Ushauri tafadhali, mchumba akataliwa ukweni

Ushauri tafadhali, mchumba akataliwa ukweni

Bree ven

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
375
Reaction score
368
Habari za majukumu wanajamvi,

Nina rafiki yangu wa kike ambaye hivi majuzi alimpeleka rafiki yake wa kiume ambaye ni mume mtarajiwa huko kwao yaani kwa wazazi wa mwanamke kwa utambulisho zaidi kabla ya kutoa mahari. Walipokelewa vizuri siku ya kwanza na siku ya pili kuku kachinjwa ikawa safi kabisa. Huyo mwanaume alizaliwa na ulemavu kidogo ktk miguu yake ,na ni mfupi kwa kimo.

Ana akili zake safi kabisa na ni mtu makini, 'inshort he has a great personality' Wote wawili ni wacha Mungu na ukweli hawajashirikiana tendo la ndoa. Sasa mara baada ya kurudi huko kwao mjini wazazi wa mwanamke wakampigia simu na kutuma sms kwa mwanao wa kike kwamba hawamtaki huyo kijana kwa sababu ya ulemavu wake na itakua aibu pale kijijini kwao, inasikitisha lakini ndo hali halisi kwa wazazi hao.

Hivo wamemtaka binti yao akate mahusiano hayo haraka sana kwani hawatompa support ktk hilo. Binti anampenda kijana na kijana anampenda binti. Binti kachanganyikiwa kwani anamuonea huruma sana huyo kaka na hajui afanyaje. Akiolewa ndio atatengwa na ukoo wote, na kijana hana baba wala mama. Binti bado yuko sokoni kwani kuna vijana wengi bado wanajitokeza kwake.

Sasa amebaki njia panda je afanye nini? Wazazi wanaendelea kumsisitiza hasa mama yake kua ni bora aolewe hata na mtu mlevi au kijana asiye na kazi kuliko huyo kaka, kwa madai kua anaweza kuwaletea hata wajukuu walio na ulemavu. Ama hakika sikuamini kwamba bado kuna familia kama hizi lakini hii ndo hali halisi.

Ushauri wenu tafadhali kwa binti huyu
 
mpe pole, japo kuna usemi wasema "RADHI YA WAZAZI", atafute wazee wenye hekima awashirikishe kidogo tuu...atakayopata achanganye na akili yake inasemaje.....
 
huyo jamaa hakumwaga hela ndio maana wazazi wamekuja na huo ujinga.

laiti wanavyoondoka angemwachia mama kitenge cha 50000 na laki ya shati la mzee hakuna ambaye angefungua mdomo.
 
Wazazi wa binti hawajui kuwa ''kabla hujafa hujaumbika''?

Kama issue ni ulemavu wa kijana hapo wazazi wanakosea, what if kama binti yao angekuwa mlemavu na akakataliwa ukweni, wangejisikiaje?

Binti ni mtu mzima, japo ushauri wa wazazi ni wa muhimu lakini imefika wakati wa yeye kufanya maamuzi yake. hatuwezi kumwambia afanye nini au aamue vipi ila yapo mambo ya kuangalia katika maamuzi

1. Anawaelewa vizuri wazazi wake? je hao wazazi ni watu wa aina gani? Wapo wazazi wengine majanga tu so hata ushauri wao nao pia unautazama mara mbili mbili...

2. Yeye anaonaje, je issue ya mume ni ya kuchaguliwa na mzazi/ au ya kupata approval kutoka kwao?

3. Anampenda kweli huyu kijana mwenye ulemavu au anamuonea huruma tu kwa sababu ya ulemavu na uyatima wake?

4. je kijana mlemavu, anatosha kuwa mume bora kwake?


Ahsante.......
 
Duu,mpe pole sana ivi hao wazazi wa huyo mdada ni wacha mungu kweli au wana moyo wa ubinadamu? kwani huyo mkaka amependa kua hivyoau wao wamejiumba wenyewe? kwakua ni wazazi awasamehe bure....
 
huyo jamaa hakumwaga hela ndio maana wazazi wamekuja na huo ujinga.

laiti wanavyoondoka angemwachia mama kitenge cha 50000 na laki ya shati la mzee hakuna ambaye angefungua mdomo.
Hahaaaaa
 
Wazazi wa binti hawajui kuwa ''kabla hujafa hujaumbika''?

Kama issue ni ulemavu wa kijana hapo wazazi wanakosea, what if kama binti yao angekuwa mlemavu na akakataliwa ukweni, wangejisikiaje?

Binti ni mtu mzima, japo ushauri wa wazazi ni wa muhimu lakini imefika wakati wa yeye kufanya maamuzi yake. hatuwezi kumwambia afanye nini au aamue vipi ila yapo mambo ya kuangalia katika maamuzi

1. Anawaelewa vizuri wazazi wake? je hao wazazi ni watu wa aina gani? Wapo wazazi wengine majanga tu so hata ushauri wao nao pia unautazama mara mbili mbili...

2. Yeye anaonaje, je issue ya mume ni ya kuchaguliwa na mzazi/ au ya kupata approval kutoka kwao?

3. Anampenda kweli huyu kijana mwenye ulemavu au anamuonea huruma tu kwa sababu ya ulemavu na uyatima wake?

4. je kijana mlemavu, anatosha kuwa mume bora kwake?


Ahsante.......

Asante kwa hili..
 
Hilo ni moja ya mambo ambayo wazazi wanaweza kushauri lakini sio kulazimisha. Binti atafakari mwenyewe na afanye uamuzi.

Je kama wangeenda akiwa mjamzito kama ilivyo fashion siku hizi hao wazazi wangefanya nini?
 
Huyo kijana alienda mikono mitupu inaelekea,
 
Hilo ni moja ya mambo ambayo wazazi wanaweza kushauri lakini sio kulazimisha. Binti atafakari mwenyewe na afanye uamuzi.

Je kama wangeenda akiwa mjamzito kama ilivyo fashion siku hizi hao wazazi wangefanya nini?

Wazazi wamemtumia message na kumwambia "na kama una ujauzito wa huyo kaka wewe zaa tuu lakini hatumtaki huyo kijana"
 
Wazazi wamemtumia message na kumwambia "na kama una ujauzito wa huyo kaka wewe zaa tuu lakini hatumtaki huyo kijana"

Kweli hapo kazi. Ina maana wapo tayari asiolewe ili kumkwepa kijana. Wanasahau kwamba kila hutokea kwa sababu maalum.
 
Hata sisi watanzania tunabagua wenyewe kwa wenyewe jaman kisaa ulemavu daaaa kazi kwel kwel
 
Mmmh!!!!!! lakini mtu anaweza kuwa mlemavu lakini ni mtafutaji kiasi cha familia yake kuto lala njaa, bidada aangalie kama anaamini huyo anafaa kuwa baba sio shida, akiendekeza habari za wazazi wakati mwingine ataishia kulambwa na kuachwa hadi kuzeeka kwake, mambo mengine hata laana aipenyi bhana.
 
Sasa kama anampenda kweli habari za kuoneana huruma na bado kuwa sokoni zinatoka wapi? Ye mwenyewe inaonekana condition ya Mshkaji inamsumbua. Ampe za uso tu, he'll be alright. Guilt conscious atajifariji na siasa za wazazi.
 
Achane nae tu. Yeye asikilize wazazi kwani huko mbeleni akija pata shida watasema si tulikuambia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom