WA KISHUA
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 365
- 130
Habari zenu wafuasi wa mtandao pendwa na wale wapenzi wa jukwaa hili la mahusiano, natumaini wote ni wazima na mko imara kama Simba sema sio Simba hii ya kina Manara ni uimara wa Simba mnyama.
Pasi na kupoteza wasaha ningependa niendee moja kwa moja kwenye dhumuni la kuandika uzi huu ambao umekuwa sponsered na kampuni yangu inayojihusisha na masuala ya usafirishaji mizigo ndani ya Tanzania na nchi jirani.
Baada ya kupambana na kuweza kuhamia kwenye kibanda changu(Ghorofa moja) maeneo ya Tabata Kinyerezi, nikaona ni vyema nikafanya mambo mengine ya kimaendeleo maana Wahenga husema Muda ni Mali.
Sasa nikawa nimehifadhi gunia za mahindi kama 300 hivi lengo nije kuuza kwa bei ya juu zaidi, hilo suala nikawa nimemshirikisha wife, tatizo ni kwamba kulikuwa kuna kama milioni 25 kwenye akaunti yangu ambayo nilitaka ninunue hizi gari aina ya 'Toyota Crown Athlete' jambo ambalo Wife alilipa baraka kwa mikono miwili.
Lakini wakati nikiwa kwenye mchakato wa kuanza kuagiza nikapata habari njema ya kwamba kuna eneo moja Bagamoyo wanauza viwanja kwa bei poa kabisa na vimepimwa, ikabidi nifunge safari kwenda kuviangalia na jamaa yangu mmoja yupo pale wizara ya Lukuvi.
Basi nikaona ni vyema ninunue hivi viwanja chapchap, kwaiyo ile hela ya gari nika-invest kwenye viwanja viwili nilivyovipata huku bwagamoyo japo sikumshirikisha mke.
Sasa baada ya kupita kama mwezi mke akawa ananiuliza kuhusiana na gari maendeleo yake, nikamwmbia bwana kusema ukweli sikuagiza sema kuna jambo nimefanya, akahoji! jambo gani? nikamwambia nimeamua kununua viwanja.
Baada ya kumwambia hivyo, maneno yakaanza kumtoka kama mtu aliyefungwa mota, mara ooh! utakuwa na mwanamke mwingine nje umeamua kumnunulia ndio maana sikuamua kumshirikisha.
Amenuna sio kawaida, yaani hapo napoandika nimenyimwa unyumba inaelekea mwezi sasa, tunalala mzungu wa nne, no story na amani hakuna, anasema atanipa mpaka atakapomjua mwizi wake.
...Maana uzalendo naona unanishinda... Ushauri wenu
NB : Sio kama gari hatuna, tuna gari mbili, Rav 4 pamoja na Noah, ambayo nilikuwa kwenye mpango wa kuiuza tubaki na gari mbili tuu.