Elections 2010 Ushauri wa Bure kwa CHADEMA!

wewe bwana timua zako huko nenda kawashauri hao hao CCM wenzako. huna mema yoyote na CHADEMA wewe! muone kwanza, umekaa kiudini udini!!

Wewe mwenye mema na CHADEMA na usiye mdini mbona huna hoja yoyote ya maana zaidi ya kudai eti "timua zako?"
 
Amani au vita ni suala ambalo jamii huchagua kufuata one of the two.
JWTZ ni sehemu ya jamii ambayo haipo kutishia jamii ya Watanzania, maneno yao yalipaswa kusemwa na jeshi au mtu aliyeko nje ya mipaka yetu. Jeshi linalopaswa kulinda raia wake halipaswi kuwa tishio kwa raia hao.

Nasimama mbele ya kadamsnasi kusema kwamba, uteuzi wa makamanda wa majeshi yeu umetawaliwa na ladha za kisiasa na si kitaalam. hisia zanu zipo sahihi kwakuwa wengi wa makamanda hawa baada ya kustaafu wamekuwa wakijiingiza kwenye siasa za chama tawala. jamani hii sio ile jamii ya hewala bwana. tunaona, tunasikia na TUTAAMUA. Mnadhimu wa JWTZ aliyekubali kubeba maneno ya mtawala na kuja kututishia sisi wananchi anapaswa kujiuzulu maana anaonekana anaweza kutoa amri kwa vikosi vyake kuwashambulia na kuwadhuru raia. Angelikuwa na busara kuwaita hao ambao wanatoa huo uchochezi na kuwaelezea tishio la kuvunjika kwa amani kisha kama hawangemsikiliza ndo angekuja kwetu na kuwashtaki.
CCM mmechemsha big time this year
 
Kwa yeyote aliyesoma mambo ya kijamii atakubaliana na mimi kwamba maendeleo ya binadamu yameambatana na conflict, ingawa conflict does not necessarily means violence. Watanzania tunapotajiwa damu kumwagika tusiogope, Kenya wameanza kuheshimiana baada ya kumwaga damu, Zanzibar hivyo hivyo na nchi nyinginezo. Sisi ni waafrika it seems we are following the same path just like other African countries, people don't learn from mistakes of other countries. Hao wanajeshi tunawalipa sisi wakiwa kwenye makambi yao. Hivi unaweza kumuogopa mfanyakazi wako? Sijawahi kuona ! Sisi ndo waajiri therefore i passionately believe that the CCM strategy of using military men will backfire.
 
CHADEMA ni chama cha matumaini. Matumaini kwamba Tanzania bila ya ufisadi inawezekana. Matumaini kwamba Tanzania inaweza kunufaika
kutokana na maliasili zake. Dr Slaa ameshasema kuwa atapunguza baraza la mawaziri, na hivi kupunguza matumizi ya serikali, na hivi kuongeza matumizi katika elimu ya watanzania. Elimu bure kwa Watanzania inawezekana, kama tutaipa kipaumbele. Na Tanzania inayojitegemea inawezekana, siyo hii ya omba omba mpaka tunaambiwa tungekufa njaa kama Kikwete asingeenda safari za nje.

Elimu bora bure ni zana iliyopitwa na wakati, ilikuweza kushinda katika mabadiliko ya dunia ya sasa elimu bora ya bure 100% imepitwa na wakati...swala la muhimu ni uwezekano wa kuwa na elimu inayotolewa kwa unafuu/bure kutokana na msaada wa serikali bila kuaribu mfumo wa elimu inayotolewa na vyombo binafsi unaoleta ushindani.
Elimu ya bure wakati wa Nyerere nayo ilikuwa na matatizo yake, tukiacha mabaliko ya kijamii, population nk yaliyoko sasa . Hoja kwamba kwa sababu wakati wa Nyerere elimu ilitolewa bure hivyo tunaweza kutoa elimu bure sasa, haitoshi kwa sababu huu ni wakati tofauti na ule wa Nyerere. Inabidi kuleta hoja yenye mchakato mzima utaonyesha vipi elimu ya bure inaweza kutolewa katika kipindi hikii! Tusisahau pia asilimia ngapi % ya budget ya serikali inatoka nje....
 
Kama damu ni kumwagika itamwagika tu whether limesemwa or not. Pili hao unaosema kura zao zitapotea hawafiki hata buku. Utasema watashawishi wengine. Sio rahisi. Tatu hao wanaotilia shaka elimu ya bure waendelee na ccm. Kama wanadhani chadema ni gharama wajaribu ccm
 
Moto umeisha waka hauwezi kuzimika, naona aridhi imeisha chimbika, lazima watu wachague tegemeo lao.

Nimefurahi baada ya kusikia hata wana CCM (hata amabao ni viongozi wa chama) kuwa mwaka huu wanachagua mtu na siyo chama.
 
Hapa unazungumzia idadi ya hao mafisadi na madc nk kutopigia kura chadema?.........kwa harakaharaka unaonekana umeishiwa cha kusema..............90% ya utajiri wa nchi unaliwa na 10% ya watu mafisadi, wenye uchungu na nchi ni zaidi ya 88% ya watz ambao hawafaidi rasilimali za taifa..................slaa kuwalenga hao wachache inasaidia wale wengi wanaokandamizwa kuamka haraka na ndivyo ilivyo na kumpigia kura dr.slaa

1. Ccm hadi hivi sasa imefanya juhudi kubwa za kuifanya chadema ionekane kama chama chenye fujo na kinaharibu "utulivu na amani" wa watanzania!
Chadema bila kujua hila za ccm kimeingia mkenge hasa viongozi wake wanapodai kwamba kura zikiibiwa "damu itamwagika!" kauli hii iliwagharimu cuf na kilionekana ni chama kinachokusudia kuleta fujo, sasa hisia hizo zimehamia chadema!

2. Kauli zinazoashiria kupunguza idadi ya wapiga kura:
- nikiingia madarakani nitamtimua mhariri wa daily news: Mpiga kura huyo baada ya kuisikia kauli hiyo ataipigia kura chadema?
- nikiingia madarakani nitafuta vyeo vya u-dc: Hapa ina maana ma-dc wote hawatampigia kura dkt slaa kwa kuwa automatically vibarua vyao vitaota nyasi.
- nikiingia madarakani nitawaburuza mahakamani mafisadi wote: Hapa ina maana kuwa wale wanaojihisi kuwa ni mafisadi (kwa bahati mbaya hawa wako wengi)hawataipigia kura chadema!
Nk.
Kauli hizi zirekebishwe ili zilenge electorate wote kwa ujumla na si kubagua kwa namna yoyote, hata kama nia ipo ya kufanya hayo! Lugha nzuri itumike ili kuwaelimisha watz maana kila jambo jipya huwa haliaminiki mwanzoni!

3. Ahadi za huduma za jamii (km elimu) kuwa bure: Ahadi hii imekuwa questioned hata na watu wasioenda shule (watu wa kawaida). Hapa yanahitajika maelezo ya ziada na si kudai kuwa tutachukua fedha za epa ambapo hizo fedha zikiisha ndio inakuwaje! Majibu yangekaa kitakwimu zaidi, km kuna idadi kadhaa za wanafunzi, then kila mwanafunzi anagharimiwa kiasi fulani, then bajeti yetu ni kiasi fulani, etc.

haya ndio yangu kwa leo wanajf hasa wanaoitakia mema chadema!

Tujadili!
 
Hivi kazi ya JWTZ ni nini? Kwani kuna watu wanataka kupindua nchi? Ninaona JWTZ wanaingilia kazi za Polisi, kitu ambacho siyo jukumu lao. Kungekuwa na tetesi za machafuko ya kupindua nchi, hapo ningeweza kusema wana haki, lakini kama swala ni wananchi kutaka kulinda kura zao sioni nafasi ya JWTZ kwenye huu uchaguzi.

Sana sana Mnadhimu Mkuu wa JWTZ anazidi kuthibitisha kwamba hali ya CCM ni mbaya na sasa wameamua kutumia hata wanajeshi ili kutisha wapiga kura na wananchi.

Kwa mara ya kwanza serikali iliyoko madarakani imetikiswa na inaona kila dalili kuwa kama kura itapigwa bila mizengwe yeyote wana nafasi ndogo sana ya kuendelea kukaa madarakani.
Ni mara ya kwanza kwa rais aliyeko madarakani kupingwa wazi wazi kwenye kampeni na wananchi wake (Bukombe na Nzega wananchi walimpinga hadharani kwa kumwonyesha alama zinazotumiwa na vyama pinzani kuonyesha kutoridhishwa kwao na maamuzi anayoyachukua kama rais na mwenyekiti wa chama tawala).
Kwa hiyo wanaanza kuleta chokochoko ili uchaguzi uvurugike ama wapate kibari bandia cha kulitumia jeshi la wananchi kusimamia zoezi la kuipiga kura na hivyo iwe rahisi kwao kuchakachua kura!
Kama CHADEMA hawatatumia busara watafanikiwa, lakini kama Chadema watakuwa makini na kuvishawishi vyama vingine kuwa wananchi waruhusiwe kukaa kwenye vituo baada ya kupiga kura na wawahubiri wananchi na wapenzi wao umuhimu wa kutoonyesha dalili zozote za fujo hata pale watakapochokozwa! Wahakikishe hawakubali kuingizwa kwenye malumbano na watu wanaovamia mikutano yao, wasiruhusu kuingia kweny fujo kwa namna yoyote ile!
Vinginevyo uchaguzi utasimamiwa na JWTZ na hakutakuwa na mtu wa kuhakikisha kuwa kura haziibiwi kwani wote watakuwa majumbani mwao
 
Kwa nini wanaotaka kumwaga damu wasiende Muhimbili ambapo zinahitajika?

Be realist man,unajua kabisa kuanzia kampeni mpaka uachaguzi na mwisho utangazwaji wa matokeo utakuwa biased.Na unajua fika ni kwanini ccm haitaki kutoka madarakani,Hakuna anayependa damu imwagike,haki ya mtu haibiwi kirahisi.Hatuna tofauti na nchi nyingine za Afrika,viongozi waliopo madarakani hawa hawakubali kushindwa kirahisi.
 
Mkuu Buchanan,

Nakubaliana na wewe kuhusu swala la kauli za damu itamwagika. Tatizo la siasa za Tanzania ni kwamba chama kikishaonekana kuwa threat kwa CCM, whether utumie lugha laini au nyepesi au kauli nzuri, bado tu utavikwa ubaya hata kama ni wa kuokoteza. So, hai-make any difference.

Swala la mafisadi/Mkumbwa Alli, nadhani hapo wanaweza kutamka tu kwamba serikali mpya itafuata utawala wa sheria. Including kuwashughulikia hao mafisadi. Hata asipotaja kwamba atawafikisha mafisadi mahakamani, bado mtu yeyote ambaye anajijua ana matatizo ya kifisadi, hawezi kukipigia kura chama ambacho anajua kitakuja kufuata utawala wa sheria. Hivi unategemea mtu ambaye amezowea kuishi kwa misheni town anaweza kuipigia kura CHADEMA hata wasiposema kwamba watawashughulikia mafisadi? Bado proportion ya mafisadi ni ndogo sana hata ukijumlisha na extended family zao. Mafisadi kwanza huwa hawana undugu wala ujamaa, unaweza kushangaa mtu fisadi lakini some of his/her extennded family wako choka mbaya na wakisikia kwamba jamaa kapatwa na kasheshe wanashangilia kabisa. Mzee mzima alipoachia Uwaziri Mkuu kuna some of his extended family members walishangilia sana.

Kumwagika kwa damu kumeanza leo au kutaanza leo? Au hatujui kuwa uongozi ulioko mikono yao inanuka damu. Damu mnayoiongelea ni ipi hasa? Ile ya rangi nyekundu? Ama mpaka uchinjaji ufanyike ndo mnaouita damu kumwagika?
Mimi damu ni unyanyasaji wa waziwazi, watu kukosa haki yao, watu kukosa huduma stahili, watu nkutopata elimu stahili, watu kunyimwa haki za kumiliki mali halali za nchi yao, vijana wetu kukosa ajira kisa tumekumbatia wageni nk. Huko ndiko kumwagika damu. So damu zinamwagika kila siku tangu miaka hiyo. Hii ya CHADEMA kusema hivyo itakuwa hivyo kama watu WATAHISI KUWA HAWAKUTENDEWA HAKI! Enzi za kuwadanganya Watu umefikia Tamati, ufike wakati watu unaowaongoza uwaeleze jibu sahihi na sio kama wakati ule unamwona mama ana mimba unaambiwa anakula sana kashiba mara anakuja na mtoto mchanga unaambiwa kadondoshwa na ndege! Watoto wa miaka ya sasa wanajua mama ana mimba na huko tumboni kuna mtoto! Kwa nini tusibadilike na kuona kuwa hawa watu sasa wana akili na sio wale wa utawala ule?
 
Hatutaki kura za criminals. Hivyo sikubaliani nawe. Maana si watanzania wote ambao ni criminals. wengi wa watanzania ni watu wema sana na wamechoka na umaskini wa kufanyiziwa.
Tunahitaji hatua kali zichukuliwe kwa criminals full stop.
ni kweli , kabisa wapenda mabadiliko wengi ni watu ambao sio criminal, kwahiyo mafisadi wananafasi ndogo sana ktk ushindi wa CHADEMA
 
Wapiga kura ni lazima wajue wanachochagua. Hakuna kuwalaghai. Ni lazima nchi igawanyike kati ya wanaounga mkono CCM na wanaounga mkono Chadema. Wananchi wajue Dr. Slaa akiingia atafanya nini. There is no middle ground.
kabisa mkulu
 
Back
Top Bottom