Ushauri unahitajika hapa tafadhali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Una kiwanja Bunju lakini kwa sasa unaishi kwa kaka. Umepata mchumba mnategemea kufunga ndoa. Bugdet ya harusi mliyonayo mkononi ni milioni 10. Hii ni pesa wachumba waliweka kwa pamoja kwa miaka miwili.

Hawataki michango wameomba zawadi kwa atakaeweza. Mama wa mke anataka watumie milioni 2 kwa harusi simple na milioni nane wajenge nyumba ya nyuma kwenye kiwanja chao.

Maharusi wanasita, ingawa walipanga harusi ndogo lakini si ya milioni 2.
 
Mil 3 tu unafanya harusi nzuri tu na ya kufana. Muhimu upate wasimamiaji wazuri, tena ndugu na marafiki wa damu hawawezi shindwa kuwaongezea lak 5 - mil1.
Mil 7 unashusha hata kijumba cha kawaida kuanzia maisha.
 
Waambie waamke asubuhi moja waende kwa paroko huku wakiwa na washenga wao ,mama mkwe,baba mkwe na watu wasiozidi kumi ,pale nyumbani wapike chai kwa mikate nafikiri harusi itakuwa imekwisha baada ya wiki waanze ujenzi wa nyumba ya ndoto yao .Nyumba itajengwa na wao wasisikilize miluzi ya nje
 
Huu ushauri wa dizasta nadhani utakufaa

Tungeweka kifusi cha mchanga, ukachagua harusi ya kisasa

Ukalia machozi ukavunga mpaka sasa tunaishi kwenye nyumba ya kupanga

Kisa unasema dunia tunapita mpango gani huu, ndani hatuna hakiba ya pesa ni vidani tuu

Sitasahau siku madeni ya harusi bado sijalipa ukanilazimisha nikope ili twende honeymoon
 
Kwakweli ni ujinga utumie pesa uliyochanga kwa miaka miwili ndani ya siku moja halafu uanze tena kuhangaika.
 
Mama wa mke aache upuuzi


Kama anataka kufanya maamuzi akafanye kwenye ndoa yake na mumewe.Kifupi hayo mawazo ayatumie kwenye ndoa yake binafsi iwe nzuri zaidi.

Ushauri si lazima kufuata asianze kumbelembele kwenye ndoa za watu
 
Wafanye sherehe maana hakuna muomba ushauri asie na majibu ya tatizo lake.
 
Nimemkubali mama mkwe.

Utashangaa jamaa wanafanya harusi ya milioni 13,milioni 3 wanakopa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom