Ushauri wenu juu ya siri hii inayonitesa kwa muda mrefu

Mkuu tunza iyo siri aisee, endapo ikijulikana huyo mtoto akiwa mkubwa akijua itamuaribu kiasaikolojia... Vumilia tu lea mtoto kisiri.
 
Mkuu yuzazifu ni wakati wakutumbua jipu hilo bila kujali maumivu yake maana maumivu hayo ndo yatakufanya upone. Ukiendelea kuficha hatujui ya kesho huenda ukafa au mama yake akafa hapo atakae baki hatoeleweka hata akiongea ukweli.

Sasa fanya hivi. Katika Familia kila family member huwa ana mtu anaemsikiliza sana na kufata kauli zake. Sasa anza research ya kila mkubwa wa ukoo/familia nani anaemsikiliza. Tafuta mtu wa karibu wa Mjomba, mtu wa karibu wa baba/MAMA, mtu wa karibu wa shangazi au viongozi wa dini wenye busara nenda kaa chini na shekh/mchungaji/Padree mwambie unataka kuungama hii zambi. Ko hao nilowataja ndo watawaiteni kikao cha kuwasuruhisha then utawapigia magoti na kama kuna faini utalipa ( kwa sisi ungetozwa mbuzi/kondoo) then kuanzia apo utakuwa huru.

Usiishi na zambi kwa kuhofia kusemwa vibaya we tumbua2 na Mungu atakusimamia machungu hayatokua makali kama unavyofikiria.. utakapo kwama nitafte nikupe mbinu zaidi
 
Fanya
Natumai hamjambo wakuu.

Miaka 7 iliyopita nili-date na binamu yangu, bahati mbaya alipata ujauzito nikamtaka autoe akakataa katakata. Nilimtaka autoe sababu mila zetu haziruhusu mahusiano ya kimapenzi na binamu, nyumbani aliwaambia aliyempa mimba ni mtu wa mbali ambaye walikutana shule na hawana mawasiliano tena.

Baada ya kukataa kuitoa ilibidi tufanye kiapo cha kutunza siri ili tusije leta ugomvi katika familia, alipojifungua mtoto alifanana na mimi kila kitu, wazazi wake wakaamua kumpa jina langu eti kafanana na mjomba ake.

Mila zetu zinasema ukilala na mtoto wa shangazi/mjomba ni sawa na kulala na shangazi/mjomba wako, na hapa ndo panaleta ugumu wa suluhu wa hii siri ya muda mrefu.

Wakuu nawaombeni kwa busara zenu mchangie mawazo ambayo huenda yakazaa suluhu ya jambo hili kwa hekima bila kuleta mtafaruku kifamilia.
fanya hivi:) uwe unamlea huyo mtoto ujidai kuwa sababu ni kufanana nawe na baba yake hajulikani. Jamii itakuelewa kuwa umefanya jambo zuri la kujitoa mhanga. Toka hapo ni mtoto wako kiaina. Hili uwahusishe huyo dada na familia yote. Watakubali kwani hakuna atakayekuwa na shaka kuwa mtoto si wako.
 
Natumai hamjambo wakuu.

Miaka 7 iliyopita nili-date na binamu yangu, bahati mbaya alipata ujauzito nikamtaka autoe akakataa katakata. Nilimtaka autoe sababu mila zetu haziruhusu mahusiano ya kimapenzi na binamu, nyumbani aliwaambia aliyempa mimba ni mtu wa mbali ambaye walikutana shule na hawana mawasiliano tena.

Baada ya kukataa kuitoa ilibidi tufanye kiapo cha kutunza siri ili tusije leta ugomvi katika familia, alipojifungua mtoto alifanana na mimi kila kitu, wazazi wake wakaamua kumpa jina langu eti kafanana na mjomba ake.

Mila zetu zinasema ukilala na mtoto wa shangazi/mjomba ni sawa na kulala na shangazi/mjomba wako, na hapa ndo panaleta ugumu wa suluhu wa hii siri ya muda mrefu.

Wakuu nawaombeni kwa busara zenu mchangie mawazo ambayo huenda yakazaa suluhu ya jambo hili kwa hekima bila kuleta mtafaruku kifamilia.
Lea
 
Baba yangu mdogo alipeleka shauri kama lako kanisani akafunga ñdoa kwa faida ya watoto hivyo hata ww huyo ñi halali yako
 
Back
Top Bottom