Ushauri wenu, dunia naona mviringo!

Heri wewe dunia unaona mviringo na hivyo ndivyo ilivyo,sisi je tunaoiona pembe tatu tusemeje..?

Ukimla tu huyo mke wa mtu basi utaona dunia inavyokubadilikia na kuwa mstatiri wenye mizingo na vipenyo vimvuli!.
Kweli dunia mviringo.
Jamaa kaanza na muke ya mutu, kamuokoa maisha, huyo bibi bado muke ya mutu.
Muke ana matatizo.
Lakini jamaa aingie mitini.
 
kiufupi umepigwa........


yaani umetumika unatumika na utatumika kutimiza malengo ya mcheps ........


hapo bado mkeo hajajua....


pole sana....
 
ushauriwe nini?

wewe ni reserve wa clara

anajua udhaifu wako ni utupu wake na anaendelea kukutumia kwa faida zake

umeamua kutumika

endelea tu!!!!!!
 
Dah....we bro nashukuru kwa kunielewa.

Nakuelewa ndio maana nakuomba ufanye maamuzi magumu sasa hivi.

Kuna hatari mbili kama sio tatu zinakukabili usipokua makini...

1. Mikosi kwa kumdhulumu huyo mme wa Clara, hii inawezekana ikapelekea biashara zikayumba na kujiletea madhsra yasiyoelezeka. Kumbuka mambo kukuendea vizuri ni neema na baraka, kwa kuwa umeshatenda wema kwa huyo binti, itoshe kuendelea na kulea mtoto, mtunze kama mzazi.

2. Hatari nyingine, najua utacheka na kuona masihara. Unaweza kujikuta unamuoa huyo Clara ndio anakuwa mke wako. Usiniulize mkeo wa sasa ataenda wapi. Na utaona kama jambo la kawaida tu kuoana na Clara.

3. Kuvunjiwa heshima na kupelekea kumpoteza mkeo wa sasa, hiyo itaambatana na mambo yako mengi kuyumba.
Hii ni kama inakua combination ya namba 1 na namba 2.

Tatizo la haya mambo, kadri unavyodhamiria kuacha ndivyo mvutano na sumaku ya kuwaweka karibu na upofu wa mahaba unavyozidi kupendeza.

Itafute movie moja ya kitambo inaitwa Match Point
 
Mke wa mtu anatakiwa anipe papuchi na pesa pia. Yaani nikimpa msimbazi, siku nikihutaji ananipa msimbazi na tembo.

Nimfungulie biashara nilimzaa mimi? Kawa mke wangu?

Itokee tu bahati mbaya nimempa laki halafu niende mbali. Kama nipo hapohapo, nampelekea moto na hiyo hela lazima irudi whether directly or indirectly.

Awe mke wa mtu au mwanamke huru, ewe mwanaume usiwekeze kwa nia ya kuendelea kuwa naye. Wanawake hawana huruma hata siku moja. Unampa pesa anampa mume mwenzio.
 
Hiyo ndo ilikuwa akili yangu, nampiga mimba tena, jamaa alee nitakuja kumchukua mwanangu. Mali ulizompa zitumiwe na wanangu.
 
Dogo kafunga ndoa na mke wa mtu, pana ndoa hapo wakati mke ana mtoto wa mtu?

Tunarudi kulekule, single mother huwa wanapasha viporo na wazazi wenzao
 
Weka wazi mpango wako na evelynSalt
 
Mkuu naona umefanywa jogoo la kuazimwa na umeazimwa kweli kweli...

Tatizo ya jogoo la kuazimwa, itapofika kipindi haliwezi fukuzia mitetea tena huwa linachinjwa na hadithi yake kuishia hapo...

Sasa mkuu, wewe kama jogoo hapo kati ulishachinjwa lakini naona kama wataka kufanya unimaginable kwa kufufuka na kurejea tena enzi...

Ulifanya kosa mara moja, pengine mara mbili au zaidi, haina maana sasa urudie kosa lile lile...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…