Mimi si mwanachama na mchanguaji sana huku MMU, lakini hata bubu aking'atwa ataongea hata neno.
Huku kuna walimwengu wa maisha halisi ya kibantu.
Hadithi ni ndefu lakini nitaifupisha.
Nina mke na watoto, tena wakubwa tu.
Katika mishe mishe za safari mikoani huko, sitaji mkoa lakini nilikaa mwaka.
Hili na lile katika kuchapa ripoti za kazi tukaelewana sana dada mmoja, kwa kweli alikuwa mzuri na ni figure 8.
Kwa utani tu nikatongoza, hakujibu wala kukataa.
Bado nikaendelea kutongoza, mwisho baada ya miezi 3, akakakubali na akasema nikuambie kitu?
Nikastuka kidogo, ila akaniambia nitakuambia tukionana.
Kweli tukaenda outing, na tukala na kunywa.
Kwa kweli tuli enjoy.
Fukuto langu lilikuwa kujua anachotaka kuniambia.
Na wakati huo alivyo mzuri na umbo la kutia hamasa, moyo unanidunda ndi.. ndi..ndi...!
Nikamsihi aniambie.
Akaanza taratibu.
Kaka mimi nimeolewa.
Moyo wangu ukadondoka pwaa....!
Sasa itakuwaje tena kumpenda mke wa mtu?
Nikamwuliza na kujiuliza, na nikaanza kusononeka.
Yule dada aliona kusononeka kwangu, lakini akanituliza, akaniambia usijali kaka.
Akaniambia amenichunguza sana muda wote huu licha ya kuolewa, na amenipenda ndio maana ana kitu cha kunieleza.
Ha!
Nikajiuliza , kuna kingine tena ?
Nikamwuliza kuna kitu gani?
Yule dada kwa unyonge akasema nitakuwa pamoja na wewe ila nifichie siri yetu!
Nikamwambia mbona hilo si tatizo mpenzi!
Akanidakia tena, akaniambia tukisex hataki condom!
Hapo nikapigwa butwaa!
Sasa nami nikadakia, mbona sielewi?
Nikamwambia si utapata mimba?
Huku nikijzuia kumwambia magonjwa je?
Hapo ndii akanieleza taratibu, kuwa ameoana na mume wake miaka miwili na hajapata mimba.
Ikabidi waende hospitali wapimwe na ikagundulika mume wake hana uwezo wa kutengeneza mbegu za kiume.
Na kwamba wameenda hospitali tatu tofauti, majibu ni yale yale.
Akaniambia ,nami natafuta mtoto, nimekupenda.
Nilichanganyikiwa!
END OF PART I
Wadau ushauri wenu, part zingine NNE zitakuja mbele.