Ushauri wa Bure kwa CHADEMA: Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili! - Kuepusha Shari, Kubalini Kosa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Hakuna ubishi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kiko kwenye mgogoro mkubwa!. Ushindi wa Zitto kwenye pingamizi, ni nusu shari tuu, shari kamili ni ushindi wake kwenye kesi ya msingi ambao utatengua maamuzi yote ya CC ya Chadema yaliyomvua nyadhifa zake kinyume cha sheria, taratibu na kanuni kwa mujbu wa katiba ya Chadema!, aminini msiamini, Chadema itaaibika, itafedheheshwa, itafedheheka na itatahayari! huku ikiendelea kupoteza credibility yake ambayo tayari imeishaanza kupotea!, hivyo naishauri Chadema, yote yaliyotokea mpaka hapa, hiyo ni nusu shari tuu, ni a "Heri Nusu Shari, kuliko Shari Kamili!", wenye busara wa Chadema kama mpo, nawashauri muepushe shari kamili!.

Kunapotokea mgogoro unaotokana na makosa ya wazi ya kiutendaji kutaka kukomoana kwa kutunishiana misuli, kwa kawaida kuna mwashishaji na mmaliziaji yaani "Anza wewe, mimi namaliza!", ipo namna kwa Chadema kujiponya na dhahama hii ilioianzisha, kabla mmaliziaji hajaimaliza!, dawa ni kujishusha tuu kwa kukubali yaishe bila kutafuta mshindi na mshindwa, wakaitana, mkosaji akaomba msamaha, mkosewaji akaifuta kesi, na kukubali ama kuendelea kama zamani, au kuachsana kwa usalama na sio kufukuzana, kutimuana na kutunishiana misuli!.

Wana Chadema wengi kwanza hata hawaelewi katiba yao inasema nini!, sikuile nimeuliza humu kuhusu kile kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya katiba ya Chadema kiliondokaje, Katibu Mkuu Mzima wa Chadema alikuja humu, akatamka wazi kuwa kipengele hicho hakikuwahi kuwepo!, ndipo JJ. Mnyika akaokoa jahazi kwa kueleza kilicho tokea!. Hivyo watu humu wanapiga kelele nyingi, huku hawaelewe maudhui ya kesi ya msingi, Zitto ameomba muhtasari wa kikao kilichomvua uongozi ili aweze kukata rufaa!, kikao hicho kilichomvua uongozi kilifanya madudu ya ajabu!, halafu watu wanakuja humu kusifia ujinga!, Chadema hapo ilipo, ni kama mtu anaoga mtoni, kisha mwendawazi kaja na kukimbia na nguo zako!, mwenye busara, atachutama tuu na kuendelea kujisetiri mpaka msaada uje, lakini inachofanya sasa Chadema, ni kutoka ndani ya maji hivyo hivyo kama ilivyozaliwa, na kuanza kumkimbiza mwendawazimu anayekimbia na nguo zake!.

Kwenye baadhi ya migogoro, kuna mkosaji na mkosewaji. Kwenye hili la Zitto, Chadema ndie mkosaji, ndie aliyelianzisha, anachofanya Zitto ni kumalizia tuu!. Dawa ya tatizo kwanza ni kulitambua kosa ni lipi, ukiisha litambua kosa, unakubali makosa, unajishusha na kujinyenyekeza, unatubu kosa, unaomba msamaha, mnasameheana, mnashikana mikono, mnakumbatiana, mnayasahau yaliyopita sii ndwele, mnaganga yajayo ikiwemo Zitto kufuta kesi!.

Mimi Pasco wa JF, siku zote nimekuwa nikilia na matatizo ya Chadema kufanya maamuzi ya papara, kibabe, jazba ambayo ni kinyume cha katiba yake kwa kuwaadhibu wanachama wake kwa kuwafutia uanachama!. walianza na Kafulila, hadi akaitwa sisimizi!, mimi nililalamika humu!. Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA -
Kama ni kufukuzani, fine, lakini kutumia taratibu, sheria na kanuni walizo jipangia , sababu zisiwe chuki binafsi, makundi, au kutofautiana kambi,hali ilivyo CCM kwa sasa ingetakiwa iwe ndio oportunity kwa Chadema ku-seize, lakini nanyi ndio mnaanza...
Walipowatimua wale madiwani wa Arusha, mimi nililalamika humu ....Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
Kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama madiwani wake wa Arusha, is "A Big Mistake"!, and there is a price to pay, so Chadema must pay the price which is very high!.

1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni 'unconstitutional' na kiwe struck out from the books of law!. Naamini Chadema hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho ambacho ni bad law, to its advantage, is "A Big Mistake!".

2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is "A Big Mistake!".

3. Sisi ambao hatuna vyama, lakini tuna shauku ya kuona Tanzania inaongozwa na chama mbadala, tumekuwa na imani kubwa sana na Chadema kama ndicho chama pekee mbadala ambacho kimethibitisha kikiaminiwa, kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo tunategemea Chadema kitafanya maamuzi yanayofuata misingi ya haki. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".
Walipowatimua kina Shonza na genge lake, nililalamika sana humu kuhusu ukiukwaji wa katiba sgeria na kanuni kwa kuendesha kangaroo court na nilililalamika humu...Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...
Tangu jana baada ya uamuzi wa BAVICHA kuwavua uanachama wake baadhi ya wanachama wake hivyo kuwafanya wanachama hao kupoteza uanachama wao wa CHADEMA, naomba kutoa wito kwa Uongozi wa CHADEMA, kuwatendea haki wanachama wake, ili kujenga imani kuwa CHADEMA itawatendea haki Watanzania come 2015 just in case!.

Ushauri huu lengo lake ni kutuaminisha sisi Watanzania wengine tusio wanachama wa CHADEMA, kuwa Chadema ni chama cha haki na kinafanya maamuzi yake kwa kufuata misingi ya haki hivyo kutupa matumaini kuwa CHADEMA inaweza kuaminika na kukabidhiwa nchi mwaka 2015!, vinginevyo kwa mambo haya kama yalivyo sasa, na kama CHADEMA haitabadilika, then kwa 2015 CHADEMA itakuwa bado haijakomaa kiasi cha kutosha kuaminika na kukabidhiwa nchi!.

Chadema walipojidai hawamtambui JK na kuisusia ile hotuba yake, niliwalalamikia humu kuwa ile ilikuwa ni zuga tuu!. Zitto alisimama kwenye ukweli na sio kujiunga na hiyo zuga! na hapa ndipo dhana ya usaliti ilipoanza kukolezwaChadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua JK kama Rais, Wanampongeza! Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.
Mbowe amewashukuru wapiga kura kwa kura walizoipigia Chadema!.
Hiki Mbowe alichokifanya Bungeni, ndicho Dr. Slaa alichotakiwa kukifanya ile siku ya kutangazwa matokeo!
Nilisema that was a golden missed opportunity. Sasa Mbowe amerekebisha makosa ya Dr. Slaa. Chadema sasa inarudi juu!
Chadema sasa tusonge mbele, hata mimi nikirudi uraiani, naweza kufikiria kujiunga Chadema, kuimarisha nguvu!
Asante sana Mhe. Freeman Mbowe!.
Na sio mara ya kwanza kwa Chadema kufanya makosa ya kimsingi kabisa ya kisheria, taratibu na kanuni!, Waliposusia mchakato wa katiba na kutoka nje, niliwaeleza humu kuwa Lissu amewapoteza!, hakuupinga muswada ule kwa mujibu wa kanuni, bali yeye ndie alitoa go ahead ukapita kisha wakajifanya kususa, nililisemea sana hili hapa!.Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.
Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja CCM kuhodhi madaraka yote ya dola.

Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.

Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).

Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.

2015 sio mbali kihivyo!.
Sasa na hili la Zitto, kufuatia Chadema kuzoea vile vya kunyonga kwa kangaruu court zake, kwa Zitto, wamekutana na vya kuchinja!. Wao walidhani Zitto ni jina tuu, wakijiaminisha sio mzito!, wala hana uzito wowote, wakatunisha msuli wakidhani ni chepesi, kumbe kiukweli, Zitto ni Zitto kweli, sio jina tuu, bali ni Mzitto haswa!, sio mtu wa kukisukumizia kule kama kila ki "sisimizi!", hapa sasa Chadema imekutana na kisiki!, tena kisiki chenyewe cha mpingo!, kutoka kulee mwisho wa reli!. Kilichoshafanyika ni kwa Chadema kujikwaa tuu katika kisiki hiki, na kujikwaa sio kuanguka!, busara ni kwa Chadema kuangalia imejikwaa wapi, ili mbele ya safari isije kujikwaa tena, na hatimaye hata ikaja kuanguka!.

Kama kwenye Chadema bado kuna wenye busara wachache, nawashauri watafute legal ipinion kwa wanasheria nguli zaidi ya hao inaowategemea, wawaambia position yao kwenye shauri la msingi!, dawa ni kumuangukia tuu Zitto, kumuomba msamaha kwa yote, kumuomba afute kesi, na amini nawaambieni Zitto, baadada ya kuujua ukweli wa mambo kuhusu Chadema, atajiondokea zake, kistaarabu na kwa heshima!.

Alipojiunga kuna mambo hakuyajua kuhusu Chadema!, kuna baadhi ya viongozi wake alidhania ni watu wenzake!, kumbe "machoni tuu ni kama watu!. Alipojiunga alidhania Chadema ni chama cha wote!, kumbe Chadema ni chma cha watu, kina wenyewe!, hivyo kesi ataifuta, atawaachia wenyewe chama chao na ama aamue kuendelea na siasa ila kama anajipenda maisha yake!, aachane kabisa na siasa! wenye uelewa wataelewa ni kwa nini!.

Moja ya makosa makubwa kabisa ya Chadema, ni not doing the right thing at the right time and doing it right!. Niliwaeleza hapa!, Kwenye hili sakata la Zitto, Chadema did the wrong thing!, at the wrong time, and did it wrongly!.But it still has the chance to do the right thing kurekebisha makosa, tena at the right time, before its too late, and it got to do it right!.Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
Chadema is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.

  • Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.
  • Imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.

Naongea kama nani au nashauri kama nani?!. Mimi sio mwanachama wa chama chochote, ila ni mlipa kodi wa JMT. Chadema is a public party paid by taxpayers money, hivyo Chadema kinaendeshwa kwa kodi yangu!. The public has the right to know its public and private conduct, and when it does wrong!, ni haki yangu kukiambia, kukikosoa na kukishauri.

Why kila siku Chadema tuu, kwani vyama vingine havipo?!. Jibu ni "mti wenye matunda!".

Mpira uko uwanjani, its up to Chadema kuamua kusuka au kunyoa!.

The choice is yours!.

Pasco.
 
Hahha!
At it Again,
Hivi Huo Muhtasari unajua jinsi mchakato wake wa kuuandaa ulivyo?
By the way unajua kuwa Muhatasari upo Tayari kwa sasa?

Pili wengi wenu mnataka aadhibiwe na Baraza Kuu, Hivi umeisoma Katiba yao, Mfano angeadhibiwa na Baraza kuu angeenda Kukata Rufaa wapi? Au kwa Msajili wa vyama?

Kifupi karibia yote uliyo yashabikia umeshindwa kuanzia kafulila, Madiwani arusha, Shoza , Na hili naamini Utahaibika tu.
 
usiishauri chadema kwa hisia za ccm ........punguza hisia wewe hata siku moja huoni kosa la zito ni chadema tu,chadema inasimamia katba yake...nibora chadema ife kuliko huyo zitto aendelee kuwa chadema kamati kuu fukuzeni huyo aliyeleta ubaguzi mbaya kabisa kwenye chama..
 
Wisdom misused is wisdom abused. Why should you care ilhali unajulikana sio tu ni CCM damu bali pia mmoja wa watu wanaoombea CDM ife kifo hata cha ghafla?

Baadhi ya Watanzania wenzetu wana tabia ya dharau flani dhidi ya wenzao. Do you seriously think Chadema nzima haina watu wenye kuweza kuipa ushauri wa busara na manufaa kwao? Rules are simple, never ever entertain "free offers" from your enemy. Ushauri wowote 'mwema' kutoka kwa wana-CCM kwa CDM unaambatana na 'dua za kimoyomoyo' kutamani chama hicho cha upinzani kife.

Kwanini 'busara' hizo zisielekezwe CCM? Hicho ni chama tawala, na kwa maana hiyo lolote linaloihusu linawagusa Watanzania wote.Ifike mahala mjiskie aibu wenyewe: hamwezi kuiombea dua jema CDM huku mnahangaika 'kuiroga'

All I'm expecting from CDM is a big THANKS, BUT NO THANKS.
 
wakimuacha zitto itakuwa hakuna tofauti kati ya ccm na chadema kwani tofauti kubwa hivi sasa ni kitendo cha chadema kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia na kitendo cha madiwani wa ccm bukoba kuitisha ccm na mwenyekiti wa taifa kutishika na kuwarudishia udiwani wao kilionyesha udhaifu mkubwa sana kwa ccm kwahiyo chadema wasiige mfano huo kabisa. pasco anataka chadema itumie formula mbaya ya ccm kuendeshea chama chao that is insane.
 
Habari Pasco,
Kama ilivyo kawaida,ni kwa uchache nakutana na post za maana kama zako huku ndani..
Nafarijika sana ninapokutana na mtu sober kama mimi kwenye masuala ya vyama,hasa zaidi paleanapoamua kutoa mchango wake kwenye haya yanayoondelea nchini!
Kama ulivyoelezea hapo juu kuwa sober hakumzuii mtu kuchangia,kukosoa au kutoa mawazo ya aina yoyote ili mradi yawe ndani ya uzio wa ustarabu,kama vyama vinapata ruzuku na hiyo ruzuku ni kodi yangu basi niko sahihi kushauri upande wowote unapokosea!

Tangu hapo kupitia matukio ya nyuma nilishaanza kujiaminisha wafuasi wengi wa hivi vyama vya siasa hawana elimu tosha juu ya vyama vyao,sio CHADEMA,sio CCM..
Hilo suala la Zitto sasa ndo limekuja kufanya confirmation kichwani kwangu yale niliyokuwa nayadhania ni ya kweli,wafuasi wengi wa hili sakata hawana details za issue nzima
Wengi wa wanachama kama sio wafuasi wa CHADEMA ni emotional driven creatures,rational functioning imelala doro
Unamuuliza mtu mbona unatoa matusi hivyo,anasema zitto msaliti unauliza kivipi,na kama mmeshajiaminisha kasaliti kambi katika yenu inasemaje juu ya kosa hilo,mchakato wa kumpa adhabu unakuwa exercised vipi?hana majibu! Ndo kwanza umempandisha jazba,anamultiply yale matusi anamtukana mara 5 yake sasa..

Sasa unakaa chini unajiuliza,hivi vyama vya siasa si department ya maana sana kwenye maendeleo ya nchi yoyote?mbona watu wanavichukulia so lightly hivi?
Mbona watu wamevigeuza team za mpira,yaani huhitaji kujua mmiliki nani,uongozi ukoje,uko focused tu kwenye dakika 90 pale upate either entertainment na results nzuri au frustrations!
Yaani idadi kubwa ya washabiki wa hili sakata hawajui hata Zitto ana hoja gani pale mahakamani,achilia mbali uongozi wenye kiburi na ubabe uliokwishaelezea vizuri hapo juu..

Nimalize kwa kusema,kaka..waweza kuwa umetumia muda wako wa maana sana kuandika andiko hilo la ushauri ila ukubaliane na mimi hakuna kitu kigumu kama kumshauri au kubadilisha stance ya an emotional driven person,CHADEMA wengi ni emotional driven ni sawa sawa na kwenda sasa hivi kumuambia kijana wa miaka 16 wa kipalestina waisrael sio watu wabaya,wakae chini wasolve tofauti zao..ngumu sana!
Ukisharuhusu hisia zikutawale unafunga milango mingi ya ufahamu!

Tarajia ngonjera,vijembe na vurugu zao wakiamka
Nawaitaga the E-Team(whereby E stands for EMOTIONS)
Subiria the E-Team ije usadiki niliyoandika!
Usiku mwema!
 
Hahha!
At it Again,
Hivi Huo Muhtasari unajua jinsi mchakato wake wa kuuandaa ulivyo?
By the way unajua kuwa Muhatasari upo Tayari kwa sasa?

Pili wengi wenu mnataka aadhibiwe na Baraza Kuu, Hivi umeisoma Katiba yao, Mfano angeadhibiwa na Baraza kuu angeenda Kukata Rufaa wapi? Au kwa Msajili wa vyama?

Kifupi karibia yote uliyo yashabikia umeshindwa kuanzia kafulila, Madiwani arusha, Shoza , Na hili naamini Utahaibika tu.
Mkuu nadhani mnashindwa kuelewa ni kwamba hukumu ya kamati kuu ilipokelewa japo ZZK mwenyewe alisema hakuhojiwa ili atoe utetezi wake. Hilo hatulitazami zaidi isipokuwa unaposhtakiwa kwa makosa kadhaa kusomewa mashataka ama kupewa karatasi iloandikwa mashtaka ili uyatolee utetezi haina maana yoyote ikiwa tayari hukumu imeshatolewa. Hivyo kilichotakiwa ni kamati kuu kumpa HUKUMU yao kimaandishi ili apate kuweka pingamizi la hukumu hiyo. Huwezi kuwakilisha mashtaka 11 tena kwa baraza kuu ili kukata rufaa, bali kutokubaliana na hukumu yenyewe. Kama tunavyokata rufaa ktk kesi za mahakamani uraiani, hupekleki madai uloshtakiwa bali hukubalinai na hukumu. Chombo cha juu kinatazama hukumu hiyo kulinganisha Utetezi na ushahidi yalokuwepo!

Sasa maadam uongozi wetu wamekataa kumpa hukumu hiyo ili apate kukata rufaa, hapo ndipo wanapochezeana akili. Kwa nini hawataki kumpa ili akate rufaa na kisha baraza kuu liamue kuhsu hukumu alopewa kama anastahili au laa! Je, kuna uwezekano ya kwamba wajumbe wa baraka kuu nao wanaamini kunatakiwa mageuzi ya uongozi ndani ya chama hivyo kamati kuu inahofia hilo? au kamati kuu ina wasiwasi na wajumbe wengi kuwa upande wa Zitto kama ilivyokuwa CCM ktk kesi ya Magamba walipotaka kumwengua Lowassa na kundi lake?
 
Wanabodi,

Hakuna ubishi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kiko kwenye mgogoro mkubwa!. Ushindi wa Zitto kwenye pingamizi, ni nusu shari tuu, shari kamili ni ushindi wake kwenye kesi ya msingi ambao utatengua maamuzi yote ya CC ya Chadema yaliyomvua nyadhifa zake kinyume cha sheria, taratibu na kanuni kwa mujbu wa katiba ya Chadema!, aminini msiamini, Chadema itaaibika, itafedheheshwa, itafedheheka na itatahayari! huku ikiendelea kupoteza credibility yake ambayo tayari imeishaanza kupotea!, hivyo naishauri Chadema, yote yaliyotokea mpaka hapa, hiyo ni nusu shari tuu, ni a "Heri Nusu Shari, kuliko Shari Kamili!", wenye busara wa Chadema kama mpo, nawashauri muepushe shari kamili!.

Kunapotokea mgogoro unaotokana na makosa ya wazi ya kiutendaji kutaka kukomoana kwa kutunishiana misuli, kwa kawaida kuna mwashishaji na mmaliziaji yaani "Anza wewe, mimi namaliza!", ipo namna kwa Chadema kujiponya na dhahama hii ilioianzisha, kabla mmaliziaji hajaimaliza!, dawa ni kujishusha tuu kwa kukubali yaishe bila kutafuta mshindi na mshindwa, wakaitana, mkosaji akaomba msamaha, mkosewaji akaifuta kesi, na kukubali ama kuendelea kama zamani, au kuachsana kwa usalama na sio kufukuzana, kutimuana na kutunishiana misuli!.

Wana Chadema wengi kwanza hata hawaelewi katiba yao inasema nini!, sikuile nimeuliza humu kuhusu kile kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya katiba ya Chadema kiliondokaje, Katibu Mkuu Mzima wa Chadema alikuja humu, akatamka wazi kuwa kipengele hicho hakikuwahi kuwepo!, ndipo JJ. Mnyika akaokoa jahazi kwa kueleza kilicho tokea!. Hivyo watu humu wanapiga kelele nyingi, huku hawaelewe maudhui ya kesi ya msingi, Zitto ameomba muhtasari wa kikao kilichomvua uongozi ili aweze kukata rufaa!, kikao hicho kilichomvua uongozi kilifanya madudu ya ajabu!, halafu watu wanakuja humu kusifia ujinga!, Chadema hapo ilipo, ni kama mtu anaoga mtoni, kisha mwendawazi kaja na kukimbia na nguo zako!, mwenye busara, atachutama tuu na kuendelea kujisetiri mpaka msaada uje, lakini inachofanya sasa Chadema, ni kutoka ndani ya maji hivyo hivyo kama ilivyozaliwa, na kuanza kumkimbiza mwendawazimu anayekimbia na nguo zake!.

Kwenye baadhi ya migogoro, kuna mkosaji na mkosewaji. Kwenye hili la Zitto, Chadema ndie mkosaji, ndie aliyelianzisha, anachofanya Zitto ni kumalizia tuu!. Dawa ya tatizo kwanza ni kulitambua kosa ni lipi, ukiisha litambua kosa, unakubali makosa, unajishusha na kujinyenyekeza, unatubu kosa, unaomba msamaha, mnasameheana, mnashikana mikono, mnakumbatiana, mnayasahau yaliyopita sii ndwele, mnaganga yajayo ikiwemo Zitto kufuta kesi!.

Mimi Pasco wa JF, siku zote nimekuwa nikilia na matatizo ya Chadema kufanya maamuzi ya papara, kibabe, jazba ambayo ni kinyume cha katiba yake kwa kuwaadhibu wanachama wake kwa kuwafutia uanachama!. walianza na Kafulila, hadi akaitwa sisimizi!, mimi nililalamika humu!. Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA - Walipowatimua wale madiwani wa Arusha, mimi nililalamika humu ....Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"
Walipowatimua kina Shonza na genge lake, nililalamika sana humu kuhusu ukiukwaji wa katiba sgeria na kanuni kwa kuendesha kangaroo court na nilililalamika humu...Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...

Chadema walipojidai hawamtambui JK na kuisusia ile hotuba yake, niliwalalamikia humu kuwa ile ilikuwa ni zuga tuu!. Zitto alisimama kwenye ukweli na sio kujiunga na hiyo zuga! na hapa ndipo dhana ya usaliti ilipoanza kukolezwaChadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.

Na sio mara ya kwanza kwa Chadema kufanya makosa ya kimsingi kabisa ya kisheria, taratibu na kanuni!, Waliposusia mchakato wa katiba na kutoka nje, niliwaeleza humu kuwa Lissu amewapoteza!, hakuupinga muswada ule kwa mujibu wa kanuni, bali yeye ndie alitoa go ahead ukapita kisha wakajifanya kususa, nililisemea sana hili hapa!.Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!
Sasa na hili la Zitto, kufuatia Chadema kuzoea vile vya kunyonga kwa kangaruu court zake, kwa Zitto, wamekutana na vya kuchinja!. Wao walidhani Zitto ni jina tuu, wakijiaminisha sio mzito!, wala hana uzito wowote, wakatunisha msuli wakidhani ni chepesi, kumbe kiukweli, Zitto ni Zitto kweli, sio jina tuu, bali ni Mzitto haswa!, sio mtu wa kukisukumizia kule kama kila ki "sisimizi!", hapa sasa Chadema imekutana na kisiki!, tena kisiki chenyewe cha mpingo!, kutoka kulee mwisho wa reli!. Kilichoshafanyika ni kwa Chadema kujikwaa tuu katika kisiki hiki, na kujikwaa sio kuanguka!, busara ni kwa Chadema kuangalia imejikwaa wapi, ili mbele ya safari isije kujikwaa tena, na hatimaye hata ikaja kuanguka!.

Kama kwenye Chadema bado kuna wenye busara wachache, nawashauri watafute legal ipinion kwa wanasheria nguli zaidi ya hao inaowategemea, wawaambia position yao kwenye shauri la msingi!, dawa ni kumuangukia tuu Zitto, kumuomba msamaha kwa yote, kumuomba afute kesi, na amini nawaambieni Zitto, baadada ya kuujua ukweli wa mambo kuhusu Chadema, atajiondokea zake, kistaarabu na kwa heshima!.

Alipojiunga kuna mambo hakuyajua kuhusu Chadema!, kuna baadhi ya viongozi wake alidhania ni watu wenzake!, kumbe "machoni tuu ni kama watu!. Alipojiunga alidhania Chadema ni chama cha wote!, kumbe Chadema ni chma cha watu, kina wenyewe!, hivyo kesi ataifuta, atawaachia wenyewe chama chao na ama aamue kuendelea na siasa ila kama anajipenda maisha yake!, aachane kabisa na siasa! wenye uelewa wataelewa ni kwa nini!.

Moja ya makosa makubwa kabisa ya Chadema, ni not doing the right thing at the right time and doing it right!. Niliwaeleza hapa!, Kwenye hili sakata la Zitto, Chadema did the wrong thing!, at the wrong time, and did it wrongly!.But it still has the chance to do the right thing kurekebisha makosa, tena at the right time, before its too late, and it got to do it right!.Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Naongea kama nani au nashauri kama nani?!. Mimi sio mwanachama wa chama chochote, ila ni mlipa kodi wa JMT. Chadema is a public party paid by taxpayers money, hivyo Chadema kinaendeshwa kwa kodi yangu!. The public has the right to know its public and private conduct, and when it does wrong!, ni haki yangu kukiambia, kukikosoa na kukishauri.

Why kila siku Chadema tuu, kwani vyama vingine havipo?!. Jibu ni "mti wenye matunda!".

Mpira uko uwanjani, its up to Chadema kuamua kusuka au kunyoa!.

The choice is yours!.

Pasco.
Nasikia harufu ya Bangi tu!
 
Habari Pasco,
Kama ilivyo kawaida,ni kwa uchache nakutana na post za maana kama zako huku ndani..
Nafarijika sana ninapokutana na mtu sober kama mimi kwenye masuala ya vyama,hasa zaidi paleanapoamua kutoa mchango wake kwenye haya yanayoondelea nchini!
Kama ulivyoelezea hapo juu kuwa sober hakumzuii mtu kuchangia,kukosoa au kutoa mawazo ya aina yoyote ili mradi yawe ndani ya uzio wa ustarabu,kama vyama vinapata ruzuku na hiyo ruzuku ni kodi yangu basi niko sahihi kushauri upande wowote unapokosea!

Tangu hapo kupitia matukio ya nyuma nilishaanza kujiaminisha wafuasi wengi wa hivi vyama vya siasa hawana elimu tosha juu ya vyama vyao,sio CHADEMA,sio CCM..
Hilo suala la Zitto sasa ndo limekuja kufanya confirmation kichwani kwangu yale niliyokuwa nayadhania ni ya kweli,wafuasi wengi wa hili sakata hawana details za issue nzima
Wengi wa wanachama kama sio wafuasi wa CHADEMA ni emotional driven creatures,rational functioning imelala doro
Unamuuliza mtu mbona unatoa matusi hivyo,anasema zitto msaliti unauliza kivipi,na kama mmeshajiaminisha kasaliti kambi katika yenu inasemaje juu ya kosa hilo,mchakato wa kumpa adhabu unakuwa exercised vipi?hana majibu! Ndo kwanza umempandisha jazba,anamultiply yale matusi anamtukana mara 5 yake sasa..

Sasa unakaa chini unajiuliza,hivi vyama vya siasa si department ya maana sana kwenye maendeleo ya nchi yoyote?mbona watu wanavichukulia so lightly hivi?
Mbona watu wamevigeuza team za mpira,yaani huhitaji kujua mmiliki nani,uongozi ukoje,uko focused tu kwenye dakika 90 pale upate either entertainment na results nzuri au frustrations!
Yaani idadi kubwa ya washabiki wa hili sakata hawajui hata Zitto ana hoja gani pale mahakamani,achilia mbali uongozi wenye kiburi na ubabe uliokwishaelezea vizuri hapo juu..

Nimalize kwa kusema,kaka..waweza kuwa umetumia muda wako wa maana sana kuandika andiko hilo la ushauri ila ukubaliane na mimi hakuna kitu kigumu kama kumshauri au kubadilisha stance ya an emotional driven person,CHADEMA wengi ni emotional driven ni sawa sawa na kwenda sasa hivi kumuambia kijana wa miaka 16 wa kipalestina waisrael sio watu wabaya,wakae chini wasolve tofauti zao..ngumu sana!
Ukisharuhusu hisia zikutawale unafunga milango mingi ya ufahamu!

Tarajia ngonjera,vijembe na vurugu zao wakiamka
Nawaitaga the E-Team(whereby E stands for EMOTIONS)
Subiria the E-Team ije usadiki niliyoandika!
Usiku mwema!
Harufu nziiito ya bangi!... umesoma katiba? au unakurupuka tu!
 
Mkuu nadhani mnashindwa kuelewa ni kwamba hukumu ya kamati kuu ilipokelewa japo ZZK mwenyewe alisema hakuhojiwa ili atoe utetezi wake. Hilo hatulitazami zaidi isipokuwa unaposhtakiwa kwa makosa kadhaa kusomewa mashataka ama kupewa karatasi iloandikwa mashtaka ili uyatolee utetezi haina maana yoyote ikiwa tayari hukumu imeshatolewa. Hivyo kilichotakiwa ni kamati kuu kumpa HUKUMU yao kimaandishi ili apate kuweka pingamizi la hukumu hiyo. Huwezi kuwakilisha mashtaka 11 tena kwa baraza kuu ili kukata rufaa, bali kutokubaliana na hukumu yenyewe. Kama tunavyokata rufaa ktk kesi za mahakamani uraiani, hupekleki madai uloshtakiwa bali hukubalinai na hukumu. Chombo cha juu kinatazama hukumu hiyo kulinganisha Utetezi na ushahidi yalokuwepo!

Sasa maadam uongozi wetu wamekataa kumpa hukumu hiyo ili apate kukata rufaa, hapo ndipo wanapochezeana akili. Kwa nini hawataki kumpa ili akate rufaa na kisha baraza kuu liamue kuhsu hukumu alopewa kama anastahili au laa! Je, kuna uwezekano ya kwamba wajumbe wa baraka kuu nao wanaamini kunatakiwa mageuzi ya uongozi ndani ya chama hivyo kamati kuu inahofia hilo? au kamati kuu ina wasiwasi na wajumbe wengi kuwa upande wa Zitto kama ilivyokuwa CCM ktk kesi ya Magamba walipotaka kumwengua Lowassa na kundi lake?

Labda sijuhi, Ila nilivyoelewa mimi ni kuwa kila kinachotokea Kamati kuu lazima kiandaliwe na baada ya Kuandaliwa kithibitishwe na Kamati kuu ndipo kinaweza kutoka kama kitu kilichokamilika.

Juzi tumesoma na tumesikia baada ya Kikao ch KK, hiyo ripoti unayoililia ipo tayari na imepitishwa na Mtuhumiwa akiitaka akaichukue ofisini ili aendelee na Pricedure nyingine za kukata rufaa.

Au hujalisikia hilo?

Hivi hata mahakamani hukumu ikitolewa ripoti inapatikana hapohapo?

Pia umengangania sana kuhojiwa, hivi ni kweli hakuhojiw anadani ya kikao ? Kama hakuhojiwa ilikuwaje wakubali kujivua wenyewe Vyeo?

Kuhusu Baraza kuu:
Naamini wewe sio mgeni Unless ilikuwa ni Cinema, Hivi nimarangapi tumesikia Baraza kuu likiwaka moto na watu hawamtaki Zitto na wanataka achukuliwe hatua? UmesAhaau? Au ilikuwa ni Maigizo? Maana mara zote inasemekana Mbowe alikuwa akiingilia na Kumtetea.

By the way Mkandara hivi unadhani CHADEMA inaenda kufa kisiasa au ZITTO anaenda kufa kisiasa ?
 
Last edited by a moderator:
Siasa za vyama huendeshwa kwa ufanisi tu iwapo kuna mshikamano mkubwa sana miongoni mwa key players hata kama wanatofautiana kimtizamo. Ndiyo maana baada ya primaries ambamo huwa key players anaburuzana, huwa wanakutana tena kuondoa tofauati zao na kujenga masikamano tena. Ndani ya CDM hali imekuwa siyo shwari tangu uchaguzi wa 2010 ambapo Zitto alizuiwa au aliombwa kutogombea uenyeketi. Hata zile kampeini za mwaka huo, Zito hakutumia influence yake vya kutosha kukisaidia chama chake bali aliwasaidia marafiki zake tu. Na baada ya uchaguzi kuisha mambo yamekuwa vivyo hivyo. Miaka minne tangu uchaguzi na bado kuna rift kubwa sana baina ya key players wakati umebaki mwaka mmoja tu kuelekea uchaguzi mwingine wala hakuna uwezekano wa kukutana na kujijenga tena ni hatua ya kuua chama. Drastic measures may be necessary kuokoa chama.
 
usiishauri chadema kwa hisia za ccm ........punguza hisia wewe hata siku moja huoni kosa la zito ni chadema tu,chadema inasimamia katba yake...nibora chadema ife kuliko huyo zitto aendelee kuwa chadema kamati kuu fukuzeni huyo aliyeleta ubaguzi mbaya kabisa kwenye chama..

pamoja kamanda..
 
Kweli PASCO umepotea kabisaa kitaluma,kijamii na kisiasa! labda niseme wazi kabisa kuwa huwa husomi general comments za wanachama wa chadema humu ndani. kwa maoni ya walio wengi,ZZK is already regarded a non persona grata.hahitajiki tena.sababu zilizomfikisha hapo ni nyingi na anazijua vizuri!! Ni ndumila kuwili.

Pili sidhani PASC0 m ccm 100% unaweza kuiombea mazuri CHADEMA! na kimsingi na wewe huna jipya kama ZZK, do not waste your time kuiandika vibaya CDM,kuiombea mabaya CDM, you will never win!! ZZK hata akishinda kesi zote, na tunajua ndivyo itakavyo kuwa lakini kamwe CHADEMA HII ZZK HATOKUBALIKA,LABDA KAMA ATAENDESHEA SHUGHULI ZAKE HUKO MAHAKAMANI.
 
Wisdom misused is wisdom abused. Why should you care ilhali unajulikana sio tu ni CCM damu bali pia mmoja wa watu wanaoombea CDM ife kifo hata cha ghafla?

Baadhi ya Watanzania wenzetu wana tabia ya dharau flani dhidi ya wenzao. Do you seriously think Chadema nzima haina watu wenye kuweza kuipa ushauri wa busara na manufaa kwao? Rules are simple, never ever entertain "free offers" from your enemy. Ushauri wowote 'mwema' kutoka kwa wana-CCM kwa CDM unaambatana na 'dua za kimoyomoyo' kutamani chama hicho cha upinzani kife.

Kwanini 'busara' hizo zisielekezwe CCM? Hicho ni chama tawala, na kwa maana hiyo lolote linaloihusu linawagusa Watanzania wote.Ifike mahala mjiskie aibu wenyewe: hamwezi kuiombea dua jema CDM huku mnahangaika 'kuiroga'

All I'm expecting from CDM is a big THANKS, BUT NO THANKS.

Hahahahah ila Mh. Mbowe ameentertain free offers from Rostam Aziz,Sabodo and,Mkono aren't they CDM's enemies??
 
Kweli PASCO umepotea kabisaa kitaluma,kijamii na kisiasa! labda niseme wazi kabisa kuwa huwa husomi general comments za wanachama wa chadema humu ndani. kwa maoni ya walio wengi,ZZK is already regarded a non persona grata.hahitajiki tena.sababu zilizomfikisha hapo ni nyingi na anazijua vizuri!! Ni ndumila kuwili.

Pili sidhani PASC0 m ccm 100% unaweza kuiombea mazuri CHADEMA! na kimsingi na wewe huna jipya kama ZZK, do not waste your time kuiandika vibaya CDM,kuiombea mabaya CDM, you will never win!! ZZK hata akishinda kesi zote, na tunajua ndivyo itakavyo kuwa lakini kamwe CHADEMA HII ZZK HATOKUBALIKA,LABDA KAMA ATAENDESHEA SHUGHULI ZAKE HUKO MAHAKAMANI.

Kwa hili ttz lililipo CDM Ina kazi kubwa sana,watu wa CDM mind zao zimekuwa blindfolded,ht waambiweje ukweli hawackii,they digging their own grave
 
Tatizo ni viongozi na wanachama misukule kwenye vyama vyote vya siasa.Wewe ukimkosoa kiongozi ukiwa CCM utaambiwa wewe ni CHADEMA,ukiwa CHADEMA utaambiwa wewe ni CCM.Chadema kama Chadema ebu iangalie walioipigia kura 2010 sio Chadema pekee yake bali ni wapenda mageuzi kama PASCO kwa hiyo sio kila anayetofautiana nanyi kifkra lazima awe CCM auCUF tofauti za kifkra ndio ukomavu wa demokrasia ndani ya chama chochote, tuondoe hii dhana ya usaliti.
 
ukishauliwa na -------- na wewe ukaufanyia kazi ushsuri wake vasi utakuwa -------- kuliko David...
 
Tatizo ni viongozi na wanachama misukule kwenye vyama vyote vya siasa.Wewe ukimkosoa kiongozi ukiwa CCM utaambiwa wewe ni CHADEMA,ukiwa CHADEMA utaambiwa wewe ni CCM.Chadema kama Chadema ebu iangalie walioipigia kura 2010 sio Chadema pekee yake bali ni wapenda mageuzi kama PASCO kwa hiyo sio kila anayetofautiana nanyi kifkra lazima awe CCM auCUF tofauti za kifkra ndio ukomavu wa demokrasia ndani ya chama chochote, tuondoe hii dhana ya usaliti.

pasco yupi huyu huyu, au wa David, huyu hanalolote anawaza tumbo lake lishibishwe na lowasa...
 
Kwa hili ttz lililipo CDM Ina kazi kubwa sana,watu wa CDM mind zao zimekuwa blindfolded,ht waambiweje ukweli hawackii,they digging their own grave

tatizo ni Zitto hatumtaki...na tutameondoa galafu chadema haiwezi kudgauliwa na vibaraka wa lowasa/ccm, eti ccm inaishauri chadema namna ya kumaliza matatizo yake ------- kabisa, pasco kaanze na matatizo ya mjinga wako lowasa ndiyo ufikiliehuku gata hivyo hatuhitaji ushauli qakijinga ulioletwa na --------...
 
Back
Top Bottom