Ushauri wa Bure kwa CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wa Bure kwa CHADEMA!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Oct 1, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  1. CCM hadi hivi sasa imefanya juhudi kubwa za kuifanya CHADEMA ionekane kama chama chenye fujo na kinaharibu "utulivu na amani" wa Watanzania!
  CHADEMA bila kujua hila za CCM kimeingia mkenge hasa viongozi wake wanapodai kwamba kura zikiibiwa "damu itamwagika!" Kauli hii iliwagharimu CUF na kilionekana ni chama kinachokusudia kuleta fujo, sasa hisia hizo zimehamia CHADEMA!

  2. Kauli zinazoashiria kupunguza idadi ya wapiga kura:
  - Nikiingia madarakani nitamtimua Mhariri wa Daily News: Mpiga kura huyo baada ya kuisikia kauli hiyo ataipigia kura CHADEMA?
  - Nikiingia madarakani nitafuta vyeo vya U-DC: Hapa ina maana ma-DC wote hawatampigia kura Dkt Slaa kwa kuwa automatically vibarua vyao vitaota nyasi.
  - Nikiingia madarakani nitawaburuza mahakamani mafisadi wote: Hapa ina maana kuwa wale wanaojihisi kuwa ni mafisadi (kwa bahati mbaya hawa wako wengi)hawataipigia kura CHADEMA!
  nk.
  Kauli hizi zirekebishwe ili zilenge electorate wote kwa ujumla na si kubagua kwa namna yoyote, hata kama nia ipo ya kufanya hayo! Lugha nzuri itumike ili kuwaelimisha watz maana kila jambo jipya huwa haliaminiki mwanzoni!

  3. Ahadi za huduma za jamii (km elimu) kuwa bure: Ahadi hii imekuwa questioned hata na watu wasioenda shule (watu wa kawaida). Hapa yanahitajika maelezo ya ziada na si kudai kuwa tutachukua fedha za EPA ambapo hizo fedha zikiisha ndio inakuwaje! Majibu yangekaa kitakwimu zaidi, km kuna idadi kadhaa za wanafunzi, then kila mwanafunzi anagharimiwa kiasi fulani, then bajeti yetu ni kiasi fulani, etc.

  Haya ndio yangu kwa leo wanaJF hasa wanaoitakia mema CHADEMA!

  Tujadili!
   
 2. M

  MC JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ama kweli kila mtu na mtazamo wake,

  kwa mtazamo wangu mimi, Mr. Bucha analysis yako ni ya uongo na haina mema yeyote unayoitakia Chadema, Siasa za kisasa zanahita msema kweli na anayeusimamia ukweli, hakuna mwafaka wowote au lugha nzuri ya kuongea na Fisadi ili upate kura yake, ukifanya hivyo ni ufisadi mwingine na ndio chanzo cha viongozi kushindwa kutimiza walichaoahidi.


  Kuhusu Elimu bure, Yes, watu maskini wata-question kwa kuwa wamashazoeshwa kuwa wao ni maskini na maisha yao yatakuwa hivyo tu, kwa hiyo waki-question hiyo ni hatua muhimu sana ya ujumbe kuwafikia, kinachotakiwa ni kuwahakikishia ambacho ndiocho CHADEMA na wadau wengine wa maendeleo wanafanya kwa sasa.
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hatutaki kura za criminals. Hivyo sikubaliani nawe. Maana si watanzania wote ambao ni criminals. wengi wa watanzania ni watu wema sana na wamechoka na umaskini wa kufanyiziwa.
  Tunahitaji hatua kali zichukuliwe kwa criminals full stop.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashukuru kwa maoni yenu wadau wote mliochangia! Mnasemaje juu ya lugha za vitisho? Kumbukeni kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ ametahadharisha juu ya hatari ya amani kutoweka wakati huu wa uchaguzi!
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Buchanan,

  Nakubaliana na wewe kuhusu swala la kauli za damu itamwagika. Tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba chama kikishaonekana kuwa threat kwa CCM, whether utumie lugha laini au nyepesi au kauli nzuri, bado tu utavikwa ubaya hata kama ni wa kuokoteza. So, hai-make any difference.

  Swala la mafisadi/Mkumbwa Alli, nadhani hapo wanaweza kutamka tu kwamba serikali mpya itafuata utawala wa sheria. Including kuwashughulikia hao mafisadi. Hata asipotaja kwamba atawafikisha mafisadi mahakamani, bado mtu yeyote ambaye anajijua ana matatizo ya kifisadi, hawezi kukipigia kura chama ambacho anajua kitakuja kufuata utawala wa sheria. Hivi unategemea mtu ambaye amezowea kuishi kwa misheni town anaweza kuipigia kura CHADEMA hata wasiposema kwamba watawashughulikia mafisadi? Bado proportion ya mafisadi ni ndogo sana hata ukijumlisha na extended family zao. Mafisadi kwanza huwa hawana undugu wala ujamaa, unaweza kushangaa mtu fisadi lakini some of his/her extennded family wako choka mbaya na wakisikia kwamba jamaa kapatwa na kasheshe wanashangilia kabisa. Mzee mzima alipoachia Uwaziri Mkuu kuna some of his extended family members walishangilia sana.
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hivi kazi ya JWTZ ni nini? Kwani kuna watu wanataka kupindua nchi? Ninaona JWTZ wanaingilia kazi za Polisi, kitu ambacho siyo jukumu lao. Kungekuwa na tetesi za machafuko ya kupindua nchi, hapo ningeweza kusema wana haki, lakini kama swala ni wananchi kutaka kulinda kura zao sioni nafasi ya JWTZ kwenye huu uchaguzi.

  Sana sana Mnadhimu Mkuu wa JWTZ anazidi kuthibitisha kwamba hali ya CCM ni mbaya na sasa wameamua kutumia hata wanajeshi ili kutisha wapiga kura na wananchi.
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Buchanan
  Salaam sana.

  Naomba utupe ushahidi wa matamshi ya "damu itamwagika" - kasema nani, wapi na lini?

  Pia naomba utushauri pale anapoinuka mtu na kusema "Vyama vyote vikubali matokeo ili kudumisha amani" - which means, no matter how fair and free/unfair and unfree, lazima matokeo yakubalike.

  Tusaidie.
   
 8. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mbona kauli za makasisi na wachungaji kutoa kauli za kumpigia debe slaa ndani ya makanisa hukuzitaja? Au hii sio dalili kuwa chadema ni chama cha wakiristo? Hivyo wasiokuwa wakiristo nao watafute vyama vyao kuvipigia kura? Au kwa maoni yenu chama cha siasa kikihusishwa na ukiristo sio udini ila pale kinapohusishwa na uislamu ndio udini?

  Mwenye akili atanijibu kwa hoja labda awe mwendawazimu huyu atakuja na matusi au dharau nami namsamehe maanake ni punguwani!!!
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  CHADEMA ni chama cha matumaini. Matumaini kwamba Tanzania bila ya ufisadi inawezekana. Matumaini kwamba Tanzania inaweza kunufaika
  kutokana na maliasili zake. Dr Slaa ameshasema kuwa atapunguza baraza la mawaziri, na hivi kupunguza matumizi ya serikali, na hivi kuongeza matumizi katika elimu ya watanzania. Elimu bure kwa Watanzania inawezekana, kama tutaipa kipaumbele. Na Tanzania inayojitegemea inawezekana, siyo hii ya omba omba mpaka tunaambiwa tungekufa njaa kama Kikwete asingeenda safari za nje.
   
 10. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  HAYA NDIYO MATEGEMEO YA WATANZANIA WALIO WENGI

  [​IMG]
   
 11. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  unaonekana akili unazo ila umeamua kuzihifadhi uje uzitumie umri ukisogea zaidi.....
  kwanza hauna mema yoyote na CHADEMA, hata hivyo watu wanafiki kama wewe hawahitajiki CHADEMA....
  kama kuna kiongozi wa CHADEMA amesema kuwa damu itamwagika wakiiba kura ni kweli kwa kuwa itamwagika kiukweli...afadhali imwagike nchi iondolewe hapa ilipo...kama rais wa nchi anasema Rost tamu ni mtu safi anasingiziwa tu! ni nani anamsingizia? alisema Ed L ni safi alisingiziwa wakati yeye ndo kaongoza yote yaliyomkuta EL kwenye chama na bungeni...lawama kwa watz eti wanamsingizia!!!duh nachukia mimi.
  jeshi tangu wakahusika na mambo ya uchaguzi??au ndo kutetea vibarua vyao haramu?
  mabank yameporwa hapa...mabasi yanatekwa na maharamia kila siku....watu wanafunga mitaa wanaiba na kufanya unyama mwingine jeshi wamenyamaza leo wanasema ambaye atakataa matokeo tutapambana naye!!!!kwa nini lakini? mimi nikatae matokeo nipambane na jeshi?how? au jeshi la polisi limeasi?mtuambie maana tunaumia nchi yetu kuendeshwa kama familia ya mtu.
  CHADEMA lazima watangaze mikakati ya kuiongoza nchi hii.ktk mikakati ni pamoja na kupunguza matumizi serikalini, kupiga chini UDC si kitu cha ajabu....hata wakimnyima kura wooote na familia zao bado hawataweza kubadili matokeo..na ujue wengine wana elimu watapigia CHADEMA na wanaconfidence ya kuishi kivingine kulingana na profession zao..kuna watu wako huko kwa sbb ya uwoga tu ila kichwani wako vyema..niwataje??

  wewe wa wapi lakini?takwimu zinatolewa kila siku na wewe unaziuliza tena hapa...nyerere alisomesha watu bure mpaka chuo kikuu bure na walikula na kusafiri vizuri akiwa na wasomi wachache sana na hakuchimba madini wala gesi....leo tuna gesi,mafuta,madini...kwa nini tusiweze jamani? kwa nini mtu akikuambia wewe ni masikini unakubali kirahisi hivyo?ndugu hawawezi hata kukusanya kodi...wameng'ang'ania vyanzo vilevile vya mwaka 47! leo hii kuna watu wana nyumba kila mtaa,wanaincome ya mpaka 20millioni kwa mwezi lakini hawalipi hata shs tano....serikali wanajua ila wamekaa kimya kwa kuwa wao ndo wanufaika wa uozo huo....halafu mmekaririshwa kuwa kwa kuwa CHICHIEMU wameshindwa basi haiwezekani!semeni mmeshindwa....!!!na wengine wenye kuweza watawaonyesha kuwa inawezekana..
  namshukuru baba askofu Kakobe kwa elimu ya uraia aiyoitoa kupitia chanel 10 leo...kama hujapata kuona angalia chanel10 kesho i mean leo baadae jioni na star tv jumatatu...najitahidi nipate dvd na nitairusha hapa watu wapate elimu ya uraia ambayo serikali haijaweza kuitoa...
  angalia midahalo ya vyama,hudhuria mikutano ya chadema utajifunza mengi sana.

   
 12. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #12
  Oct 2, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hao viongozi wa dini walitoa kauli ipi hasa? Kuhusu uislamu kuhusishwa na udini kuliko ukristo ni kwamba uislamu umeleta maangamizi na balaa la ugaidi duniani!
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Oct 2, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naitakia mema CHADEMA ili isije kukosa mwelekeo kama CUF baada ya kufanyiwa hila na CCM! Watz wengi bado hawana elimu ya kutosha, wakoneshwa picha za mauaji ya Rwanda wanahusisha kauliza "damu itamwagika kura zikiibiwa" na mauaji hayo, na CCM mara zote huwa inatamba kuwa ni chama kinachodumisha amani na utulivu, huoni kwamba CHADEMA kinahitaji kujirekebisha hapo?
   
 14. telele

  telele Member

  #14
  Oct 2, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe bwana timua zako huko nenda kawashauri hao hao CCM wenzako. huna mema yoyote na CHADEMA wewe! muone kwanza, umekaa kiudini udini!!
   
 15. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #15
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Buchanan, kumbuka kuwa serikari na utawala wa kimla wa nchi nyingi za kiafrika huwa haziondolewi madarakani on ballot paper! hiyo ndo historia yetu africa na mabadiliko huwa hayaji kwa lele mama kuna sacrifies need to be made to achieve any CHANGE in Africa,

  Remember iligharimu maisha ya wakenya 1500 to get a new constitution na kupata serikari ya umoja wa kitaifa, however iligharimu maisha ya wazanzibari kuweza kufikia muafaka wa maridhiano zanzibar na chama hiki hiki cha mapinduzi, Ni imani yanggu pia CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa ballot paper kwani tumeshuhudia kila hila na dhuluma kwa kutumia either msajiri wa vyama vya siasa, NEC na vyombo vya dola, state machinery like state media kuuhujumu upinzani hususani CHADEMA.

  Kwa hiyo mood ya watanzania wanataka mabadiliko na tuta march on street peacefuly kupinga matokeo ya uchaguzi kama hautafanyika kwa uhuru na haki lakini kama vyombo vya dola vita taka ku surpress people's power basi hapo ndipo damu itakapo mwagika na nchi haitatawalika.

  Martin Luther King Jr. ni mmoja wa wahanga wa matumizi ya nguvu za dola pale wananchi walipokuwa wanadai haki zao kwa maandamano ya amani na Dr King alikamatwa na kuwekwa jela na maneno yafuatayo aliyasema wakati yupo jela nanukuu ""Our lives begin to end the day we become silent about the things that matter." mwisho wa kunukuu Remember, when Dr. King wrote that, he wrote it from a jail cell in Birmingham, Alabama in 1963
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani damu kumwagika ni big deal? Si ndiyo kawaida kwa nchi za Kiafrika zenye siasa za hovyo hovyo? Na unaweza kuniambia Tanzania ni unique? Sema labda wakati wetu ndiyo bado haujawadia, lakini jinsi mambo yanavyoenda, nadhani hiyo si mbali sana, with or without intimidation from JWTZ!
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Oct 2, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa nini wanaotaka kumwaga damu wasiende Muhimbili ambapo zinahitajika?
   
 18. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CHADEMA iendelee kuonesha msimamo wake juu ya U-DC, Ufisadi, Ukuu wa Wilaya etc. Suala si kupata kura tu suala ni kusimamia msimamo. CCM kwa nia ya kuupata kura tu wamedanganya hadi waislamu kupata mahakama ya kadhi. Sasa hivi ili kuwazubaisha waislamu, wanapandikiziwa idea ya Chadema wadini. Ni tatizo. Buchanan naye kadakia stori za mitaani. Nina hakika hajasoma vizuri magazeti ama kutazama TV kwa kuwa hakuna chombo chochote cha habari kilichodai Mbowe au Chadema wamesema damu "itamwagika" kura zikiibwa.
   
 19. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Buchanan nikuulize, Ni ipi kati ya hizi statements zilitolewa na Kiongozi wa Chadema?:


  1. Kura zetu zikiibwa damu itamwagika
  2. Wananchi hakikisheni mnalinda kura zetu hata kama damu zenu zitamwagika
  Nasubiri jibu.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Oct 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wapiga kura ni lazima wajue wanachochagua. Hakuna kuwalaghai. Ni lazima nchi igawanyike kati ya wanaounga mkono CCM na wanaounga mkono Chadema. Wananchi wajue Dr. Slaa akiingia atafanya nini. There is no middle ground.
   
Loading...