Ushauri tafadhali kuhusu wakwe kuongea kilugha

ajifunze yeye lugha yao hakuna namna!
 
Kwani wakiongea kilugha yeye anachunika ngozi???

Pyeeee mbona kuna binadamu wanapenda kukompliketi maisha???
 
Mtu akimuacha mkewe kwa sababu ya lugha ujue hakumpenda tu aisee......
 
Rahisi tu hiyo,mwezi tu watosha. Ayi laway,baba laway,a i doma,... Hâta JPM anaimanya
 
Rahisi tu hiyo,mwezi tu watosha. Ayi laway,baba laway,a i doma,... Hâta JPM anaimanya
Nshaisikiliza sana sielewi, nimekaa na wanyiramba miezi Sita tu nikajua kinyiramba, hicho kimenishinda
 
Ishue happ unajaribu kutumia bsara kwa kuwa huelwi means wamekuengua mazungunzo...tafuta playstation portable wao wakiogea we cheza mortalkombat au resident evil
 
wanawake msijifanye hakuna mnachojifunza na kung'ang'ania kujifunza kupaka rangi kucha tu. wewe kujifunza lugha ya ukweni inakushinda nini?? mbona ukiwa na wa kwenu unaongea cha kwenu??
 
unapokubali kuchanganya kabila haya mambo hayakwepeki.
mimi huwezi ukanifanya nianze kumtesa mama yangu kuongea kiswahili wakati hakijui. kuna vitu ni vyepesi tu. jifunze hata cha kuombea maji
 
Mtu akimuacha mkewe kwa sababu ya lugha ujue hakumpenda tu aisee......
Ngoja nikupe mfano huu:

Mume kaoa msichana mzuri tu lakini kila ndugu zake (wazee, mawifi na mashemeji) wakija kuwatembelea anakuwa kanuna au hawachangamkii. Hili sio kosa la kumuacha mke lakini litafanya hii ndoa isiwe na amani kwa sababu mume hatajisikia raha ndugu zake wakija kuwatembelea.

Vile vile, kama mke hataonesha ukaribu na vitu anavyopenda mume wake (marafiki, michezo, starehe za jioni, au kuzungumza kilugha na ndugu) haisababishii kuachwa bali itamfanya mume asiwe karibu (kihisia) na mkewe.

Kujifunza lugha ya ukweni sio utumwa au udhalilishaji, bali unamuashiria mumeo kuwa ungependa kushiriki mazungumzo anapoongea na ndugu zake. Hivyo hivyo mume nae ajitahidi kujua lugha ya ukweni kama nao wanapenda kukiongea kilugha chao wanapokutana.

Hiki sio kitendo cha ukandamizaji bali ni kitendo cha mapenzi/mahaba. Ni sawa na mke kujifunza kucheza pool (billiards) ili acheze na mumewe asubuhi - siku ya kazi (hii nimechapia tu).
 
Sio lazima kujifunza lugha ya mtu,hata mimi yangu hajui nitafutiwe mume kwetu?
 
Ewe ka salt hujui kujifunza lugha ya wakwe ni kama umekubalika? Akikoroge tu akivunje vunje tu ila mme wake naye ndo bomu kwanini asimlazimishe tuition week moja kabla ya kuja ili wakifika ana kianzio?
 
Sio lazima kujifunza lugha ya mtu,hata mimi yangu hajui nitafutiwe mume kwetu?
Kujifunza lugha ya mpenzi wako ni kitendo cha mahaba na sio ukandamizaji. Nyie watu hamjui hata hizi romance za vijijini jamani? Mkoje nyie?

Hujui ni kiasi gani mume wako anavyokunwa anapokuona unaongea na kucheeeka na mama yake. Huyo mume hata kama alikuwa ameficha mgao wake wa Escrow mtungini atautoa tu akupeleke Dubai. Muwe na vijiujanja ujanja kidogo wakina dada. Hee! Lugha tu ndiyo unayogangamalia hivi? Wengine wanasema "MWE!"
 
Sasa mbona inaongelewa kama lazim?nisinge react hivi.kama ni hiyari.ntajifunza nikitaka lakini sio itumike kama fimbo,ungeoa dada zako wanaijua vizuri tu
 
Sasa mbona inaongelewa kama lazim?nisinge react hivi.kama ni hiyari.ntajifunza nikitaka lakini sio itumike kama fimbo,ungeoa dada zako wanaijua vizuri tu
Huyu bwana alipokuja kukuoa wewe aliwapita wengi tu wa kabila lake. Hii ina maana amekupenda wewe zaidi. Tunachozungumzia hapa ni njia ipi ya kumfanya mke awe karibu na watu wa ukweni (hasa kama wanapenda kuongea kilugha).

Mfano rahisi.
Sio lazima kila mke ajue kupika.

Kutojua kupika (chakula alichopenda mumeo wakati anakua - comfort foods) sio kosa lakini kutotaka kujua kupika anachopenda mumeo ni kosa. Sio kosa la kuachika bali usilalamike mnapotembelea kwao ukamuona na shamra shamra anapokula chakula kilichopikwa na mama yake.

Ushauri - Jifunze kupika chakula anachokichekelea mumeo wakati kikipikwa na mama yake (mama mkwe wako).

Lugha haiko mbali sana na chakula katika mfano huu.
 
Mimi wakiongea lugha yao mbele yangu najua hayanihusu. Wakitaka kunihusisha wataongea lugha ninayoelewa.
Najua salamu
 
Nimekupima sana we mwanamke unaonekana una mahaba sana,
 
Hiyo lugha wanayoongea inamkera nini rafiki yako?

Kule kwetu mimi peke yangu ndio nimebahatika kujua japo kiswahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…