Maundumula
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 7,553
- 3,070
MSiku zote mwanasiasa na hasa mbunge wa chama cha Upinzani unatakiwa kuwa kinyume cha maamuzi ya sera za chama tawala,
Nakushauri sana mkuu wangu achana na siasa za CCM inapofikia maswala ya kamati yako ya bunge. Kama mbunge wa Upinznai unachotakiwa ni kutafuta makosa ktk sera zao na kuweka wazi ubadhilifu unaofanyika laa sivyo hakuna sababu ya kuwa na upinzani maana sote tunakubaliana na sera za Chama tawala. Kazi yako ni kupinga sera hizo na sio kujaribu kurekebisha utekelezaji wa miradi ndani ya sera mbovu.. Siasa haijengwi hivyo mkuu wangu.!
Mkandara,
Upinzani wa kupinga kila kitu umepitwa na wakati.
Halafu kazi ya kamati sio kukosoa sera za Chama. Hii kamati ya POAC wanachofanya wao ni kama Auditing zaidi kuingia deep na kuainisha makosa ya kiutendaji na kushauri sasa unaposema afanye kazi za POAC kama mwanasiasa wa upinzani hapo sikubaliani na wewe labda useme wapinzani wakatae kabisa hata kuingia kwenye hizo kamati.
Kipindi cha Impeachment ya rais Clinton kule marekani walijitokeza hata wabunge wa Republicans wakaokoa jahazi wakati ilikuwa ni fursa nzuri ya kumtoa Clinton wao wachukue nchi. Siasa haziendi hivyo mazee.