhu ananiambia kama unaweza tafuta ufumbuzi ndo maana nahitajia mawazo yenu huenda nikasaidika mkuu
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
7,016
2,000
mila zetu zinasema ukilala na mtoto wa shangazi/mjomba ni sawa na kulala na shangazi/mjomba wako,


Hizo ni mila potofu zilizopitwa na wakati, kuendelea kuzishika katika zama hizi za dunia kupanuka kielimu (elimu za dini na kijamii) ni ujinga.

Iweje "unapotembea" na binamu yako eti ni sawa na kutembea na shangazi au mjomba wako?!!!-- hayo ni matusi makavu.

Wewe kwanza pingana na hiyo mila ya hivyo, pili eleza ukweli kwani ukweli utakuweka huru na jaribu kutafuta suluhu za kimila zilizokuwa "sahihi" na zinazoingia akilini juu ya jambo hilo ambalo ni irrevisible, mtoto kishazaliwa na atahitaji haki zote kutoka kwa baba sasa ni hadi lini jambo hilo liwe siri??!!!--- hadi Yesu atakaposhuka!!!, asiposhuka jee??!🤣
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom