Dah unanikumbusha jamaa yangu ila yeye ni Muethiopia tulikuwa tunafanya kazi pamoja muda mrefu nchi za watu, alikuwa anasomesha mchumba wake USA na karibu likizo zoote alikuwa anaenda huko. Dada kagraduate jamaa karudi toka likizo USA tuna muona kabadilika, yupo peke yake muda mwingi, hamuongelei mchumba wake tena kama alivyozoea, anacharaza kinywaji sana, anakuwa mmbishi sana kazini na mgomvi, utendaji wa kazi ukaanza kuwa mbaya sana sana.Ila muda woote hatukuwa tunajua ni kitu gani kimemtokea. Kuna wakati aliugua akapewa likizo ya muda mfupi ya matibabu, aliporudi ikawa mambo yaleyale - Cha kushangaza kuna siku aliamua kuondoka kurudi nchini kwakwe bila ofisi kujua. Ofisi ikaamua kumfuta kazi na vifaa vya kazi akaambiwa aviwasilishe hukohuko nchini kwake kwenye ofisi yetu ya Addis Ababa...... Baadaye taharifa zikaja kuwa chanzo cha mabadiliko ya tabia ya mwenzetu kumbe ni mchumba wake. Inasemekana alipoenda likizo ya mwisho mwanamke wake alimwambia amepata mchumba mwingine hivyo yeye asahau mahusiano yao kabisa.... Jamaa yake mpya wa huyo aliyekuwa mchumba wake naye akasiliba kabisa kwa kumuonya kuwa asijaribu kuingilia mahusiano na demu wake anayedai mpya kwake la sivyo atamchapa risasi. Na jamaa tunamjua ni mwoga sana hivyo aliamua kurudi bila kutunishiana misuli na mwizi wake.......Baadaye Boss wetu wa kazi alisitikika sana alipopata hizi details na kuishia kusema laiti angelijua tatizo lilikuwa ni la mahusiano angempa msaada zaidi wa kisaikolojia badala ya kumfukuza.....Alikuwa jamaa poa sana sana kazini ..Dah mahusiano wakati mwingine huzaa majanga jamaa alipoteza kazi nzuri nadhani na waliokuwa wanamtegemea nyumbani nao waliathirika pia.
Ni afadhari ujikite kwenye shughuri zako za msingi maana ukimwazia sana huyo demu akili inaweza haribika kaka, amekutana na maisha mapya huko...