Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Hii idara ya ndoa na mahusiano inaongoza kwa kuwa na figisu figisu nyingi ni idara pasua kichwa mkweli humjui muongo humtambui! ushauri wangu wee fanya unavyoona maana sina ushauri mwingine.
 
Ndoa ya kikristo haivunjwi bibie......Mtafute mumeo kwa njia zozote zile....

Ujio wa huyo mtu ni shetani anataka kuharibu ndoa yako

Uliapa mtakuwa wote katika shida na raha

Hizi ndizo shida zenyewe

Mtafute mumeo...

Kama akikupa talaka hapo muachane...sasahivi huja prove chochote usiwe na huyo mtu katika committment...labda kuchepuka tu
 
Hebu vaa viatu vya huyu dada just for a while uone kama vinakutosha. Mwenzi wako akiondoka akaacha kuwasiliana na wewe kwa miaka kadhaa bado utamuhesabu kama mwenzako?

Hata kama amefanya kosa gani hii sio fair treatment. Wapo wanawake wanachukua vimikopo pride hawafanyii la maana wanashindwa kulipa nyumba zao za kuishi zilizowekwa rehani tena bila mume zinatakapigwa mnada na bado waume zao hawawatelekezi ije iwe kutumia visenti tena kwa ajili ya familia? Ukiniuliza mimi alikuwa anatafuta sababu ya kusepa mazima baada ya kupata chombo kipya na alipopata huo mwanya hakugeuka.

Maamuzi yako Chiomaizwe yaangalia welfare ya watoto wako na kazi yako basi.


Ndoa ya kikristo haivunjwi bibie......Mtafute mumeo kwa njia zozote zile....

Ujio wa huyo mtu ni shetani anataka kuharibu ndoa yako

Uliapa mtakuwa wote katika shida na raha

Hizi ndizo shida zenyewe

Mtafute mumeo...

Kama akikupa talaka hapo muachane...sasahivi huja prove chochote usiwe na huyo mtu katika committment...labda kuchepuka tu
 
Last edited by a moderator:
Hapo kwenye rangi umeongea kitu kikubwa sana ambacho nilitaka kukiweka kwenye post yangu lakini nikakisahau. Kama ataamua kuolewa uwezekano mkubwa mume mtarajiwa anaweza kumtaka ahamie nchini kwake. Kwa maoni yangu asiache kazi yake na kuhamia nchini kwa "mume mtarajiwa" mpaka amepata kazi ambayo akifika tu anaanza. Anaweza kuhamia bila kazi na mume mpya akamwambia huna haja ya kufanya kazi uwe ni mama wa nyumbani tu.

Hebu vaa viatu vya huyu dada just for a while uone kama vinakutosha. Mwenzi wako akiondoka akaacha kuwasiliana na wewe kwa miaka kadhaa bado utamuhesabu kama mwenzako?

Hata kama amefanya kosa gani hii sio fair treatment. Wapo wanawake wanachukua vimikopo pride hawafanyii la maana wanashindwa kulipa nyumba zao za kuishi zilizowekwa rehani tena bila mume zinatakapigwa mnada na bado waume zao hawawatelekezi ije iwe kutumia visenti tena kwa ajili ya familia? Ukiniuliza mimi alikuwa anatafuta sababu ya kusepa mazima baada ya kupata chombo kipya na alipopata huo mwanya hakugeuka.

Maamuzi yako Chiomaizwe yaangalia welfare ya watoto wako na kazi yako basi.
 
Hizi anonymous hazina maana sometimes
jinsi dada alivyo jieleza ni obvious waliotoa ushauri wengine wanamjua kabisa
makampuni ya gesi na semina za SA na Ghana ni network ya watu wanaojuana
na wengine wako humu humu...
si ajabu hata mumewe wanajua kamuoa nani huko na ana watoto wangapi....
 
Mytake:

Nimesoma maelezo yako nimepata mashaka mengi kidogo

1. Hii ni stori ya upande mmoja na umejaribu kujifagilia zaidi kuwa umekuwa mwema siku zote, natamani kusikia stori ya mumeo naye anasemaje

2. Sijaona popote ambako umejitahidi kufahamu ni kwanini mume wako amekutenga baada ya matumizi ya pesa kinyume na makubaliano

3. Inaonyesha umekuwa na matendo yasiyoridhisha kwa mumeo hasa kwenye matumizi ya pesa ila hapa hujawa mkweli ila umewatumia wanao kama kinga

4. Inaonyesha hauna mahusiano mazuri na wakwe zako na mawifi zako na ndio maana hukuona haja ya kushirikiana nao kujua kwanini mumeo kakususa.

5. Kuhusu huyu DB sitaki kukushauri chochote lakini kama ulishatoka naye sioni kwanini leo unaomba ushauri hapa ila tahadhari angalia sana kuolewa na foreigner usiyemfahamu vizuri unaweza kuja kujuta na kuwajutisha wanao.

Mokoyo...
 
Da pole sana dada yangu, wakati ulionao ni mgumu sana na ni rahisi sana ktk hali kama hiyo kufanya maamuzi ya haraka bila kufikiria. Najua unahitaji upendo pia as human being, ila nakushauri sana kama hujamfahamu DB vizuri tulia na pata nafasi ya kumfahamu. Pia piga goti zungumza na Mungu atakupa jibu sahihi juu ya mzigo ulionao.

Zaidi mmeo ni mmeo tu mlishaweka agano hivyo muombee halafu Mungu atakufungulia mambo usiyoyajua, pia kumbuka umekaa muda mrefu bila mwanaume hivyo usione shida kukaa walau mwaka umsome huyo DB na kumuomba Mungu.
 
Pole sister! Ww umekosea kuchukua maneno ya wifi yako alivyokwambia et kaka ake kaoa ukakubaliana naye ni
 
you have made a very crucial point Tamalisa
Da pole sana dada yangu, wakati ulionao ni mgumu sana na ni rahisi sana ktk hali kama hiyo kufanya maamuzi ya haraka bila kufikiria. Najua unahitaji upendo pia as human being, ila nakushauri sana kama hujamfahamu DB vizuri tulia na pata nafasi ya kumfahamu. Pia piga goti zungumza na Mungu atakupa jibu sahihi juu ya mzigo ulionao.

Zaidi mmeo ni mmeo tu mlishaweka agano hivyo muombee halafu Mungu atakufungulia mambo usiyoyajua, pia kumbuka umekaa muda mrefu bila mwanaume hivyo usione shida kukaa walau mwaka umsome huyo DB na kumuomba Mungu.
 
Last edited by a moderator:
pole xana,miaka 3 ni mingi sana kupoteza mawacliano na umpendaye tena ktk ulimwengu huu wa kidigital,halafu ndoa za kikristo hazivunjwi dada angu,labda huyo jamaa umfanye kama mchep......!otherwise mme halali akirudsha moyo na kutambua kuwa alifanya kosa inaweza kukuletea shida.
 
Wa kwa mume wamekwambia kaoa

Alikuja hapo mjini na wanajua kuwa hakukutafuta na hata kuwapanga wafanye aone wanae hata kama haupo

Sasa wewe bado unapenda nini? Unataka arudi akuue uache watoto wenyewe?

Mwambie DB ukweli wa kinachoendelea una bahati kuwa kweli haujaonana kimwili na mumeo kwa miaka mingi...mtihani kwake new mr ni itakuwaje ukimuona sura kwa sura je utajipendekeza kwa mumeo?

Hapo sasa ni uamuzi wako..
Natumaini umemtumia hiyo e-mail inaelekea anakuwaza sana...ila ukipata mgeni lazima utaarifu hata ndugu zako wajue...usikaribishe mgeni tena wa mbali bila kuwaambia....na bado hakikisha analala hotelini

Na wewe huyo mume anakuchezea so kaombe talaka haraka sana maana anakudharau nduguye kukuamboa kaoa ulaya alipo, hiyo ni umepewa kwaheri ila tabu ipo kwa umpendavyo.

Haya tumia kinga pia na huyo mpya.

Usipige ubalozini labda atakuwa sio mtanzania na utamwaribia alichofanya na itakuwa tatizo kwako...mwache na maisha yake. Omba Mubgu akuongoze
 
Pole sana dada maisha haya ama lweli binadamu tunapitia mengi sana pole sana kwanza uliumia sana 3 years no mawasiliano lazma upasue kichwa pole sana
 
yawezekana hyo ndo rizk yako ila kabla ya kuchkua maamuz n vzur kushriksha familiia yke kuepusha migogoro baadae kwako na kwa watoto pia
 
Wana jamvi habari za siku tele,

Mimi nimekuwa naingia hapa jamvini kama guest baada ya kuelezwa na rafiki yangu juu ya uwepo wa hili jamvi. Nimekuwa msomaji wa mada mbali mbali ambazo kwa namna moja zimenifunza mengi sana.

Leo hii nimeamua kujiunga ili nilete swala langu japo mnishauri manake nimekuwa nalo kwa mdua sasa na sijaweza kuomba ushauri kwa mtu yeyote yule.Nianze hivi hii ni habari ya kweli na kama ukiona nimekuudhi naomba uniwie radhi lakni sina budi tu kuisema manake muda mwingine mwiba wa kujidunga mwenyewe unahusika.

Mimi ni mwanamke mwenye miaka 39 sasa, nikiwa na watoto wawili na ndoa ya kikristo. Kwa bahati njema sana Mungu alitupa watoto wazuri na wenye afya katika kipindi ambacho sote mie na mume wangu tukiwa chuoni tunasoma. Yeye alikuwa anasoma digree ya 2 na mie nilikuwa nasoma ya kwanza katika fani tofauti.

Maisha yetu japo yalikuwa ya kimaskin lakin tuliishi kwa raha amani na upendo furaha na heshima na yakawa yana afya za rohoni na mwilini pia. Kiukweli mume wangu ni miongoni mwa wanume ambao ni wazuri wana upendo wa kweli, anajali na mtu anayependa zaid familia kuliko kitu kingine chochote.

Mimi kama mama nilijitahd sana kuwa na heshima na kutimiza wajibu wangu kama mama na hata kusaidia katika kuijenga familia kiuchumi.Miaka 5 iliyopita mume wangu alipata safari ya kwenda masomoni na ukweli nilijitahdi sana kuhakikisha kila kilichotakiwa alikipata ili aende nikiamini kwamba anaenda kwaajili ya manufaa ya famili. Wakati anaondoka nilikuwa ni mjamzito hivyo nilimwambia aende tu mie sina neno.

Kwa bahati nzuri mtoto alizaliwa baada ya mwezi toka asafiri na ukweli alifurahi sana. Alipopata likizo alikuja akamkuta tayari mtoto ni mkubwa na alikuwa kama na miezi 11 hivi. Siku chache kabla ya yeye kurudi tena ulaya tulipata ajali mbaya sana ya gari na familia nzima ilihusika, ingawa majeruhi tulikuwa mimi na mtoto huyu mdogo.

Nililazimika kumruhusu mume wangu kurudi shule kwasababu ticket yake ilikuwa hawez kuiahirisha kwa siku nyingi zaid, na nilijitahd sana japo mgonjwa kuhudumia wanangu akiwemo huyu mdogo ambaye alikwua amevunjia mguu.Hata hivyo maisha yalikwua mazuri na tuliishi kwa mapenzi sana, na kila alipopata likizo alikuja nyumban kutuona.

Sasa tatizo lilianza mwaka juzi kuna hela amabzo alinipa kwaajili ya kujengea mie nikazitumia hazikuwa nyingi sana ila pia zingeweza kufanya jambo kwenye ujenzi hata kama ni dogo, fedha zile sikuzitumia ivyo ila nilizitumia kwa kumtibu mtoto mguu na matumiz ya nyumban, alipokuja akakuta sikuzitumia nilimuelewesha akaelewa maisha yakaendelea.

Sikujua kama mume huyu ameweka kinyongo ila alipoondoka sasa toka mwaka 2013 hadi leo hajawah kuwasiliana na mimi wala watoto. Mara ya kwanza nilijua ni utan lkn nikashangaa miezi iankatika simsikii mara akanibock skype, tweeter na kila kitu, mara nikipiga hapokei simu yangu, mara email zangu kablock nikaishiwa nguvu kabisa.

Nikaona isiwe tabu wala sina sababu ya kuanza kuitisha vikao vya ukoo kujadili haya nikaamua sasa kuwa siriazi na watoto wangu wasome, wavae, na waishi maisha mazuri. Mungu bariki nikapata kazi kwenye kampuni moja ya utafiti na ushimbaj wa gesi.

Maisha yakaanza kuenda vizuri zaid kwa upande wangu. Ila mume nikawa bado sina mawasiliano naye. Mwaka ukakatika sijampata kwenye mawasiliano mama yake anaongea naye na dada zake lkn mie mkewe hapana niaksema siwez kununiana na wakwe zangu mie kisa yeye nikaachana na hayo mambo.

Huu sasa ni wamaka wa 3 sijamtia machoni ingawa kuna kipindi alikuja Tz akapokelewa na dada yake akakaa siku alizokaa na kurudi huko ulaya kwake mie hata sikuumiza kichwa nikasema watoto wangu ni bora zaid kuliko huyo aliyeko huko so niakjipa moyo maisha yakaendelea.Niliamuaga kawa na mchepuko ili nipate liwazo lakin pia vikanishinda manake sikupata ambaye tuko compatible nikaona nitulize akili kazini na kwenye malezi ya watoto manake hawa ndio watakao nitoa baadae.

Mwaka 2012 mwezi dec nilipata nafasi ya kwenda SA kwenye makao makuu ya kampuni ninayofanyia kazi, kulikuwa na mkutano wa wadau wakuu wa uchimbaj wa mafuta nagesi dunian nilikutana na watu wengi sana akiwemo Bwana mmoja DB ambaye ni mhadisi wa petroleum. Kama kawaida kwenye mikutano kunakupeana contacts basi na mie nikawa nimepata za watu wengi tuu.

Mwaka 2014 june kukafanyika mkutano mwingine Ghana nilipokwenda nikakutana na almost watu wengi niliokutana nao huko SA akiwemo DB hivyo network ikazidi kukomaa katika kazi. Mwaka huu mwezi jana pakafanyika kongamano la gesi la mafuta lililoandaliwa na ubalozi wa Canada hapa nchini mie nikawa naiwakilisha kampuni nikakutana tena na watu almost wale wale hivyo kibiashara nikawa nina watu wengi zaid kwenye huu upande ambao nawajua sana na tumezoeana.

Jambo la ajabu sna Bwana DB alikuwa ni mtu wangu wa karibu kikazi na yeye huyu tulikuwa tunawasiliana hasa pale ninapokwama kikazi kuomba ushauri nk na amekuwa akinimentor sana kwenye huu upande. japo kuwa tulikwa karibu lakin hatukuwah kupata muda wa kuongea maswala yetu ya kijamii kwa muda wote toka nimfahamu. Alipokuja hapa Tanzania sasa kwa mara ya kwanza akaniomba tutoke dina mie na yeye nikamkubalia.

Kweli kwenye dina tuliongea sasa mambo ya kijamii zaid kuliko ya kazi ndipo aliponieleza mkasa wa maisha wote, na kwamba mkewe ni marehemu, na anayemtoto wa kuasili muafrica wa Ghana, jamaa alifunguka sana na mie nikamwambia ukweli juu ya maisha yangu kwamba niko kwenye hali ya sintofahamu ya ndoa yangu.

Basi katika kuongea akaniambia kwamba anapenda basi kama nitaridhia anioe na yuko tayari kuwa na mimi na awe baba mlezi wa watoto wangu. Sikumjibu kwa haraka manake mie sijielewi na naogopa sana kutoa ahadi za uongo. Ila nilimkaribisha nyumban kwangu siku moja kabla hajasafiri kurudi kwao akawaona wanangu na akala chakula cha jion kisha akaondoka kurudi hotelin kwake.

Toka ameondoka DB amekuwa akinitumia salam anachat na mie kila mara kwenye messenger nk, pia amekuwa akiwasalimu watoto na kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kua na mimi. Mie bado sijampa jibu manake sijui hatima yangu, ingawa kutoka kwa dada wa mume wangu nimeambiwa mume wangu kaoa binti huko anaish nae. Nilishtuka sana lakin nikasema maisha ndivyo yalivyo sina ujanja zaid.

Leo asubuhi nimefika tu ofisini DB akanipigia anataka kuja Tanzania kuniona na hapa amenipa email adress ya kampuni anayofanyia kazi niwatumie email kuwaomba wamruhusu aje kuniona na niseme kwamba namuhitaj kwa haraka sana. Nimejikuta napata kigugumizi nimjibuje wapendwa wangu.

Ugumu kwangu unakuja hapa, bado nampenda sana mume wangu ingawa amekosea. Pili kuanza maisha na mtu mwingine mgeni kabisa katika uzee huu najionea kama nitapata shida kwenye kuishi.Kitu ambacho nakiamini kutoka kwake ameniambia yuko tayari kulea watoto wangu, yeye anachotaka ni kupendwa, kujaliwa na kuheshimiwa tu katika maisha yake yaliyobaki. Yeye ana umri wa miaka 48.
BiDada unastahili sifa, nastahili Reward kubwa kwa kutunza familia na kuwasomeasha wanao!! HONGERA... Una bahati kuwa DB kaniwahi mie, angelichelewa mie nilikuwa second runner !! Anyhow wasiliana na wakwe (wifi/mkwe) wamlazimishe huyo Bwana (mpuuzi) akupe divorce/talaka!! Bila kuwaambia utaolewa...!! Nami nakusihi umkubalie DB haraka na mjulishe unamaliza paper work zako.!!

Ninaamini utaishi maisha mapya na kufunguwa ukurasa mpya !! you are still young usijizeeshe bure !! Maisha matamu kwani umesha Play "role yako vizuri" Good luck and be blessed !!
 
Back
Top Bottom