Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Ushauri wako ni muhimu zaidi kwangu

Haya maisha jaman...changamoto ni nyingi...kwa uelewa wangu dada swala la kuolewa futilia mbali kabisa....lea watoto na tumikia kazi kwa moyo...Acha kaz iwe mume wako .....!mwombe tu mungu uendelee kuwa na moyo wako huo wa kupenda kaz na watoto...ndo mtazamo wangu hui
 
hivi gfsonwin na BADILI TABIA, Mtu miaka 3+ hakuna barua wala nini halafu eti asijicommit hadi ajue hatma? Kama uko na ndoa hamna mawasiliano, umekuwa blocked kwa maneno na matendo, na mtu amerudi hadi mtaa wa tatu hana habari na wanae wala wewe. Halafu ati unaendelea kumpenda? Unampenda nini hapo kwa mfano?
Sasa hebu niambie nitawambiaje wanangu endapo nitajicommit kwa mtu mwingine?
Wanangu ni wakubwa kiasi cha kujua ishu zinaendaje, na hapa nilipo nalazimika kumpenda tu nikiwa na imani kwamba atarudi.
Nimekuja kujikuta niliachwa na 34 leo hii nina 40 tayari bado ndoa yangu ni ya makaratasi tuu lakin ndani haipo
 
Sasa iyo L.M.A hairuhusu na mie ninavyo vyeti vya ndoa hapa nilipo manake hakuondoka navyo lakin je nitasaidika vipi ikiwa ndo amesha zamia huko na huyo mwanamke mwingine? Natamani arudi nyumban hata leo.
DB ukweli japo ndo ivyo sijampa msimamo wangu lakin ukweli amekuwa akinishauri vingi sana na hasa juu ya hatma ya hii ndoa yangu manake yeye amesema kama kaoa basi na wewe nikuoe kwakua hatuna haja ya watoto wengine tulepo maisha basi.

Ugumu kwangu mpendwa wangu unakuja kwa wanangu, ivi ninaanzaje kuwaambia kwamba nimeachana na baba yao na sasa watalelewa na baba mwingine?

Nimesoma vyema maelezo yako samahani ntakuita "dada Chiomaizwe" nimeona bado unampenda Mumeo hata kama kakutenda na kuhusu hilo jambo nadhani tulia kwanza usiharakishe maamuzi may be yataku cost at last..? Mueleze DB that you need time to think about it..!? Najua L.M.A hairuhusu but jee inaruhusu Kutelekezwa thats it..? Tuachane na hayo cha muhimu Kuwa mvumilivu mambo mazuri hayana haraka Chiomaizwe
 
Haya maisha jaman...changamoto ni nyingi...kwa uelewa wangu dada swala la kuolewa futilia mbali kabisa....lea watoto na tumikia kazi kwa moyo...Acha kaz iwe mume wako .....!mwombe tu mungu uendelee kuwa na moyo wako huo wa kupenda kaz na watoto...ndo mtazamo wangu hui
Sawa ndugu lakini sasa je nitaishije mie ukweli upo wakati kabisa natamani na mimi kutimiziwa haja zangu za kimwili. Nimevumilia hadi nimekuwa kama kikongwe manake kila leo mara mgongo, unauma mara akili aikai tu sawa yaani nipo nipo tu sijielewi. Nimejaribu kumtafuta mshauri nasaha anishauri lakin nimegundua kwamba ushauri unafanya kazi na akili zaid lakin sio na vichocheo vya mwili
 
Sasa iyo L.M.A hairuhusu na mie ninavyo vyeti vya ndoa hapa nilipo manake hakuondoka navyo lakin je nitasaidika vipi ikiwa ndo amesha zamia huko na huyo mwanamke mwingine? Natamani arudi nyumban hata leo.
DB ukweli japo ndo ivyo sijampa msimamo wangu lakin ukweli amekuwa akinishauri vingi sana na hasa juu ya hatma ya hii ndoa yangu manake yeye amesema kama kaoa basi na wewe nikuoe kwakua hatuna haja ya watoto wengine tulepo maisha basi.

Ugumu kwangu mpendwa wangu unakuja kwa wanangu, ivi ninaanzaje kuwaambia kwamba nimeachana na baba yao na sasa watalelewa na baba mwingine?

Sio bure nenda kaombewe kwanza utoke hilo fungo alilokufunga
Miaka 5 bila mawasiliano na wewe wala watoto unajinadi una mume?
 
Nimesoma vyema maelezo yako samahani ntakuita "dada Chiomaizwe" nimeona bado unampenda Mumeo hata kama kakutenda na kuhusu hilo jambo nadhani tulia kwanza usiharakishe maamuzi may be yataku cost at last..? Mueleze DB that you need time to think about it..!? Najua L.M.A hairuhusu but jee inaruhusu Kutelekezwa thats it..? Tuachane na hayo cha muhimu Kuwa mvumilivu mambo mazuri hayana haraka Chiomaizwe
Ukweli ni kwamba nina mpenda kwasabbu sina jinsi. Hii inatokana na ukweli kwamba sitaki kuwaumiza wanangu kwa mimi kuwa mbinafsi. Lakin kwasasa hapa ninategwa zaidi na huyu DB
 
Sio bure nenda kaombewe kwanza utoke hilo fungo alilokufunga
Miaka 5 bila mawasiliano na wewe wala watoto unajinadi una mume?
Kwani ndugu yangu kinachosababisha ndoa isiwepo ni kukosekana mawasiliano peke yake?
Mie mpaka sasa nasema ninandoa manake tayari nilishaapa hasa ndoa za kikristo hazinaga kuvunjika.
 
Nakushauri umtafte mtumishi wa Mungu unayemwamini ili uongee nae. Watumishi ni wawakilishi wa Mungu na wamepewa hekima na Mungu kwa njiapanda kama hizi, kama we ni mkiristo lakini.

Umevumilia miaka mitatu inatosha kabisa kukupa nguvu ya kuendelea kuvumilia.

Nakuhakikishia, chozi la mwanamke linanguvu sana kama akisimama kuwa mwaminifu siku zote. Ila ukijichanganya shetani atapata nafasi ya kukuongezea mateso. For ua children sake, endelea kusubiri. Najua mmeo ipo siku atarudi kwa machozi na kulia, na hiyo ndio itakuwa funzo kubwa kwa wanao juu ya ujasiri ulouonyesha.

Pole sana, Yesu akutane na haja ya moyo wako utakaposoma.
 
Mmmhhh!!!

Hivi miaka 39, watoto wawili, kazi nzuri lakini bado tu wataka kuolewa mara ya pili???

Halafu kuna mahali kama umetumiksi hivi, ukiwa chuo mlipata watoto wawili wewe na mumeo...halafu mbele ya stori tena mumeo akiwa anaondoka ukawa na ujauzito wa mtoto wa pili...sasa sijui stori hii yote itakuwa na viuongo uongo vya kihivyo!!!
 
Mh, hivi kumbe kuna kampuni ambazo kuomba ruhusa anakuombea mtu mwingine asiye kazini?!...mh:tape2:
 
Mmmmmmmmmmmmh! KUNA APPROACH 2 HAPO!

1. KATE MIDLETON APPROACH! Hii ilimlipa sanaa Kate, hii unatuliza mpapa tuliiiiiiiiiiiii kama unanyolewa vuzi mpaka hio siku isio na jinaaa atakaporudi huyo mume. Believe atarudi even fter 10 years. Mungu anajibu japo kwa kuchelewa mda mwingine lakini anajibuuu. Akirudi hio siku iso na jina na kukuta umekituliza mambo byeeeeeeeeeeee! Akikuta umekitembeza ana ghairi. Kate aliachana na prince akakituliza tuliiii, wenzie wanaolewa miaka ishirini na ngapi huko yeye anafukuza upepo wa prince tu, siku iso na jina ikafika bwanaa. Angtia tamaa kujichulia looser si ingekula kwake?

2. MTAANI UNTD! Hii unakuwa a woman of double faces. Huku kwa wanao kujua unajitia kuendelea kumngoja mumeo kwa unyonge, huku kwa bwana BD mnakandamiza mavituz kama kawaidaaaaaaaa. Kwa raha zenu. Unacheza ligi international! Dubai, South, Nairobi hivo yani. Unapata kitu roho inapenda huku unafukia tracks zako. Siku iso na jina ikifika kama sio yule uliejiachia na boloyanki la DB! Hahahaaaaaa! HII NI WIN WIN! Ila usiwe mzembe tu, na uwe na roho ya korosho hubby akirudi unamuangalia usoni kama sio yule ulieshika mic ya DB! Hahahaaaaaaaaaaa!
sikutegemea kucheka aisee mchana wa leo.
naamin huyu mdada hapa kajifunza jambo.
lakin turudi tu mbele yaani wee mwenzio unao uhakika kabaisa kaoa af wewe unajivundika ili siku akirudi akukute kweli iko fair?
mie kwakweli kama DB wake yuko tayari hadi kuja kwa mujibu wa maneno yake amwache aje waoane kisheria kabisaa akale zake bata maisha mafupi haya bhanaa
 
Mmmhhh!!!

Hivi miaka 39, watoto wawili, kazi nzuri lakini bado tu wataka kuolewa mara ya pili???

Halafu kuna mahali kama umetumiksi hivi, ukiwa chuo mlipata watoto wawili wewe na mumeo...halafu mbele ya stori tena mumeo akiwa anaondoka ukawa na ujauzito wa mtoto wa pili...sasa sijui stori hii yote itakuwa na viuongo uongo vya kihivyo!!!
eti mie nilimuelewa kama vile walianza kuzaa wakiwa chuo na mpaka sasa wanawatt wawili.
lkn unafkiri ni rahisi sana mtu kuish bila kuwa na aliwazo?
 
Kwanza nikupe pole kwa yote uliyoyapitia na hongera kwa kuipigania familia yako ubarikiwe sana.

Kwangu mm naona unahitaji muda juu ya kufanya uamuzi ni kweli hubby wako kaondoka na mpaka sasa huna taarifa Naye na una kila sababu ya kusema Mr DB is right for you lakini nani ajuaye moyo wa mwanadam.

Kwanza tafuta kujua hatima ya ndoa yako kadri uwezavyo kwa njia yoyote ile, iwe kupitia ndugu zake au rafiki zake hata kwa kumsikia mwenyewe yy hubby akisema jambo juu yako, lakini kuwa makini usidhihirishe adhma yako kwamba yupo MTU.

Pili nakuona ni fear God woman lia na Mungu wako akupe hekima ya kudil na hili jambo, omba hata viongozi wa kiroho unaowaamin wakusaidie kwa maomb na ushaur.

Tatu unesema bado unampenda sana mumeo ina maana hata ukijiforce kwa DB itakuwa kazi bure, najua upendo wa kweli hubadilisha mambo, na hii inakutesa kwa sababu hujamskia hubby mwnyw akikuambia kwamba hakutaki tena, inahitajika hekima katika hili.

Kuhusu safar ya DB km huna amani juu ya hilo usiiaprove, mpe sbb nzuri tu ambayo itamfanya akuelewe bila kuumiza moyo wake.

Jipe muda, Mungu akupe hekima itokayo kwake jinsi ya kukabiliana na hili jambo
 
Sawa ndugu lakini sasa je nitaishije mie ukweli upo wakati kabisa natamani na mimi kutimiziwa haja zangu za kimwili. Nimevumilia hadi nimekuwa kama kikongwe manake kila leo mara mgongo, unauma mara akili aikai tu sawa yaani nipo nipo tu sijielewi. Nimejaribu kumtafuta mshauri nasaha anishauri lakin nimegundua kwamba ushauri unafanya kazi na akili zaid lakin sio na vichocheo vya mwili

Yaan hapo ni kwel kwenye swala na mahitaji ya mwili ni changamoto kubwa pia...!Embu jaribu kufanya mambo taratibu kidogo...!I can imagine hali yako jamani ....Kama ni uvumilivu mungu akuzidishie zaid ili mazuri yanye na neema.POLE MNOO...Naamin kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata taarifa zote za mumeo ili kujua maisha yake ya huko nje...Tumia muda kidogo unaoupata ili upate ukweli...ujiridhishe ili kila maamuzi utakayofanya usijue kuyajutia....I CAN IMAGINE..ITS MORE THAN PAIN JAMAN...POLE MPENDWA BT THERE IS A BRIGHT FUTURE AHEAD OF U SOON.
 
Mmmhhh!!!

Hivi miaka 39, watoto wawili, kazi nzuri lakini bado tu wataka kuolewa mara ya pili???

Halafu kuna mahali kama umetumiksi hivi, ukiwa chuo mlipata watoto wawili wewe na mumeo...halafu mbele ya stori tena mumeo akiwa anaondoka ukawa na ujauzito wa mtoto wa pili...sasa sijui stori hii yote itakuwa na viuongo uongo vya kihivyo!!!

Nitakuwa sijaeleweka kiaandishi ndugu yangu. Sisi tunao watoto wawili na tulianza kuzaa tukiwa chuoni, mpaka sasa ni hao hao wawili. Alipoondoka kwenda masomon aliniacha na ujauzito wa mtoto wa pili ukiwa unakaribia kwenye term
 
hivi gfsonwin na BADILI TABIA, Mtu miaka 3+ hakuna barua wala nini halafu eti asijicommit hadi ajue hatma? Kama uko na ndoa hamna mawasiliano, umekuwa blocked kwa maneno na matendo, na mtu amerudi hadi mtaa wa tatu hana habari na wanae wala wewe. Halafu ati unaendelea kumpenda? Unampenda nini hapo kwa mfano?
Mahaba niue nigalagaze hadi unizike.:eyebrows:
 
Mh, hivi kumbe kuna kampuni ambazo kuomba ruhusa anakuombea mtu mwingine asiye kazini?!...mh:tape2:

Iko hivi DB anaish nje na anafanyia kazi huko, sasa ili kazini kwao aweze kuomba ruhusa ni pamoja na mimi kuandika email kuonyesha kwamba ni mtu wangu na ninamuhitaj kwa haraka sana. Kwa wao wanawake wanathaminiwa sana iwapo wataonyesha concern yyte ile na ukumbuke ni recently tu katoka huku
 
Shikamoo dada gfsonwin,
ama baada ya salamu nikuulize kwa nini mimi sijaitwa? Halafu tangu nirudi mjini sijakuona...u hali gani???!

BACK TO TOPIC...
Namfahamu mmama mmoja ambaye hakuolewa tena tangu mumewe amuache, hadi leo ana matumaini mumewe atarejea. Sijawahi kuelewa mental psychology ya mwanamke ila nikiwaza huyo mama anachofikiria kumtegemea mumewe 10+ years after amemuacha na watoto (halafu watatu..coincidence!!!???) sipati jibu.

My thought ni...kama huyo DB (BD?) anakuja aje...wakae tu pamoja waongee tena, kwa kirefu...amweleze hofu yake...wahenga wanasema 'two heads are better than one'. wakikaa pamoja wakaongea nadhani watapata suluhisho.

From there filing for divorce na mengine yatafuata.

Hofu yangu tu ni mwanamke ambaye bado ana mapenzi kwa mtu mwingine -in my view - ni hatari kuliko mwanaume mwenye mapenzi na mtu mwingine. Ni heri angebaki single tu kuliko kumuingiza DB (BD?) kwenye maumivu kama aliyonayo yeye.

Ni hayo tu...!

Cc: Paloma Watu8 ....
 
Last edited by a moderator:
Mmmhhh!!!

Hivi miaka 39, watoto wawili, kazi nzuri lakini bado tu wataka kuolewa mara ya pili???

Halafu kuna mahali kama umetumiksi hivi, ukiwa chuo mlipata watoto wawili wewe na mumeo...halafu mbele ya stori tena mumeo akiwa anaondoka ukawa na ujauzito wa mtoto wa pili...sasa sijui stori hii yote itakuwa na viuongo uongo vya kihivyo!!!

Ndugu yangu ninahitaj faraja jamani, hebu niambie for 5 yrs mtu amekuwa nje, na katika miaka iyo amewah kurudi nchini kuonana na mie mara 2 tu na kwa maiaka 3 hana mawasiliano na mie kabisaa. Ivi kweli hata yale mahaitaj ya kimwili pesa zitanisaidia nini?

Nina fanya kazi sehemu nzuri sana niasafiri kila mwezi nje ya nchi nalala mahoteli makubwa nakutana na watu wa kila aina ivi nisipokuwa na wangu si ndio nitajikuta natembea na kila ninayekutana naye kwenye mikutano sijui ama mahotelini?
 
Back
Top Bottom