Ushauri wangu kwako Rais Magufuli

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,526
17,430
Tangu uingie madarakani kumekuwa na hii teka teka ya watu ambayo imezua taharuki!!

Wewe kama kiongozi unapaswa kuweka sawa na kutufahamisha kuwa hawa watekaji au wahuni ni kina nani na wana malengo gani hasa, kwani kukaa kwako kimya ni kuhalalisha utekaji na kuonyesha hautujali sisi wananchi.

Kama jeshi letu limeshindwa kuwapata watekaji omba msaada nje ya nchi ili haya matukio yakome.

Tangu tumepata uhuru hakuna utawala ambao Watanzania wamesikia na kushuhudia utekaji tekaji kama huu unaoendelea.

Kazi ya baba kiongozi katika familia ni kuhakikisha usalama wa wanafamilia na wewe kama kiongozi hakikisha usalama wa raia wako kwa sababu ndo wanaokulipa mshahara na unawatumikia wao.

Unapokaa kimya raia wanajiuza maswali yafuatayo ambayo sio mazuri:

1. Je kukalia kimya utekaji unaonyesha upo nyuma ya watekaji?

2. Je vyombo vya ulinzi vimeshindwa kuwakamata watekaji? Yaani watekaji ni smart sana kuliko jeshi letu?

3. Je watekaji ni watu wanao shirikiana na jeshi letu?

4. Je utekaji ndo sera mpya ya chama tawala?

5. Au serekali ya awamu hii haiwezi kutekeleza majukumu yake bila kuwepo utekaji?

6. Au serikali ndio mtekaji mkuu wa raia wake na haina njia mbadala ya kujibu hoja za ukosoaji wa sera?

7. Umeamua kuacha utekaji uendelee ili Watanzania wachoke utawala wako ili 2020 usigombee tena kwasababu umechoka kazi ya urais?

Tunaomba ukemee utekaji, Utekaji unazua maswali mengi sana kwa sisi wapiga kura.
 
#Nyumbu bhana ni shida sana nyie wakati wa JK mlianzisha maandamano na mauaji ili kusingizia serikali ionekane mbaya, mkaanzisha ugaidi ukamalizwa Kibiti huko na mahali kwingineko
Sasa mmeanzisha utekaji na mabwana zenu refer to Zitto Kabwe na Uzushi wa kutekwa msaidizi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Nyumbu bhana ni shida sana nyie wakati wa JK mlianzisha maandamano na mauaji ili kusingizia serikali ionekane mbaya, mkaanzisha ugaidi ukamalizwa Kibiti huko na mahali kwingineko
Sasa mmeanzisha utekaji na mabwana zenu refer to Zitto Kabwe na Uzushi wa kutekwa msaidizi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maana hiyo Nyumbu ni werevu kuliko Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom