USHAURI: Uandishi wa Thread Titles kwenye Forum hii

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
880
327
Habari wakuu!

Kuna hili suala la uandikaji wa title za thread zetu naomba niliongelee kidogo. Mimi naamini kichwa cha habari kina uzito mkubwa sana tu katika habari husika, kichwa cha habari kinaweza kukushawishi uisome habari hiyo au kinaweza fanya usitake kabisa kujua kilichopo ndani kutokana na picha uliyoipata kwa kusoma tu heading.

Mda huu naoandika hapa kuna nyuzi/threads 2 zenye title msaada, inawezekana sio tatizo kwa mtazamo wa wengine lakini kwa mtazamo wangu hili linanitatiza. Kuna threads nyingi tu zenye title za aina hii, msaada, msaada wa haraka, naomba msaada, nisaidieni katika hili, mimi zinanitatiza kwasababu haujui zinazungumzia nini na kuzifungua au kutozifungua inategemea na mood yako kwa wakati huo.

Ushauri wangu;
Mi nashauri kuwe na prefix ya msaada then kwenye title mtu aandike anachohitaji kusaidiwa. Title kutokuwa specific ndio sababu kubwa ya kukuta thread imerudia kitu ambacho bado kipo current kinajadiliwa kwasababu mwenye tatizo hakuona hiyo title. Pia hata kufanya searching inakuwa shida kwasababu huwezi pata majibu ya unachohitaji kama ulitumia query ya topic.

Mfano huu wa title naona utatafaa zaidi Msaada Tafadhali: Keyboard Hai-respond..
Tilte ipo brief and specific, hii itatusaidi kupata response kwa haraka. Naomba wana jamvi tuliangalie hili jambo na kama linafaa basi tufanye hivyo kwa manufaa ya wengi.

Asanteni.
KXY.
 
kuna thread niliweka inafanana na hii ila yenyewe ina deal na contents. Mtu anaweka thread kama hivi:
title: Msaada haraka!
Content: Jamani computer yangu imezima nimejaribu haiwaki. Naomba mnisaidie

inasikitisha! Kwanza lazima mtu ajue hapa watu wanafanya volunteer hivyo title yenye mwonekano wa kulazimisha mambo itakimbiza watu badala ya kuvuta msaada. Pili elezea kwa undani kilichotokea na weka message unayopata. Nitoe mfano wa swali zuri

title: Computer Imezima ghafla na haiwaki tena
content:
wandugu wanaJF, nina Laptop yangu Presario C400 ambayo nimeitumia kwa muda mrefu haijawahi kunisumbua. Jana nilipokuwa naitumia, ikazima ghafla na haijawaka tena. Nikiiwasha inabip mara mbili mfululizo kisha inazima tena. Nimejaribu kubadili battery na charger bila mafanikio. Nitashukuru kwa msaada wowote toka kwenu,
HT

hapa ata least mtu anapata idea aanzaje kukusaidia. Nakubaliana na mtoa hoja!
 
Naunga mkono hoja. Pia kuna ile kutoa maelezo mafupi. Mfano mwanajamv anatoa post inasema 'pc yangu imezima nisaidieni wanajf ' kwanza hajaspecify laptop au desktop.imezimaje? Yani mpaka uje kuelewa shida yake basi umeshamuuliza maswali sana hapo. Wanajf wajitahidi kuwa clear ili wasaidiwe.
 
@ 3D, salito, bampami, RDI, FF na MpigaKelele nawashukuru kwa kuunga mkono hoja.

@ HT na Mr. Cool ushauri wenu ni vizuri ukizingatiwa pia.

Kikubwa sasa ni utekelezaji sijui tutafanya vipi ili watu wafuate haya maoni, tuchangie way forward inakuaje?
 
Hii ndiyo raha ya jf bana enaelimishwa kila kitu.

Ngo ngo ngo ngo ngo ngo naunga mkono hoja.
 
Kweli kabisa, hakuna kinachoniudhi kama kufungua JF na kukuta Thread 3-4 zote zenye vichwa visivyokuwa na maana "Msaada", "Msaada Tafadhali", "Nimekwama.."
 
@ 3D, salito, bampami, RDI, FF na MpigaKelele nawashukuru kwa kuunga mkono hoja.

@ HT na Mr. Cool ushauri wenu ni vizuri ukizingatiwa pia.

Kikubwa sasa ni utekelezaji sijui tutafanya vipi ili watu wafuate haya maoni, tuchangie way forward inakuaje?

utekelezaji ndiyo pagumu KXY
 
@ 3D, salito, bampami, RDI, FF na MpigaKelele nawashukuru kwa kuunga mkono hoja.

@ HT na Mr. Cool ushauri wenu ni vizuri ukizingatiwa pia.

Kikubwa sasa ni utekelezaji sijui tutafanya vipi ili watu wafuate haya maoni, tuchangie way forward inakuaje?

ingekua bomba zaidi hii inshu ingezingatiwa kwnye majukwaa yote.hii thread ingehamishiwa kule kwnye jukwaa la macoplaints .........naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom