Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

Ushauri: Siyaelewi haya maisha ya ndoa

"...Dharau,kuzira zira,,gubu,kununa muda wote na mwenye kinyongo muda wote.

Mabadiliko mengine nadhani ni ya kawaida kama kuninyima penzi".

Pole sana.

Zungumza naye ujue umemkosea Nini ili muyamalize.

Ila Kuna possibly ya yeye kutokuwa huru na wewe kwa sababu wazazi wanamshinikiza kwamba hawajapata mahari yake n. k. Gubu la wazazi linaweza kuwa linamuweka njia 🐼 panda.
 
Hizo tabia ni mbovu sana ,anajificha nazo akishaingia huko ndani anaanza kuzifungua moja moja akijuwa hutamgundua,aisee tabia ya kununua na Kila wakati ni shida Bora kuishi mwenyewe,maana unajaribu kuleta amani yeye amenuna TU. ukimuuliza anasema yupo sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo tabia ni mbovu sana ,anajificha nazo akishaingia huko ndani anaanza kuzifungua moja moja akijuwa hutamgundua,aisee tabia ya kununua na Kila wakati ni shida Bora kuishi mwenyewe,maana unajaribu kuleta amani yeye amenuna TU. ukimuuliza anasema yupo sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu anitie nguvu aisee mwanamke hapendi suluhu inaboa sana.

Najikuta muda mwingi niko karibu na Simu na kuongea nae wengi inanibidi niongee nawatu wengine
 
"...Dharau,kuzira zira,,gubu,kununa muda wote na mwenye kinyongo muda wote.

Mabadiliko mengine nadhani ni ya kawaida kama kuninyima penzi".

Pole sana.

Zungumza naye ujue umemkosea Nini ili muyamalize.

Ila Kuna possibly ya yeye kutokuwa huru na wewe kwa sababu wazazi wanamshinikiza kwamba hawajapata mahari yake n. k. Gubu la wazazi linaweza kuwa linamuweka njia [emoji209] panda.
Na mimi sio kwamba nimeamua kutolipa mahari mambo yangu hayajakaa sawa tu kwa kipindi hiki ila nilipata hela nyingi tu ,nikamwambia naenda kutoka mahari nkamkuta anakataa yeye mwenyewe na kuniambia tukafanye issue Fulani kiuhalisia ilituletea hasara tu .kwa sasa nashindwa kupata hela ya mkupuo
 
Ongea nae abadilike! Kama hadi ndugu zake wamemsusa kisa wewe, muoe tu bhana
Kwanini Yeye hataki kuwa upande wangu ihali anakumbuka nimesimama nae katika hatua zote nimeamua kukubali ujauzito.
Wengine wanakataaa .

Mimi mpaka leo naishi nae na ninalea mtoto vizuri tu.
 
Kwao wamemkataa coz inaonekana kabisa hakusikia ushauri wa wazazi wake na akaja kwako kwa mapenzi yake kwako,

Wazazi wake sio kwamba wanataka mahari coz ya hela bali mahari maana yake ni kua binti yao anaolewa na sio kuishi na mwanaume bila ndoa,

Familia ya huyo Mwanamke inaonekana wanajitambua sana na walimlea binti yao kwenye maadili mema ila mapenzi yake kwako yakamtia upofu.
So Hapo hamna undugu je nikija kulipa mahari inakuaje hapo?
 
1. Nimekuwa nikipata stress sana kama huyu mwanamke ananifanyia visa hivi naishi nae sijamua nikimuoa itakuaje atabadilika kweli au atakuwa mbogo tu?
Tabia ni kama ngozi, haibadiliki.

2. Je, upande wa mwanamke wameniziria mtoto wao kisa sijatoa mahari je Siku nikitoa mahari Kuna undugu au ndo tumemalizana.
Inategemea: kuna ambao huchukulia poa, husamehe na maisha huendelea na wengine hubaki na vinyongo kwa muda mrefu.

3. Kuna muda nawaza tuachane tu tulee watoto maana sioni future kwa huyu mwanamke na hata kama nitasema niforce nimuoe naona nitakuwa napalia makaa.
Sikiliza moyo wako. Mwisho wa siku hayo ni maisha yako.

Ushauri wangu:
▪︎ Usihangaike kumbadilisha tabia, hautaweza
▪︎ Hakuna mwanadamu mkamilifu: kama unaweza kuvumilia mapungufu yake muoe na kama hauwezi achana naye. The earlier the better
▪︎ Sikiliza moyo wako. Usiangalie watu wanasemaje. Mwisho wa siku utawajibika kwa kila uamuzi unaoufanya maishani mwako
▪︎ Ushauri ni ushauri, siyo amri. Usikubali mtu akuamulie maisha yako. Fanya uamuzi wako na uwe tayari kuwajibikia matokeo yake
▪︎ Kama utaamua kumwoa; toa mahari na fuata taratibu zote
 
Back
Top Bottom