twende taratibu dada (nakuchukulia kama mdogo wangu).
Unampenda huyu bwana? Manake moyo nao una kiherehere. Tulia kwanza mchecheto upite, manake kuchat na mtu miezi sita sio sababu ya kumpenda. Wewe uko lonely and vulnerable (take note, kwa hiyo husisha akili kwenye maamuzi)
Nimefurahi unaangalia mambo ya msingi:
1. Unahitaji kujua kama unampenda huyu ndugu. Lakini still wewe sio binti mdogo na kukimbilia ndoa sio muhimu sana ( angalia usiwe unakimbilia sex pia). Ndoa ni commitment ya maisha.
2. Hakikisha jamaa anaonana na ndugu wachache sana unaowaamini, pamoja na wanao. Waambie watoto that is your good friend na uwaone wanamchukuliaje. Na wewe unahitaji kukutana na wanae
3. Nafurahi kuwa unawaza kazi yako pia. Come what may, usiache kazi. tafuta kazi ya hadhi hiyo hiyo ama zaidi na hiyo ndio condition ya kuhamia huko. Hata kama itabidi msioane hadi upate kazi. Kubalianeni mambo ya msingi ikiwemo wewe kufanya kazi. Hao wenzetu wana tamaduni tofauti, ukimuambia mtoto wa binamu wa mjukuu wa ukoo wao baba kwa upande wa mama anahitaji msaada hawaelewagi. So kazi yako ishikilie haswaa.
4. Wakati huo mnaendeleana kujuana na huyu ndugu, unaweza kufanya mipango ya talaka. Lakini ningekuwa wewe, nisingesaka talaka ili niolewe na DB. Ningesaka talaka kwa sababu nimechoka kuishi kwa suspension ya kungojea mtu ndio nianze kuishi wakati huo yeye anaendelea kuishi na kufurahia malimwengu. Huyu DB asiwe sababu ya kutaka talaka manake nae akikuacha utaumia sana
Haya maneno yako, kuwa its too early kujicommit yanaonyesha maturity yako. Nimekupenda bure kabisa. Muambie ni mapema sana kufunga ndoa, ni muhimu tuongee mambo yote na kuyamaliza, na tukutane na ndugu pia.
Kila la kheri. Mwisho wa siku trust your guts. Ni sawa kukosea kuamua, ila utakosea usipoamua kabisa na kupelekwa kama jahazi bovu