Ushauri: Tabia ya mke wangu kunidharau inaniumiza sana

sitaki raha

Senior Member
Jun 8, 2016
127
112
Naomba niende kwenye mada, mke wangu alikuwa mama wa nyumbani nilikaa nae kwa upendo sana sijawahi kujutia na upendo sana na heshima mpaka dada yangu akasema nifanye mpango mke wangu awe na kazi, basi nikaanza mchakato kumpa elimu pia nikamtafutia kazi kabla ya kuanza kazi tulikuwa tunawasiliana kila siku maana nimezaa nae mtoto1. Nikamtafutia kazi mimi nipo Arusha akapangiwa kazi Bukoba sasa ndio tatizo limeanzia hapo.

Wiki ya kwanza kuripoti mawasaliano yalikuwa mazuri sana maana hela ya kuanzia nilimpa sasa alipoanza kupokea mshahara duuuuh! Akaaanza kunifanyia dharau napiga simu hapokei hata miss calls 30 akija hakutafuti anakutafuta siku akipenda, nikimuuliza Mara nilikuwa busy na kazi hata Jumamosi na Jumapili busy usiku busy basi umerudi home mbona unitafuti Mara simu haikuwa na Salio, nikimuliza tafadhali nipigie kwenye simu hukuwa nazo mbona ulipokuwa ujaanza kazi hukuwa na tabia hiyo umefika uko umekuwa busy.

Kunipigia simu kwa mwezi Mara 1 tena aniuliza mzima wewe nilikuwa nakusalimia au naomba kuongea na mtoto basi, unaweza kumuona online whatuaspp online ukituma SMS asubuhi anakujibu usiku ukiuliza nilikuwa unachat na best zake dah! Niliumia siku ambayo aliniambia kwa sasa siwezi kufanya lolote ana kazi yake siku hiyo nilitaka nimfanyie kitu ambacho hawezi kusahau maishani mwake nilitaka niende kazini kumharibia kazi ila dada yangu aliniomba nisifanye hivyo baada ya kumwambia nakuja kufanya hivyo akamwambia mama yake.

Mama yake akaniomba nisifanye hivyo sikutaka kumsikiliza ila nilisikiliza ushauri wa daada yangu mwaka 1umeisha sina mawasiliano mazuri mama yake akaniomba nimsamehe nikakubali ila kasema atajirekebisha wiki 1 tu baadae akaanza tabia yake toka anze kazi sijawahi kumuomba hela yake najua mshahara anapokea bei gani kuna siku nikamuomba hela kidogo akasema nakutumia baadae akaniambia sina nilimuuliza hela yako unafanyia nini maana sijawahi kukuomba hela yako wala kukuuliza mshahara wako unapeleka wapi hana cha kuniambia.

Kwanza kuongea nae kwa mwezi 1 moja mapaka nimeamua nikae kimia simuulizi lolote nimemuacha afanye anachojisikia sikuwahi kumuuliza sasa mimi kwa sasa nimekuja Dar kikazi nina miezi 2 wala sijawahi kumwambia kama nipo Dar nimekaa kimya, nina mpango wa kusafiri nje ya nchi kwa muda wa miaka 2.

Sijamuambia nyumba ya Arusha nimemuweka mtu nataka niuze nyumba ya Dar na gari yangu niondoke zangu bila kumwambia, mwanangu nimepeleka kwa dada yangu na nimemtafutia shule nzuri, mimi najiandaa kuondoka nikifika nje ya nchi namba itakuwa haipatikani ya Tanzania hawezi kunipata. Nirudi Tanzania nitaaanza maisha mapya na mwanangu kuoa tena sitaki.

Je, nimefanya kosa au pia ndugu zake nimeacha mawasiliano nao kabsia baada ya ndugu yako kunifanyia sivyo.
 
Mkuu wa kazi nina mambo 2 hapo ya kukuambia...

1. Kwa maneno mengine ninafikiri unatafuta mwanamke wa kupunguzia machungu af akijielewa huyo ndo awe mkeo sio? Ipo ile page ya love connect sijui.

2. Unamuumiza sana dadaako achana na hiyo tabia ya kumwambia mambo ya ndoa yako na kama na yeye huwa anakumbia basi shida ilianza kwenye malezi.

Oveeeer!
 
Haya maisha kwel hayana formula m2 umeona umsaidie msaidiane katka maisha mara ghafla anabadlka.... Ungemuacha vilevile nayo ingekua shida maskin pole jipe moyo... Upendo ni gharama unaweza ruka mkojo ukakanyaga kinyesi mfate uko aliko and talk to her ucwe una assume tu ukiwa arusha nenda mzungumze.... Upendo ni gharama sana kumpenda m2 ni gharama kubwa na lazma ukubal yote ila kuna muda ukifka inabd umuache mtu kwa ajil yako mwaya.... Kukaa kmya co suluhisho... Soln ni kuongea nae na ukajua msmamo wake uko wapi katika ndoa...!
 
Aaah, nimesoma kisa chako kw kweli kimeniumiza sana, kwanza pole kw yote yaliyokukuta, ndg yangu wanaake wanavitimbi vingi kilichokukuta wewe ni wengi tu kimewakuta, kifupi ulichokifanya ni sawa kw mtazamo wangu
Nashukuru sanaaaa ndio najiandaaa kusepa najua nitasahau najua huko niendako naenda kufany juhuku la nchi nitarudi kuishi na mwanangu
 
Mkuu wa kazi nina mambo 2 hapo ya kukuambia...

1. Kwa maneno mengine ninafikiri unatafuta mwanamke wa kupunguzia machungu af akijielewa huyo ndo awe mkeo sio? Ipo ile page ya love connect sijui.

2. Unamuumiza sana dadaako achana na hiyo tabia ya kumwambia mambo ya ndoa yako na kama na yeye huwa anakumbia basi shida ilianza kwenye malezi.

Oveeeer!
Mm lzm niombe ushauri kwa MTU wng wa karibu uwezi kukaaa kimia wkt una tatizo hrf mm sina mpg na mwanamke tabia zao ni hizo hizo
 
Hayo mambo alikuwa nayo toka zamani... Sema hakuyaonesha kwa sababu ya shida zake... Baada ya kumtoa kwenye wanga kidogo ndiyo karudi kwenye tabia zake...


Pole sana... Dunia hadaa walimwengu mashujaa...
 
Usitumie akili kubwa kudeal na mtu asiyenazo...mtimizie mahitaji mwanao huyo piga chini tena mazoea na ndugu zake wala kumtafuta acha.

Utakuja kujinyonga mwisho wa siku.
Kuna siku nilifikilia kichwa chake kiwe zaidi ya familia yake niliwaza sanaaa mwanangu tu ataishi maisha magumuu
 
Back
Top Bottom