Watanzania na Waafrica kwa ujumla tunapenda vitu vizuri na vipya. Mimi naishi Texas, USA na nataka kuwajulisha reli zenye manufaa makubwa sana kwenye uchumi wa nchi hii ni reli za kizamani "metre gauge railway" na sio "Standard Gauge Railway" za umeme.
Hizi reli za kizamani ndizo zinasafirisha mafuta, magari, mifugo na mavuno mengi ya kilimo sehemu tofauti za nchi kwa bei rahisi.
Mfano kuna reli kutoka California mpaka Texas kote huko inapita kukusanya mafuta sehemu tofauti mpaka yanafika Houston, Texas ambako yanasafirishwa kwenda nje ya nchi au kusafishwa kwa matumizi ya ndani.
Nimesema yote hayo kuhimiza na kushauri upanuaji wa metre gauge railway hasa sehemu zenye kilimo kuanzia kusini mwa nchi yetu kote, Tanga mpaka Mwanza, Arusha mpaka Nairobi, Tanga mpaka Mombasa na sehemu nyingine muhimu.
Hii itasaidia sana kukuza Kilimo kwa kupunguza gharama kubwa za usafirishaji wa magari ya mizigo. Lakini uzuri hizi reli ni za bei nafuu kutengeneza. Lengo kubwa liwe Kilimo huu ni ushauri wangu.