Ushauri wa haraka unahitajika, ndoa inapumulia oksijeni

Ushauri wa haraka unahitajika, ndoa inapumulia oksijeni

ETI RAV 4 OOH ETI NOAH HAHAHAAA ET TOYOTA CROWN HALAFU MIL25 BANK,.. BASI PATAMU HAPO ETI KATEGESHA SASA ANANGOJA Sister ajilengeshe teh tehe T.heeee
Hahaaaaaaa........ila maisha haya.
 
Kwahyo unataka tukusaidie mkeo akupe unyumba ama? Teh teh teh ndoa bana wakati mwingine ka igizo hivi loh! Unataka kutuambia umeshindwa kabisa kumbembeleza mkeo akupe utyam mwezi mzima?mweeh teh! Pole bana! Mi hata sijui nkusaidieje sa khaa!
Mpe mbinu apate unyumba. Teh teh teh
 
Nadhani umepewa hati yenye jina lako kwa hiko kiwanja na huo ndio uthibitisho tosha so ka bado haamini basi kuna ukweli ambao hujatueleza kuhusiana na ndoa yenu
 
Inabidi utambue mke ni kama mtoto...hutakiwi kutumia hata nguvu nyingi,,,,kaa nae chini muelekeze kwa utulivu...wewe ni mwanaume nina imani unao uwezo wa kumuweka sawa!!! Uvumilivu ni muhimu ktk hili....chukua uamuzi mzur kulinda ndoa yako ili mjenge familia bora
 
Hahaaaaaaa........ila maisha haya.
Ila kweli bhana haya ni maisha na kila mtu ana mipango yake na hisia zake,so mwenzetu kategesha ili akate KIU yake kwa kuopoa miss Maukwaju na atawapata wengi tu,yaani ni kama kusukuma mlevi.
 
Mpe mbinu apate unyumba. Teh teh teh
Habari zenu wafuasi wa mtandao pendwa na wale wapenzi wa jukwaa hili la mahusiano, natumaini wote ni wazima na mko imara kama Simba sema sio Simba hii ya kina Manara ni uimara wa Simba mnyama.

Pasi na kupoteza wasaha ningependa niendee moja kwa moja kwenye dhumuni la kuandika uzi huu ambao umekuwa sponsered na kampuni yangu inayojihusisha na masuala ya usafirishaji mizigo ndani ya Tanzania na nchi jirani.

Baada ya kupambana na kuweza kuhamia kwenye kibanda changu(Ghorofa moja) maeneo ya Tabata Kinyerezi, nikaona ni vyema nikafanya mambo mengine ya kimaendeleo maana Wahenga husema Muda ni Mali.

Sasa nikawa nimehifadhi gunia za mahindi kama 300 hivi lengo nije kuuza kwa bei ya juu zaidi, hilo suala nikawa nimemshirikisha wife, tatizo ni kwamba kulikuwa kuna kama milioni 25 kwenye akaunti yangu ambayo nilitaka ninunue hizi gari aina ya 'Toyota Crown Athlete' jambo ambalo Wife alilipa baraka kwa mikono miwili.

Lakini wakati nikiwa kwenye mchakato wa kuanza kuagiza nikapata habari njema ya kwamba kuna eneo moja Bagamoyo wanauza viwanja kwa bei poa kabisa na vimepimwa, ikabidi nifunge safari kwenda kuviangalia na jamaa yangu mmoja yupo pale wizara ya Lukuvi.

Basi nikaona ni vyema ninunue hivi viwanja chapchap, kwaiyo ile hela ya gari nika-invest kwenye viwanja viwili nilivyovipata huku bwagamoyo japo sikumshirikisha mke.

Sasa baada ya kupita kama mwezi mke akawa ananiuliza kuhusiana na gari maendeleo yake, nikamwmbia bwana kusema ukweli sikuagiza sema kuna jambo nimefanya, akahoji! jambo gani? nikamwambia nimeamua kununua viwanja.

Baada ya kumwambia hivyo, maneno yakaanza kumtoka kama mtu aliyefungwa mota, mara ooh! utakuwa na mwanamke mwingine nje umeamua kumnunulia ndio maana sikuamua kumshirikisha.

Amenuna sio kawaida, yaani hapo napoandika nimenyimwa unyumba inaelekea mwezi sasa, tunalala mzungu wa nne, no story na amani hakuna, anasema atanipa mpaka atakapomjua mwizi wake.

...Maana uzalendo naona unanishinda... Ushauri wenu

NB : Sio kama gari hatuna, tuna gari mbili, Rav 4 pamoja na Noah, ambayo nilikuwa kwenye mpango wa kuiuza tubaki na gari mbili tuu.
BASI POOOLE BWANA AWE NAWE .,,.,,..AMEEEEEEN.
 
Ila kweli bhana haya ni maisha na kila mtu ana mipango yake na hisia zake,so mwenzetu kategesha ili akate KIU yake kwa kuopoa miss Maukwaju na atawapata wengi tu,yaani ni kama kusukuma mlevi.
Wajinga ndiyo waliwao. ..
 
Ndio maana niliwai kusema MMU ndio jukwaa pekee ambalo unaweza kupost uzi wowote bila kujali kama ni uongo,uzushi ama ni hadithi

mtoa mada umeleta uzi wako kiutani zaidi pale ulipoitaja SIMBA SC bingwa wa kihistoria kwa kuidhihaki...inaonyesha wewe ni poyoyo wa yeboyebo

wahakiki wa kazi ya fasihi baada ya kuifanyia uhakiki hii thread yako tumegundua wewe ni mchekeshaji (comedian) ambaye mara nyingi unapenda kuwasilisha ujumbe wako katika hali ya kufanya watu wacheke au wafurahi kwa kile ulichokisema mfano.kuitaja kampuni yako,sh,mili 25,ghorofa na kununua gari mpya pamoja na viwanja

kitu ambacho sio kweli ila ni ndoto tu unazoota kila siku sidhani hata kama kuoa umeshaoa
 
In general, pride is at the bottom of all great mistakes.
 
kukunyima unyumba mbona azabu kali kuliko kosa washirikishe wazeee
 
Rudini kwa viongozi wenu wa dini mtafute suluhu, issue ndogo saa hiyo...
Alafu usishindane nao hawa viumbe hata kama u didnt do anything wrong we kuwa mdogo tu..
 
Sijaona ndoa kupumlia oksejeni nimeona uwekezaji uloufanya tu hapo hakuna ushauri unaotafutwa
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada ila ulitaka ndoa hio ipumulie gesi gan?!?
 
Back
Top Bottom