Ushauri wa haraka unahitajika, ndoa inapumulia oksijeni

Ushauri wa haraka unahitajika, ndoa inapumulia oksijeni

Yaani ameamua kukunyima unyumba?...hiyo siraha aliyoamua kukupiga nayo siyo!...
 
Mtoe outing mpe optional achague arusha ngurudoto au sehemu yoyote yenye utulivu,Zanzibar au mwanza namanisha badilisha mazingira mkishafika huko mwombe msamaha na mbembeleze uza noah mnunulie Gari atakayo chagua kuendana na mfuko wako.Usisahau ukishaoa mnashirikishana maisha ya ubachelor yanaisha usishi ubachelor kwenye ndoa hata kama vilikuwa viwanja vya haraka ulipaswa umpigie simu umwambie umeitiwa viwanja.
 
Habari zenu wafuasi wa mtandao pendwa na wale wapenzi wa jukwaa hili la mahusiano, natumaini wote ni wazima na mko imara kama Simba sema sio Simba hii ya kina Manara ni uimara wa Simba mnyama.

Pasi na kupoteza wasaha ningependa niendee moja kwa moja kwenye dhumuni la kuandika uzi huu ambao umekuwa sponsered na kampuni yangu inayojihusisha na masuala ya usafirishaji mizigo ndani ya Tanzania na nchi jirani.

Baada ya kupambana na kuweza kuhamia kwenye kibanda changu(Ghorofa moja) maeneo ya Tabata Kinyerezi, nikaona ni vyema nikafanya mambo mengine ya kimaendeleo maana Wahenga husema Muda ni Mali.

Sasa nikawa nimehifadhi gunia za mahindi kama 300 hivi lengo nije kuuza kwa bei ya juu zaidi, hilo suala nikawa nimemshirikisha wife, tatizo ni kwamba kulikuwa kuna kama milioni 25 kwenye akaunti yangu ambayo nilitaka ninunue hizi gari aina ya 'Toyota Crown Athlete' jambo ambalo Wife alilipa baraka kwa mikono miwili.

Lakini wakati nikiwa kwenye mchakato wa kuanza kuagiza nikapata habari njema ya kwamba kuna eneo moja Bagamoyo wanauza viwanja kwa bei poa kabisa na vimepimwa, ikabidi nifunge safari kwenda kuviangalia na jamaa yangu mmoja yupo pale wizara ya Lukuvi.

Basi nikaona ni vyema ninunue hivi viwanja chapchap, kwaiyo ile hela ya gari nika-invest kwenye viwanja viwili nilivyovipata huku bwagamoyo japo sikumshirikisha mke.

Sasa baada ya kupita kama mwezi mke akawa ananiuliza kuhusiana na gari maendeleo yake, nikamwmbia bwana kusema ukweli sikuagiza sema kuna jambo nimefanya, akahoji! jambo gani? nikamwambia nimeamua kununua viwanja.

Baada ya kumwambia hivyo, maneno yakaanza kumtoka kama mtu aliyefungwa mota, mara ooh! utakuwa na mwanamke mwingine nje umeamua kumnunulia ndio maana sikuamua kumshirikisha.

Amenuna sio kawaida, yaani hapo napoandika nimenyimwa unyumba inaelekea mwezi sasa, tunalala mzungu wa nne, no story na amani hakuna, anasema atanipa mpaka atakapomjua mwizi wake.

...Maana uzalendo naona unanishinda... Ushauri wenu

NB : Sio kama gari hatuna, tuna gari mbili, Rav 4 pamoja na Noah, ambayo nilikuwa kwenye mpango wa kuiuza tubaki na gari mbili tuu.
Vipi ile Murano uliuza? Sasa wewe na ushua wako unanunua viwanja viwili kwa 25m kwenye akaunti unakosa hata hela ya kununua hio 10yrs old toyota crown??!!!! Acha ubahili hebu mnunulie shemeji huo mtumba!
 
hivyo viwanja viko bagamoyo ipi na mimi nataka, kuhusu ndoa itadumu tu, mmbeleze anatingisha kibiriti tu, anadeka mana hata kosa silioni, kwani si umesema vina hati muonyeshe hizo hati zina jina gani. ila jinsi unavyoongea huonekani hata kama una woga na hiyo ndoa, halafu kabila gani wewe MANA HAYO MAJISIFU ULOTOA LOL.
Mara umenasa kwenye mtego wake,khaa kina dada kuweni makini jamani au vipi?,.,,.,yaani mara umenasa kwenye ULIMBO, ghafla unasema NA MIMI NATAKA ,,KHAA,sasa hii si itakua JAMAA katega na MABINTI wanaingia nzima DOOOOOOOH.
 
Sasa tatizo ni viwanja. Sababu ya kusema
1). Nina orofa
2). Benki kuna Tsh 25M/-
3). Nimehifadhi gunia 300 za mahindi.

Sioni lolote la kukusaidia zaidi ya kukutaka uachane na makidai (showoff) yasiyo ya lazima
 
Sasa tatizo ni viwanja. Sababu ya kusema
1). Nina orofa
2). Benki kuna Tsh 25M/-
3). Nimehifadhi gunia 300 za mahindi.

Sioni lolote la kukusaidia zaidi ya kukutaka uachane na makidai (showoff) yasiyo ya lazima
mpaka anatia kichefuchefu! tukitaja mali zetu humu hataingia tena humu jf
 
hili sio la kupayuka huku unatabasamu.....hujahonga umenununua viwanja, tena kwa faaida yenu.....hawa wadudu sida sana....we kauka,,,,kimbizana na maendeleo...hongera pia....
 
Hivi na wewe hujagundua huu ni mtego? umepakazwa ULIMBO,mademu sasa hivi watanaswa na KUTAFUNWA.
Ndiyo hvyo anatikisa kiberiti kwa wanawake ambao wataweza kutikiswa haya imekula kwao.
 
Sijaelewa unahtaji msaada gani
1.unahitaji unyumba(mapenzi)???
2.unahtaji kusolv matatizo ya ndoa?
 
Umekuwa na maneno mengi ya kujisif kama watan zangu bhana,
Isikute kuna mtu unataka umuende pm hapa maana hamkawii?

asmaa80 naye anataka kuwekeza bwagamoyo umemuona.
 
Ndiyo hvyo anatikisa kiberiti kwa wanawake ambao wataweza kutikiswa haya imekula kwao.
Nashukuru umeshtukia maana na urembo wako wote huo,halafu ukachunguliwe na LIKANJANJA halina hata mvutooo,.,.,,KHAAA NI SOOOO.
 
ndg. WA KISHUA
Be serious "Rijali uoneshe makucha yako na macho mekundu..." Ulichofanya ni sahihi na Utimamu !! Viwanja ni bora kuliko gurudumu la barabarani !!!
 
Ni sawa taarifa imefika I,e una ghorofa,gari mbili,viwanja viwili...na a/c worth 25 mil.
Nshomile with no course......
 
Nashukuru umeshtukia maana na urembo wako wote huo,halafu ukachunguliwe na LIKANJANJA halina hata mvutooo,.,.,,KHAAA NI SOOOO.
Hahaaaaaa ukiona mtu anataja alichonacho imabidi utoke mbio mana ni kama kuku anatupiwa mtama afu ndiyo akamatwe.
 
Hahaaaaaa ukiona mtu anataja alichonacho imabidi utoke mbio mana ni kama kuku anatupiwa mtama afu ndiyo akamatwe.
ETI RAV 4 OOH ETI NOAH HAHAHAAA ET TOYOTA CROWN HALAFU MIL25 BANK,.. BASI PATAMU HAPO ETI KATEGESHA SASA ANANGOJA Sister ajilengeshe teh tehe T.heeee
 
Kwahyo unataka tukusaidie mkeo akupe unyumba ama? Teh teh teh ndoa bana wakati mwingine ka igizo hivi loh! Unataka kutuambia umeshindwa kabisa kumbembeleza mkeo akupe utyam mwezi mzima?mweeh teh! Pole bana! Mi hata sijui nkusaidieje sa khaa!
 
Back
Top Bottom