Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Mentor Kama na mimi nataka kufurahia Aiseee haiwezekani kabisa lazima nikufeel kwanza ila kufunika kombe mwanaharamu apite inawezekana....
 
Last edited by a moderator:
Duu Pole sana na matatizo. Waheshimu wanao kama ulivyopewa ushauri na wadau... achana na swala la kuolewa na DB
 
Hahahaha, na mimi nimeshangaa..eti bibie mpaka awaandikie email "kazini" kwa DB ndiyo DB apate ruksa....mh, si mke si mchumba si mama si bibi, ni mtu baki tu aandike barua kazini kuwa "anamtaka haraka"! Haya bana, endeleeni na mjadala wacha mi nikapange zangu mkeka wa leo maana jana nimekula za uso mbili!

Hahahaha chezea mahaba hayo!!!! Pole sana kwa kula za uso........
 
Being a person who is trained at finding flaws and finding answers naomba unisamehe kwa hili..ukitilia maanani ukitaka ushauri kuwa mkweli 100% ili anayeshauri atoe kitu chenye mashiko

Una uhakika toka alipoondoka akatuma hela hapo katikati ambayo uliitumia nusu vilivyo nusu visivyo na mpaka anarudi anakuta hukuitumia kwa kadiri ya makubaliano...dadangu, in all honesty hukutembea na mwanamume? kabisaaaa? Mungu anakuona ujue so sema ukweli

Hiyo hela yenyewe hiyo..hukumhonga mwanamume hata senti? kabisaaa

Because the issues centers around that time (hela kama hukuihonga na kweli uliitumia kutibia na mengineyo haiwezi kumbadilisha namna hii) so nitakomaa na time..what did you do in that specific time duration?
 
Wana jamvi habari za siku tele.
Mimi nimekuwa naingia hapa jamvini kama guest baada ya kuelezwa na rafiki yangu juu ya uwepo wa hili jamvi. Nimekuwa msomaji wa mada mbali mbali ambazo kwa namna moja zimenifunza mengi sana. Leo hii nimeamua kujiunga ili nilete swala langu japo mnishauri manake nimekuwa nalo kwa mdua sasa na sijaweza kuomba ushauri kwa mtu yeyote yule.

Nianze hivi hii ni habari ya kweli na kama ukiona nimekuudhi naomba uniwie radhi lakni sina budi tu kuisema manake muda mwingine mwiba wa kujidunga mwenyewe unahusika.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 39 sasa, nikiwa na watoto wawili na ndoa ya kikristo. Kwa bahati njema sana Mungu alitupa watoto wazuri na wenye afya katika kipindi ambacho sote mie na mume wangu tukiwa chuoni tunasoma. Yeye alikuwa anasoma digree ya 2 na mie nilikuwa nasoma ya kwanza katika fani tofauti.
Maisha yetu japo yalikuwa ya kimaskin lakin tuliishi kwa raha amani na upendo furaha na heshima na yakawa yana afya za rohoni na mwilini pia. Kiukweli mume wangu ni miongoni mwa wanume ambao ni wazuri wana upendo wa kweli, anajali na mtu anayependa zaid familia kuliko kitu kingine chochote.

Mimi kama mama nilijitahd sana kuwa na heshima na kutimiza wajibu wangu kama mama na hata kusaidia katika kuijenga familia kiuchumi.

Miaka 5 iliyopita mume wangu alipata safari ya kwenda masomoni na ukweli nilijitahdi sana kuhakikisha kila kilichotakiwa alikipata ili aende nikiamini kwamba anaenda kwaajili ya manufaa ya famili. Wakati anaondoka nilikuwa ni mjamzito hivyo nilimwambia aende tu mie sina neno. Kwa bahati nzuri mtoto alizaliwa baada ya mwezi toka asafiri na ukweli alifurahi sana. Alipopata likizo alikuja akamkuta tayari mtoto ni mkubwa na alikuwa kama na miezi 11 hivi.

Siku chache kabla ya yeye kurudi tena ulaya tulipata ajali mbaya sana ya gari na familia nzima ilihusika, ingawa majeruhi tulikuwa mimi na mtoto huyu mdogo. Nililazimika kumruhusu mume wangu kurudi shule kwasababu ticket yake ilikuwa hawez kuiahirisha kwa siku nyingi zaid, na nilijitahd sana japo mgonjwa kuhudumia wanangu akiwemo huyu mdogo ambaye alikwua amevunjia mguu.

Hata hivyo maisha yalikwua mazuri na tuliishi kwa mapenzi sana, na kila alipopata likizo alikuja nyumban kutuona.
Sasa tatizo lilianza mwaka juzi kuna hela amabzo alinipa kwaajili ya kujengea mie nikazitumia hazikuwa nyingi sana ila pia zingeweza kufanya jambo kwenye ujenzi hata kama ni dogo, fedha zile sikuzitumia ivyo ila nilizitumia kwa kumtibu mtoto mguu na matumiz ya nyumban, alipokuja akakuta sikuzitumia nilimuelewesha akaelewa maisha yakaendelea.

sikujua kama mume huyu ameweka kinyongo ila alipoondoka sasa toka mwaka 2013 hadi leo hajawah kuwasiliana na mimi wala watoto. Mara ya kwanza nilijua ni utan lkn nikashangaa miezi iankatika simsikii mara akanibock skype, tweeter na kila kitu, mara nikipiga hapokei simu yangu, mara email zangu kablock nikaishiwa nguvu kabisa.

Nikaona isiwe tabu wala sina sababu ya kuanza kuitisha vikao vya ukoo kujadili haya nikaamua sasa kuwa siriazi na watoto wangu wasome, wavae, na waishi maisha mazuri. Mungu bariki nikapata kazi kwenye kampuni moja ya utafiti na ushimbaj wa gesi. Maisha yakaanza kuenda vizuri zaid kwa upande wangu. Ila mume nikawa bado sina mawasiliano naye. Mwaka ukakatika sijampata kwenye mawasiliano mama yake anaongea naye na dada zake lkn mie mkewe hapana niaksema siwez kununiana na wakwe zangu mie kisa yeye nikaachana na hayo mambo.

Huu sasa ni wamaka wa 3 sijamtia machoni ingawa kuna kipindi alikuja Tz akapokelewa na dada yake akakaa siku alizokaa na kurudi huko ulaya kwake mie hata sikuumiza kichwa nikasema watoto wangu ni bora zaid kuliko huyo aliyeko huko so niakjipa moyo maisha yakaendelea.

Niliamuaga kawa na mchepuko ili nipate liwazo lakin pia vikanishinda manake sikupata ambaye tuko compatible nikaona nitulize akili kazini na kwenye malezi ya watoto manake hawa ndio watakao nitoa baadae.

Mwaka 2012 mwezi dec nilipata nafasi ya kwenda SA kwenye makao makuu ya kampuni ninayofanyia kazi, kulikuwa na mkutano wa wadau wakuu wa uchimbaj wa mafuta nagesi dunian nilikutana na watu wengi sana akiwemo Bwana mmoja DB ambaye ni mhadisi wa petroleum. Kama kawaida kwenye mikutano kunakupeana contacts basi na mie nikawa nimepata za watu wengi tuu.

mwaka 2014 june kukafanyika mkutano mwingine Ghana nilipokwenda nikakutana na almost watu wengi niliokutana nao huko SA akiwemo DB hivyo network ikazidi kukomaa katika kazi.

Mwaka huu mwezi jana pakafanyika kongamano la gesi la mafuta lililoandaliwa na ubalozi wa Canada hapa nchini mie nikawa naiwakilisha kampuni nikakutana tena na watu almost wale wale hivyo kibiashara nikawa nina watu wengi zaid kwenye huu upande ambao nawajua sana na tumezoeana.

Jambo la ajabu sna Bwana DB alikuwa ni mtu wangu wa karibu kikazi na yeye huyu tulikuwa tunawasiliana hasa pale ninapokwama kikazi kuomba ushauri nk na amekuwa akinimentor sana kwenye huu upande. japo kuwa tulikwa karibu lakin hatukuwah kupata muda wa kuongea maswala yetu ya kijamii kwa muda wote toka nimfahamu. Alipokuja hapa Tanzania sasa kwa mara ya kwanza akaniomba tutoke dina mie na yeye nikamkubalia.

Kweli kwenye dina tuliongea sasa mambo ya kijamii zaid kuliko ya kazi ndipo aliponieleza mkasa wa maisha wote, na kwamba mkewe ni marehemu, na anayemtoto wa kuasili muafrica wa Ghana, jamaa alifunguka sana na mie nikamwambia ukweli juu ya maisha yangu kwamba niko kwenye hali ya sintofahamu ya ndoa yangu. Basi katika kuongea akaniambia kwamba anapenda basi kama nitaridhia anioe na yuko tayari kuwa na mimi na awe baba mlezi wa watoto wangu. Sikumjibu kwa haraka manake mie sijielewi na naogopa sana kutoa ahadi za uongo. Ila nilimkaribisha nyumban kwangu siku moja kabla hajasafiri kurudi kwao akawaona wanangu na akala chakula cha jion kisha akaondoka kurudi hotelin kwake.

Toka ameondoka DB amekuwa akinitumia salam anachat na mie kila mara kwenye messenger nk, pia amekuwa akiwasalimu watoto na kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kua na mimi. Mie bado sijampa jibu manake sijui hatima yangu, ingawa kutoka kwa dada wa mume wangu nimeambiwa mume wangu kaoa binti huko anaish nae. Nilishtuka sana lakin nikasema maisha ndivyo yalivyo sina ujanja zaid.

Leo asubuhi nimefika tu ofisini DB akanipigia anataka kuja Tanzania kuniona na hapa amenipa email adress ya kampuni anayofanyia kazi niwatumie email kuwaomba wamruhusu aje kuniona na niseme kwamba namuhitaj kwa haraka sana. Nimejikuta napata kigugumizi nimjibuje wapendwa wangu.

Ugumu kwangu unakuja hapa, bado nampenda sana mume wangu ingawa amekosea. Pili kuanza maisha na mtu mwingine mgeni kabisa katika uzee huu najionea kama nitapata shida kwenye kuishi.

Kitu ambacho nakiamini kutoka kwake ameniambia yuko tayari kulea watoto wangu, yeye anachotaka ni kupendwa, kujaliwa na kuheshimiwa tu katika maisha yake yaliyobaki. Yeye ana umri wa miaka 48.
Hongera kwa malezi bora unaowapatia watoto wako, kama mume wako kaoa mke mwingine unasubiri muujiza mwingine wa kurudiana? Chukua hatua
 
ushauri wangu dada yangu baki tz fanya kazi yako somesha watoto endeleleza maendeleo yako binafsi,kimwili date tu na huyo mwanaume ila usiende huko nchini kwake kama hataki sitisha malengo yakuwa nae bali kuwa rafiki ktk kazi,ishawahi mkuta jirani yetu alienda alimfata mwanaume kama ww hivyo kule ilikuwa kuliwa tigo na maisha mabovu mwanaume kamuharibia maisha,mama akili nyako kichwani ungekuwa una miradi tz na watoto wako ni wakubwa ambao wanaweza kujisimamia kimaisha ningekushauri nenda hapo bado unasafari ndefu
 
Mentor; talaka haimzuii mtu kupenda.....

Ila mie sijataka kubase sana kwa huyo DB sijui BD.....long distance relationship ni headache tu....pia hata muda wa kuchunguzqna ni majanga...asije ruka mkojo.....

Ila shida ni huyu dada awe huru na hicho kifungo (hapa sijazungumzia kikatoliki loh)....

Labda itampa courage ya kupeleke moyo wake kwengine....ya kuanza upya na kupenda tena ( ukizingatia alichepuka akachemsha akaamua kikitunza-----kitaliwa na nyenyere buuuuuuuure) vilevile hata ukweni ni kimeo bora apate talaka ili wasimtafutie sababu

kitu haijatumiwa tangu kikwete aingie ikulu kwa mara ya pili unasoma mileage kweli!??

Talaka ndo inamzuia mtu kupenda eti?

hivi nyie wadada, hamuwezi ku-do bila kuhusisha hisia zenu!!????

Ni mara chache kwa mwanamke kudo na mtu bila hisia ( only pale anapokua horny na kumtamani mtu muda mfupi)
 
Last edited by a moderator:
Fanya kwanza uchunguzi kujua kwamba je mmeo kaoa kweli Na km itawezekan jitahdi japo ukafike huko il upate uhakik zaidi. Pia ukiweza kwenda kwa huyo Db kumchunguza pia itapendeza zaidi kuliko kufany maamuzi bila uchunguzi
 
Kula nanasi kwahitaji nafasi hivyo tengeneza kwanza nafasi kwa huyo DB wako kwa kujua ukweli wa yale ambayo unaambiwa kuwa mumeo kaoa huko aliko,ukipata uhakika kuwa sasa ndoa yako imeingiliwa basi huna budi kuweka wazi kwa wazazi na ijulikane kuwa wewe umefanyiwa kitu mbaya na umebwaga manyanga kuliko ilivyo hivi sasa unajifanya kumsubiri mtu ambaye hujui atarudi lini na hujui kama ana mapenzi tena na wewe.
Kwa sasa inawezekana ukasamehewa ukiamua kubanjuka na huyo jamaa maana inawezekana una ukame wa kuhondomola hivyo wakati unafanya mambo ya kujua kama jamaa kamwaga mboga ili wewe umwage ugali.
Zaidi ha hapo pole sana kwa yaliyokukuta ndio changamoto za ndoa zetu kila siku.
 
Duuhh kazi kweli kweli, wakati mwingine WOGA ni Hekima, hebu huyo DB mwombe avute subira kwanza kabla hujaingia mzima mzima, (mechi za kirafiki rukra). KUHUSU NDOA YA KIKRISTO, kama ni RC unaweza kuvunja na ukapewa Talaka. Huyo mumeo ni Kabila gani? Kuna makabila mengine yakiacha mke hata kama ni miaka 10, akirudi anaendelea kuwa mkewe. Kama Kazaa nje wale watoto wa nje "automatic" wanakuwa ni watoto wake na haki zote anazo juu ya watoto.
 
Si yule shosti wako nnaemfanyia crunches za hasira, talk of usefull revenge.

About sponging i never say never. Ila basi tu ngoja nimezee, rudi bwana tukupe BOT uendeshe, bongo tambararez
Shosti gani tena huyo? Halafu unanichokoza halafu unadai eti unatolea mfano tu....dawa yako inachemka.

With me the thing is, I have never ever been a sponger in my life and I don't plan on being one.
 
eti mie nilimuelewa kama vile walianza kuzaa wakiwa chuo na mpaka sasa wanawatt wawili.
lkn unafkiri ni rahisi sana mtu kuish bila kuwa na aliwazo?

Nimejaribu kudokoa dokoa toka katika simulizi...

Wakiwa chuo walikuwa na watoto wazuri...(watoto ina maana ni zaidi ya mmoja ambao ni wawili)

Mwanamama akiwa na umri wa miaka 34 akawa na ujauzito ambaye pia tunaelezwa ni mtoto wa pili...

Ndio maana nikawa-confused na hii simulizi kuhusu idadi halisi ya watoto na majira waliyozaliwa...

Kwa bahati njema sana Mungu alitupa watoto wazuri na wenye afya katika kipindi ambacho sote mie na mume wangu tukiwa chuoni tunasoma.

Miaka 5 iliyopita mume wangu alipata safari ya kwenda masomoni....

Wakati anaondoka nilikuwa ni mjamzito hivyo nilimwambia aende tu mie sina neno....
 
Nitakuwa sijaeleweka kiaandishi ndugu yangu. Sisi tunao watoto wawili na tulianza kuzaa tukiwa chuoni, mpaka sasa ni hao hao wawili. Alipoondoka kwenda masomon aliniacha na ujauzito wa mtoto wa pili ukiwa unakaribia kwenye term

Shaka ondoa hili si la muhimu sana...

Ushauri wangu ni ule ule kama niliotoa pale awali...

Kwa umri ulionao ni vyema ukatulia kulewa wanao badala ya kuanza kuhangaika na wanaume...

Kama ulivyoeleza kuwa una kazi nzuri na watoto wanapata matunzo mazuri, sioni haja ya wewe kuhangaika kutafuta bwana mwingine...

Kitu nikionacho kwako labda umetindikiwa na upweke uliokithiri na umekuwa ukimiss kudinyana, hilo pekee ndio limekuwa likikusukuma kuwa na mwenzi mpya...

Wasiwasi wangu ni kwamba usijekuta badala ya kutatua ukaishia kuimarisha zaidi tatizo kwa kuwa moyo wako ungali umepiga kambi ndani ya moyo wa mumeo...

Rudi nyuma hatua moja, ongea na wazazi wako na mumeo, ongea na viongozi wa kiroho waliofungisha ndoa yenu...

Kama ni kukuacha huyo mumeo akiri mbele ya hao wote, hili litakusaidia wewe kama kweli unataka ku-move on
 
Ok, Mungu hakuumba taasisi ya ndoa iwe ni kifungo cha mateso kwa mtu. Lengo la ndoa ni ili mtu apate faraja kwa ampendaye na tena anayefanana naye iwe ki mawazo, sura,rangi,nia,dini,haiba,taifa nk ili mradi walingane pale wanapofarijiana pia kila mmoja ajisikie fahari kwa kuwa na mwenziwe. Pili pia katika unganiko hilo wapate watoto (wakijaaliwa) na tena bila zinaa(mke halali anayejulikana kwa wazazi pia majirani ndo maana kuna mahali na Harusi kutambulisha jamii).Sasa kuna vitu au matukio matatu muhimu ktk kuhitimisha hayo ingawa nengine si lazima:

Ndoa,Kuoa/kuolewa na Harusi. Ndoa ni viapo kwa mdomo au maandishi kuwa wawili hawa wamekubaliana kwa ridhaa ya kila mmoja bila kulazimishwa wala kudhurutishwa kuwa wameridhiana kuwa pamoja hivyo wanakwenda kwa mtu mwenye mamlaka au wakala wake kuthibitisha na kutia muhuri iwe ni nyumba za Ibada, Bomani au hata kwa chifu kule ujivuni. Baada tu ya ndoa wake wanaingia ktk hali inayoitwa wameoana/ameoa/ameolewa. Kinschofuata ni sherehe ya ndoa ile ambayo inaitwa Harusi. Hakuna harusi kama hakuna ndoa, hakuna harusi kama hakuna wanandoa, ila kunaweza kuwa wanandoa bila harusi wala ndoa rasmi kwa wenye kutia muhuri lkn msingi wake ni ridhaa ya wawili waliopendana kuridhika kuishi pamoja kwa upendo,kufarijiana,kujamiiana,kuuguzana,kufuraiana.

Kama hii ridhaa isipokuwepo kwa wote au hata kwa mmoja hiyo taasisisi ya ndoa kwa dhana ya ndoa haipo! Hivyo si haki wala si mpango wa Mungu mmoja aishi kwa mateso kwa kisingizio eti wslifunga ndoa(ambayo haipo) kanisani! Kwa kuwa wote watakuwa subjected kutenda dhambi kwa mwenzie pia kwa Mungu wake! Ushauri:

tafuta ushahidi wa kuwa kampata mweza anayeendana naye, la huna pata au kusanya vielelexo kuwa kakutelekeza kwa miaka mingi na hata huwa anskuja nchini hakutafuti wala kushiriana nawe halafu uende kwenye mamlaka iliyowafungisha ukadsi haki yako ya ndoa, wape muda wamtafute hata hso dada zske waitwe kusaidia kupatikana, halafu nenda mahakamani kadai talaka hata kama hatakuja, off course watakuambia kaanzie baraza la kata au tarafa/ ustawi badi mwisho wa siku utakuwa na barua ya baraza la usuluhishi na vile hakutaki tena, talaka utapata bila kipingamizi. Usije ukakubali kuingia mkatsba mwingine wa ndoa bila huo uliopo sasa haujavunjwa rasmi. Huyo jamaa ysko mwambie avute subira kidogo mambo yatakuwa shwari. Hakuna kumuwazia au kumuenzi asiye na ridhaa nawe maana, hamfanani!
 
Sawa ndugu lakini sasa je nitaishije mie ukweli upo wakati kabisa natamani na mimi kutimiziwa haja zangu za kimwili. Nimevumilia hadi nimekuwa kama kikongwe manake kila leo mara mgongo, unauma mara akili aikai tu sawa yaani nipo nipo tu sijielewi. Nimejaribu kumtafuta mshauri nasaha anishauri lakin nimegundua kwamba ushauri unafanya kazi na akili zaid lakin sio na vichocheo vya mwili

Mi nashauri endelea na DB kama hawala tu kwa sasa, msifunge ndoa kwanza kwa sasa, hadi uwe huru kisheria. Wakati huo huo tafuta mwanasheria akushauri namna ya kupata talaka yako. Sina uhakika sana lakini nahisi kwa situation yako mahakama inaweza kukupa talaka.

Muache tu DB aje ila jitahidi kujificha watoto wasigundue kitu, nendeni mbali huko hotelini au popote pale mbali. Ila mweleze wazi DB ajue kwanini unasita kuhalalisha kwa sasa, na kwanini ni muhimu watoto wasijue uhusiano wenu kwa sasa. Mweleze tu ataelewa ingawa nahisi si mtanzania so anaweza kuchugulia easy tu kikwao kwao

cc gfsonwin
 
Pole sana dada yangu kwa kadhia iliyokupata, pia nikupongeze kwa uvumilivu wako. Unaweza kuolewa na mtu mwingine lakini baada ya kuwa na uhakika kuwa mmeo kweli kaoa mke mwingine, usiyaamini maneno ya wifi yakouenda jamaa kapigika hata nali hana. Kama utachagua kuolewa na huyo Mghana pia kuna mambo ya kujiuliza na kuyapatia majibu. Kwanza yakupasa uwe na uhakika kama huyo mghana anachokwambia ni kweli maana Waghana nao uongo wanauweza. Nahisi kama hujafunguka vizuri kuna mambo yanayokuhusu umeyaficha, haiwezekani mwanaume atokomee na kukata mawasiliano ghafla.
 
Mkubalie huyo DB na maisha yaendelee. Sababu naamini mtakuwa mnakutana mara chache sababu mnafanyakazi nchi mbili tofauti. Au ukiolewa utaacha kazi na kumfwata huyo DB?
Ila kama moyo wako kweli upo kwa mumeo mwambie jamaa ukweli.kwamba pindi mume akirudisha majeshi nitakuacha na nitaambatana na mume wangu wewe nipe kampani tu kwa kipindi hiki cha upweke ambacho akijulikani hatima yake.
Ila mimi naona hata kama moyoni bado unampenda mumeo jua kwamba yeye hakupendi na maisha yanaenda kwa kupendana pande zote mbili hata akirudi atakusumbua tu. Mkubalie huyo DB jumla jumla maisha yaende.
 
Yaani huyu hajamtia mumewe machoni kwa mwaka wa tatu sasa, huyu mumewe haulizii chochote kuhusu watoto wanaendeleaje, wamekula nini, kuhusu elimu yao kama mama yao ana uwezo wa kuwatunza hajawahi kuleta hata senti moja tangu 2013 n.k. bado kweli anastahili kuitwa mume!? Kuna sheria nyngine za ndoa kwa kweli zimepitwa sana na wakati na zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa sana ili dada kama huyu kama akiamua kuolewa tena basi sheria isimnyime haki yake ya kuolewa tena na mume mtarajiwa ampendaye ambaye ameshaonyesha mapenzi kwake na kwa watoto wake.

Back
Top Bottom