Heshima kwenu wakuu. Usipite bila kushauri.
Kuna issue ya kimahusiano inaleta utata kwenye familia.
Tuna kaka yetu mkubwa ameo mwaka wa Saba sasa na hawajabahatika na mkewe kupata mtoto. Familia imewahi wasidia sana kujua nini chanzo cha tatizo mara kadhaa na taarifa rasmi za kitabibu tunayoijua kama familia ndugu yetu ana tatizo la kutokua na mbegu za kiume yaani azoospermia . Hali hii aina uhusiano na kufanya mapenzi na kulizishana bali ni kwamba mwanaume anakua hana mbegu za kiume kwenye manii yake.
Sasa hivi karibuni imeripotiwa case kuwa amempa mdada ujauzito. Brother amekili kuwa amewahi kutembea bila kinga na huyo dada ila hana uhakika kama dada alikua hana jamaa mwingine. Dada huyo amekua akifuatwa na family member akiulizwa kuwa ujauzito ni wa nani ili kuhepusha mgogoro unaoendelea kwenye familia. Mara zote dada amekua akisema hakua na mtu mwingine kipindi icho wanakutana, na ana uhakika kuwa ujauzito ni wa brother.
Mwanzoni brother inaonekana alikua anampa msaada wa kujikimu dada huyo ila baada ya tafaruku kubwa linaloendelea home kasitisha saport ,kwani mkewe amedai yuko tayari kuachika kama kaka etu ataendelea kuwasiliana na huyo dada na kumsaidia. Fujo na kelele kila siku home aziishi na kuitwa familia kutatua mgogoro.
Dada huyo aliyepewa ujauzito alikua amepanga na anafanya shughuri zake ndogo ndogo . Ila ujauzito umekua ukimsumbua ,kutapika kama kote na kila week hospitali, hali iliopelekea kushindwa kujihudumia na amerudi kwa wazazi wake.
Mama wa huyo dada kaleta mashitaka home akitaka kaka yetu aendelee kumsapot huyo dada hadi atakapojifungu ili watatue mgogoro kwa kipimo cha DNA.
Wife wa brother kusikia pendekezo hilo kagoma katu katu kuwa ana uhakika mmewe anabambikiwa mimba na kuwa dada huyo anataka mtu wa kumlelea ujauzito. Kifupi ahamini mmewe kamtungisha mimba dada huyo.
Juzi tu wamerudi hospitali na bado jibu ni lile lile kua kaka hana mbegu za kiume.
Sasa wakuu katika mkasa kama huu
Busara ni nini ?
Kuikana mimba hadi mtoto azaliwe huku unajua kuwa yule dada anateseka na familia yake imekomaa hawana uwezo wa kumtunza mtoto wao ?
Au kaka amsapoti mdada huyo hadi ujauzito ukamilike na kipimo cha DNA kifanyike.
Familia imekwama nini kifanyike kwani vikao haviishi home kila siku
Wakuu ushauri wenu ni upi kwenye kisa kama hiki?