Ushauri wangu kwa Zuberi Zitto Kabwe

Huyoy hashauriki ana msimamo mkali
Wasukuma wanasema "Kwigwa kwa mbulu, mpaka mininga mguto=Kenge hasikii, mpaka damu zimtoke masikioni" Waswahili wanasema "Asiyefunza na mamaye, hufunza na ulimwengu" Sasa hivi magamba ndo wanamfunza siasa za maji taka zilivyo! Kwa vile magamba rushwa ni sehemu ya maisha yao, wako tayari waji-expose ili wamuaibishe mmoja anaye pinga rushwa!
 
Ni ushauri mzuri ila nahofia Zitto anaweza kujibu kama alivyotueleza wakati tunamdodosa atupe sababu za kupigia chapuo mitambo ya Dowans....

Kwa ufupu Zitto alitueleza kuwa sie ambao tuko nje ya Bunge hatuelewi kitu.....!!

Naamini huu upepo utapita na kumwacha salama hata kama atakuwa amejeruhiwa!!
 
Chadema wanatakiwa wawe na wataalamu wa uongozi maadili na collective responsibility. Lazima waahakikishe kila mbunge atakayesimama na bendera ya chama hata kurupuka pale atakapokuwa anatoa kauli na matendo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakinzana na katiba, mwendo na kanuni za Chama.

Zito ndio ni kati ya wanasiasa ambao wamekisaidia sana chama na wameweza kufanikiwa sana kisiasa ndani na nje ya chadema. Ila ni ukweli usiopingika Zito amesaidia sana kuisambaratisha Chadema na kutamani akiona chama hiki kikubwa cha Upinzani kinapotea. Siamini kabisa kama Zitto ana misimamo kwani mwenye misimamo hayumbi wala habadili kauli zake kila kukicha.

Zito ni nani na kwanini anafanya anavyofanya, sijui ila kwa sasa anatumika kumaliza CDM kwa faida ya CCM, ameamua kufanya kazi solo na ninaamini hawezi na kamwe hatabadilika hiyo ni tabia na haina dawa ni kuishi nayo au kuamua kuachana naye one of the two.

Ni Zito huyu huyu kwenye saga la Dowans wakati chama kina msimamo wa kuikataa mitambo ile akiwa yuko upande wa Chama mara akaibuka yuko upande wa akina Rostam kuhusu ile mitambo.

Ni Zito huyu huyu kama naibu wa kiongozi bungeni wabunge wa chadema waliamua kuisusia hotuba ya JK yeye akakimbia na kali zaidi akaitisha mkutano kuonyesha kwamba yeye hayuko na wabunge wenzake wa Chadema.

Ni Zito huyu huyu wakati viongozi wote na wanachama wako Arusha wanasaka kura za kuongeza mbunge wa CDM mjengoni yeye akatoka na kauli za kuutaka uraisi dar es salaama bila kujali wakati huo ni wakumtafuta mbunge wa Arumeru.

Ni Zitto huyu huyu kwa kauli zake mwenyewe alisema hawezi kugombea ubunge 2010 kwani anakwenda masomoni. Ni zito Huyu huyu ambaye alitaka kuacha Jimbo lake la kigoma kaskazini nakuanza kushop around majimbo.

Ni Zito huyu huyu kwenye kauli zake nyingi anasema wazi hana imani na kiongozi wake mkuu wa chama na hawaheshimu wala hawajali.

Zito ndiye anatumika kwa kiasi kikubwa kuvuruga upinzani na doa hili likiangaliwa kwa undani linaweza kuwa ni mikakati ya kupaka chadema matope ili wapate la kusema. Kama Zito anamisimamo kwanini yote haya yana utata je hii ndio sifa ya mtu mwenye misimamo. Duniani wenye misimamo hawayumbishwi wala hawajali matokeo mabaya au mazuri ya misimamo. Raisi aliyepita wa Marekani G Bush aliishi misimamo yake na hakuogopa matokeo ya misimamo yake, alinukuliwa akisema hapendi wanasiasa kwani wengi ni wanafaki na hawana misimamo dhabiti.

Kinachonifanya ni taharuki ni kwanini Zito hata ahisiwe kwamba kuna uwezekano wa kupokea Rushwa kwanini ??? Msafi huwezi kumhisi kwani usafi wake utakuumbua. Hata huko kwenye janga la kitaifa ambapo rushwa sio adui wa haki (CCM) wako ambao huwezi kuwahusisha na Rushwa hata ukiwataja kila mtu atakuona wa ajabu. Leo Zito katajwa kila mtu anasema inawezekana mara ana mali nyingi mara anatumia mali za mashirika husika mara anawatetea something is very wrong.

Zito ndiye mbunge wa CDM ambaye yuko karibu sana na watawala wa chama tawala pamoja na vyombo vyake vya ulinzi na usalama, tangia ndoa hii imefungwa Zito kajitenga kabisa na chama na anaona Viongozi wote wa CDM hawafai kuwa viongozi. Hili nalisema kwani Kwa kauli yake nimemsikia akiwakandia viongozi wa juu wa chadema.

Madaraka, fedha na tamaa anayo Zito ndio maana anasahau bila chama asingefika hapo alipo, anasahau hao viongozi leo anaowanao hawafai ndio walimsaidia Zito kuwa Zito hawakumwonea wivu wala hawakumtakia ubaya walimlea na wakampa nafasi ya kufanya kazi wakijua wanamlea kijana ili naye siku moja ashike hatamu.

Nilimpenda sana Zito nilimwamini sana ila kwa sasa imani naye imeshuka sana, labda afanye turn around ambayo kwa tabia yake sioni kama anaweza.

Hasira yangu kwa Zito ni kwasababu tulimtegemea sana na alionekana kama nuru ndani ya taifa leo huwezi kumjua Zito ni nani, mwenyewe anasema hanunuliki ila tunaoona tunaona thamani yake na gharama yake. Sio ubaya kama Zito anaona sera na mwendo wa chama haumfai aseme wazi.

NB:
Naomba viongozi wa Chama wasiaangalie tuhuma hizi za rushwa kama rushwa tu waangalie mbali zaidi, kama ni za uongo waangalie kwanini zimezushwa nani kazizusha kwa faida ya nani. Vile vile waangalie mwenendo wa ZIto je unafaida kwa chama au hauna na kama hauna wamwajibishe ili chama kiweze kujengwa na kujengeka. Wako wengi wenye matumaini na imani na chama, tunaomba enyi viongozi mjue ninyi sio mali ya chama wala chama chama sio mali yenu.

Chadema lazima tuwe makini sana na yeyote anayeshutumiwa kwani huanza na shutuma then ukweli. Mimi ukishashutumiwa unapoteza credibility.

Chief Mkwawa
Tusibadilishwe kwa tamaa Zetu.
 
Mkuu wangu binafsi yangu sidhani kabisa kwamba Zitto anasukumwa na tamaa ya Pesa - Hapana.. sio kweli kwa sababu namjua Zitto japo sii kwa saana hivyo. Sii mla rushwa tena nadhani anapiga vita rushwa kuliko watu wengi sana hata ndani ya chama chake mwenyewe hupenda kuhoji matumizi ya chama..Ni mtu safi sana inabidi uwe naye karibu ndio utamjua..

Tatizo la Zitto ni imani yake kwa kuelewa kwamba nchi yetu tajiri sana na hakuna sababu ya watu wake kuwa maskini na kwa ambiton yake anafikiri yeye ataweza kufanya mabadiliko. Lakini njia za mageuzi hayo ndizo zinazo mponza kwa kujishirikisha na sera za CCM iwe ktk makaa ya mawe Mchuchuma, bomba la gas, kesi ya Mhando na Maswi na uwekezaji mwingine nchini. Hii sio kazi yake kama Mpinzani, kazi yake ni kuonyesha sera mbovu zinatumika na ndio maana matumizi mabaya yanafanyika. tatizo lolote ktk uwekezaji wa Tanesco au wizara angeliwakilisha kama hoja ya chama chake au upinzani..

Kila napomsoma Zitto huwa kama vile Chadema ndio ipo madarakani, yaani yeye husisitiza hili ama lile litawezekana kufanyika under his watch..Litafanikiwa vipo kwa kutumia sera za CCM. Na ndio maana mimi husema Zitto sio mwanasiasa bali mtekelezaji mzuri na kazi hiyo ataiweza tu kuifanya kama Chadema wataingia madarakani maana sera zake zinaendana na makusudio yake. Nimesema sana kuhusu UONGOZI, kiongozi bora mwanasiasa lazima awe spiritual, awe innovator ktk what he preach, na sii Pedegee, a good Managing Director au CEO ktk muundo wa Utekelezaji wa sera mbovu iwe economic development, ajira ama client retention.
- Ni hayo tu...

INGAWAJE nakubaliana na wewe kwenye main thread kwa asilima kubwa tu (but not 100%), lakini hapa nakubaliana na wewe kwa 101%++
 
Mkandara Heshima mbele
Mimi nikiwa muumini mzuri wa mageuzi na niliyekubaliana na Zito katika harakati zake siwezi tetea kuhusu uhusika wa mtu yeyote yule kwenye tuhuma za Rushwa. Wote waliopata tuhumiwa watu wao waliwatetewa kwa nguvu zao zote. Hii ilileta madhara pale ilipothibitishwa vinginevyo.

Ninaweza nikawa siamini kweli Zito kala rushwa, ila kinachonipa tabu kwanini atajwe, ahisiwe kwanini hata mtu afikiri anaweza kula Rushwa, nilivyomwamini Zito pamoja kwamba kunamambo mengi huwa hatukubaliani naye sijawahi kufikiri anaweza kula Rushwa wala kutoa. Ila kwa sababu rushwa ni matokeo ya madaraka, tamaa, na uchu wa utajiri lolote linawezekana.

Kazi ya chadema ni kuweka wazi kuwa Rushwa haikubaliki ndani ya chama kipimo kile kile tunachokitumia kwa watawala na viongozi wa serikali ndicho kitumike kwa watuhumiwa wa CDM kama wapo. Huanza na tetesi, shutuma then udhibitisho.

Rushwa imeharibu wengi sana Nyerere alimwamini sana Mkapa hata akaitwa Mr Clean leo unaweza kutumia hilo jina. Kinachoniudhi sana ni kubadilika kwa viongozi wetu kitabia na utendaji.
 
Ili kurally behind CHADEMA liwe jambo la maana kwa Zitto kwanza inabidi vikao vya CHADEMA viendeshwe kidemokrasia na sio kiubabe ubabe wa mwenyekiti na wazee wa chama.
Chama ambacho katiba yake inasema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi lakini ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wengine wanaambiwa wasigombee kwa sababu "they are from nowhere" ukikiendekeza utaishia kuwa tambaa la deki.
 
Ushauri mdogo waraka wa kuusoma mpaka tunasinzia, jee, ungekuwa ushauri mkubwa ingekuwaje?
Dah umesahau mdahalo ulivyokuwa ukimwaga majibu millioni kwa swali dogo tu?.. Ni rahisi sana kumshauri mtu kwa jambo dogo lakini linatakiwa kumwonyesha wapi alipokosea..
 
Mimi wala sioni ni nini wanachogombania. Kama EL alijiuzulu, basi Mizengo, na huyo Muhogo au Mwasi sijui Sungwi na Mhando nao wajiuzulu.
Kwa sababu noma walizofanya ni zile zile.
Zito ni skapegoat, Mkulo alijaribu same tactics.
 
Mkandara Heshima mbele
Mimi nikiwa muumini mzuri wa mageuzi na niliyekubaliana na Zito katika harakati zake siwezi tetea kuhusu uhusika wa mtu yeyote yule kwenye tuhuma za Rushwa. Wote waliopata tuhumiwa watu wao waliwatetewa kwa nguvu zao zote. Hii ilileta madhara pale ilipothibitishwa vinginevyo.

Ninaweza nikawa siamini kweli Zito kala rushwa, ila kinachonipa tabu kwanini atajwe, ahisiwe kwanini hata mtu afikiri anaweza kula Rushwa, nilivyomwamini Zito pamoja kwamba kunamambo mengi huwa hatukubaliani naye sijawahi kufikiri anaweza kula Rushwa wala kutoa. Ila kwa sababu rushwa ni matokeo ya madaraka, tamaa, na uchu wa utajiri lolote linawezekana.

Kazi ya chadema ni kuweka wazi kuwa Rushwa haikubaliki ndani ya chama kipimo kile kile tunachokitumia kwa watawala na viongozi wa serikali ndicho kitumike kwa watuhumiwa wa CDM kama wapo. Huanza na tetesi, shutuma then udhibitisho.

Rushwa imeharibu wengi sana Nyerere alimwamini sana Mkapa hata akaitwa Mr Clean leo unaweza kutumia hilo jina. Kinachoniudhi sana ni kubadilika kwa viongozi wetu kitabia na utendaji.
Zitto hasemwi ovyo ovyo isipokuwa wanajua Zitto ndiye kiungo kikubwa cha pande mbili za mtazamo kitikadi ndani ya Chadema. Navyoamini mimi, ktk swala la Uchaguzi mkuu na utawala -chama cha CCM huchukulia hili kama wako vitani na ndio maana wanasema - Ushindi wa Uchaguzi mkuu utapatikana kwa njia yoyote ile..Na siku zote CCM hutafuta sehemu inayoweza kukiyumbisha chama mbadala cha Upinzani kwa kutafuta their weakest point of entry..Hivyo wakaona mahala ambapo wanaweza penyeza ngome ya Chadema ni Zitto. Ndio maana Zitto alipewa wenyekiti wa kamati ya JK kuhusu madini wakati uleee, Mnyika akaja juu sana kupinga uteuzi ule kinyume cha matakwa ya chama, lakini kwa furaha kubwa Zitto akaingia mzima mzima. Toka pale CCM wakamkamata na kuhakikisha anaambukizwa gonjwa la upinzani wowote ndani ya Chadema dhidi yake ni kwa sababu yeye Muislaam..

I know all these things toka vijiwe vya mujini, tena walimpa Zitto hadi mafaili ya kina Mbowe na viongozi wengine waliopokea rushwa ama kuwa upande wa kina RA na EL kumpitisha JK uchaguzi wa 2005. Vitu vingine vilitungwa kuhakikisha Zitto anaweka mashaka ktk dhamira ya viongozi wake. Na wala sii kosa lake tu, uongozi wa Chadema pia kwa kuelewa hivyo walianza kumtenga, kutomwamini maana mtu yeyote anayefanya kazi na serikali wakati hakuna makubaliano ya Bipartisan ina maana yuko upande wa pili..

Sijui kama unakumbuka Senator Joe Lieberman wa Marekani, huyu alikuwa Presidential material alipokuwa Democratic lakini kutokana na msimamo wake wa ndumila kuwili, alianza kutengwa akajikuta pekee na kila siku hakosekani CCN kwa kashfa na misimamo yake, mwisho ilifikia kuhama chama na leo hii kabakia senator tu ambaye hana mbele wala nyuma..Hivi ndivyo siasa inavyoweza kukujenga ama kukubomoa.

Mambo yote hyanayohusiana na Zitto yametengenezwa na CCM ili wanaCHadema mzidi kukosa matumaini naye na kwa kufanya hivyo mtagawanyika. Zitto ana watu wanaomwamini sana na ambao wanajua fika kwamba ndani ya Chadema kuna mtandao vile vile.. Na tumeyaona mengi hapa JF jinsi Zitto anavyosakamwa na WanaChadema wenyewe. Kuna makundi ndani ya chama na pengine naweza kusema kwamba tunaweka sana matumaini kwa Dr.Slaa wakati ikifika 2015, sidhani kama kiafya na Umri, atakuwa na nguvu kama za jana na leo - simwombei mabaya lakini nasema what if?.....

Let's say kwa hali ambayo haikutegemewa Dr.Slaa hatagombea Urais - Je, tuna chaguo gani jingine -Ni Tundu Lissu? Mbowe? Mnyika? au Prof. Safari?....Na kwa nini jina la Zitto lisiwepo?
Zitto anapakazwa sana kwa malengo na hasa wabunge ambao wanapokea posho ilihali Zitto ndiye sababu ya kukatwa ongezeko..Zitto na Makamba wana maadui wengi tu muhimu ni wao kufahamu makosa yao kama vijana mnaowategemea kesho.
 
kuna program moja niliangalia inaitwa "you are what you eat".... I guess it sums up Zitto conundrum

He has tried too hard to be a philosophical spinner, strong believer of his own pathways and incognito indeed when it comes to his ideology... and everything rounds up on him... unfortunately
 
Hey,its truth....nothing but the truth.....and only truth.i beleave ZITTO has seen and read this.
 
kuna program moja niliangalia inaitwa "you are what you eat".... I guess it sums up Zitto conundrum

He has tried too hard to be a philosophical spinner, strong believer of his own pathways and incognito indeed when it comes to his ideology... and everything rounds up on him... unfortunately
Kamba hizo.
 
Ili kurally behind CHADEMA liwe jambo la maana kwa Zitto kwanza inabidi vikao vya CHADEMA viendeshwe kidemokrasia na sio kiubabe ubabe wa mwenyekiti na wazee wa chama.
Chama ambacho katiba yake inasema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi lakini ikifika wakati wa uchaguzi wagombea wengine wanaambiwa wasigombee kwa sababu "they are from nowhere" ukikiendekeza utaishia kuwa tambaa la deki.

Hakuna ubabe ndani ya chadema kuna taratibu zake. Ni ukweli kabisa ZIto asingeweza kumshinda Mbowe uenyekiti na kwa sasa hawezi kushinda lolote ndani ya Chama. Amekuwa ndumila kuwili mno.

Zitto hasemwi ovyo ovyo isipokuwa wanajua Zitto ndiye kiungo kikubwa cha pande mbili za mtazamo kitikadi ndani ya Chadema. Toka pale CCM wakamkamata na kuhakikisha anaambukizwa gonjwa la upinzani wowote ndani ya Chadema dhidi yake ni kwa sababu yeye Muislaam..

I know all these things toka vijiwe vya mujini, tena walimpa Zitto hadi mafaili ya kina Mbowe na viongozi wengine waliopokea rushwa ama kuwa upande wa kina RA na EL kumpitisha JK uchaguzi wa 2005. Vitu vingine vilitungwa kuhakikisha Zitto anaweka mashaka ktk dhamira ya viongozi wake. Na wala sii kosa lake tu, uongozi wa Chadema pia kwa kuelewa hivyo walianza kumtenga, kutomwamini maana mtu yeyote anayefanya kazi na serikali wakati hakuna makubaliano ya Bipartisan ina maana yuko upande wa pili..

Sijui kama unakumbuka Senator Joe Lieberman wa Marekani, huyu alikuwa Presidential material alipokuwa Democratic lakini kutokana na msimamo wake wa ndumila kuwili, alianza kutengwa akajikuta pekee na kila siku hakosekani CCN kwa kashfa na misimamo yake, mwisho ilifikia kuhama chama na leo hii kabakia senator tu ambaye hana mbele wala nyuma..Hivi ndivyo siasa inavyoweza kukujenga ama kukubomoa.

Let's say kwa hali ambayo haikutegemewa Dr.Slaa hatagombea Urais - Je, tuna chaguo gani jingine -Ni Tundu Lissu? Mbowe? Mnyika? au Prof. Safari?....Na kwa nini jina la Zitto lisiwepo?
Zitto anapakazwa sana kwa malengo na hasa wabunge ambao wanapokea posho ilihali Zitto ndiye sababu ya kukatwa ongezeko..Zitto na Makamba wana maadui wengi tu muhimu ni wao kufahamu makosa yao kama vijana mnaowategemea kesho.

Mkubwa Mkandara
Kwangu mimi sifa kubwa ya kiongozi ni uwezo wake wa kuelewa mambo mitego na kutumia akili kwa kila anachoona, ambiwa, sikia na nukishwa. Kama unayosema ni kweli basi Zito hafai kuwa kiongozi hivi ataweza fitina za nchi tajiri duniani??? Ni nani asiyejua hakuna mtawala anayetaka kuona anatolewa madarakani. Zito kukubali teuzi za JK ni tamaa tu ya madaraka. Huwezi kaa meza moja na adui ukafikiri utatoka salama. Kimsingi tukubaliane Zito ni daraja kubwa la kubomoa CDM akitumiwa na CCM. Kitu pekee CDM watapona ni kuachana naye kama Shibuda. Wakiendelea kumlea kwa sababu zozote zile maneno ya Wasira yatatimie na dalili ndizo hizi. CDM haina tatizo la mgombea wa Uraisi wako wengi sana wenye uwezo kwani Obama alitokea wapi, Uraisi ni team sio mtu mmoja akiingia Zito amnaye anaamini anakili zote kuliko mtu yeyote nchi itasimama hakuna Raisi anaweza kufanya kazi bila ushauri, busara na hekima. Raisi anayeamini ni super man hayupo duniani Zito atakuwa wa kwanza.
 
Kwa haya uliyoandika Mkandara wewe ni mwamba.Umemaliza kila nilichotaka kusema.Niseme tu Zitto anapaswa kujifunza kwa tukio hili.Wanachadema hawamchukii Zitto kama Zitto bali wanachukia tabia yake ambayo wanaona ni ya usaliti.Wanachadema hawako tayari kumvumilia mtu yeyote wanayeona anataka kukwamisha juhudi za kuipeleka CDM Ikulu.Kitendo cha Zitto kuropoka kila mara mambo ya Urais huku wenzake wakiwa wamejichimbia vijijini kuimarisha chama hakika kinakera sana na kinasababisha wengi kuwa na chuki kuu dhidi yake.Yampasa kuiga busara za Mbowe,Dr Slaa,Mnyika,Dr Kitila na wengine.Asipobadilika tena sasa naamini hatakaa abadilike milele.
 
Mjomba, hutaniwi?
[/QUOTE]Si unajua utani wa Simba na Yanga? ni lazima kurudisha majibu wasojua ndio hushikana mashati.
Mkubwa Mkandara
Kwangu mimi sifa kubwa ya kiongozi ni uwezo wake wa kuelewa mambo mitego na kutumia akili kwa kila anachoona, ambiwa, sikia na nukishwa. Kama unayosema ni kweli basi Zito hafai kuwa kiongozi hivi ataweza fitina za nchi tajiri duniani??? Ni nani asiyejua hakuna mtawala anayetaka kuona anatolewa madarakani. Zito kukubali teuzi za JK ni tamaa tu ya madaraka. Huwezi kaa meza moja na adui ukafikiri utatoka salama. Kimsingi tukubaliane Zito ni daraja kubwa la kubomoa CDM akitumiwa na CCM. Kitu pekee CDM watapona ni kuachana naye kama Shibuda. Wakiendelea kumlea kwa sababu zozote zile maneno ya Wasira yatatimie na dalili ndizo hizi. CDM haina tatizo la mgombea wa Uraisi wako wengi sana wenye uwezo kwani Obama alitokea wapi, Uraisi ni team sio mtu mmoja akiingia Zito amnaye anaamini anakili zote kuliko mtu yeyote nchi itasimama hakuna Raisi anaweza kufanya kazi bila ushauri, busara na hekima. Raisi anayeamini ni super man hayupo duniani Zito atakuwa wa kwanza.
Mkwawa hata Nyerere hakuaminika alipoingia CCM na hata mjia alizotumia. Canada kuna mtu anaitwa Harper ambaye ni Prime Minister leo naye hakuaminika..walichokifanya hawa wote ni kuonyesha spritual power zao juu ya kile wanachopigania wakati wote hadi kupata imani za watu.

Sii rahisi kabia kupata bahati kama ya Dr.Slaa na sii watu wote wanakubalika kirahisi hivyo..Labda nikukumbushe tu ya kwamba AbdulWahid Sykea alikubalika muda wote na Nyerere alionekana kibaraka wa wazungu na pengine hakuwa mkweli lakini viongozi ndani ya chama TANU na hasa AbdulWahid na Mwapachu waliweka imani zao kwa Nyerere na wakaunda maadui sana tu.. Mwisho wa yote Nyerere akkiwa na na umri mdogo miaka 35 tu alichukua uenyekiti na baadaye kuwa rais wetu wa kwanza..

Kwa hiyo, sisi wengine tusimhukumu kwa lolote zaidi ya kumpa upendo na kumuonyesha njia yetu sisi kuliko kufanya unafiki wa kumchukia na kumrushia madongo wakatin hajui sababu. Kama viongozi wa chama wana imani naye na wanaheshimu mchango wake he can be who he wonna be..

La muhimu tumetoa donge letu.. I wish I had a chance to sit down with him before all this na siwezi kuumia rohoni wakati najua kabisa Zitto is clean isipokuwa bado hajakomaa kisiasa na anajiamini sana kupita kiasi badala ya yeye kuaminiwa kupita kiasi..
 
The story goes on. Question still remains will Zito learn from this or trash this away? Is still the one fighting for changes or changes have already become history for him? Do we have to bank on him anymore or leave him alone and move on?

The confusions comes from our believe support and future expectation on him, life and growth changes everything on the way. We better pick the road and move on those who fall behind should not hinder our way to economic freedom and true social and democratic independent. Rulers always will be trying to shut or slow down citizen movement for their own benefit, many will use our sound and situation to resemble like us never they are even close just a step to achieve own dreams.The story goes on. Question still remains will Zito learn from this or trash this away? Is still the one fighting for changes or changes have already become history for him? Do we have to bank on him anymore or leave him alone and move on?

The confusions comes from our believe support and future expectation on him, life and growth changes everything on the way. We better pick the road and move on those who fall behind should not hinder our way to economic freedom and true social and democratic independent. Rulers always will be trying to shut or slow down citizen movement for their own benefit, many will use our sound and situation to resemble like us never they are even close just a step to achieve own dreams.
 
Mkwawa hata Nyerere hakuaminika alipoingia CCM na hata mjia alizotumia. Canada kuna mtu anaitwa Harper ambaye ni Prime Minister leo naye hakuaminika..walichokifanya hawa wote ni kuonyesha spritual power zao juu ya kile wanachopigania wakati wote hadi kupata imani za watu.

Sii rahisi kabia kupata bahati kama ya Dr.Slaa na sii watu wote wanakubalika kirahisi hivyo..Labda nikukumbushe tu ya kwamba AbdulWahid Sykea alikubalika muda wote na Nyerere alionekana kibaraka wa wazungu na pengine hakuwa mkweli lakini viongozi ndani ya chama TANU na hasa AbdulWahid na Mwapachu waliweka imani zao kwa Nyerere na wakaunda maadui sana tu.. Mwisho wa yote Nyerere akkiwa na na umri mdogo miaka 35 tu alichukua uenyekiti na baadaye kuwa rais wetu wa kwanza..

Kwa hiyo, sisi wengine tusimhukumu kwa lolote zaidi ya kumpa upendo na kumuonyesha njia yetu sisi kuliko kufanya unafiki wa kumchukia na kumrushia madongo wakatin hajui sababu. Kama viongozi wa chama wana imani naye na wanaheshimu mchango wake he can be who he wonna be..

La muhimu tumetoa donge letu.. I wish I had a chance to sit down with him before all this na siwezi kuumia rohoni wakati najua kabisa Zitto is clean isipokuwa bado hajakomaa kisiasa na anajiamini sana kupita kiasi badala ya yeye kuaminiwa kupita kiasi..

Ndugu yangu Mkandara,

Umesema kuwa Nyerere alipata watu muhimu ndani ya TAA na TANU wakamwamini na kumuuza kwa wenzao, tena kwa gharama kubwa....Je, Zitto anao watu wa namna hiyo ndani ya chama? Na kama hana, anajaribu kuwavuta watu ili wawe upande wake au anawatimulia mbali??

Pamoja na uzuri wa Zitto, makosa ya kiufundi anayoyafanya, ama kwa kujua au kutojua, lazima yatamzuia kufikia malengo yake.

Tatizo kubwa la sisi wanadamu (including Zitto), ni kuhangaika kutafuta wabaya wetu wanaotukwamisha badala ya kujifanyia tathmini sisi wenyewe ili kuona ni kwa kiasi gani tumechangia kujikwamisha!
 
Back
Top Bottom