USHAURI: Tufute vyama vyote vya siasa tuanze upya.

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
1,250
2,000
Tuanze na CCM chama ninachokipenda.

Yaani CCM, ilikua mbovu kweli wakati mimi nakua. Siku zote hizo nilikua najipa moyo kwamba ndani ya CCM kuna watu wazuri na tutajirekebisha tu mimi mwenyewe nikiwemo.

Alipoichaguliwa Magufuli nikaona chama ndo kimepoteza muelekeo kabisaaaa, lakini watu alioanza kuwateua Magufuli kwenye nafasi za juu ndani ya chama wakaanza kukipa uhai tena.

Sikuwahi kuwaza kwamba katibu Mkuu wa CCM atakuwa msomi mwenye Phd( na Bashiru ni msomi kweli kweli). Kwahiyo, tukawa tumepiga hatua kuuubwa sana kuelekea upande sahihi. Wasomi nao wakaona CCM imeanza kuwatambua, hivyo tukaanza kuona utashi ndani ya CCM.

Sasa baada ya kifo cha Magufuli, tumerudi nyuma tena. Tumeanza kujaza mizigo kwenye chama. Akina Kinanana ambao waliihujumu nchi na chama wameanza kupata nguvu ndani ya chama.

Nimegundua namna pekee ya sisi kwenda vizuri kisiasa ni kuvunja vyama vyote vya siasa tuanze upya. Wabaya wajulikane na wasijifiche ndani ya wasafi.

Watu wanatumia CCM kama sehemu ya kujipatia nguvu. CHADEMA hamna chama hapo mnapoteza muda tu, viongozi wa chadema hawana nia ya dhati ya kuleta taswira mpya nchini kwetu.

CHADEMA mfumo wake wote wameiga CCM, chadema kuna kamati kuu ambayo siyo ya muhimu kwa chama chenye demokrasia ndani yake. Matawi yote ya CHADEMA ni copy and paste kutoka CCM, ni sawa kuwa na CCM isiyo na nguvu.

Mwenye uwezo wa kuvuruga siasa za nchi yetu, avuruge tuanze upya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom